Division Zero na Mauaji ya Albino

Division Zero na Mauaji ya Albino

Ng`wanakidiku

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2009
Posts
1,195
Reaction score
232
Greath Thinkers,
Ni ajabu sana kuona watu eti wamepata zero wanashangaa. Na hivyo hivyo ndivyo watanzania majority wanavyoamini utajiri/umaarufu n.k. ni kuua albino. Hivi huu ujinga utaisha lini? Kwa nini umuue mtu ili uwe tajiri? Mbona hatujifunzi kuwa maisha bora yanakuja kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa? Hakuna nchi iliyopata kuendelea kwa kwa uchawi, na hakuna aliyetajirika kwa uchawi akadumu. Nadhani kuna umuhimu wa kuanzisha kipindi cha kuelimisha watu juu ya ujasiria mali.
 
kwa bahati mbaya ujinga (ukosefu wa elimu ya kweli) umeenea ngazi zote kuanzia wasioenda kabisa shule hadi wasomi wa vyuo vikuu. Ndio maana utakuta waziri, mbunge, mkurugenzi, nk anaenda kwa Sangoma eti anyoshewe mambo yake, na kuendeleza unyanyasaji/uuaji wa maalibino na maovu mengine.

Ndio - ukienda kwa Sangoma unachangia maovu hayo kwani Sangoma hutumia viungo vya watu au namna zingine zenye madhara.

Unajiita msomi, lakini unaenda kwa Sangoma - mchafu kama nini huyo Sangoma na maskini hohehahe - ati akusafishie njia! Yalaaaaa. Kweli ujinga ni kitu mbaya!
 
Sasa sijui nani amuelimishe mwenzake. Kama professor (mwenye PhD ya kusomea darasani) anaenda kwa sangoma ili ashinde ubunge, apewe cheo, ajilinde na uchawi, apendwe na wafanya kazi n.k. kweli Tanzania tuna majanga mengi. Wakati mwingine mi nasema bado sana kufikia level ya maendeleo tunayoyataka, kwani bado tuna tongo tongo nyingi machoni. Tuzidi kuliombea taifa labda wajukuu wa wajukuu zetu ndiyo watakuja kufaidi unono wa nchi.
 
Back
Top Bottom