Its too lateNaandika hii thread kwa machungu sana, hili limeniwia vigumu sana kulisema hapa, lakini imenibidi!
Siandiki nionekane nilisema, wala sipendi siku thread hii ije kufukuliwa kwamba yametimia, wala siandiki kama umbea. Hili ni suala serious juu ya kijana mwenzetu huyu maarufu pengine kuliko kijana yeyote kutokea katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.
Ni nini kimekusibu Naseeb? Kwanini ulifikia uamuzi huo wa kutumbukia huko ulikotumbukia? Imeniumiza sana, kweli!
Mimi sio shabiki wako, ila siwezi kupinga wewe ni Icon, watu wanakutazama kama nembo ya upambanaji!
Na sidhani kama unajua wewe ni mtu mkubwa kiasi gani! Mambo mengi ambayo huwa unafanya yanathibitisha hilo, hili pia likiwemo.
Ndugu unayesoma haya, kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya wasanii na maisha yao hasa hapa kwetu Bongo lazima utakuwa umewahi kusikia tetesi za Diamond kutumia madawa ya kulevya, mengi yamesemwa… wengi wamesema.
Alianza Harmonize kipindi wapo kwenye ‘bifu’ kali baada ya kuachana na iliyokuwa label iliyomsimamia katika safari yake ya muziki ambayo mmiliki ni Diamond, kila mtu anajua jinsi mtifuano ulivyokuwa mkali baada ya Harmonize kuondoka.
Na katika mtifuano huo ndipo Harmonize alituhabarisha kuwa Diamond ni mteja wa madawa ya kulevya, binafsi sikuamini na niliomba isiwe kweli.
Sikuamini kwakuwa katika ugomvi kila mmoja atasema lolote la kumuumiza mgomvi wake, haikuwa na mashiko sana.
‘Dada wa Taifa’ Mange nae mwaka huu amehakikisha kwa kujiamini kabisa kuwa Diamond anatumia madawa ya kulevya, amesema hivyo mara nyingi… pia sikuamini.
Sasa baada ya maneno na tuhuma hizo juu yake mimi binafsi nikaingia ‘chimbo’
Kila mmoja ana chanzo chake kikuu cha habari, hasa kwa sisi wadau wa habari zote ngumu na nyepesi…
Nikauliza ili nijihakikishie je ni kweli yanayosemwa!
Nilichoambiwa ndicho kimenifanya niandike hii thread, nilijibiwa kiufupi kabisa, “NI KWELI ANATUMIA”
Siko hapa kubishana wala kumshawishi yeyote akubaliane na chanzo changu, mimi mwenyewe ndio naujua uzito wa chanzo changu hicho nyeti. Kiufupi ni kwamba chanzo changu hiki kikiniambia kesho nitafariki naanza kabisa kutubu!
Lengo kuu ni kuongea na muhusika mkuu, Jamii Forums ni platform kubwa pengine atafikishiwa haya.
Tafadhali Naseeb, badili mwenendo. Bado hujafikia hatua mbaya, unaweza kuacha kuanzia sasa ukarudi ktk hali yako ya kawaida.
Hukuona yaliyomkuta Whitney Houston? Wewe una ukubwa gani kumzidi malkia yule wa muziki wa muda wote?
Mifano ni mingi, kwa maslahi ya Taifa tusingependa siku ifike na wewe tukutolee mfano.
Wewe ndiye unayeujua ukweli zaidi kwanini umefikia hatua hiyo, ila tafakari nafasi yako ulipo na ubadilike.
Nifah
Kwa ile afya aliyo nayo sasa kwenye hii nyimbo mpya aliyoimba na Kofii mwezi uliopita mimi Buskdokta kwa uzoefu wangu wa miti shamba ni ngumu kuamini kwamba jama Hali Sembe.hata afya yake imekongoroka, uwezo wa kutunga umeporomoka ana flow nyimbo za matusi tu.. he is loosing mentally and physically kila siku.. in 10 years anaweza kuwa vibaya maana balaa la madawa ni kwamba the more you take the more u need it.
wanaomzunguka waache uchawa na upambe wameambie ukweli, family na ma manager wamsaidie..
vita za madawa huwez ishinda mwenyewe , amuulize Lord Eyez katokaje huko.
Jipe moyo ukanya barabarani tukuseme then uamini ndio mafanikio yako.Vijana wa ki Tanzania mnao tafuta maisha, hivi ndivyo wa Tanzania walivyo mkizipata mtakuwa mnazungumziwa, na ukiona watu wanakuzungumza ujue kuna kitu kikubwa unakifanya ambapo huo uwezo wao kufanya hawawezi.
Hujanielewa kumbe!Kwahiyo mkuu na wewe unaweza kutumia madawa ya kulevya ili kuupata utajiri?
Nimekosa kabisa cha kuongea!
Wa Tanzania walio wengi wana roho za chuki,visasi na chuki binafsi, ndio maana umasikini na wao ni ndugu.Jipe moyo ukanya barabarani tukuseme then uamini ndio mafanikio yako.
Wema sepetu yuko wapi?
Bogus. Ulitegemea aseme ndio natumia?"machungu sana"
Diamond is doing very well, he is way better financial, humzidi hata ukijumlisha ukoo wako wote na ukoo kwa mkweo humzidi.
Kama hiyo ndo akili ya drugs, acha avute, maana yako timamu haijakufikisha popote zaidi ya kukusaidia kupata uchungu
Diamond was asked once kama anatumia madawa, alikataa, akasema hatumii, in that case nachagua kuamini maneno yake kwamba hatumii.
Teh teh 😂😂😂😂 noma sana
Umeongea point kubwa sanaa.. unaweza kuta ndani ya masaa 24 yy ana mawili tuu.Mbaya mbovu ya wasanii wengi kutumia vilevi ni vile wanataka ku maintain vibe wakiwa juu ya stage,pili watu maarufu wanakuwa na pirukushani nyingi kiasi kwamba hata muda wa kupumzika unakuwa finyu hivyo anajikuta anaingia kwenye vilevi kama sehemu ya kumpumzisha na kumuasha vibe ili pesa siku nyengine iingie!.
Refer msanii mkubwa kama Michael Jackson alishawahi sema kitu ambacho alikuwa hakipendi ni tour!!!, Na hizo ndizo zilikuwa zinamuingizia mshiko maana msanii bila show sawasawa na kazi bure!,Sasa kumaintain hiyo ili aendane na vibe la watu kama hatatumia midawa hapo itakuwaje!,mashabiki mtalalama mmetoa hela zenu halafu hamna kitu na mtu anatandika show ya masaa kadhaa..
Nafikiri ni muhimu wasanii wahaswe na wafatiliwe maana nje na kazi wanafamilia pia na watu wanaowategemea.
Wacha ujuaji na upuuzi dogo. Nyie ndio mashoga na hamtaki muanbiwe eti mku..... ni wako. Pumbavu kabisa wewe.Mtu anapata wapi ujasiri wa kumfuatilia na kumpangia mtu maisha ya kuishi ?
Ikizingatiwa wewe sio Baba ake wala sio mama ake.?
Jiulize swali mmoja tu Kutumia kwake madawa kunaathir nin ktk maisha yako?
Ama akiwa sio mtumiaji wa madawa kunakunufaisha nin ktk maisha yako.?
Yaani mtu unaamka asubuh asubuh na kushusha kitabu kizima cha maneno kwa kumpangia mtu maisha ya kuishi.
Itoshe kusema kama hakuna lote unalofaidika nalo ungeacha kufatilia maisha ya watu.
Kwa hiyo hata MO naye anatumia unga kwa kuwa ni bilionea?Sasa utafutaji una namna nyingi na hiyo namna ndio inayomtesa simba hadi atumie hayo makitu!!
Duh....inasikitisha.Huo ni ukweli mchungu, mwamba alianza kwenye upunda na sasa kaamua alambe kabisa, wanavyoanza wanasema wanapandisha energy wakishakua addicted ndio vile tena....
Wasi wasi wangu asije akamuharibu na kale kabinti
AiseeIbilisi akitaka kumchukua mtu, anaandaa mazingira mapema
Sahihi ✔️Umaarufu ni mtego. Wachache sana hua wanaweza kuutegua.