Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 (Tanzania Development Vision 2025)...

Kwa matanuzi yenu ya Serikali yalivyo makubwa yaliyojaa anasa, kwa ukubwa huu wa Wizara na Idara, Kwa ufisadi huu - aisee hiyo ni ndoto ya mchana; wadanganyeni watu wa Iramba!!
 
2025 mbona mbali? Lakni uzembe kazini au kufanya kazi kwa kiundugu undugu hatufiki popote watakao pata maendeleo ni watu wachache na sio taifa zima.
"Miaka 100 ijayo Tanzania itakua nchi iliyoendelea zaid ya zile zilizoendelea".Shemeji akiwahutubia vijana pale 7/7 mwaka huu,sasa unashangaa hapo 2025 si ndo dira ya taifa inavyosema?tujiulize huo mpango wa taifa wa miaka mitano unatekelezwa?wananchi wanaujua?wameupitia?,kwanza zipo doc 2 sijui ipi inatekelezwa
 
Ayaaa shemeji noma anaongelea maendeleo ya kitukuu atakapo kuwa mkubwa. Sasa hapo kila awamu ya uongozi, kiongozi ahakikishe anakuwa tajiri kuliko matajiri wote waliotangulia hadi miaka mia ipite ndo tulifikilie taifa.
 
yeye asema tutaipeleka tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati 2015-2025.
Naibu waziri wa fedha aliyetokea kugusa mioyo ya watanzania masikini na kufufua matumaini yao ndg mwigulu nchemba juzi alikonga nyoyo za wananchi wa tabora waliofurika igunga kumsikiliza. Mwigulu aliyekuwa akishangiliwa kila alipofafanua hoja aliwaacha wanaigunga wakibaki makundi makundi mpaka giza lilipoingia wangali viwanja vya sokoine kutafakari hotuba yake iliyokuwa na sura ya kiongozi wa taifa.

Katika hotuba yake mwigulu alirudiarudia neno "tutaipeleka tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo 2025" na kushangiliwa kwa kishindo.

Mwigulu alibainisha kuwa mambo ya msingi kufikia hatua hiyo kuwa ni

1) maadili na uzalendo wa wasimamizi wa rasilimali za taifa. Mwigulu alisema wanahakikisha kwamba kila fedha inakwenda kutoa huduma iliyokusudiwa, tunahakikisha kodi za wananchi zinakwenda zilipokusudiwa. Tukikusanya fedha kwa ajili ya umeme, tunasimamia iende kwenye umeme, tukikusanya fedha ya barabara tunahakikisha zinakwenda kwenye barabara, hivyohivyo kwenye afya, elimu nk. Mwaka jana tumegundua tulitoa zaidi ya 48bil kwa ajili ya dawa mawilayan lakkni ni 7bil zilitumika kununua dawa huku kila mgonjwa akienda hospital anahundulika na homa na kuambiwa kanunue dawa kiosk kile, huu ni wizi, kiosk kinatoa wapi dawa ambazo serikali haiwezi kupata kama sio kufanyia biashara dawa zilizonunuliwa kwa kodi za watanzania. Naagiza hili likome na hatua zitachukuliwa, madiwan na vyombo vya dola simamien hili. "tutaipeleka tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati"

2) kuachana na kufanya kazi kwa mazoea.

Mabadiliko ni vitendo na yanaonekana kwa kubadili style ya kufanya kazi ili kulinda fedha za umma. Timebadili ulipaji wa mishahara kipambana na mishahara hewa. Tumebaini zaidi ya wafanyakazi elfu kumi na nne (14,000) walioyeyuka tjlipoomba akaunt zao na 1,900 wa keshi nao wameondolewa kwenye malipo. Tumeokoa zaidi ya bilion 40. Naagiza maofisa wote wahakiki watimishi waliopo kazini na walete akaunt. Tukibaini makosa yule aliezembea atafute kazi ya kufanya na hatua zitachukuliwa. Mpk sasa waliozembea tumewapeleka polisi na takukuru wafikishwe mahakamani.

Tumekagua madai tukagundua udanganyifu, kwenye bilion 500 tumegundua halali ni bilion m100 tu, tumeokoa bilion 400 na tumewapeleka polisi wote waliodanganya. Naagiza wakaguzi watimize wajibu wao kabla ya kuleta madai wizani kwangu. Wakileta tutskagua, tukigundua udanganyifu aliyeleta hiyo atafute kazi nyingine ya kufanya na tutamburuza mahakamani. "tutaipeleka tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati"

3) tutapunguza pengo kati ya walionacho na wasionacho kwa kutekeleza vyema sera za kodi.

