Did they exist: Viumbe wenye utata kwenye BIBLIA

Nimekuelewa sana mkuu hili nafikiri ndio jibu sahihi la uzi huu ingawa cha kujiuliza mbona biblia inasema WALIUMBWA na MUNGU wakiwa na mfumo huo huo?? Mfano Leviathan na Behemoth maneno ya Mungu mwenyewe zaburi na Ayoub wanamnukuu akisema ALIWAUMBA je ina maana baada ya kuwaumba ndipo wakavamiwa na hao malaika huko baadae?

Pia ikiwa waliingiliwa na malaika wabaya ndio wakabadilika hivyo tunaona kibiblia hao wanefili waliangamizwa kwenye gharika ila cha kujiuliza hao wanyama wenye damu ya kimalaika waliwezaje kurudi kipindi cha kina nabii isaya au ina maana malaika wengine walikuja tena kuwavamia wanyama

Pia swali la mwisho unisadie je unafikiri nni kimewatoesha kiasi sahivi hawapo duniani tena??

Ubarikiwe

Cc mitale na midimu Mnabuduhe mpite huku wakuu
sorry I was driving, nitajaribu kukuelezea kwa kadri ya upeo wa fikra zangu.
Kuna kitu kinaitwa bloodlines ,hiki kitu ni chepesi kutamka lakini kukiongelea ni kigumu. Kuna mada alizitoa mshana jr zinazohusu viwakilishi katika ulimwengu wa roho. Halafu Kuna mada ilitupiwa humu nikaipitia inahusisha mambo ya uumbaji. sasa kwa fikra zangu : mungu aliumba dunia na vyote kwa ( free will) ina maana aliumba hakutaka kiumbe chochote kisimfahamu, kwa hiyo aliwapa uhuru. note : from the beginning....
Tunapoongelea hawa wanyama nimeandika kwamba wale malaika waasi walikua wanawaingilia mpaka wanyama pamoja na binadamu. na issue nyingine ni kwamba sayansi inathibitisha kwamba maandiko ya dini yako sahihi.
Cpl

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LEVIATHANS
The Leviathan ni kiumbe mwingine mwenye utata anayetajwa kwenye biblia ya kiebrania baadhi ya vifungu hivi Ayubu 3:8, Ayubu 40:15–41:26, Amos 9:3, zaburi 74:13–23, zaburi 104:26 and Isaya 27:1.
View attachment 836027

Leviathan ni kiumbe aliyetajwa kwenye Biblia kama kiumbe wa kutisha ambaye alikuwa tishio na hana mpinzani baharini sura nzima ya Ayubu 41 inamsifia kiumbe huyu kwamba ana ngozi ngumu kama chuma,anatema cheche na moto mdomoni nisitie chumvi Isaya mwenyewe anasema

Isaya 41
27 Yeye huona chuma kuwa kama nyasi,Na shaba kama mti uliooza.
28 Mshale hauwezi kumkimbiza;Na mawe ya teo kwake hugeuka kuwa kama makapi.
29 Marungu huhesabiwa kama mabua;Naye hucheka mshindo wa mkuki ukitupwa.
30 Pande zake za chini ni kama vigae vikali;Hutandika malazi kama kuweka chombo cha kupuria nafaka juu ya matope.
31 Yeye huchemsha kilindi mfano wa nyungu;Hufanya bahari kuwa kama mafuta.
32 Hufanya mapito yake kung?aa nyuma yakeHata mtu angedhani kilindi kina mvi.
33 Juu ya nchi hapana aliyefanana naye,Aliyeumbwa pasipo oga


Kuna hoja nilikutana nayo kwa mkuu GuDume kwamba lugha iliyotumika ni ya picha jambo ambalo nakubali lakini majibu yote tunayapata zaburi kwamba ni mnyama na aliumbwa na Mungu.

