Diwani Kata ya Kyela Matatani Kufuatia Kuanzishwa Mamlaka ya Mji Mdogo!

Kilitime,

Hapa vurugu tupu na wacha tuone mwisho wake utakuwaje.

Sikuandika jana kwasababu hata mimi yamenikuta, nimechongewa kwenye uongozi wa wilaya kwamba namwandika vibaya mbunge JF.

Eti mbunge amepewa IP ya computer ninayotumia na uongozi wa JF. Hiyo ni JF where we dare to speak openly!

Wote tunaotumia hiyo kompyuta ya kazini tuliwekwa kitimoto ila hawana ushahidi ni nani. Nitawajulisheni zaidi baadaye. Watu wanashindwa kufuatilia maendeleo, kazi ni kufuatilia wale ambao wanapingana nao kimawazo. Engineer hayumbishwi na mtu yeyote.

Kuna vikao vingi bado vinaendelea. Mwenyekiti amekataa kuomba msamaha ingawaje sasa ni kama anakubali tafsiri yake ya hiyo sheria ilikuwa na makosa.

Leo siku ya tatu watu hawafanyi kazi na wanaongelea mgogoro huo tu.

Nikipata maelezo zaidi nitawajulisheni. Wacha nilinde kibarua changu kwanza.

Pole sana mzee, kibarua ndo maisha ntaendelea kutafuta vyanzo vingine muhimu kutoka huko nna nduguzangu huko na sehemu ya wakwe zangu bado ipo likini ni kaaaaazi kwelikweli! habari nilizopata hivi punde ni kweli mbunge yupo huko na bado ngoma nzito kweeeeeeli kweli!

leo naingia kazini usiku kwahiyo naamini ntayajua mengi kweli kutoka huko hebu nambie nafasi ya mwakyembe inaendelea kuimarika?
na wakazi walipokeaje swala la posho mbili?
 
Naomba kujua hatua iliyochukuliwa na mwekiti wa almashauri ya kyela ina baraka za wakina nani na kuna ulazima wa kupata baraka kutoka wapi?

Pia nini kilipaswa kufanyika? nasikia mkuu wa wilaya amegoma uamuzi huu je inaashiria ana nafasi ya kuwa na maamuzi?? wenye mtu wao je yaan CCM wanasemaje?

Nyepesi nyesi zinasema hii imekuja mara baada ya mh Mahenge kuhoji kwenye balaza la madiwani nanukuu"KUNAHAJA YA MWENYEKITI KUENDELEA KUWEPO MADARAKANI IKIWA FEDHA ZINARUDI WAKATI KUNA MATATIZO MENG WILAYANI?" mwisho wa kunukuu hesabu za kyela zimegubikwa na matatizo lukuki Mmmh waheshimiwa kyela kuna mambooooo
 
Tarehe 13 nov 2009 ndio tarehe iliyoandikwa barua na M/KITI WA HARMASHAURI YA WILAYA YA KYELA kwenda kwa diwani wa Kyela Mh Mahenge maarufu kwa jina la MAKETE/HALF LONDON nakala kwa tamisemi dodoma, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi wa wilaya, afisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji mdogo wa Kyela, katibu wa ccm.

Kuwa kuwepo kwa mamlaka ya mji mdogo ktk oneo la kata ya Kyela mjini kunapelekea kata ya kyela isitambulike tena kwa maana kata hiyo kwa sasa imefutika hivyo diwani,wenyeviti wa vijiji kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa ya 1982 kifungu no.45(1) cha kushangaza ni namna nzima zoezi lilivyoendeshwa ni dhairi limegubikwa na mazingira ya visasi na kukomoana yaanI ukimwaga ugali mi ntamwaga mboga duh yaan sasa tunakoelekea si kwema Mwakyembe unayaona haya tunaujua uhusiano wako na makete si mzur

Wakazi wa Kyela tunaomba usimamizi wako na maelakezo yako tunazijua kazi na umuhim wa diwan huyu naogopa kufananisha ya richmond na posho mbili picha kama hiyo ipo kivingine hapa wilayani upeo wangu ktk sheria si mpana lakini sitoshelezwi na hatua zilizochukuliwa ingawa nna maswala kadhaa ya kujiuliza nisaidien kuujua ukweli na hatua stahili!

Tchao Kilitime!!

jamani nini kinaendelea?
 
Jamaan habari nilizozipata hivi punde ni kwamba mkuu wa wilaya ta kyela ametaka apewe muda kutafsiri maana sahihi ya kifungu cha sheria kilichotumika.

Ametuma watu ja waende Mbeya ili ijiridhishe zaid ingawa mwanasheria wa wilaya ameshaonyesha sheria haikutumiwa vizuri mmh yaelekea haya yatakua ni mazito kulingana na mazingira ya siasa za kyela yalivyo kwa sasa!
 
Wana JF mliopo kyela vp? sisi watu wa huko mmetushitua tunafuatilia mtandao kwa karibu tujulishane yanayojiri kila dakika
 
Kama ni kweli Mwakyembe kajiingiza kwenye mkenge huo, atakuwa amekosea sana.

Kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa Na. 7 ya 1982, Diwani hakomi kuwa Diwani kwa sababu tu ya kubadilika kwa Hadhi ya eneo.

Bali diwani hukoma kuwa Diwani kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Serrikali za Mitaa na si vinginevyo.
 
Sielewi ni kwanini mwenyekiti alichukua jukumu la kumwandikia diwani menzake barua ya kumtaarifu kuepo na mamlaka ya mji mdogo na vile vile kutengua nafasi yake.

Hicho ni kinyume cha sheria. Mwenyehaki kabisa ya kumwandikia barua diwani ni Mkurugenzi mtendaji wa wilaya kwani yeye pamoja na kuwa ndio mtendaji mkuu wa wilaya lakini vile vile ni katibu katika baraza la madiwani.

Kuepusha shari mwenyekiti amuombe radhi tu huo diwani ili yaishe.
 
Kilitime,

Hapa vurugu tupu na wacha tuone mwisho wake utakuwaje.

Sikuandika jana kwasababu hata mimi yamenikuta, nimechongewa kwenye uongozi wa wilaya kwamba namwandika vibaya mbunge JF.

Eti mbunge amepewa IP ya computer ninayotumia na uongozi wa JF. Hiyo ni JF where we dare to speak openly!

Wote tunaotumia hiyo kompyuta ya kazini tuliwekwa kitimoto ila hawana ushahidi ni nani. Nitawajulisheni zaidi baadaye. Watu wanashindwa kufuatilia maendeleo, kazi ni kufuatilia wale ambao wanapingana nao kimawazo. Engineer hayumbishwi na mtu yeyote.

Kuna vikao vingi bado vinaendelea. Mwenyekiti amekataa kuomba msamaha ingawaje sasa ni kama anakubali tafsiri yake ya hiyo sheria ilikuwa na makosa.

Leo siku ya tatu watu hawafanyi kazi na wanaongelea mgogoro huo tu.

Nikipata maelezo zaidi nitawajulisheni. Wacha nilinde kibarua changu kwanza.
Eheeeeeee bado uko kibaruani?? tunakutegemea san utupe za huko home!
 
Engineer said:

Mzee Engineer;

Umeenda mbali sana na hizo allegations zako. Kwakweli umenishangaza, sikutegemea kama mtu kama wewe kuandika hayo niliyoyakuza.

Yaani unataka kuharibu CREDIBILITY ya forum nzima kwasababu ya kutompenda Mwakyembe?

Ukiwa kama mtaalamu wa IT au communication unaelewa wazi kuwa hata ukipewa access na uongozi wa JF huwezi kuona IP address ya mtu, utakachoona ni GATEWAY ambayo inatumika na watu wote kwenye domain ya IP provider au kampuni husika.

Sasa Dr wa LAW ana akili gani ya kwenda beyond GATEWAY? au hata JF team ina uwezo gani wa kwenda beyond GATEWAY?, Kinachowezekana kufanyika ni kujulikana kwa GATEWAY ambayo ni moja na inatumika na komputa nyingi, baada ya hapo ndo admin wa hiyo internet service provider wako aseme ni mteja gani anatumia hiyo njia, na baada ya hapo administrator wa mteja naye aanze kutafuta ni computer gani imetumika na ni saa ngapi.

Nina uhakika kuwa hiyo ni kazi ya siku kadhaa kwa wabongo, hata usalama wetu wa taifa watatumia siku sio chini ya tatu na kwa kupata vibali vya hizo taasisi mbili (ISP na mteja) na wafanye kazi pamoja na wawe wana shule ya hiyo kazi.

Sasa kama unatuambia KYELA kuna watu wamepewa IP address iliyotumika ninashindwa kukuelewa. wadanganye wengine lakini sio sisi ambao IT and IS tulizijua kabla ya 1990.

Anyway, nilikuwa na kusapoti sana dhidi ya Mwakyembe lakini kwa sasa naanza kuona UPUPU taratiiiiibu.

Ila sikata tamaa kuwa unaweza kuwa mbunge Kyela, punguza spinning kidogo.

Wasalaamu

FP
 
Hamna mpya zaidi ya kuspin tu. Masanilo wa Texas taratiibu naanza kuwakubali

Imekuchukua muda sana kuanza kuona ukweli, rafiki yangu itabidi uniombe msamaha si unakumbuka ulienda nje ukanitusi na maneno makali?

Respect Mkuu!
 
Eheeeeeee bado uko kibaruani?? tunakutegemea san utupe za huko home!
Kilitime,

Hapa mambo bado ni magumu na ni rusha ngumi na mimi nirushe. Mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya ameandika barua ya kukanusha barua ya mwenyekiti wa halmashauri. Kwanza mwenyekiti hana power hizo na badala yake mwenye powere ni mkurugenzi na pia tafsiri yake ya sheria na hao waliomshauri ni mbofu mbofu. Kuwepo kwa mji mdogo hakuui kuwepo kwa kata na diwani.

Ila sasa limetokea lingine, sheria eti inataka madiwani watatu kuingia kwenye baraza la mji. Mwenyekiti kateua majina matatu bila kumweka diwani wa kata ambayo ndio mji upo. Na lenyewe wanapigana nalo ili kufuta uteuzi wake.

Mbunge na mwenyewe yupo Kyela na naamini ndiye anasimamia hii vita kwa upande wa Mwenyekiti.

Juhudi zinafanywa ili kuitisha kikao cha dharura cha madiwani kujadili mtafaruku huu na kuwachukulia hatua wale waliousababisha.

Kwasasa siwezi kuandika tena nikiwa ofisini. Wanataka kunifukuzisha kazi shauri ya siasa. Ila mimi ni engineer na nitapata sehemu nyingine ya kwenda. Tukishindwa mapambano ya kwenye JF, tutaendeleza ya mpaka kwenye vilabu.

Ninatafakari kilichotokea na japo mkurugenzi anasema tusiwe na wasiwasi lakini hawa mafia wa siasa za Kyela naona wako tayari kuua mtu.
 
Hizi sasa ni bange(i)... kilabuni huko mtakwenda wenyewe na Mwakalinga wenu.
 
Imekuchukua muda sana kuanza kuona ukweli, rafiki yangu itabidi uniombe msamaha si unakumbuka ulienda nje ukanitusi na maneno makali?

Respect Mkuu!

Huyo FP ndio zake hizo...... anapenda sana vijembe na udaku.
 
Kwasasa siwezi kuandika tena nikiwa ofisini. Wanataka kunifukuzisha kazi shauri ya siasa. Ila mimi ni engineer na nitapata sehemu nyingine ya kwenda. Tukishindwa mapambano ya kwenye JF, tutaendeleza ya mpaka kwenye vilabu

Mh Mbunge

This is very low, can you rephrase for records?

Masa aka Shalom
 
Kilitime,

Hapa mambo bado ni magumu na ni rusha ngumi na mimi nirushe. Mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya ameandika barua ya kukanusha barua ya mwenyekiti wa halmashauri. Kwanza mwenyekiti hana power hizo na badala yake mwenye powere ni mkurugenzi na pia tafsiri yake ya sheria na hao waliomshauri ni mbofu mbofu. Kuwepo kwa mji mdogo hakuui kuwepo kwa kata na diwani.

Ila sasa limetokea lingine, sheria eti inataka madiwani watatu kuingia kwenye baraza la mji. Mwenyekiti kateua majina matatu bila kumweka diwani wa kata ambayo ndio mji upo. Na lenyewe wanapigana nalo ili kufuta uteuzi wake.

Mbunge na mwenyewe yupo Kyela na naamini ndiye anasimamia hii vita kwa upande wa Mwenyekiti.

Juhudi zinafanywa ili kuitisha kikao cha dharura cha madiwani kujadili mtafaruku huu na kuwachukulia hatua wale waliousababisha.

