Diamond kainuliwa na Mungu mwenyewe. Binadamu hawezi kumshusha

Achana na mapungufu yake, haya tumeumbiwa wote chini ya jua.. Kwakuwa sisi wa mwili wa damu na nyama si wakamilifu.

HAPA UMEANZA MKUTAKATISHA, NI KWELI KILA BINADAMU ANAMAKOSA YAKE.
HUYU MTU NI WAKALA (UNAJUA VIZURI), NA NDIO MAANA KAKUMBATIA MASHOGA KWENYE LEBO YAKE.

MASHOGA+MUSIC+MEDIA=?
OK basi sawa
 
FB_IMG_1659502337527.jpg
 
Kwa hivyo nikifikiria kuwa pembetatu duara ipo, hilo linamaanisha pembetatu duara ipo?

Nikikwambia uongo wowote, kwa mfano, wewe ni shetani, ukabisha, nikakwambia hilo jambo ni mfano wa fikra, halionekani, utakubali kwamba wewe ni shetani?

Unajuaje Mungu yupo na haonekani? Unajuaje hii si hadithi iliyotungwa na watu tu na Mungu kiukweli kabisa hayupo?
twende taratibu, ikiwa ukweli/uongo unaoujua unatokana na fikra zisizoonekana, ni wapi unapata nguvu ya kukanusha uwepo wa mungu kisa haonekani kwa macho ya mwili?

hoja yako ni ipi sasa, ikiwa unakiamini A kisichoonekana then unakikanusha B kisichoonekana?
 
Achana na mapungufu yake, haya tumeumbiwa wote chini ya jua.. Kwakuwa sisi wa mwili wa damu na nyama si wakamilifu..

Mungu huwainua wachache kati ya kwa kila taifa, ukoo hata familia.. Huwainua kwa vipawa na vipaji mbalimbali... Na wengine baada ya kujitenga na dunia hutunukiwa karama mbalimbali za kiroho

Diamond Mungu kamtunuku kipaji cha uimbaji wa nyimbo za kidunia na kipawa cha kuweza kufanya mambo makubwa ambayo kuna mamilioni ya wasomi wameshindwa kufanya

Usimwangalie Diamond wa sasa bali mwangalie pale alipoanza kuonekana kwenye mwanzo wa msingi wa mafanikio kupitia wimbo wake wa Mbagala..Na baada ya hapo kuzindua brand yake ya WASAFI iliyoanza kama utani

Mtoto wa fukara aliyelelewa na mzazi mmoja, aliyeshindwa kusoma shule bora na pengine kushindwa kumaliza masomo yake kutokana na changamoto za karo sare nk... Mungu hujidhihiri kupitia watu kama hawa
Kumbuka ni mzazi gani ambaye hapendi mwanawe awe kama Diamond? Na ndio maana kila mzazi mwenye uwezo anajitahidi kumpatia mwanawe elimu bora ili aje kuwa fulani katika maisha...

Njia aliyopita Diamond ni ngumu, nyembamba na iliyojaa taabu na misukosuko mingi, lakini kuna sauti na nguvu ya kiroho iliyokuwa inampa hamasa kwa kila hatua aliyopitia.. Ni wengi wamepita na wanapita aliyoptia Diamond.. Wanapambana kufa na kupona, lakini kwa Mungu kila mmoja ana kipimo chake

Diamond sio wa level ya wasanii wengi kwa sasa kitaifa kikanda na hata kidunia.. Usiangalie followers wake tuu mitandaoni, na mali anazomiliki. Bali mwangalie jinsi alivyoweza kutengeneza legacy yake kwa kuwatengeneza wasanii wengine kupitia yeye mpaka wakajulikana mpaka nje ya mipaka ya Tanzania.. Ana hiki kipawa cha kumbrand mtu.

Tuna wasanii wengi na wazuri sana lakini bado hakuna mpaka sasa aliyeweza kufanya aliyofanya Mond..hata kama baadhi wameweza kujisimamia lakini kusimamia wengine wakawa kama wao wameshindwa kabisa.. Kwasasa WASAFI ni BRAND tishio kwenye hilo...!

Nitarejea

Naendelea
Dunia ina wasanii wakubwa wengi, maarufu na matajiri sana waliofikia mafanikio yao kwa njia mbalimbali haramu na halali lakini Mungu akamuinua mmoja tu kati yao naye si mwingine bali ni mfalme wa pop duniani Mwendazake Michael Jackson mwafrika kwa jina la mmarekani mweusi... Ukimwengu utapita vizazi vingi kabla ya kumpata MJ mwingine

Diamond is almost there.. Japo hajafika lakini aliyoyafanya mpaka sasa anastahili kupewa heshima yake kitaifa.. Huyu ni mmojawapo ya tunu za taifa kupitia sanaa ya mziki wa kisasa.. Ni mbunifu, ni mtunzi ni muibua vipaji na mwendeleza vipaji, ni mjasiriamali na yuko very smart kwenye kazi zake..!