Tutawatoza kodi matajiri ili fedha hizo tuwasomeshe watoto wa masikini. Tutatoza kodi matajiri ili fedha hizo tupeleke huduma za maji, madawa, umeme na barabara vijijini. Hatuwezi kuwasamehe kodi matajiri mabilioni ya shilingi, wakwepe mabilioni ya shilingi halafu sisi tukimbizane na wajane wanauza matembere kulipa ada elfu 20 mashuleni. Tumefuta misamaha kwa matajiri tuache kuwssumbua wajane na masikini kutafuta elfu 20 za sekondari. "tutaipeleka tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati"

4) tutasimamia mgawanyo wa rasilimali ili keki ya taifa iwanufaishe watanzania wote kwa usawa.

Tumebana matumizi ya serikali yasio ya lazima ili fedha hizo ziende kwenye miradi ya maendeleo. Tutahakiki bajeti za kila taasisi ya umma na kufuta matumizi ya anasa. Hatuwezi kuwa na shirika la umma linatumia fedha kwa anasa huku watoto wakikaa chini. Kupewa kuvuna rasilimali za umma ni dhamana tu sio shamba binafsi na mashirika na taasisi zote za umma mnaokusanya fedha tokea rasilimali za taifa mlielewe hili. Hatuwezi kuwa na watanzania hapa wanaishi tanzania na wengine wakiishi kama ulaya wakiwa hapahapa kisa wamepewa dhamana ya kusimamia shirika la umma. "tutaipeleka tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati"

5) tutatoza kodi kwa matajiri, tuwapinguzie kodi walimu na wafanyakazi wengine, tutatoza kodi tuziwezeshe sekta zinazotoa maisha kwa watanzania wengi ili kuondoa uhusiano wa kukua kwa uchumi huku umasikini nao ukikua.

Tukiwedha fedha kwenye sekta zinazolisha na kuendesha maisha ya watu wengi tutakuza uchumi huku umasikini wa watu wa chini ukipungua.

6) kuna watu walinunua viwanda vyetu, wamelipa, wamewekeza, wameendeleza, wametengeneza ajira, wameheshimu mikataba, wanalipa kodi nawapongeza sana. Lakini nimeangalia kumbukumbu kwenye mafaili kuna watu walinunua viwanda, hawajawekeza, hawajaviendeleza, wamegeuza viwanda kuwa magodauni, wameuza vyuma chakavu, wamepeperusha ajira, wameua mazao ya wakulima kwa kuua viwanda vya nguo, wameua mazao ya mifugo kwa kuua viwanda vya ngozi, viatu, hawajaheshimu mikataba, hawajalipa serikalini, wametajirika kwa kuchukua mali ya umma. Nawambia wakaangalie upya mikataba inasemaje, vinginevyo wajiandae kisaikolojia.video inakuji soon

why mambo yote ya ahadi as if na yeye ni chama pinzani akiomba kura?
Atahakikisha lini and not now?
Apiga kampeni ya uchaguz sahivi nini!
 
why mambo yote ya ahadi as if na yeye ni chama pinzani akiomba kura?
Atahakikisha lini and not now?
Apiga kampeni ya uchaguz sahivi nini!

Tumechoka na maneno tumewapa kura miaka 50 bado ndio tunaendea nyuma kutoka na jinsi rasilimali zinavyovunwa sasa hivi
 
Ayaaa shemeji noma anaongelea maendeleo ya kitukuu atakapo kuwa mkubwa. Sasa hapo kila awamu ya uongozi, kiongozi ahakikishe anakuwa tajiri kuliko matajiri wote waliotangulia hadi miaka mia ipite ndo tulifikilie taifa.
Kwanza wanaoutaka uongoz hasa urais wanapaswa kuhakikisha kwamba wanaitekeleza hii mipango ya maendeleo,nna shaka kuna docs zitatupwa,mfano BRN kuna watu wakija wanakuja na zao,ila kulikua na MTWARA CORRIDOR leo haitajw tena,watu wamekuja na SAGCOT si mbaya ila where is MTWARA CORRIDOR?.Utajiri ni kweli,watawala wetu wanaingia maskin ila wanatoka matajiri sana,hili wala halifichiki,iko wapi sheria ya kutenganisha biashara na siasa?hata wapinzani hawaiulizii kwakua nao ni wafanya biashara
 
Nchi hii inasheria lakni inaongozwa kisiasa siasa, mfano fundi ujenzi umpe tenda ya kukujengea nyumba vifaa vyote umpe halafu mwisho wa siku fundi auze simenti yote, na wewe umwambie fundi nimekusamehe endelea na ujenzi unadhani atajenga vipi bila simenti.

