SoC02 Uhalisia wa maisha ya chuo; Madhara kwa yule atayekuta utofauti na kile alichotarajia

Stories of Change - 2022 Competition
Jul 19, 2022
48
47
Kwanza nipende kuwapongeza wanafunzi wote mliofaulu katika masomo yenu ya Advanced level yaani kidato cha sita na hivyo mnatarajia kujiunga na masomo ya Elimu ya juu (Chuo kikuu). Niliona kuna clip fupi mitandaoni hasa kwenye account (Kurasa) za instagram za vyuo tofauti zinazoendeshwa na Wanafunzi wenyewe zikionesha Furaha kubwa waliokuwa nayo Wanafunzi wa shule ya secondary, haifahamiki ni shule gani baada ya Kumaliza Kidato cha Sita ( Form six) wakiwa wanaimba maneno haya “jamani twedeni , jamani twendeni na kiitikio CHUO, kuna BOOM la bure, Kuna internet ya bure, kuna wadada wazurii, Kuna mabonanza Chuo” Wakishangilia kwa furaha kubwa kuyakaribia maisha ya chuo Hii inamaanisha kua wao wanataraji kukuta maisha mazuri sana wakifika chuo.

Muda mwingine unatamani uwajibu pale pale ilimradi ukweli na uhalisia wa kile wanacho kiimba waufahamu, lakini ndo huwezi wapata kwa wakati huo

Sasa napenda kushiriki nanyi kuelezea uhalisia wa maisha ya chuo, hii kwa hapa Tanzania maisha ya Vyuo vingi yanafanana Japo kuna tofauti lakini sio sana maisha ya chuo ndio yaleyale, Ewe mwanafunzi unae Tarajia kusoma Elimu ya chuo kikuu na Ewe Mzazi unae tarajia kusomesha chuo kikuu.

Huko Chuo kikuu ni muendelezo wa Taaluma yako amabayo umepanga kuisomea, lakini pia tukiwa mtaani tunaambiana chuo ndipo mahali pazuri unaweza pata watu watakao kusaidia kimaisha yaani connection, Hii ni kweli lakini inategemeana na marafiki ulio nao na ucheshi wako chuoni wengine huenda chuo kusoma tu na sio kujihusisha kwenye shughuli zingine zozote kama kushiriki kwenye Siasa, midaharo na matamasha mbalimbali, Semina vyuoni na shughuli zingine zinazo weza kufanyika chuoni bila kuathiri Usomaji wako hizi ndizo zitakukutanisha wa watu tofauti hivyo kukupushi kwa lolote.

Ni kweli tunapokua mtaani na story nyingi tunazo sikia kuhusu wanachuo na maisha yao tunaamini kabisa kule chuoni ni Kusoma kidogo afu kula bata sana, hii nakubali hufanyika kwa wachache sana na itategemea unasoma course/ taaluma gani na una mpango gani na GPA yako, Kwa wengi nilio washuhudia wanapata GPA ndogo na wengina wanafeli (DISCO) Mfumo unawakataa hivyo wanashindwa kuendelea na masomo hii haimuathiri mwanafunzi huyo pekeyake kuna wazazi wake na wengine wengi waliokua wanategemea kuona matunda yake.

Vijana wengi wanao tarajia kujiunga na Elimu hii ya Chuo kikuu huamini saana katika stori hizo zilizopo kuhusu maisha ya chuo HAPANA, Uhalisia wa maisha na stori ni tofauti wengi wanafika na stori hizo za mtaani chuo wanapotea, Chuoni kusoma sana kupo tena kosa moja linakufanya uondolewe chuo,

Utofauti mkubwa uliopo kati ya Elimu ya juu na hizi za secondary na msingi ni-:

UHURU KWA MWANAFUNZI. Huko Chuoni hakuna yeyote atakae kukumbusha kusoma, ukifeli Test hakuna atae kuchapa kwa kufeli kwako lakini kwenye mfumo wa matokeo Vyuo baadhi hutumia hizi ARIS, SR2 na zinginezo kuangalia matokeo uko ndipo utakuta Adhabu yako na siyo ya kubeba kifusi, kupasua kuni, kufyeka HAPANA ni wewe na utakacho andikiwa pale kwenye Mfumo.

Chuoni pia huwezi pangiwa ratiba zako binafsi, watapanga ratiba ya masomo na ile ya kufanya mitihani sio vinginevyo na hakuna atae kulazimisha kuingia darasani hii nikwasababu chuoni wanaamini kila mtu anajielewa na anajua nini anafanya.

KUPATA PESA ZA MALAZI NA CHAKULA ( BOOM), Huu ni Mkopo unaopewa na Serikali nah ii sio pesa ya bure kama wengi wanavyo sema ukipata Ajira pesa hii utakua unakatwa kidogo kidogo mpaka inakamilika uliyo kopeshwa wakati unasoma, Mkopo huu unasaidia sana wanafunzi wengi chuoni kwani bila hii pesa wengi, tusinge pata nafasi ya kusoma Elimu hii, Sasa changamoto na pesa hii ni kwamba pesa unapewa lakini mwanafunzi anaona ndio pesa ya kuhonga watoto wa kike, kwendea bar na kufanya starehe nyingi ambazo hakuzifanya kabla hii yote ni sababu alisikia “chuo Bata bana “ ko ndo bata lenyewe HAPANA.

Kwa wanafunzi wanao kaa nje ya chuo na wanao tambua kilicho wapeleka chuo pesa hii hutumia kulipia kodi, kununua vyakula na kufanya huduma za stationary kwa ajili ya kujisomea na sio vinginevyo na ndio lengo kubwa la pesa hii na kwa wale wanao ishi Hostel za chuoni pesa hii Hutumia kununua chakula na kuweka bill ya chakula katika cafeteria zilizopo karibu na chuo na kufanya matumizi mengine ya msingi.

Kuna upande wa pili ule wa dada zetu (girls), Kafika chuo mdada alikua hasuki nywele za gharama kubwa Zaidi ya elfu Hamsini, Alikua hana kucha za bandia, alikua hajui skert fupi na fashion mbalimbali, Basi pesa hiyo ataitumia kuhakikisha vyote hivi anafanya ili nayeye aonekane Kwa kizazi chetu cha sasa kuna baadhi ya vitu sawa tutakubali lakin angalia na nyumbani kupo vipi.

MADHARA YA KUTO KUKUBALI UHALISIA WA MAISHA YA CHUO.
Madhara yapo mengi kwa yule ataekuta utofauti na kile alichokitarajia chuo, na akashindwa kuukubali uhalisia huo na kuishi nao, Inapendeza sana kukubali ukweli na kuona kama upande ulipokuwa ulikuwa sio sahihi, matokeo ya kutokukubali ni kama-:

Kufeli masomo yako, (DSCO) Hii inaweza kutokea mapeema sana hasa ukiwa ndio bado upo Mwaka wa kwanza wa masomo, kwa sasa vyuo vingi wana mfumo wa under 16 bila kufikisha course work hii huto ingia kufanya Universty Examinatio ( UE), mtihani wa mwisho wa semester, ko hii inahitaji mwanfunzi asome vizri na sio kujihusisha na starehe nyingi kama mawazo ya wengi.

Kupata GPA ndogo, Kwa mfumo wa Ajira katika nchi yetu wanaangalia cheti chako kipo vipi na hasa wenye ufaulu mkubwa ndio wanapata nafasi nzuri ukilinganisha na wenye ufaulu mdogo na kuna baadhi ya vyuo kusoma degree ya pili yaan MASTERS wataangalia GPA pia ko ni muhimu kua na ufaulu mkubwa hii itahitaji utulie na usome.

HITIMISHO. Huu ndio uhalisia wa maisha ya chuo na hakijaongelewa kila kitu hapo ni baadhi tu ya mambo ya msingi kujua lakin sio kuwatisha kuona chuo ni shule ngumu pia hapana unaweza panga ratiba zako vizuri na kila kitu kikawa sawa.

Imeandaliwa nami. chades
 
Umesema kweli washindwe wenyewe
 
Back
Top Bottom