Action speak louder than words.. Si muongeaji sana lakini matokeo ya kazi zake yanaonekana.. Ufahari wa kununua vitu vya gharama kubwa ni kiu ya binadamu yoyote yule, lakini vilevile ni kuudhihirishia umma kwamba yeye ni above next level ...!

Ndege yake inakuja iko njiani.. Gharama za kumiliki hiki chombo si mchezo hata kama hataitumia sana Lakini tayari ameshatengeneza historia nyingine ya msanii wa kwanza Tanzania na wachache ulimwenguni kumiliki chombo Kama hicho..

Waswaheli wanasema usimwingilie aliyepewa kapewa! Mond kapewa kama wewe hujapewa mwombe sana Mungu katika ukoo wenu kama si familia basi amuinue mmoja kati yenu atengeneze legacy ya familia na ukoo... ! Chuki dhidi yake ni roho ya washindwa na kijicho..

LA Mwisho wainuliwa wengi huwa hawana maisha mengi.. Lakini kwa Mond tunaweza kumfanyia ibada mwenyezi Mungu amjaalie maisha mengi mengi
Kainuliwa na Mungu yupi?
 
Kainuliwa na Mungu yupi?
Mungu muumba wa vyote, kwa ujumla Mungu ametubariki na kutuinua kwa madaraja tofauti tofauti bt njia ya kuzifikia baraka hizo ndo ipo ktk machaguo yetu, ukichagua njia mbaya ni for ur own risk bt hakuondoi uhalisia wa wewe kuinuliwa na Mungu.
 
Mungu muumba wa vyote, kwa ujumla Mungu ametubariki na kutuinua kwa madaraja tofauti tofauti bt njia ya kuzifikia baraka hizo ndo ipo ktk machaguo yetu, ukichagua njia mbaya ni for ur own risk bt hakuondoi uhalisia wa wewe kuinuliwa na Mungu.
 
Na Mimi sijazungumzia kuimba kwake nazungumza issue ya kuinuliwa na Mungu, Sauli ambaye ni Paulo alikuwa muuaji lakini Ili Mungu amuinue Ilikuwa ninlazina ambadilishe kwanza, Mungu hamuinui mwenye dhambi, Wala mafanikoo ya mwenye dhambi hayahusiani na Mungu, sijazungumzia habari ya muimba kwaya au mhubiri na kumbuka Mungu hamuinui Mtu hivi hivi lazima Kuna kusudi(mapenzi) na kusudi la Mungu ni kuwavuta watu wote wamtumikie yeye.

NARUDIA TENA KWENYE MAFANIKIO YA DIAMOND MTOE MUNGU HAUSIKI
Uyo sauli ulimuona au umesoma kwenye hadithi
 
twende taratibu, ikiwa ukweli/uongo unaoujua unatokana na fikra zisizoonekana, ni wapi unapata nguvu ya kukanusha uwepo wa mungu kisa haonekani kwa macho ya mwili?

hoja yako ni ipi sasa, ikiwa unakiamini A kisichoonekana then unakikanusha B kisichoonekana?
Kwani wapi nimesema nakanusha uwepo wa Mungu kisa haonekani kwa macho ya mwili?

Unaweza kunionesha sehemu hiyo?

Unajua kusoma kwa ufahamu? Au unaniwekea fikra zako tu, na kuzitaja kama mambo niliyoyasema mimi?

Halafu, unaelewa kwamba, ukweli kuwa naujua kutokana na fikra zisizoonekana kwa macho hakuthibitishi Mungu asiyeonekana kwa macho yupo?

Unaelewa kwamba, hoja yako kwamba kwa kuwa mawazo hayaonekani kwa macho ya mwili, basi Mungu asiyeonekana kwa macho hayo pia yupo inahalalisha kusema kwamba, kitu chochote kinachotajwa, ambacho hakionekani kwa macho kipo?

Wewe unakubali kwamba, chochote kitakachotajwa kuwa kipo, ukaambiwa kipo ila hakionekani kwa macho tu, kipo kweli?

Unajua hoja hii inamuwezesha mtu yeyote kusema kitu chochote, hata kile ambacho hakipo, kuwa kipo, ila hakionekani kwa macho tu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom