Diwani CHADEMA arejea CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani CHADEMA arejea CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salimia, Aug 6, 2011.

1. S

Salimia JF-Expert Member

#1
Aug 6, 2011
Joined: Feb 14, 2011
Messages: 665
Likes Received: 1
Trophy Points: 35
WAKATI ikiwa katika mgogoro na madiwani wake wa Arusha, Chadema imepata pigo baada ya mmoja wa madiwani wake Singida kujiengua na kurudi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), akidai hataki kuwa sehemu ya machafuko nchini.

Diwani huyo, Simon Tyosela wa kata ya Urughu, Iramba Magharibi, alisema hayo jana katika Ofisi ya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, mbele ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM anayeshughulikia masuala ya Uchumi na Fedha, Mwigulu Mchemba.

Tyosela aliyehamia upinzani wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 baada
ya kuanguka katika kura za maoni ndani ya CCM, alisema hakushawishiwa kuihama Chadema na kurejea CCM, bali amenusa hatari kwa taifa katika siku za usoni.

Alisema, maandamano yenye sura ya uchochezi kila kukicha, yamemkosesha amani na
kujiona msaliti mbele ya Watanzania.

“Haya ya kushinikiza wananchi kuiga maandamano katika nchi za wenzetu, tena yasiyo ya amani, binafsi yamenishinda. Chadema hakuna demokrasia ya kweli na nilitarajia ingekuwa mstari wa mbele kuhangaikia maendeleo ya wananchi. Nimejiondoa kwa sababu mimi ni mpenda amani kwa nchi yangu.

“Kwa mtindo huu niliona kabisa hatuwezi kufikia malengo ya millennia, kwa sababu
kila kukicha ni maandamano, hakuna la maana linalofanyika kwa ustawi wa nchi
yetu,” alisema diwani huyo.

Alisema, hana cha kujutia kwa sababu wananchi ndio waliokuwa wamemshawishi kuingia Chadema wakitaka atumie chama kingine chochote kuingia madarakani, baada ya kushindwa kura za maoni.

Mchemba alimpongeza na kuitaka jamii kutokubali kuburuzwa na vyama vingine vya siasa kwa maslahi ya watu wachache wenye mwelekeo wa kulazimisha kushika madarakani kwa nguvu.

2. MtamaMchungu

MtamaMchungu JF-Expert Member

#2
Aug 6, 2011
Joined: Apr 10, 2011
Messages: 3,695
Likes Received: 507
Trophy Points: 280
Freedom doesnt come easily, tutafika tu.

3. L

Libaba Member

#3
Aug 6, 2011
Joined: Dec 12, 2010
Messages: 58
Likes Received: 0
Trophy Points: 13
Alizoea pesa za bure kwa magamba ila nina wasi wasi na upeo wake maana haki haiji hivi hivi kwa nchi zetu hizi "You have to fight for it". Salimia Iramba.

4. Khakha

Khakha JF-Expert Member

#4
Aug 6, 2011
Joined: Jul 15, 2009
Messages: 2,983
Likes Received: 371
Trophy Points: 180
Mpaka kufikia kilele cha democracy kuna milima na mabonde. Hyo ndo mikiki yake. At the end of the day kitaeleweka tu.

5. Tuyuku

Tuyuku JF-Expert Member

#5
Aug 6, 2011
Joined: Jan 6, 2011
Messages: 3,149
Likes Received: 1,407
Trophy Points: 280
alihamia CDM baada ya kuangushwa kura za maoni ili apate madaraka. Watu wanaokuja CDM kutafuta madaraka kama kina Shibuda hawafai kabisa. Wakati sisi tunapigania uhuru kamili wa Mtanzania, wao wanapigania matumbo yao. Njaa itawaua.

6. Crashwise

Crashwise JF-Expert Member

#6
Aug 6, 2011
Joined: Oct 23, 2007
Messages: 22,172
Likes Received: 862
Trophy Points: 280
kuna wengine leo arusha sijui wataenda chama gani lakini hii ndiyo garama za kutafuta haki..

7. Mwita Maranya

Mwita Maranya JF-Expert Member

#7
Aug 6, 2011
Joined: Jul 1, 2008
Messages: 10,569
Likes Received: 104
Trophy Points: 145

Ahaa kumbe huyo diwani ameamua kurudi kwao. Na hili bila shaka liwe ni somo tosha kwa chadema juu ya hawa wahamiaji wanapokuwa wamebwagwa huko magambani.

8. Mr. Bigman

Mr. Bigman JF-Expert Member

#8
Aug 6, 2011
Joined: May 7, 2011
Messages: 1,852
Likes Received: 628
Trophy Points: 280

ushauri wa bure Kwa CDM: Acheni kuchukua magamba na kuyaingiza ndani. Magamba hayaaminiki hata kama yakiwa ni Makapi

9. J

JACADUOGO2. JF-Expert Member

#9
Aug 6, 2011
Joined: Dec 13, 2010
Messages: 930
Likes Received: 3
Trophy Points: 35
Kwa hiyo kwa uwezo wake mdogo wa kufikiri ndo anahisi akihamia Magamba atazuia maanbmano ya CHADEMA? Huyo ni pumbavu kweli kweli na inaonekana amepigwa na njaa kali na tamaa ya ajabu!

10. Kishongo

Kishongo JF-Expert Member

#10
Aug 6, 2011
Joined: May 4, 2010
Messages: 932
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
Mwanzo wa anguko la NGO ya CDM

11. Mwita Maranya

Mwita Maranya JF-Expert Member

#11
Aug 6, 2011
Joined: Jul 1, 2008
Messages: 10,569
Likes Received: 104
Trophy Points: 145

Nasubiri kwa hamu kusikia madiwani vimeo wote wametimuliwa. Hakuna sababu kuwa na viongozi wa halmashauri wasio na nidhamu kwa viongozi wao wa kitaifa. Hao madiwani wakiachwa mbele ya safari wanaweza kabisa kukihujumu chama cha chadema wapigwe red card mara moja.

12. Mwita Maranya

Mwita Maranya JF-Expert Member

#12
Aug 6, 2011
Joined: Jul 1, 2008
Messages: 10,569
Likes Received: 104
Trophy Points: 145

haswaa, hawa wanaohamia baada ya kubwagwa kwenye kura za maoni ni wachuuzi tu. Chadema iwaamini watu wake ikiwafanyia kampeni vizuri wananchi watawachagua hata kama wasiposhinda si mbaya kwani wanabaki kuwa waaminifu kwa chama. Ona shibuda anavyowaumiza vichwa.

13. RedDevil

RedDevil JF-Expert Member

#13
Aug 6, 2011
Joined: Apr 30, 2009
Messages: 2,287
Likes Received: 903
Trophy Points: 280
Hizo ni siasa za Igunga zilishaanza!! Mwigulu Nchemba ndo atakayeongoza kampeni za CCM igunga! kama kawaida ya CCM huenda keshakula mlungula kusafisha njia ya Mwigulu kuelekea Igunga.

Kinachonifurahisha ni kwa jinsi gani huyu jamaa alivyo kwani haoni kuwa wanatanzania wa leo si wa jana, nilihuzunika sana mwaka 1995 wakati CCM walipotumia mauaji halaiki ya Rwanda kama njia ya kuwahadaa watanzania, na kweli kijijini kwetu watu waliogopa kumpa kura Mh. Mrema pamoja na CV yake nzuri aliyokuwa nayo kipindi hicho. Ila kwa sasa, siyo tena! kila mtu anajionea, anasikia na kukabiliana na hali ilivyo kila nyanja.

14. LordJustice1

LordJustice1 JF-Expert Member

#14
Aug 6, 2011
Joined: Jan 19, 2011
Messages: 2,264
Likes Received: 10
Trophy Points: 0
Mbona walishaondoka akina Kaborou CDM haijaanguka? Huyu Diwani upeo wake umekaa kimagamba! Ndani ya "utulivu na amani" kuna ufisadi wa kutisha na bila kuwapelekesha mchakamchaka Magamba yatakula bila kufuta midomo!

15. jogi

jogi JF-Expert Member

#15
Aug 6, 2011
Joined: Sep 25, 2010
Messages: 19,335
Likes Received: 12,801
Trophy Points: 280
huyo diwani amepewa hongo, mwigulu ni mtoa rushwa mkubwa, nia ilikuwa kuongoza, akapewa nafasi, naamini alidhani atakuta ulaji ndani ya cdm kama walivyozoea ccm, baada ya kutakiwa kuwatumikia wananchi kinyume na matarajio yake, ameshindwa kumkama punda. kumbukeni maneno aliyosema nchemba ndiyo amelishwa diwani kuyasema, hajasema alilazimishwa lini na nani kuandamana, anadai anakwepa kuwa sehemu ya machafuko, anataka kutuambia kwa akili yake finyu, yakitokea atajificha wapi yasimuathiri!, watz msikatishwe tamaa na wajinga, hata enzi kukoma biashara ya utumwa kuna watumwa waligoma kuachwa huru, diwani anafanana na hao, mwigulu anahusudu rushwa, kama vipi tuanze kumwaga data kwa kwenda mbele.

16. Eiyer

Eiyer JF-Expert Member

#16
Aug 6, 2011
Joined: Apr 17, 2011
Messages: 28,238
Likes Received: 3,673
Trophy Points: 280
Huu ni wakati wa kujulikana pumba na mchele,ni lazima maji yajitenge na mafuta,wasiokuwa na msimamo lazima waende kwa wanaofanana nao,hata wakati wa ukombozi "Sauzi"kuna weusi walikua upande wa wazungu na weusi hawakufa moyo,chama kipo kabla ya hao madiwani hata wakiondoka wote,chama kitasimama tu!

17. Mkuu wa chuo

Mkuu wa chuo JF-Expert Member

#17
Aug 6, 2011
Joined: Feb 3, 2011
Messages: 7,253
Likes Received: 244
Trophy Points: 160
huyo diwani ni mjinga sana!

18. figganigga

figganigga JF-Expert Member

#18
Aug 6, 2011
Joined: Oct 17, 2010
Messages: 14,975
Likes Received: 6,612
Trophy Points: 280

mia

19. Eiyer

Eiyer JF-Expert Member

#19
Aug 6, 2011
Joined: Apr 17, 2011
Messages: 28,238
Likes Received: 3,673
Trophy Points: 280

Mara mia!!!!

20. C

Campana JF-Expert Member

#20
Aug 6, 2011
Joined: Dec 2, 2008
Messages: 207
Likes Received: 9
Trophy Points: 35
Baada ya tukio hili tunataraji uchaguzi wa diwani kurudiwa. For CCM, it is too early to celebrate. Wwanaweza angukia pua uchaguzi utakapofanyika.

Loading...