Kwasasa siwezi kuandika tena nikiwa ofisini. Wanataka kunifukuzisha kazi shauri ya siasa. Ila mimi ni engineer na nitapata sehemu nyingine ya kwenda. Tukishindwa mapambano ya kwenye JF, tutaendeleza ya mpaka kwenye vilabu.

Ninatafakari kilichotokea na japo mkurugenzi anasema tusiwe na wasiwasi lakini hawa mafia wa siasa za Kyela naona wako tayari kuua mtu.

Thanks Engineer for updates! Ila naona kama upo kwenye hatua za kukata tamaa! Ukishikwa shikamana!
 
Tatizo hapa ni kuwa Mwenyekiti mwenye alikuwa hakimu katika mahakama ambazo tunasema court of no law.

Hakuna sheria ya Diwani kumfukuza diwani mwenzake, hapo jamaa kachemka sana.

Mahenge kachaguliwa na wananchi na ndio hao watakaomuondoa lakini hawezi kufukuzwa na mtu yeyote yule zaidi ya kusimamishwa na baraza la madiwani wenzake. Anasimamishwa na baraza la madiwani na sio kufukuzwa, sasa huyu jamaa ni sheria gani anazotumia hadi kuandika barua ya kijinga kama hiyo?

Mahenge amempiga bao Mwakyembe, ndio maana Mbunge anatumia kila rafu kumharibia jamaa lakini kashindwa.
 
Mzee Engineer;

Umeenda mbali sana na hizo allegations zako. Kwakweli umenishangaza, sikutegemea kama mtu kama wewe kuandika hayo niliyoyakuza.

Yaani unataka kuharibu CREDIBILITY ya forum nzima kwasababu ya kutompenda Mwakyembe?

Ukiwa kama mtaalamu wa IT au communication unaelewa wazi kuwa hata ukipewa access na uongozi wa JF huwezi kuona IP address ya mtu, utakachoona ni GATEWAY ambayo inatumika na watu wote kwenye domain ya IP provider au kampuni husika.

Sasa Dr wa LAW ana akili gani ya kwenda beyond GATEWAY? au hata JF team ina uwezo gani wa kwenda beyond GATEWAY?, Kinachowezekana kufanyika ni kujulikana kwa GATEWAY ambayo ni moja na inatumika na komputa nyingi, baada ya hapo ndo admin wa hiyo internet service provider wako aseme ni mteja gani anatumia hiyo njia, na baada ya hapo administrator wa mteja naye aanze kutafuta ni computer gani imetumika na ni saa ngapi.

Nina uhakika kuwa hiyo ni kazi ya siku kadhaa kwa wabongo, hata usalama wetu wa taifa watatumia siku sio chini ya tatu na kwa kupata vibali vya hizo taasisi mbili (ISP na mteja) na wafanye kazi pamoja na wawe wana shule ya hiyo kazi.

Sasa kama unatuambia KYELA kuna watu wamepewa IP address iliyotumika ninashindwa kukuelewa. wadanganye wengine lakini sio sisi ambao IT and IS tulizijua kabla ya 1990.

Anyway, nilikuwa na kusapoti sana dhidi ya Mwakyembe lakini kwa sasa naanza kuona UPUPU taratiiiiibu.

Ila sikata tamaa kuwa unaweza kuwa mbunge Kyela, punguza spinning kidogo.

Wasalaamu

FP

Mkuu FP,

Una maana gani? Mimi sio mtaalamu wa IT ingawaje sasa naijua IT kiasi chake.

Hayo mambo mengine naona unajichanganya bure. Sio wewe wa kwanza kuanza kuchanganya watu na unaweza ukaendelea.

Sisi tumeambiwa hivyo na sijamtuhumu mtu yeyote wa JF. Nimesema wamedai wamepewa au huelewi maana hayo maneno?
 
Thanks Engineer for updates! Ila naona kama upo kwenye hatua za kukata tamaa! Ukishikwa shikamana!

Kilitime,

Inabidi kuchagua njia nyingine ya mapambano. Nitaacha kuandika JF mpaka hapo nitakapopata njia nyingine ambayo haitahatarisha kibarua changu pamoja na vibarua vya wengine.

Kuandikia nje sio rahisi kwani sina muda na itakuwa gharama.
 
Back
Top Bottom