Diwani CHADEMA ampongeza mbunge wa CCM

Diwani CHADEMA ampongeza mbunge wa CCM

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
[h=2] [/h] Ijumaa, Julai 19, 2013 05:33 Na Shomari Binda, Rorya

DIWANI wa Kata ya Tai (CHADEMA), Godfrey Masirori amesifia jitihada zinazofanywa na Mbunge wa Jimbo la Rorya, Lameck Airo (CCM), kwa kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo jimboni humo, akisema kuwa ni wa vitendo si wa kuongea.

Kauli hiyo aliitoa katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na mbunge huyo katika Kijiji cha Sota, baada ya ziara ya kukagua shughuli za maendeleo za jimbo hilo na kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Majengo, iliyopo katika kata hiyo baada ya kuezuliwa na upepo.

Masirori alisema mbunge huyo amekuwa ni mwepesi wa kujitoa na kushiriki mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika jimbo na pale yanapotokea majanga amekuwa akifika kwa wakati na kushirikiana na wananchi kutafuta ufumbuzi.

Masirori alisema, harambee iliyofanywa na mbunge huyo katika mkutano wa hadhara japo ni wa kushtukiza, lakini inaonyesha ni jinsi gani anavyoguswa na matatizo ya wananchi wa Rorya na kutaka majengo yaliyoezuliwa na upepo yaweze kukamilika na wanafunzi waendelee na masomo.

“Ndugu zangu hii shule ni yetu na wanafunzi wanaosoma hapa ni wetu, naungana na mbunge kwa kuchangia Sh laki moja ili shule hii iweze kukamilika kwa wakati na vijana wetu waendelee na masomo.

"Katika suala la shughuli za maendeleo, itikadi za kisiasa tunaweka pembeni na kwa pamoja tunashiriki shughuli za kimaendeleo. Jambo hili linalofanywa na mbunge ni jambo jema na kila mmoja ana kila sababu ya kusifia jambo hili,” alisema Masirori.

Akizungumza katika mkutano huo, mbunge huyo alisema aliguswa na taarifa ya kuezuliwa kwa shule hiyo akiwa katika vikao vya Bunge na kuamua kuaga ili kuweza kushiriki moja kwa moja katika tatizo hilo.

“Ndugu zangu niliguswa na suala hili na kuamua kuaga bungeni, lakini kabla sijafika hapa tayari niliagiza mafundi kuja kuangalia athari iliyopatikana hapa na kuanza kwa ujenzi, lakini kazi hii inahitaji ushirikiano ili vijana wetu waendelee kusoma.

"Sasa hivi suala la elimu ndilo linaloangaliwa katika kila sehemu, lazima majengo haya yakamilike na watoto wetu wasome, naomba kila mmoja aje kuchangia ili madarasa haya yaliyoezuliwa yaweze kukamilika,” alisema Lameck.

Katika harambee hiyo, zaidi ya Sh milioni mbili zilipatikana zikiwemo ahadi ya mifuko 19 ya saruji.
 
Safi sana. Huku ndiko kukomaa kisiasa. Huu ni uthibitisho kuwa utofauti katika siasa, dini au kabila usitutenganishe.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Subiri waje Bavichaa watamtukana diwani kuwa anachelesha ukombozi
 
Vijana wa magamba, wanaogopa BAVICHA vibaya mno!
 
Magamba wanapenda sifa za kijinga ukiwakoli tu taarifa unaikuta mitandaoni!!!!!!
 
aani hata mimi mwanachama nikimsifia kikwete najua uhuru wataandika,akili ikishaondoka kichwani ndiyo tabu yake.
 
Subiri waje Bavichaa watamtukana diwani kuwa anachelesha ukombozi

...jaribu kuhusisha ubongo ili angalau tuone uhalali wa buku 7 zako za leo kuliko huu utumbo mpana...
 
...jaribu kuhusisha ubongo ili angalau tuone uhalali wa buku 7 zako za leo kuliko huu utumbo mpana...

Kwa njaa ullyokuwanayo wewe kama kweli CCM wangekuwa wanalipa buku saba ungekuwa tayari mwanachama mtiifu.
 
Kazi nzuri sana Mbubge Airo na pia kazi nzuri sana Diwani Masirori.

Pamoja na mbunge Airo kufanya vizuri na mimi naamini ataendelea kufanya hivyo lakini 2015 tunampumzisha kwakuwa uwakilishi wake bado uko below average!
 
Alichokisema diwan ni sahih kwa jambo lile yasiyo sahih yako moyon, hata jk akimudu baadh ya sekta tunamsifu bt pima mazuri na madhaif kitakachopatikana ndio tiket ya ushind 2015
 
Kazi nzuri sana Mbubge Airo na pia kazi nzuri sana Diwani Masirori.

Pamoja na mbunge Airo kufanya vizuri na mimi naamini ataendelea kufanya hivyo lakini 2015 tunampumzisha kwakuwa uwakilishi wake bado uko below average!

Mchango wa laki moja ? Lakairoanafanya magendo sana na halipi kodi .Kama huamini muulize mpambe wake Albert Machiwa diwa ni wa CCM kutoka Kinesi wote ni watu wa magendo .Kupeana sifa kwa kadiri wanavyo ishi ni sawa na ndiyo siasa za kistaaraabu japokuwa naamini kwa akili ya Lakairo na asili ya CCM inawezekana kesha penyezewa.I am talking from the experience
 
Duu huyu jamaa naye anahamasisha mambo ya harambe?
Si wakati wa kampeni nilimsikia akisema kwamba yeye atakuwa anajitolea kila kitu pesa anayo?
Naona yamemshinda.
Ila kusema ukweli lameki airo anajiweza sana kiuchumi (ni tajiri), tatizo lake ni elimu.
Na kama rasimu hii ya katiba haitabadilishwa kwenye kile kipengele cha elimu kwenye sifa za mgombea ubunge, anaweza akawa ni mmoja wa watakaokuwa wanabaguliwa na kipengele hicho.
 
Magendo kawaida kwa wenzetu? ?? Maana ndio chaka lao! !!! Ukitaka mambo yako yanyooke njoo ccccm! Fredrick sumawe
 
duuuh! kweli magamba filisika, halaf sasa kufisika kwao kubaya
 
Back
Top Bottom