Diva: Siwezi kuingia kwenye mahusiano na mwanaume asiyejua kuongea kingereza

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,845
43,318
Wasalaam wana jamvi.
Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Diva The Bosslady amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kudate na mwanaume ambaye hajui kuongea kingereza kwa kuwa yeye katika maisha yake huongea Kiingereza zaidi kuliko Kiswahili.

Akiongea na waandishi wiki hii, Diva amedai wanaume ambao amewahi kutokana nao wanazungumza lugha hiyo ambayo amedai inamvutia sana.

"Sipendi mwanaume ambaye hajui Kiingereza, napenda kudate na mwanaume ambaye anajua Kiingereza," alisema Diva.

"Yaani imetulia na inapendeza kwa sababu siyo local local, wapo ambao waliwahi kunitokea lakini baada ya kujua hawajui kingereza nikawatosa,"

Alisema wanaume wake wengi anakutana nao kwa mara ya kwanza kupitia kipindi chake cha Ala za Roho kwa kuwa ndio sehemu ambayo atakutana na watu mbalimbali.

Mtangazaji huyo ambaye pia ni muimbaji wa muziki kwa sasa anatoka kimapenzi na muimbaji 'Heri Muziki'.
 
Its true, wanawake nao wana vigezo wavitakavyo. Though Ni ngumu sana kwa mwanamke kuamua sifa na aina ya mwanaume amtakaye. Like future husband.

Time will tell.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom