Diwani CHADEMA arejea CCM

Mbwa akirejea matapishi then inaonekana ana njaa sana basi...Mwache ajiongezee siku za kuishi kwa matumaini.
 
Hakuna ubaya kuhama chama hata kama JK akiamua kuhama leo ccm haitokufa, wapo waanzilisha na wakongwe wa siasa za upinzani (acha huyu diwani) walijitoa iwe nccr, cdm, udp nk lakini leo vyama hivi bado vinadunda na tena uelewa wa watz uko juu zaidi ya mtu aliyezoea kupigiwa makofi hata kama anakohoa
 
Anatumikia mabwana zake CCM yenye siasa uchwara ndio wanachokiweza sasa hivi ngazi ya ubunge ,ukurugenzi na wenyeviti wa vyama wameshindwa kuwatoa waliwafuma akina Hizza,Kabourou wakiwatumia wanawatupa kama madabwada mpaka vitengo ilivyoanzishwa kwa ajili yao wanavifuta ,Kwa sasa kwa ngazi hiyo ,kwani hakuna anayedanganyika wamebaki na ngazi ya madiani,wenyeviti wa vijiji ,mitaa na vitongoji baada ya muda tutavuka tuu
 
Akili za watanzania enzi CCM inatawala anafikiri ndo akili za watanzania wakati ccm inaongozwa, i mean dancing according to the rythm of CDM songs. Kapotea labda secretariat akagange njaa. Kwanza shule yake imekaaje? Hajamsikia mzee Tendwa? Au hata TV hana?
 
huyo diwani amefunguka macho cdm ni chama cha wavuta bangi
Synovet juzi tuu walisema ungefanyika uchaguzi wa rais Dr Slaa wa CDM angeshinda, kweli watanzania wengi ni wavuta bangi basi kumchagua rais from CDM, pole zako na hasira zako.
 
watu waliohama ccm kuja cdm kwa kuenguliwa au kuangushwa kwenye kura za maoni sina imani nao, mfano slaa na shibuda wanafanana kila kitu, slaa anakua mkali kwa ccm kambi anayoinyea kwa hasira za kuenguliwa kuwa mgombea, shibuda anakua mkali kwa sababu hizhizo, kamati kuu iwahoji uwezo wao wa kufikiri kwa nni waliondoka baada ya kuengulia na hapo kabla hawakuona shida zetu?
 
Safari ya ukombozi inahitaji wale wenye mioyo safi, safari ni ndefu na ni wachahce tu watafika kuichukua bendera yetu ya ukombozi, uwingi wa jeshi sio uhodari wa kushinda vita.
 
Diwani huyu alizoea ulaji wa chee ccm,amekuja CHADEMA hakuna hilo ni upigaji kazi na uzalendo mwing ila haki yako utapewa.Ukiwa CDM uweke maslahi ya Taifa mbele.Huyu ni sehemu ndogo sana katika chama,aondoke arudi ufisadini,hatutaki uchafu ndani ya makamanda wapigania haki.Tusonge mbele CDM.
 
Uyo Diwani ni ziro kabisa, maandamano yapo nchi zote. Alafu huyu Nchemba naye ni kilaza ana siasa za maji taka. Tutamuona igunga
 
WAKATI ikiwa katika mgogoro na madiwani wake wa Arusha, Chadema imepata pigo baada ya mmoja wa madiwani wake Singida kujiengua na kurudi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), akidai hataki kuwa sehemu ya machafuko nchini.

Diwani huyo, Simon Tyosela wa kata ya Urughu, Iramba Magharibi, alisema hayo jana katika Ofisi ya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, mbele ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM anayeshughulikia masuala ya Uchumi na Fedha, Mwigulu Mchemba.

Tyosela aliyehamia upinzani wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 baada
ya kuanguka katika kura za maoni ndani ya CCM, alisema hakushawishiwa kuihama Chadema na kurejea CCM, bali amenusa hatari kwa taifa katika siku za usoni.

Alisema, maandamano yenye sura ya uchochezi kila kukicha, yamemkosesha amani na
kujiona msaliti mbele ya Watanzania.

“Haya ya kushinikiza wananchi kuiga maandamano katika nchi za wenzetu, tena yasiyo ya amani, binafsi yamenishinda. Chadema hakuna demokrasia ya kweli na nilitarajia ingekuwa mstari wa mbele kuhangaikia maendeleo ya wananchi. Nimejiondoa kwa sababu mimi ni mpenda amani kwa nchi yangu.

“Kwa mtindo huu niliona kabisa hatuwezi kufikia malengo ya millennia, kwa sababu
kila kukicha ni maandamano, hakuna la maana linalofanyika kwa ustawi wa nchi
yetu,” alisema diwani huyo.

Alisema, hana cha kujutia kwa sababu wananchi ndio waliokuwa wamemshawishi kuingia Chadema wakitaka atumie chama kingine chochote kuingia madarakani, baada ya kushindwa kura za maoni.

Mchemba alimpongeza na kuitaka jamii kutokubali kuburuzwa na vyama vingine vya siasa kwa maslahi ya watu wachache wenye mwelekeo wa kulazimisha kushika madarakani kwa nguvu.

...............................................................................................
Amani ipi?
Malengo yapi? huko CCM atayafikiaje hayo malengo ya millenia?
 
Hasomi alama za nyakati ana panda baiskeli ya udongo wakati mbele yake kuna mvua. Pia alijua CDM kunakushibisha matumbo kama ccm. Hapa ni haki ya wa Tz kwanza.
 
CCM yenyewe umemeguka vipande vipande kila mtu na lwake imefika wakati mwenyekiti wa CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete anasuta baraza lake la mawaziri ambalo yeye ndio mwenyekiti wake halafu Diwani anatuambia hicho ndio chama inabidi ajiangalie upya
 
Haina majotrooo!diwani!? aliondoka david kafulila chama hakikuyumba.kwenda kule gamba mkubwa wee!
 
Huyu mtu hapashwi kugombe kwa tiketi ya Chama Chetu CCM kama tunataka kushida, na hapashwi kupewa Uongozi ndani ya chama sababu ni kigeugeu. Hawa watu wa aina hii ndo wamekichafua Chama.
 
huyo diwani amefunguka macho cdm ni chama cha wavuta bangi
where is your common sense? We mtanzania wa wapi huna nidhamu? Yaani Kitila Mkumbo, Mwesiga Baregu, Mzee Mtei, Magale shibuda, John Mnyika, Tundu Lissu na baba zatu waliochukua kadi za chadema ni wavuta bangi?
You need to meet somebody named PAW
 
Back
Top Bottom