Did CHADEMA fumble on securing Presidential Votes?

Shalom,

Bado nauzi ndugu?

November 2 at 10:36pm
1. Pettition at High court to: a. stop NEC from declaring the winner of presidency of URT.b. suspend announcing and counting all presidential vote count. c. demand all ballots announced should be reounted by independent body. This should be 1st thing in the morning tomorrow.

2. Contact UN, AU, Commonwealth, SADDC, EAC President and donnors on Presidential race and voting irregularities. Request independent inquiry and intervention from UN.

3. Press conference by Slaa and Chadema leadership to Wananchi wa Tanzania t explain kinachoendelea and provide copies of foul play and court injuction on President elections.

4. Call a meeting with Police, TAKUKURU, TISS and Jeshi and declare Chadema stance on vurugu by CCM.

5. Demand meeting with Kikwete, Lipumba and other presidential candidates by 3 pm.

6. Demand unity government and powe sharing.
 
Hakuja Haja ya kulalamika.... nikutafauta ni jinsi gani sasa tuanweza kupiga kelele kupata katiba mpya yenye mambo yote haya na kuondoa huu utata...wapi pakuanzia sasa na nani wa kuanzisha....? Shinikizo linapatikana vipi ili kabla 2015 tuwe na tume huru ya uchaguzi....?
 
Hakuja Haja ya kulalamika.... nikutafauta ni jinsi gani sasa tuanweza kupiga kelele kupata katiba mpya yenye mambo yote haya na kuondoa huu utata...wapi pakuanzia sasa na nani wa kuanzisha....? Shinikizo linapatikana vipi ili kabla 2015 tuwe na tume huru ya uchaguzi....?

Je wataanza mchakato huo leo hii au watasubiri 2014 kama ilivyokuwa hapo 2005 wakasubiri mpaka 2010?
 
Binafsi nashangaa sana!
Watu wanalaumu, kosoa na ku-oni utafikiri UKOMBOZI wa nchi HII ni jukumu la CHADEMA peke yao!
Na inapofika kushangilia, ushindi unageuka kuwa WETU SOTE!
 
Je wataanza mchakato huo leo hii au watasubiri 2014 kama ilivyokuwa hapo 2005 wakasubiri mpaka 2010?
Reverend,
For CHADEMA there has not been a dull moment. To say that from 2005 walisubiri mpaka 2010 is not doing them justice. You are trying to compare CHADEMA with CCM in terms of resources and outreach. In 2005 they had 4-or 5 MP's. Today they have close to 50. That itself is an indication they have not been sitting idle on their laurels waiting for 2010. I saw first hand what CHADEMA has been up against in the rural areas and their success in no mean feat. CHADEMA won this election but did not have the resources to protect their victory. Polepole tutafika.
 
Rev.Kishoka,
Mkuu wangu labda nikwambie kitu kimoja tu. Chadema ifanye itakavyofanya CCM hawataweza kuwaachia ushindi hata siku moja, kwa hiyo wangelinda hizo kura wasilinde, CCM bado angekuwa mshindi na nasikitika sana kusema kwamba hii ngoma itaendelea kupigwa kwa miaka ijayo.

Na kibaya zaidi hata kama CCM sio chaguo la wananchi CCM itaendelea kushinda kwa sababu ya hofu waliyoijenga CCM ktk mioyo ya wananchi kuhusu Amani na Utulivu kwa kutumia vigezo vya Rwanda na Kenya. Mimi mtazamo wangu maadam kuna kuchakachua, na NEC itaendelea kupokea amri kutoka chama tawala na rais mwenye nguvu kubwa kikatiba basi haki ya demokrasia haitawezekana kabisa, haki ya wananchi itaendelea kupuuzwa na hakuna haki yeyote itakayo tendeka ktk mfumo huu..

Pengine chukua mfano wa CUF ambao wako hatua moja mbele ya Chadema katika kulilia haki ya Wazanzibar, mwaka1995 na 2000 yaliwakuta haya na Wazanzibar wakasimama kuandamana kupinga matokeo wakala fimbo sana, mwaka 2005 vile vile ushindi kwa CUF visiwani kura zikachakachuliwa akapita Karume kama zilivyochakachuliwa bara mwaka huu. Wamenyang'anywa ushindi hivi hivi mbele ya macho yetu na tumeshindwa kuona wala kulalamika. Wakati yakiwatokea huko visiwani huku bara tulikuwa tukiwacheka sana, na pengine hata watu kusimama na CCM kupinga sera za CUF na Uislaam wao, sasa haya ndiyo yanawakuta Chadema huku bara na mgawanyiko huu utaendelea kuwepo kwa sababu katiba iliyopo haiwezi kuleta demokrasia inayofuata itikadi bali Udini.

Huu ni mwanzo tu mkuu wangu kama Tanzania ni nchi moja na tumeshindwa kuelewa kwamba pasipo Zanzibar au bara hakuna kitu Tanzania lakini bado tukafanya siasa za kujigawa, basi CCM ataendelea kutumia vigezo vya udini kwani inaeleweka wazi kuwa anayeipinga Chadema leo hii ni Muislaam, na anayeipinga CUF leo hii ni Mkristu hakuna siasa za sera wala itikadi.

Mwisho, mkuu wangu imani yangu kubwa ya ushindi wa Chadema ilikuwa mwaka huu na maadam hili swala la uchakachuaji limechukua sura mpya sidhani kama Chadema wanaweza kufanya lolote kwa sababu sisi wenyewe Watanzania tumejenga utamaduni wa Ewallah bwana, kiasi kwamba vitu vingi vinafanyika kinyume cha katiba iliyopo (ingawa mbovu) lakini tunahalalisha matokeo yake, hivyo hata kama ukiondoa madaraka ya rais sijui katiba mpya iandikwe haitaweza kubadilisha hulka ya viongozi ambao wao wapo juu ya sheria.

Katiba yetu leo hii imesimama kama msahafu au Biblia, una choice ya kuifuata au kutoifuata, mwenye kutaka kuifuata aifuate asiyependa hakuna ulazima hivyo sheria haipo tena. Kwa hiyo kiongozi anaweza kuapishwa kuilinda katiba lakini matendo yake yakawa kinyume kabisa cha katiba lakini mlinzi mzuri wa katiba iliyopo kama wakristu na waislaam wanavyolinda vitabu vyao hali sii waumini wa kweli.
 
Je, katiba mpya itakuja vip wakati CCM ina 78% ya wabunge watakaokwamisha? Hatuoni hizi ni daydreams?.
 
Then who needs to bear responsibility and be accountable for this kind of gross negligence?
who said it was out of gross negligence?
I hate it when people decide not to see either side of the coin so that their point is neither right nor left/ never right and never wrong. People who wait for things to happen so that they can take a side later, a blaming side. People who know very well that there is a lot to do with resources than the matter of organization.....and that too need resources anyway.
 
Hivi mkuu,unaonaje kama swali lako lingeendana na mtizamo wako as WANGEFANYAJE kuhakikisha usalama wa taifa,tume ya uchaguzi na watendaji wake,na kila chombo cha dola hawachakachui matokeo?

Sitaki kuamini kuwa Dkt Slaa alifocus kwenye wabunge na madiwani pekee ilhali kila alipopita aliomba kura za urais na hizo nafasi nyingine.

Don't underestimate the power of the dark forces
 
tusonge mbele tuache majungu! kila mtu ajilaumu kwa uzembewe tujenge chama kuwa makini zaidi!
 
chadema hawawezi kushinda bila people power

majimbo karibuni yote chadema waliyoshinda watu walizingira ofisi ili matokeo yatolewe.
pale waTZ watakapokuwa tayari kuzingira ofisi zote (people power) ili matokeo yatolewe basi ndio chadema itakaposhinda.
TZ haitakuwa tofauti na nchi nyingine za africa katika kukitoa cahama tawala madarakani

rev chadema wamelinda kura zote lakini kura za urais zilikuwa zinatangazwa na makao makuu
 
kuna mawakala waliowekwa na CHADEMA huko remote areas ambao walihongwa na ccm kupitia wasimamizi wa uchaguzi na mawakala wa ccm.
Makao makuu wanajua na sijui wanachukua hatua gani kukabili hii hali maana inajirudia kila mwaka.
ndo maana nasema kwamba kuna watu wanajitia uzalendo lakini ni majeshi ya akiba ya ccm ili kufanikisha hila zao mbofu.

Nimekusanya taarifa mbalimbali kuhusu namna ambavyo mawakala walishughulika sana kulinda kura za madiwani na wabunge lakini kura za urais hawakuweka umakini mkubwa.
kuna tatizo na linapaswa kuundiwa mkakati wa kulitatua.
 
Mimi bado niko katik msimamo wangu uleule ambao kila nikiutoa sipingiki.

Msimamo wangu ni kwamba pale tutakapohakikisha magazeti na forums kama JF zimezunguka na kupata na kuyataja matokeo ya kituo kwa kituo basi kwa 60% naamini CHADEMA itashinda.

Tusuke au kunyoa. Tukiweza hilo tutashida. Tukiamua kulipuuzia kama tunavyolipuuzia kila tunapolileta basi sahauni ushindi tayarisheni mikakati ya kulalamika na kulialia.

Na hili halihitaji tume huru. Hakuna sheria inayomfunga mwanahabari kwa kuchapisha matokeo ya kituo kwa kituo, iwe ya nchi nzima au jimbo moja.

Labda oni langu ni kwamba kama vyombo vya habari vinashindwa kuenea nchi nzima ni afdhali 2015 tuandae harambee kuvisaidia hilo kuliko kulalama kama ombaomba.
 
Then who needs to bear responsibility and be accountable for this kind of gross negligence?

There is no doubt that CHADEMA failed to plan prior the election that caused this nightmare, it's obvious that since the beginning people were preaching about several things need to be changed to assure landslide winning. However, I don't think blame game will do any better at this moment. I will like to hear from people like Kitila concern what lessons did CHADEMA learn in 2010 election, and what methodology it will implement to improve the outcomes.
 
Then who needs to bear responsibility and be accountable for this kind of gross negligence?

Rev Kishoka and others,
Bear in Mind that CHADEMA did not do all due to its negligency as in the above post or others' contributions. My understanding is that CHADEMA did what was within their capacity, they stretched to the maximum. Now that we all see the weakness, start orhanising yourselves to make systems work.

Tostart with some of us have started meetings to open CHADEMA matawis where we live. we have agreed in our Jimbo that by 2011 june, we have stronger mashina and want to win all LGA election coming in the forthcoming election while preparinhg strongly for 2015. So please take a step ahead. We are all responsible because this is our country.

God Bless You
God Bless Tanzania
God Bless CHADEMA
God Bless Dr. Slaa
 
Mchungaji--Maybe kura haziikuibiwa and they lost fair and square. If people are unwilling to accept matokeo sasa kuna haja gani ya kupiga kura?
 
kukupa tu mfano
baada ya matokeo ya mnyika na halima mdee kutangazwa watu ilibidi waende anatoglo kushinikiza matokeo yatangazwe. kwa bahati nzuri mimi nilikuwa hapo mitaa ya lumumba, nikaona niende huko kuungana na wenzangu. kulikuwa na watu wengine kama 30 na wanatembea huku wakiimba. ghafla likatokea gari la FFU LIKAtuzuia kuelekea huo upande kwa kisingizio cha fujo. bahati nzuri mimi nilikuwa na docs za kuwaonyesha kama naenda eneo la pale karibu wakaniachia pamoja na ma dr wawili wa hospitali ya mnazi mmoja. wale jamaa wengine wote wakarudishwa walikotoka.

dada yangu alikuwa mwanza bugando ananiambia watu wamekula mabomu ya machozi sio mchezo na wamevumilia

the only thing i can say to chadema right now is "congratulations". Dr slaa ikifika end of dec chukua holiday cause you need it...
 
Mchungaji--Maybe kura haziikuibiwa and they lost fair and square. If people are unwilling to accept matokeo sasa kuna haja gani ya kupiga kura?
And just maybe kura ziliibiwa. Kulikuwa na sababu gani ya kusubiri siku tano kutangaza matokeo ya kura za urais? Usitetee system ambayo imeoza unless unanufaika nayo. Unakumbuka Kikwete alisemaje kuhusu wizi wa kura siku mbili kabla ya uchaguzi? Alijuaje? Watanzania sio wajinga kiasi unachodhania.
 
Hivi hii spirit ni ya wafuasi tu wa CHADEMA au viongozi pia? Mbona wenzetu nyinyi mkipewa maoni tofauti tu na yale mliyozoea kusikia au mnayotaka kusikia mnakuwa wakali sana. Wakati mwingine criticism ndio chacha ya mabadiliko endelevu.
 
Back
Top Bottom