Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,845
Natambua wazi alijiharibia pakubwa alipojiunga na KAYAFA kupitia kazi zake. Na niliwahi kuandika uzi kumhusu yeye na Konde boy kwamba kitendo hicho kina athari kisanii huko mbeleni.
Kuna ambao walinibeza sana lakini always muda ni hakimu wa haki na kamwe maandishi hayafutiki!
Hapa nisiwazungumzie haters wa kawaida wa Diamond. Huwezi kupendwa na kila mtu wala huwezi kuchukiwa na kila mtu. Wala nisiwazungumzie wale haters ambao kwa kushindwa kwao kimaisha basi hasira zao zote wanazihamishia kwa waliofanikiwa.
Hapa tujadiliane na wenye hoja kwa muktadha wa Tanzania kama taifa lililopitia madhila makubwa chini ya mkono dhalimu wa mtu mmoja tu. Huyu ndio alimponza Diamond!
Sometimes ni lazima kuambiana ukweli hata kama ukweli huo hatutaki kuusikia na hauna ladha wala mvuto! Kuna wakati ukweli huwa mchungu kama pakanga!
Ni ukweli usiopingika kwamba:-
- Diamond ndio msanii mwenye mafanikio zaidi kwa sasa Tanzania
- Diamond ndio msanii tajiri zaidi kwasasa Tanzania
- Diamond ndio msanii aliyetangaza mziki wa bongo ndani na nje ya nchi kuliko mwanamuziki mwingine yeyote wa bongo fleva
- Kupitia kazi zake ameweza kuitangaza Tanzania pakubwa sana Duniani
- Amekuwa ni balozi wetu kwenye tasnia ya sanaa ya mziki nje ya mipaka ya Tanzania!
Kwenye mashindano kuna washindi na washindwa! Diamond kashindwa. Na sababu za kushindwa zipo nyingi. Hata kama tutakataa ile kampeni ya watu wa jamhuri ya Twitter lakini ilichagiza pakubwa mno kudhoofisha ushindi wake!
Ana la kujifunza kubwa sana hapa. Hasa kama asiposhupaza shingo!
Mashindano yameisha! Na Diamond kashindwa sasa ni wakati wa marejeo.. Haters wake ni vifijo na nderemo kila kona! Sasa wanaenda mbali zaidi! Wanamdiss na kumdhihaki mavazi aliyovaa siku ya shindano.
Tukiwa na Tafakuri hatupaswi kumbeza wala kumcheka! Angevaa nini sasa ili amridhishe kila mmoja? Chochote ambacho angevaa kingekosolewa na kusifiwa kwa wakati mmoja! Watanzania hatuna vazi rasmi la taifa. Vazi la kimasai kwa sehemu kubwa ndio huchukuliwa kama utambulisho wa taifa.
Ubunifu wa Diamond kuvalia 'kimasai' ni wa kupongezwa japo umekutana na ukosolewaji mkubwa mitandaoni.. Lakini tukumbuke jambo moja muhimu sana. Diamond hakwenda kwenye shughuli ya kitamaduni bali kisanii. Hivyo nakshi na vionjo alivyoongeza kwenye lile vazi vilikuwa vya kisanii zaidi kuliko kuzingatia mila na tamaduni za kimasai. ASAMEHEWE!
Mwisho kabisa:
Pamoja na mashindano haya kuendelea kumpa Diamond mileage kimataifa na kuzidi kuitangaza Tanzania hata kama kakosa tuzo! Lakini ni muda sahihi kwake sasa kujirudi na kujitafakari upya! Pamoja na kuwa na haki ya kisiasa ya kuchagua chama cha siasa apendacho. Lakini kama msanii anatakiwa kuwa mwerevu sana linapokuja suala la kuwagawa mashabiki wake kwa mitazamo yake kisiasa.
Kazi yake ma mashabiki wake ni muhimu sana kuliko mapenzi yake kwa watawala wa kisiasa!
DIAMOND IKIKUPENDEZA OMBA RADHI