Did they exist: Viumbe wenye utata kwenye BIBLIA

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
19,039
28,689
UTANGULIZI
Habari za jioni wana jukwaa pendwa kufuatia maoni kwenye huu uzi
Wafahamu viumbe watatu wa kutisha wa baharini - JamiiForums kuna baadhi ya watu walinitaka niandae uzi maalum ili niweze kuelezea viumbe hivi vyenye utata kidogo kwenye Biblia. kama kawaida natoa rai uzi huu ni kwa minajili ya kujifunza tu na kujadiliana ili tuweze kuongeza maarifa ila sio uwanja wa mabishano ya kidini so sitegemei kejeli,matusi dhidi ya dini za watu wala vitabu vya dini ya yeyote.

NB: uzi huu nimeugawa katika post mbili ili iwe rahisi kusomeka na isichoshe msomaji

Kwa kusema hayo sasa tunaweza kuendelea.

UNICORN
xunicorn_scottish_national_animal.jpg.pagespeed.ic_.g2SLNDry7Y.jpg

Neno hili limetokana na neno re'em kiebrania na kigiriki MONOC’EROS ambalo kwa hapo nyuma ilifahamika kama farasi mkubwa sana mwenye pembe moja ya mbele ambaye anatazamiwa kuwa na nguvu sana kuliko wanyama wengi. Anazungumziwa kwenye Hesabu 23:22 na 24:8, ambapo Biblia inafananisha nguvu za Mungu kama nguvu za Unicorn hapa duniani.

Pia kumb. La torati 33:17, zaburi 22: 21 na 92:10 yanaongelea pembe la huyo unicorn ilivyo na nguvu.

Pia Ayubu 9:10 na 39:10 zote zinaongelea jinsi ilivyo ngumu kumkamata mnyama huyu.

Kuna wengine watasema kwamba tunasoma biblia kama gazeti ila hapa biblia iko wazi kabisa kupitia Isaya 34:17 kuwa Unicorn alikuwa mnyama na imemuweka hapa kundi moja na wanyama wengine kama ng'ombe hivyo sio lugha ya picha kabisa.
images (51).jpg

Ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi wa farasi wenye pembe yaani unicorns ila kuna vifaru wa huko siberia,Urusi ambao kisayansi wanatajwa kuwahi kuwepo hapa duniani hivyo kuna baadhi wanasema huenda ndio unicorns walioongelewa kwenye Biblia!!

DRAGONS
images (50).jpg

Dragons wameongelewa kwenye Isaya 43:20,34:14 na Micah 1:8 kama mnyama mkali ,hatari na anayenguruma huko porini. Pia isaya 91:13 na 27:1 pia zinamzungumzia kama kiumbe anayetawala na baharini pia kwa utisho mkubwa. Kiebrania jina lililotumika ni Tannin likimaanisha mnyama wa jamii kama joka ila lina miguu na mabawa. Kuna watu pia wanaweza sema ni lugha ya picha ila Isaya 13:21-22 inataja kikundi cha wanyama ambao mpaka leo wapo na mmoja anayetajwa ni Dragon hivyo sitegemei hoja hii itumike, ila swali ni je mnyama huyu amewahi kuwepo duniani na kama ametoweka nini kilisababisha??

COCKATRICE
images (49).jpg

Ni mnyama jamii ya nyoka ila ana kiwiliwili cha jogoo yaani nusu jogoo nusu nyoka na anatajwa kwenye biblia Cockatrice anatajwa kwenye isaya 11:8, 59:5,14:29. Jina lake kwenye Biblia limetokana na neno la kiebrania tse-pha ambalo kwenye kamusi ya kiebrania linazungumziwa kama Joka lenye mwili wa kuku ambalo ukiliangalia tu unakauka na jinsi pekee ya kuliua ni kulireflect yaani kama kutumia kioo au chochote kitakachomfanya ajiangalie mwenyewe. Ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi wa uwepo wake ila amezungumziwa sana kwenye maandiko. Mfano hapa katajwa kwenye mfano huu wa Nabii Isaya juu ya wafilisti.

Isaya 14:29
29 Usifurahi, Ee Ufilisti, pia wote,Kwa sababu fimbo ile iliyokupiga imevunjika;Maana katika shina la nyoka atatoka fira,Na uzao wake ni joka la moto arukaye (Dragon kwa bible ya kingereza)

SATYR
images (48).jpg

Neno hili kwenye biblia limetokana na jina la kiebrania sa'iyr ambalo kwenye kamusi ya kiebrania walikuwa viumbe ambao walikuwa ni jamii ya watu lakini wana kiwiliwili cha farasi au mbuzi yaani nusu mtu nusu farasi. Kwenye Biblia wanatajwa kwenye kitabu cha Isaya 13:21 na 34:14 kama viumbe wa porini na ambao Nabii Isaya alitabiri kuwa ufalme wa Babeli utaangushwa siku moja na kwenye mfano huo akaeleza kwamba hatoishi mtu bali wanyama wa mwituni kama simba,bundi na huyo SATYR kwahiyo mpaka hapa inaonyesha haikuwa lugha ya picha tu bali Isaya aliongelea mnyama ambaye alimfahamu na kumsikia ndio maana akamtolea mfano.

Isaya 13:21
21 Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini (satyr) watacheza huko.
00-daz3d_centaur-7-for-genesis-3-male_s_.jpg


Did they exist??
 
LEVIATHANS
The Leviathan ni kiumbe mwingine mwenye utata anayetajwa kwenye biblia ya kiebrania baadhi ya vifungu hivi Ayubu 3:8, Ayubu 40:15–41:26, Amos 9:3, zaburi 74:13–23, zaburi 104:26 and Isaya 27:1.
images (53).jpg


Leviathan ni kiumbe aliyetajwa kwenye Biblia kama kiumbe wa kutisha ambaye alikuwa tishio na hana mpinzani baharini sura nzima ya Ayubu 41 inamsifia kiumbe huyu kwamba ana ngozi ngumu kama chuma,anatema cheche na moto mdomoni nisitie chumvi Isaya mwenyewe anasema

Isaya 41
27 Yeye huona chuma kuwa kama nyasi,Na shaba kama mti uliooza.
28 Mshale hauwezi kumkimbiza;Na mawe ya teo kwake hugeuka kuwa kama makapi.
29 Marungu huhesabiwa kama mabua;Naye hucheka mshindo wa mkuki ukitupwa.
30 Pande zake za chini ni kama vigae vikali;Hutandika malazi kama kuweka chombo cha kupuria nafaka juu ya matope.
31 Yeye huchemsha kilindi mfano wa nyungu;Hufanya bahari kuwa kama mafuta.
32 Hufanya mapito yake kung?aa nyuma yakeHata mtu angedhani kilindi kina mvi.
33 Juu ya nchi hapana aliyefanana naye,Aliyeumbwa pasipo oga


Kuna hoja nilikutana nayo kwa mkuu GuDume kwamba lugha iliyotumika ni ya picha jambo ambalo nakubali lakini majibu yote tunayapata zaburi kwamba ni mnyama na aliumbwa na Mungu.

Zaburi 104:26
26 Ndimo zipitamo merikebu,Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo.
images (55).jpg


However kuna hoja za waandishi wa kiebrania kwamba mnyama huyu anaweza kuwa mamba wa mto nile ambaye alikuwa ana urefu mpaka wa mita 20 ingawa sifa ya kutema moto hakuwahi kuwa nayo!!! Na baadhi ya wanatheolojia wanadai mnyama huyu alikuwepo wakati wa chaos yani kipindi dunia haijaumbwa yaani baada ya vita ya malaika na shetani ndipo viumbe hawa waliishi na baada ya dunia kuumbwa na wanadai waliuawa na Mungu kwa kurejea Zaburi 74:13 kwa kupasuliwa vichwa na tukio hili linatazamiwa kutokea kwenye mwanzo 1:2 ambapo Roho wa Mungu alikuwa juu ya maji ikitazamiwa ndipo alipoenda kummaliza huyu lewiathani.

BEHEMOTH
images (56).jpg

Huyu kiumbe anatajwa kwenye biblia kama mnyama asiye na mpinzani ardhini na kwamba alikuwa na nguvu sana na kutikisa mwituni na aliogopeka sana. Kwa sasa anaweza fananishwa na tembo au kiboko ingawa huyu Biblia inaeleza urefu wako unalingana na mti wa mwerezi na sifa hizi zote zinatajwa kwenye Ayubu 40 ambapo sura hii nzima imetolewa kumwagia sifa mnyama huyu ili kuonyesha ukuu wa Mungu. Pia hapa haijatumika lugha ya picha pekee bali uhalisia maana Mungu anasema

Ayubu 40:15
15 Mwangalie huyo kiboko (behemoth), niliyemwumba pamoja nawe.....

Baadhi ya sifa zake
17 Yeye hutikisa mkia wake mfano wa mwerezi;Mishipa ya mapaja yake yanaungamana pamoja.
18 Mifupa yake ni kama mirija ya shaba;Mbavu zake ni kama vipande vya chuma
20140904-dreadnoughtus-udrexel-800_7A73CF5F27014B68B0E4A9B6C883060F.jpg


Wanatheolojia wanadai anaweza kuwa Dinosaur kama huyu hapa chini ambao kisayansi ushahidi wa uwepo wao unathibitishwa ila wengine wanadai ni tembo au kiboko wa kizamani ambao walikuwa wakubwa sana na waliogopeka mno maana walikuwa hawana mpinzani fikiria ukutane na mnyama kama simba mwenye size ya Tembo!!
images (54).jpg


HITIMISHO
Wanyama hawa niliowataja wengi wao hawana ushahidi wa kisayansi kuwa walikuwepo inanifanya nije na maswali yafuatayo

1. je wanyama hawa waliwahi kuwepo au ni hekaya tu za wazungu.??
2. Wanyama hawa walitoweka wapi na kama bado wapo wanaishi wapi??
3. Je walitoweka je lini na kwanini???


Naomba kuwasilisha wanajukwaa
 
Salute Comrades..
Nilikua nina mpango siku moja nilete uzi kama huu miezi kadhaa iliyopita japo ulikua umetofautiana kidogo, nilitaka kugusia hasa vitu tunavyoaminishwa vipo au vilikuwepo lakini ni uongo (hoax)
Siku moja nilikua naongea na mzee mmoja nikawa namuuliza kuhusu wanyama kama hao Dragon,vampires, Dinosaur etc...
Aliniambia kua katika ulimwengu huu binaadamu hawezi kufikiria au kutengeneza kitu ambacho hakijawahi tokea au hakipo ni Mungu pekee ndio anaweza.

Hoja yangu ni nini?
Mkuu mimi nakubaliana na hiyu mzee, sidhani watu hua wanaamua kujitungia tu yale tunayoyaona kwenye muvi na kusoma kwenye vitabu. Ikumbukwe binaadam sisi wa kawaida tunajua vitu vichache tu kutokana na elimu iliyoruhusiwa na wakubwa tuifahamu. Basi mimi naunga mkono hoja hao viumbe kuna uwezekano mkubwa walikuwepo hapa duniani.
 
binafsi ninaamini walikuwepo na kuhusu kutothibitisha kwa sayansi uwepo wao ni kwamba hakuna aliyepata masalia(fossils)yao ila inawezekana baadae wakaja kugunduliwa,kumbuka dinosour wamegunduliwa karne za hivi karibuni ingawa walipotea miaka mingi sana iliyopita,tuwe na subira.Kuhusu kupotea kwao only GOD knows
 
Salute Comrades..
Nilikua nina mpango siku moja nilete uzi kama huu miezi kadhaa iliyopita japo ulikua umetofautiana kidogo, nilitaka kugusia hasa vitu tunavyoaminishwa vipo au vilikuwepo lakini ni uongo (hoax)
Siku moja nilikua naongea na mzee mmoja nikawa namuuliza kuhusu wanyama kama hao Dragon,vampires, Dinosaur etc...
Aliniambia kua katika ulimwengu huu binaadamu hawezi kufikiria au kutengeneza kitu ambacho hakijawahi tokea au hakipo ni Mungu pekee ndio anaweza.

Hoja yangu ni nini?
Mkuu mimi nakubaliana na hiyu mzee, sidhani watu hua wanaamua kujitungia tu yale tunayoyaona kwenye muvi na kusoma kwenye vitabu. Ikumbukwe binaadam sisi wa kawaida tunajua vitu vichache tu kutokana na elimu iliyoruhusiwa na wakubwa tuifahamu. Basi mimi naunga mkono hoja hao viumbe kuna uwezekano mkubwa walikuwepo hapa duniani.
Mpaka tunafikia hapa ni kutokana na imagination tumeimagine kuna afterlife ndo maana tumekuwa tunafuata sheria na dini.. Sisi ndo viumbe pekee tunaoweza kufanya imagination
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom