Diamond Jubilee ya Uhuru wa Tanganyika

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Wakati Tanzania inaadhimisha uhuru wa Tanganyika unaotimiza miaka 60 9 Disemba, 2021, kumekuwa na kupooza kiasi kwamba mitaani, viwanjani na kwenye majukwaa hakuna dalili za kuashiria shamrashamra za muendelezo wa maadhimisho hayo yanayofikia umri mkubwa wa zaidi ya nusu karne. Hii ni bahati mbaya au imedhamiriwa/imepangwa? Ilitakiwa kuelekea 9 Disemba, 2021 kila Wilaya nchini iwe na shughuli yoyote iliyo ndani ya uwezo wake kibajeti; ya kuadhimisha siku hiyo kungali mapema:-

1. Vikosi vyetu vingeshiriki masuala ya kijamii ya maendeleo kama kutoa tiba, michezo, usafi wa mazingira, kuharakisha ujenzi wa madarasa, miradi ya maendeleo, ulinzi ndani ya jamii (kuweka doria na kukamata vibaka nk).

2. Tasnia ya sheria (Mawakili, TLS, Vyama vya kutetea watu wasio na uwezo wa kuweka Mawakili nk) wangeanzisha madawati ya kutoa ushauri wa kitaalam kwa wenye mahitaji ya huduma zao.

3. Mahakama zingetengeneza targets za muda na idadi ya kumaliza baadhi ya mashauri ndani ya muda wa maadhimisho. Iitwe "Uhuru Performance Targets"

4. Taasisi za dini zingekuwa na utaratibu wa ibada maalum kuadhimisha siku hiyo kubwa kwa kuliombea taifa.

5. Wasanii wangeghani wimbo ambao ungekuwa ni logo ya maadhimisho hayo.

6. Taasisi za kitaaluma na kitaalam zingekuwa na vipindi vya makongamano, warsha na mijadala ya kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika.

7. Tungealika Marais toka pande mbalimbali za dunia na hasa mataifa rafiki na ya kimkakati kuja kuungana nasi 9 Disemba, 2021 na tungejipanga kutumia fursa hiyo ya ugeni huo kuwauzia agenda ya uwekezaji nchini kwetu.

8. Balozi zetu zingeandaa makongamano, warsha na mijadala ya kuadhimisha siku hiyo huko huko ughaibuni wakishirikisha wanadiaspora.

9. Ujumbe maalum wa maadhimisho haya ni nini? umesambaa kiasi gani hadi sasa? Watu wameuelewa kiasi gani?

10. Mhimili wa Bunge nao ungeandaa tukio lolote ama la michezo au hata mjadala mkubwa wa kuadhimisha siku hiyo ambayo imetengeneza historia ya taifa letu kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijavyo.

11. TFF ingekuja na michuano maalum (ya timu kutoana papo hapo baada ya kufungwa) ya kombe la uhuru wa miaka 60.

12. Miradi ya kimkakati iliyokaribu kuhitimika ujenzi wake ungeharakishwa kabla ya 9 Disemba, 2021.

13. Tz inaposamehe wafungwa pia ingeomba mataifa ya nje yaliyofunga Watz kwenye magereza yao kutoa msamaha (hasa kwa wanaokaribia kumaliza vifungo vyao) au diplomasia ifanyike kuziomba nchi hizo ili wafungwa wa Kitanzania (hasa wanaokaribia kumalizia vifungo vyao) kurudishwa nchini Tz kumalizia muda wao wa vifungo uliobakia hapa nyumbani Tz. Najuwa kuna suala la bajeti ya kuja kuwahudumia kwenye Magereza ya nyumbani.

14. Mashindano ya magari (safari rally), boti, mitumbwi, baiskeli, kutembea umbali mrefu kwa miguu.

15. Punguzo za nauli (uhuru discount) kwenye vyombo vya usafiri vya umma kama BRT, TRC, ATCL.

16. Uhuru Bundle kwenye vocha za simu.

17. Upandaji miti.

18. Ujenzi wa minara.

19. Maonyesho ya vikosi.

20. Uhuru lager, Uhuru soda, Uhuru stamps.

21. Vipindi kwenye vyombo vya habari kuwahoji mashujaa wanaoendelea kuishi.

22. nk. nk nk.

NB. Lazima wananchi wafurahie uhuru wao.

1636712480973.png
1636712747756.png

1636712506357.png

1636712526465.png

1636712561068.png

Taswira zote kwa hisani ya google.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom