Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,660
- 46,350
Serikali iko katika mpango wa kuandaa dira au mpango wa maendeleo wa miaka 25 ijayo kwa nchi hii(2025-2050). Jambo hili halina tija kwa sababu nyi sana na hizi na baadhi tu.
1. Mipango ya muda mrefu hivi tumeiga kutoka nchi za kijamaa na Kikomunisti za Asia. Hata hivyo hiko ilifanikiwa katika nchi za kijamaa huko kwa sababu ya "controlled economy", Serikali ilikuwa ndiye mdhibiti mkuu wa uchumi ikipanga kila kitu. Sasa hivi tuko katika uchumi wa kibepari.
2. Hatuna uwezo mzuri wa kutabiri muda mrefu hivyo, hatuna nyenzo za kujua nchi yetu itakabiliwa na mambo gani makubwa miaka 25 ijayo.
3. Sisi bado ni taifa Masikini ambalo tunategema mikopo na misaada kwa kiwango kikubwa. Ni vigumu kupanga miaka 25 ijayo ikiwa hujui hata pesa za kutekeleza hiyo mipango itakuja.
4. Watawala wakuu wanaobadilika huwa hawazingatii au hawabanwi kutimiza mipango hii ya muda mrefu. Kila mmoja huwa anakuja na vipaumbele vyake tofauti na mwenzake aliyemtangulia.
5. Mipango ya muda mfupi ndio mizuri kuhakikisha uwajibikaji unakuwa mkubwa kuliko hiyo ya muda mrefu.
Hivyo basi tujikite katika mipango ya miaka mitano kwa sababu ndio yenye uhalisia zaidi kwa taifa letu.