"Tumewasamehe misamaha ya kodi" kesho utasikia taifa linadaiwa mabilioni, sasa mnataka azilipe nani?.
 
Kwanza huyo mjinga kwani habari ya babayake ya maisha bora kila mtanzania yameishia wapi?
 
Hii nchi ina utajir gan mpaka ianze kuwasamehe matajiri kulipa kodi?
 
Kwanza huyo mjinga kwani habari ya babayake ya maisha bora kila mtanzania yameishia wapi?
"Tuliposema Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania,hatukumaanisha Kuwajaza mapesa mfukoni,bali kuwajengea miradi ya kimaendeleo kama vile barabara,umeme,maji ili vikuwezeshe kujiletea maendeleo".SHEMEJI Mbinga ALIPOKUA AKIZINDUA BARABARA YA LAMI YA MBINGA-SONGEA.
Baada ya takriban miaka 9 ndo anaifafanua kauli mbiu yake,pole kwa waliokua wakitafsiri tofaut,hao ndo wanasiasa
 
Last edited by a moderator:
Kwanza huyo mjinga kwani habari ya babayake ya maisha bora kila mtanzania yameishia wapi?

Maisha bora kwa kila mtanzania huku mtaani mahitaji mhimu yamepanda bei sababu ya kodi, hospitalini dawa hakuna, harafu bei ya mazao ya biashara yameshuka bei. aseme maisha bora kwa kila alienacho.

Kilimo kwanza huku unamnyonya mkulima kwa kushusha bei ya mazao na kupandisha bei ya bidhaa unategemea maisha bora yatatoka wapi? Tushukuru kuwepo nguo za mitumba la sivyo wa kutembea uchi tungekuwa wengi na ukilinganisha bei ya pamba mwaka huu ilikuwa kati ya 800 hadi 1000.
 
"Tuliposema Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania,hatukumaanisha Kuwajaza mapesa mfukoni,bali kuwajengea miradi ya kimaendeleo kama vile barabara,umeme,maji ili vikuwezeshe kujiletea maendeleo".SHEMEJI Mbinga ALIPOKUA AKIZINDUA BARABARA YA LAMI YA MBINGA-SONGEA.
Baada ya takriban miaka 9 ndo anaifafanua kauli mbiu yake,pole kwa waliokua wakitafsiri tofaut,hao ndo wanasiasa

Barabara, maji, umeme na vinginevyo ni kodi za wananchi sio hela ya mtu mmoja au chama. Kinachofanya watu waongee ni usimamizi na matumizi ya kodi zetu, unatoa kwa masikini unapeleka kwa matajili. Wamepandisha bei ya umeme ikawa haitoshi wakaongeza service charge ya umeme na maji. Hapo naona hajatatua tatizo bali ameongeza.
 
Umeme bado ni anasa,maji bado ni anasa kwa mijini na vijijini,licha ya kwamba ni ghali bado hayapatikan,huwa natembelea vijijin watu wana shida sana ya maji,kwa mfano makao makuu ya wilaya ya Kilombero,Ifakara,mji umezungukwa na mito mikubwa ila dumu la maji ni 500-1000/=,kuna mto Lumemo na mto KILOMBERO,sasa nashangaa mji wenye mito una shida ya maji?.Nimegundua kuwa wanasiasa wanategea kutatua matataizo wapate nafas ya kupatia Kura
 
Sisi watanzania tuna elimu ya viwango tofauti lakni kuwepo kwa elimu hiyo hatuna elimu ya utawala bora. Leo hii ukiwaambia wananchi wenye shida ya maji, umeme na miundo mbinu wamuulize kiongozi wao maswali, hakika wengi watatoa pongezi.

Mgombea akisimama jukwaani anajinadi nitawajengea barabara, maji nitawaletea na umeme mtapata. Hakuna wa kumuuliza utafanya hayo yote kwa pesa yako au ya wananchi? Hakuna wa kumuuliza kuwa atatumia mbinu gani kupunguza ukali wa maisha japo kidogo, tunatoa kodi kubwa je, inamalengo yapi kwa taifa?
 
Back
Top Bottom