Bado nawaza na kujiuliza maswali mengi sana,ivi hii sio njia moja wapo ya serikali kunyima watu haki ya habari kijanja? Namaanisha serikali hii iliyo madarakani.
Inawezekana sana kua serikalii hii imepoteza sana umaarufu kutokana na uwazi huu wa habari,na imesalia miaka miwili mpaka uchaguzi mwingine.Miaka hii miwili inaweza kuwafumba watu macho na wasijue kinachoendelea na madudu yanayofanywa na serikali husika(kukosa haki ya habari),Au ni mdau kaja kibiashara zaidi kwa maslahi yake binafsi? Mpaka ifike 2015 mshapumbazwa sana maana watu wa hali ya chini ni wengi,ving'amuzi wataviwezea wapi maskini ya MUNGU.
Kwa tathimini ya India walivyo introduce hiyo system waliakikisha kua ving'amuzi were affordable to every citizen,kwamfano kuunganisha kuna za 20,000/- hadi 30,000/- inategemea na provider ni yupi, na malipo kwa mwezi ni Tsh.3000/-. Hapo unaweza ona difference ni kubwa sana na hapa kwetu Tanzania. Je kuna nini nyuma ya pazia?maana kama ni kuleta maendeleo lazima yawe maendeleo ambayo kila mtanzania atafaidika nayo(it should be cheap/ affordable). Vijijini kwa wazee wetu wataweza kweli kulipia?wakati walikua wanaunga tuu antena nakuweza kukamata channels japo kwa chenga chenga ila wanaona.
KUNA ULAKINI, BADO NAWAZA