Disco la wanafunzi wa secondary

Disco la wanafunzi wa secondary

By hair

Senior Member
Joined
Sep 6, 2013
Posts
141
Reaction score
37
Si mmnajua tena mambo Yale boys kupelekwa girls kukiwa na sherehe Fulani hivi.sasa wanafunzi wa Mazengo sec kipindi hicho,wakapelekwa msalato sec,ilikuwa wanaagwa form six,ikafika mda wa disco sasa, Mara blues hili hapa,Bahati mbaya form one wa Mazengo akawa anacheza na form six wa msalato,si akajikweza eti yupo form four,story story dada akamuuliza pale kwenu mna kombi ngapi? Dogo kwa kujiamini akasema tuna kombi moja tu,ya mwalimu kafumu tena ni mbovu ipo juju ya mawe, dada mmmmmhh
 
Enzi za zamani nzuri jamani!!! Nakumbuka Moshi technical walikuja kwenye shughukli za ' Red Cross' mh walikuja wamevaa ' Raba Mtoni' na Jeans, jamani enzi zile kupata Jeans mpaka uletewe na ndugu yako kutoka nje ya nchi. Mh Wasichana wa Korogwe viroho juujuu! ( mh kumbe kuja kwenye Red Cross kulikuwa kuna lengo lingine tena) Vijana wakajieleza mpaka walimu wakakubali kuvuka mipaka nje ya Moka wa Tanga. Haooo na mabasi mpaka Moshi na walimu wetu watatu.. Sharti ilikuwa lazima kurudi shule mara baada ya mziki usiku uleule. Mh wanafunzi wamepania muziki mpaka asubuhi, Madereva wa mabasi sijui wamepelekwa wapi nia tu lazima muziki mpaka asubuhi! Walimu wakang'ang'ania mara madereva wakaibuliwa saa 2 baadae muda uliopangwa kuondoka. Hao safari kurudi Korogwe Girls Secondary school.Mhh ile miziki ilikuwa mizuri saaana, those good days!
 
Umenikumbusha pugu boys na zanaki(1997_2000) then tosa boys na iringa girls(zuu)(2001_2003) ilikua hatari tupu sikuwahi kuvaa nguo yangu mwenyewe kwenye madisco ya shule ni mwendo wa kugongea kiwalo mpaka raba(nakumbuka raba za airforce one ndo zinaingia)…siku ukikosa nguo ya kuazima na disco unapenda unavaa rafu(kisela) halafu huna shobo na demu unajifanya mgumu kumbe unaogopa ukiwasogelea lazima wakusukume km wakikuogopa wanakukwepakwepa tu mtu mzima unaona itakua soo unazuga na u_hard core…na usishangae kuona boys wote wananukia perfume moja ya kuombana!!!
 
Enzi za zamani nzuri jamani!!! Nakumbuka Moshi technical walikuja kwenye shughukli za ' Red Cross' mh walikuja wamevaa ' Raba Mtoni' na Jeans, jamani enzi zile kupata Jeans mpaka uletewe na ndugu yako kutoka nje ya nchi. Mh Wasichana wa Korogwe viroho juujuu! ( mh kumbe kuja kwenye Red Cross kulikuwa kuna lengo lingine tena) Vijana wakajieleza mpaka walimu wakakubali kuvuka mipaka nje ya Moka wa Tanga. Haooo na mabasi mpaka Moshi na walimu wetu watatu.. Sharti ilikuwa lazima kurudi shule mara baada ya mziki usiku uleule. Mh wanafunzi wamepania muziki mpaka asubuhi, Madereva wa mabasi sijui wamepelekwa wapi nia tu lazima muziki mpaka asubuhi! Walimu wakang'ang'ania mara madereva wakaibuliwa saa 2 baadae muda uliopangwa kuondoka. Hao safari kurudi Korogwe Girls Secondary school.Mhh ile miziki ilikuwa mizuri saaana, those good days!

umeongea kwa hisia sana.
 
hahahahahaaa mdau wa perfume ya kuombana umenichekesha hadi nmepaliwa bhana. aah so watu wote harufu inafanana? disco nouma sana, ila kama kuna disco lilinishngaza ni mtara girls a.k.a mangamba yani ilikuwa hakuna kufuata sijui wavvulana wa wapi wala wapi. miaka yopte niliyokaa wavulana wanatoka mtaani tu. basi wakisikia tu mjini juu kuna disco masela wote wa mjini-town hao. pesa tu inaongea kwa ticha aliye mlangoni.
ILA TULIKUWAGA NA USONGO NALO: mi nilikuwa naanza kucheza kuanzia mchana wanavyotest spika kama ziko poa
 
Ha ha ha,kumbe vituko viliendelea,katikati blues kali,form one wa Mazengo na form four wa Msalato,kumbe form one alimdanganya patna wake kuwa naye ni form four,umeme na mziki ulikatika ghafla,binti toka Msalato akahamaki kwa sauti "Whats the matter?",kwa haraka Mazengo boy akajibu "Matter is anything which occupies space and has got weight"!
 
hahahaa! umeua mkuu
 
Mazengo we noma mwaka mmoja waligoma utawala wa shule kwenda disco msalato wakawapa taarfa washikaji eti tumewachagua nyie.

Uongozi ukabania mwariko masela wakajiingiza huko mziki ulipoanza mshikaji mmoja wa bush akaanzisha timbwili mwl wa msalato kakariri Wenye zhari ni mazengo tu akampigia cm head mgohamwenda akisema ni wanafunzi wako mwingine nimemshikiria huyu hapa mshikaji mmoja akazibamba.

Haraka sana masela kukusanyana kuchango na kuita haisi kwa speed nduki mpk shule wanapita local vidume vinajigeza kitandani tu cheEa mAzEnGo weye na mguhamwenda
 
Ha ha ha,kumbe vituko viliendelea,katikati blues kali,form one wa Mazengo na form four wa Msalato,kumbe form one alimdanganya patna wake kuwa naye ni form four,umeme na mziki ulikatika ghafla,binti toka Msalato akahamaki kwa sauti "Whats the matter?",kwa haraka Mazengo boy akajibu "Matter is anything which occupies space and has got weight"!

Kaka unanifunja nbavuu yaan jamaa akaanza kudefine matter
 
Duuh...! MzuKila...unankumbsha mbal xana enz hzo uzumbeni 2na head aitwae MWASHA mzee wa nyayo,ila tatzo mzumbe girls(kilakala) mlikuwa mnajkweza xana had kupelekea wadogo ze2 waliobak walivnja u1 na kuunda MzuMoro,lakn mlikuwa mna2pa kampan xana bonanza.
 
Back
Top Bottom