Diamond Platinumz ku-perfom na Davido nchini Nigeria

Diamond Platinumz ku-perfom na Davido nchini Nigeria

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
448
Reaction score
1,119
Staa wa muziki kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, anatarajiwa kuungana na nyota wa muziki kutoka Nigeria, Davido (O.B.O), kutumbuiza kwa pamoja katika tamasha maalum lililopewa jina la "Oriade".

Tamasha hilo la siku tatu mfululizo limepangwa kufanyika kuanzia Desemba 17 hadi 19 katika ukumbi wa National Theatre uliopo jijini Lagos, Nigeria, likiwa na lengo kuu la kusherehekea miaka 15 ya mafanikio ya Davido katika tasnia ya muziki.

Taarifa hizi zimeibuka mara tu baada ya wasanii hao wawili kuagana nchini Tanzania, ambapo walitumia sehemu ya wiki hii kufurahia muda wao pamoja na familia zao.

Kupitia mtandao wa Instagram, Davido aliacha ujumbe kwenye ukurasa wa Diamond akisema, "See You Soon Again" (Tutaonana hivi karibuni tena), kauli ambayo ilithibitishwa na Diamond kwa kujibu, "See You Soon Bro... Dec 17th We Active In Lagos" (Tutaonana hivi karibuni kaka... Desemba 17 tutakuwa Lagos), na kuweka wazi rasmi kuwa wawili hao watapanda jukwaa moja nchini humo.
IMG_7701.jpeg


SaveClip.App_900102734_18387807448227783_256264871920400922_n (1).jpg
 
Back
Top Bottom