Ifike mahali watu mfiche ujinga wenu. Unapomlinganisha Diamond na wanasiasa au wananasheria hivi unakuwa unatumia kichwa cha wapi? Hivi hata kwa akili ya kawaida tu huoni kama hao watu wanatofautiana katika vipawa vyao? Mwanasiasa mlinganishe na mwanasiasa mwenzake, mwanasheria mlinganishe na mwanasheria mwenzake vivyo hivyo mwanamziki mlinganishe na mwanamziki mwenzake na siyo kuleta masuala ya Sokoine kwenye muziki. Au hao majaji, Mtikila, Sokoine nao ni wanamuziki? Tunapozungumzia kuwa Diamond ni nembo ya taifa, tunamaanisha nembo ya Taifa katika muziki, ambayo ndio kazi anayoifanya, na ndio kazi aliyotumia kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.
Asante mkuu ila kuwa icon wa taifa hata kwa huo mziki wenyewe diamond anaanzia wapi au kisa katoboa BET ??? Binafsi sijawahi kuona mtu kama krs one,run d mc,Rakim wakiitwa na kupewa heshima na serikali ya marekani kwa kukuza mziki wa rap ,Sana Sana wataishia kwenye hall of fame ,tunachimba tanzanite hapa ila India ndio wanaongoza kuuza kwenye soko la dunia ,kwa ujinga wetu tu vitu vya kupewa kipaombele ndio vinadharaulika
Bila Nyirenda Leo bendera ya taifa ingekua inapepea Kilimanjaro ?? Nyirenda mwenyewe yuko wapi
Kina Bregedia Hashim mbita wanaenziwa Vipi ??
Hiyo title ya icon wa taifa ..ingesomeka hivi icon wa bongofleva