Zaburi 104:26
26 Ndimo zipitamo merikebu,Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo.
View attachment 836028

However kuna hoja za waandishi wa kiebrania kwamba mnyama huyu anaweza kuwa mamba wa mto nile ambaye alikuwa ana urefu mpaka wa mita 20 ingawa sifa ya kutema moto hakuwahi kuwa nayo!!! Na baadhi ya wanatheolojia wanadai mnyama huyu alikuwepo wakati wa chaos yani kipindi dunia haijaumbwa yaani baada ya vita ya malaika na shetani ndipo viumbe hawa waliishi na baada ya dunia kuumbwa na wanadai waliuawa na Mungu kwa kurejea Zaburi 74:13 kwa kupasuliwa vichwa na tukio hili linatazamiwa kutokea kwenye mwanzo 1:2 ambapo Roho wa Mungu alikuwa juu ya maji ikitazamiwa ndipo alipoenda kummaliza huyu lewiathani.

BEHEMOTH
View attachment 836030

Huyu kiumbe anatajwa kwenye biblia kama mnyama asiye na mpinzani ardhini na kwamba alikuwa na nguvu sana na kutikisa mwituni na aliogopeka sana. Kwa sasa anaweza fananishwa na tembo au kiboko ingawa huyu Biblia inaeleza urefu wako unalingana na mti wa mwerezi na sifa hizi zote zinatajwa kwenye Ayubu 40 ambapo sura hii nzima imetolewa kumwagia sifa mnyama huyu ili kuonyesha ukuu wa Mungu. Pia hapa haijatumika lugha ya picha pekee bali uhalisia maana Mungu anasema

Ayubu 40:15
15 Mwangalie huyo kiboko (behemoth), niliyemwumba pamoja nawe.....

Baadhi ya sifa zake
17 Yeye hutikisa mkia wake mfano wa mwerezi;Mishipa ya mapaja yake yanaungamana pamoja.
18 Mifupa yake ni kama mirija ya shaba;Mbavu zake ni kama vipande vya chuma
View attachment 836031


Wanatheolojia wanadai anaweza kuwa Dinosaur kama huyu hapa chini ambao kisayansi ushahidi wa uwepo wao unathibitishwa ila wengine wanadai ni tembo au kiboko wa kizamani ambao walikuwa wakubwa sana na waliogopeka mno maana walikuwa hawana mpinzani fikiria ukutane na mnyama kama simba mwenye size ya Tembo!!
View attachment 836032

HITIMISHO
Wanyama hawa niliowataja wengi wao hawana ushahidi wa kisayansi kuwa walikuwepo inanifanya nije na maswali yafuatayo

1. je wanyama hawa waliwahi kuwepo au ni hekaya tu za wazungu.??
2. Wanyama hawa walitoweka wapi na kama bado wapo wanaishi wapi??
3. Je walitoweka je lini na kwanini???


Naomba kuwasilisha wanajukwaa
kama viumbe vinavozaliana kikawaida, ilikuwaje kuwaje mpaka wakafa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama viumbe vinavozaliana kikawaida, ilikuwaje kuwaje mpaka wakafa

Sent using Jamii Forums mobile app
Cjui kwa wanyama wengine ila biblia inaeleza tu jinsi leviathan walivyokufa ya kwamba Mungu alipasua vichwa vyao hivyo akatowesha kizazi chao ila hao wanyama wengine kma cokcatrice na behemoth sifahamu walikufaje maana hakuna rekodi ya kisayansi au kiacholojia juu ya uwepo wao ili tuweze kutambua life span yao na hapo ndipo changamoto inaanza kwamba kama walikuwepo kwanni hakuna rekodi yao kisayansi??

Kuna viumbe wengi tu wametoweka ila huwa wanafahamika baada ya mifupa yao kugunduliwa lakini sifahamu kwanni hawa wanyama wa ajabu mifupa yao haipatikani mpaka leo ili yaweze kuthibitisha uwepo wao
 
UTANGULIZI
Habari za jioni wana jukwaa pendwa kufuatia maoni kwenye huu uzi
Wafahamu viumbe watatu wa kutisha wa baharini - JamiiForums kuna baadhi ya watu walinitaka niandae uzi maalum ili niweze kuelezea viumbe hivi vyenye utata kidogo kwenye Biblia. kama kawaida natoa rai uzi huu ni kwa minajili ya kujifunza tu na kujadiliana ili tuweze kuongeza maarifa ila sio uwanja wa mabishano ya kidini so sitegemei kejeli,matusi dhidi ya dini za watu wala vitabu vya dini ya yeyote.

NB: uzi huu nimeugawa katika post mbili ili iwe rahisi kusomeka na isichoshe msomaji

Kwa kusema hayo sasa tunaweza kuendelea.

UNICORN
View attachment 836013
Neno hili limetokana na neno re'em kiebrania na kigiriki MONOC’EROS ambalo kwa hapo nyuma ilifahamika kama farasi mkubwa sana mwenye pembe moja ya mbele ambaye anatazamiwa kuwa na nguvu sana kuliko wanyama wengi. Anazungumziwa kwenye Hesabu 23:22 na 24:8, ambapo Biblia inafananisha nguvu za Mungu kama nguvu za Unicorn hapa duniani.

Pia kumb. La torati 33:17, zaburi 22: 21 na 92:10 yanaongelea pembe la huyo unicorn ilivyo na nguvu.

Pia Ayubu 9:10 na 39:10 zote zinaongelea jinsi ilivyo ngumu kumkamata mnyama huyu.

Kuna wengine watasema kwamba tunasoma biblia kama gazeti ila hapa biblia iko wazi kabisa kupitia Isaya 34:17 kuwa Unicorn alikuwa mnyama na imemuweka hapa kundi moja na wanyama wengine kama ng'ombe hivyo sio lugha ya picha kabisa.
View attachment 835982
Ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi wa farasi wenye pembe yaani unicorns ila kuna vifaru wa huko siberia,Urusi ambao kisayansi wanatajwa kuwahi kuwepo hapa duniani hivyo kuna baadhi wanasema huenda ndio unicorns walioongelewa kwenye Biblia!!

DRAGONS
View attachment 835976

Dragons wameongelewa kwenye Isaya 43:20,34:14 na Micah 1:8 kama mnyama mkali ,hatari na anayenguruma huko porini. Pia isaya 91:13 na 27:1 pia zinamzungumzia kama kiumbe anayetawala na baharini pia kwa utisho mkubwa. Kiebrania jina lililotumika ni Tannin likimaanisha mnyama wa jamii kama joka ila lina miguu na mabawa. Kuna watu pia wanaweza sema ni lugha ya picha ila Isaya 13:21-22 inataja kikundi cha wanyama ambao mpaka leo wapo na mmoja anayetajwa ni Dragon hivyo sitegemei hoja hii itumike, ila swali ni je mnyama huyu amewahi kuwepo duniani na kama ametoweka nini kilisababisha??

COCKATRICE
View attachment 835985

Ni mnyama jamii ya nyoka ila ana kiwiliwili cha jogoo yaani nusu jogoo nusu nyoka na anatajwa kwenye biblia Cockatrice anatajwa kwenye isaya 11:8, 59:5,14:29. Jina lake kwenye Biblia limetokana na neno la kiebrania tse-pha ambalo kwenye kamusi ya kiebrania linazungumziwa kama Joka lenye mwili wa kuku ambalo ukiliangalia tu unakauka na jinsi pekee ya kuliua ni kulireflect yaani kama kutumia kioo au chochote kitakachomfanya ajiangalie mwenyewe. Ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi wa uwepo wake ila amezungumziwa sana kwenye maandiko. Mfano hapa katajwa kwenye mfano huu wa Nabii Isaya juu ya wafilisti.

Isaya 14:29
29 Usifurahi, Ee Ufilisti, pia wote,Kwa sababu fimbo ile iliyokupiga imevunjika;Maana katika shina la nyoka atatoka ****,Na uzao wake ni joka la moto arukaye (Dragon kwa bible ya kingereza)

SATYR
View attachment 835986

Neno hili kwenye biblia limetokana na jina la kiebrania sa'iyr ambalo kwenye kamusi ya kiebrania walikuwa viumbe ambao walikuwa ni jamii ya watu lakini wana kiwiliwili cha farasi au mbuzi yaani nusu mtu nusu farasi. Kwenye Biblia wanatajwa kwenye kitabu cha Isaya 13:21 na 34:14 kama viumbe wa porini na ambao Nabii Isaya alitabiri kuwa ufalme wa Babeli utaangushwa siku moja na kwenye mfano huo akaeleza kwamba hatoishi mtu bali wanyama wa mwituni kama simba,bundi na huyo SATYR kwahiyo mpaka hapa inaonyesha haikuwa lugha ya picha tu bali Isaya aliongelea mnyama ambaye alimfahamu na kumsikia ndio maana akamtolea mfano.

Isaya 13:21
21 Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini (satyr) watacheza huko.
View attachment 835988

Did they exist??
Salaam mkuu Zitto jr.
Nimefuatilia kwa makini mjadala huu uliouamsha kuhusu viumbe wenye Utata kwenye biblia nakupongeza sana kwa kweli si kazi ndogo.

Naomba nijikite kwenye hao Unicorn tu kwa leo!
Kwanza tuanze kutazama asili ya neno lenyewe - Unicorn -Limetoholewa kutoka Lugha ya kingiriki/kiyunani - Monokeros na kwenda Kilatini unicornus na kuja Kingereza - unicorn na mara zote hizo likiwa na maana moja tu "Pembe Moja".
Tabibu na mwanahistoria wa Kiyunani Ctesias of Cnidus ndio mtu wa kwanza kabisa kuandika kuhusu habari za mnyama mwenye pembe moja - katika kitabu chake cha - Indica alikchokiandika mnamo mwaka 400 KK.
Katika uandishi kihusu India,upo ushahidi ya kwamba aliandika kuhusu india lakini hakuwahi kufika kabisa bara hindi.
Inasadikika kabisa kuwa alipokuwa akiandika kuhusu bra hindi alikuwa tayari na picha ya Faru wanaopatikana bara hindi wenye pembe moja tu si kama faru wanaopatikana bara la Afrika na kwingineko wenye Pembe Mbili zilizopangana pamoja.
Wanazuoni walipokuwa wakitafsiri Biblia toka Lugha ya Kiebrania kwenda Kiyunani walikutana na habari za Mnyama wa ajabu na mwenye Nguvu - ambaye kwa kiebrania alijulikana kama ( Re'em) - Megafauna. Ambaye katika Biblia ya kiebrania ametajwa mara nane.
Basi hawa watafsiri waliamua kuweka neno Monokeros katika neno Re'em na ilipofikia kutafsiliwa kwa Kilatini wakaweka - unicornus ambaye katika Biblia ya Kiswahili ametafsiliwa kama - Nyati.

Hivyo Utata unatokana na Wasomi wa Kiyunani walipokuwa wakitafsiri Biblia ya Kiebrania kwenda katika targeted language ambayo ni Kigiriki ndipo huyu Unicorn anajitokeza hapa - Kimsingi katika eneo hili aliyekuwa anazungumziwa ni Ng'ombe pori - (Auroch) ancient mega fauna, ambao hawapo tena duniani.
Muhimu hapa ni kwamba - Hao Re'em walikuwa na Pembe Mbili wala si Moja.
1.png


Hivyo UNICORN ni Mnyama wakufikirika tu - Hajawahi kuwepo duniani- Hii inatokana na misconception ya Mtu wa kwanza kuelezea habari za Huyu Mnyama - Bwana Ctesias.Alikusudia kuelezea Faru wenye Pembe moja wanaopatikana bara hindi pekee mpaka leo.
Asante sana.
 
..
quora hakuna mambo ya hivi zaidi ya kila mchangiaji kujàza alichotafiti,sasa kwa stail hii ya midahalo isiyo na hitimisho tunapataje muafaka, ila sio kesi bongo ni bongo tu.
Mkuu JF ya zamani ndio ilikuwa kama Quora Yaani ukichokoza mada tu watu wanakuja na essay nzima za tafiti zao ila sasa hivi watu wanabishana kwa mawazo yao tu sio tafiti ndio maana mtu inakuwa ngumu kupata ukweli wa jambo

Ila kma nlivyosema kwa namna hali ilivyo inatakiwa usome tu mada then upime na michango ya watu mbalimbali alafu uje na conclusion yako binafsi ila jibu kma jibu ni ngumu kulipata humu unless watu waje na fact tupu.
 
..

Mkuu JF ya zamani ndio ilikuwa kama Quora Yaani ukichokoza mada tu watu wanakuja na essay nzima za tafiti zao ila sasa hivi watu wanabishana kwa mawazo yao tu sio tafiti ndio maana mtu inakuwa ngumu kupata ukweli wa jambo

Ila kma nlivyosema kwa namna hali ilivyo inatakiwa usome tu mada then upime na michango ya watu mbalimbali alafu uje na conclusion yako binafsi ila jibu kma jibu ni ngumu kulipata humu unless watu waje na fact tupu.
Sawa mkuu...ila daah ckuizi kunabore humu imekuwa kama ngonjera!!!
 
Salute Comrades..
Nilikua nina mpango siku moja nilete uzi kama huu miezi kadhaa iliyopita japo ulikua umetofautiana kidogo, nilitaka kugusia hasa vitu tunavyoaminishwa vipo au vilikuwepo lakini ni uongo (hoax)
Siku moja nilikua naongea na mzee mmoja nikawa namuuliza kuhusu wanyama kama hao Dragon,vampires, Dinosaur etc...
Aliniambia kua katika ulimwengu huu binaadamu hawezi kufikiria au kutengeneza kitu ambacho hakijawahi tokea au hakipo ni Mungu pekee ndio anaweza.

Hoja yangu ni nini?
Mkuu mimi nakubaliana na hiyu mzee, sidhani watu hua wanaamua kujitungia tu yale tunayoyaona kwenye muvi na kusoma kwenye vitabu. Ikumbukwe binaadam sisi wa kawaida tunajua vitu vichache tu kutokana na elimu iliyoruhusiwa na wakubwa tuifahamu. Basi mimi naunga mkono hoja hao viumbe kuna uwezekano mkubwa walikuwepo hapa duniani.
Huyo mzee kaongea point muhimu mno.
 
Kwanza kabisa Hongera kwa uzi mzuri.

1.Umeuliza je! :Wanyama hawa waliwahi kuwepo au ni hekaya tu za wazungu?

Walikuwepo na hawahitaji science kuwathibitisha maana kuwepo kwao ni kutoka kwenye (credible source) na Huwezi sema eti lewiathan ni mamba alieishi mto Nile (hii ndio hekaya na satire za kina Charlie hebdo)

Kwa hio leo akatokea mamba wa hizo ulizosema mita 20 huko nachingwea tutamwita Lewiathani?

Hukuona lewiathani akielezwa kuishi baharini tu.!

2.Wanyama hawa walitoweka wapi?
Wapo na hawajatoweka maana chanzo makini kilichoonyesha wapo hakina taarifa ya ukomo wao (hawa viumbe ni wasiokufa kama wenye damu)

Kama wapo wanaishi wapi?
Lewiathani yupo baharini,,,majini yako porini,,majangwani na sehemu chafu,,,hao dragon ni majini tu kwa hio hakuna darubini wala kifaa cha kisayansi cha kuonyesha uwepo wa majini au viumbe roho ila wapo kwa mamilioni.

3.Je walitowekaje?
Wapo na hawajatoweka na hawatatoweka.

Mwisho kabisa Adam ndio binadamu wa kwanza na hao unaosema walikuwepo ni hadithi za kupuuza kwa sababu fuvu limekaa ardhini limepimwa na kimashine cha kubabaisha na hakina hata accuracy ya 100% then kinaandika eti fuvu lina miaka billion 8 wewe uliosoma kwa nini usiseme hii ni error...science yako huitumii kwa nini? Ingekuwa mimi hata hicho kimashine ningekiweka mvunguni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom