Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,752
- 7,850
95. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha awamu ya tatu tumeweza kupata mafanikio mengi katika kukuza uchumi wetu. Hata hivyo, ili kuweza kufikia malengo ya Dira ya Taifa 2025, na kuweza kulingana na nchi zenye kipato cha kati, uchumi wa nchi unatakiwa kukua kwa kiwango kisichopungua asilimia 8 juu ya kiwango cha ongezeko la idadi ya watu. Kiwango cha ongezeko la idadi ya watu kinakua kwa asilimia 2.9. Hivyo hatuna budi kuboresha na kuendelea kusimamia utekelezaji wa Sera na mikakati yetu ili tuweze kufikia malengo makuu ya Dira ya Taifa 2025, kama ilivyokusudiwa.
96. Mheshimiwa Spika, napenda kuelezea kuwa tegemeo kubwa la kuleta mabadiliko ya kiuchumi nchini liko kwa wananchi wenyewe ambao wanatakiwa kutumia fursa zilizopo na kukabili vikwazo kwa lengo la kuongeza tija kwa kasi kubwa na kukuza uchumi wetu ili tuondokane na umasikini tulio nao. Hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kuchukia umasikini na kuhimizana kufanya kazi kwa bidii na kutumia kwa umakini, fursa na rasilimali zilizo katika uwezo wetu ili kujiletea maendeleo. Serikali itaendelea na jukumu la kuunga mkono juhudi za wananchi kwa kuandaa sera na mikakati ya kuelekeza namna ya kuratibu, kusimamia pamoja na kutathmini ili tuwe na maendeleo yenye kuwiana katika kila ngazi. Nina hakika kuwa kila mmoja wetu akitimiza wajibu wake sawasawa tutakuwa na kasi ya ukuaji wa uchumi unaopanda mwaka hadi mwaka na kufikia malengo yetu ya Dira ya taifa 2025, na kufanikisha kupunguza umasikini kwa kiwango kikubwa. Hakika, Serikali ya Awamu ya Nne, itayalinda na itayaendeleza mafanikio ya Awamu ya Tatu kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya.
ili kukabiliana na Kiwango cha ongezeko la idadi ya watu kinachokua kwa asilimia 2.9 ili uchumi wa nchi uweze kukua kwa kiwango kisichopungua asilimia 8.
1. Wagonjwa wa UKIMWI wasipewe dawa za kurefusha maisha ili kuondoa mzigo kwa taifa, nalo kuwa fundisho tosha kwa wapenda ngono wajigharamie wenyewe matibabu.
2. Kila familia mwisho (kuzaa) watoto wanne. Watoto wawili wa kwanza (Bonus yao) wasomeshwe bure mpaka chuo kikuu.
3. Ruksa kuoa, au kuolewa kwa mujibu wa itikadi za dini yako, lakini wembe ni huo huo, hakuna kuzaa zaidi ya watoto wanne!!!
4. Ili kukabiliana na idadi ya wahamiaji 'haramu' nchini, kila mmoja wao atalazimika kulipia 100% ya huduma za jamii anazostahiki Raia, mfano hospitali, shule, vyuo, nk
5. Ili kudhibiti tatizo la familia za Omba omba ambao kuzaana kwao ni ajira ya pili, serikali kwa kushirikiana na ustawi wa jamii iwanyang'anye watoto hao, kisha wapelekwe kwenye vituo maalumu ambavyo vitakuwa vinawatayarisha kielimu ili hao watoto/vijana kuwa taifa bora la kesho bila kutegemea fedha za 'wahisani'.
wajemeni, mtaoniona 'mkatili' huu ni mgongano wa mawazo tu... nauchukia mno umaskini wetu wa kujitakia!
2025 ni miaka kumi na nane tu ijayo hapo mbele
ENGLISH VERSION
SWAHILI VERSION