division 1 point 9

emoshi

Member
Apr 2, 2011
28
1
wana JF mimi nimemaliza form 6 HKL na nimepata division 1 point 9 yaani CCC naombeni mnishauri nikasome kozi gani yenye soko hapa tz maana sitaki kumaliza chuo then nigange njaa mtaani na kisomo changu naombeni mnisaidie kimawazo maana najua mnauwezo sana.thankx.
 
mkuu hkl 1.9 bado upo kwenye competition kubwa sana... kwani kipindi umeamuwa kusoma hkl malengo yako yalikuwa nini ..? tuanzie hapo then wadau tutajaribu kukupa muongozo.
 
social work italipa maana social problems zinaongezeka zana. Soko linapanuka kwa kasi!!
 
mkuu hkl 1.9 bado upo kwenye competition kubwa sana... kwani kipindi umeamuwa kusoma hkl malengo yako yalikuwa nini ..? tuanzie hapo then wadau tutajaribu kukupa muongozo.

Mkuu Viper umepointi kitu cha muhimu sana. Hauwezi kushauri mtu bila kwanza kujua yeye alikuwa na malengo gani. Na tatizo kubwa la wanafunzi na pia mfumo wa elimu katika nchi hii ni kuwa hakuna 'career counselling' au kitu kinachofanana na hicho. Mwanafunzi anasubiri matokea na chochote kitakachotokea then atafanya hivyo-hivyo, kwa kifupi ni kuwa yeye mwenyewe na mfumo wa elimu haukumwandaa kwa ajili ya chochote.

Ndugu emoshi, wewe ulikuwa na ndoto gani? Na je, katika matokea haya unaona kama ndoto yako inawezekana? Tuanzie hapo.
 
Kweli kabisa waliotangua hapo juu wana point muhimu!social sciences au kama una msuli piga law sio mbaya sana ingawa milolongo mengi!pia usijiwekee sana kuwa hutaki kukaa mtaani hilo ni zali tu na kama una network nzuri komaaa tuu
 
mkuu hkl 1.9 bado upo kwenye competition kubwa sana... kwani kipindi umeamuwa kusoma hkl malengo yako yalikuwa nini ..? tuanzie hapo then wadau tutajaribu kukupa muongozo.
nilikuwa na ndoto za kusoma Law.
 
Kusoma ni jambo moja,kupata kazi ni jambo la pili, hakuna anayependa kukaa mtaani badala ya kufanya kazi,kwa chochote utakachokisomea kwanza mtangulize Mungu na pia kujuana siku hizi ni determining factor nyingine,kama uko poa kwa hayo waweza kwenda law ila kama hauna mtandao soma social pofessions utaweza baadae kutoka independently
 
Hiyo ya kujuana ni ukweli kabisa ingawa kuna wanaokataa. Lakini kama uko well-connected inasaidia sana, tena si kupata nafasi ya kusoma tu bali hata kazi.

It is just the nature of the beast.
 
Nakushauri ukasome education kama hutaki kuganga njaa, piga zako bed arts, utapata ajira serikalini na pia kama ukiwa mjanja, utakuwa na uwezo wa kuendelea na mastars katika issue nyingine kama dev. Studies au m.p.a

soma education mdogo wangu, kwa point ulizonazo hutapata llb katika chuo kizuri, na hizo degree nyingine kama huna baba ako au mjomba atakayekuja kukushika mkono, lazma viatu viishe soli na bahasha mkononi.
 
Hongera kwa kufaulu vizuri! Pia nakupongeza kwa kuomba kupata ushauri mapema. Wana jf wamekupa ushauri mzuri. Ni kazi yako kupima lipi zuri au baya! Wengi wamejilaumu kwa kusomea masomo ambayo walikosa kupata ushauri sahihi mapema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom