Mlioona clip ya juzi ikimuonyesha Diamond akiwa Rwanda na kukutana na Rais Kagame utaona Approach yake kwa kiongozi huyo ilivyokuwa na kasoro, jinsi Diamond alivyokuwa anamuongelesha Rais huyo ilikuwa kama vile anaongea na Babu Tale au mtu mwenye hadhi ya kawaida tu.
Pia alionekana mara nyingi yeye akimpa mkono Rais na hata kuutikisa. Itifaki inatuongoza kuwa kiongozi ndiye awe wa kwanza kutoa mkono wake, na ni kiongozi tu ndiye atakayetikisa mkono wako.
Simlaumu Diamond ila namshangaa Meneja wake kwa kuwa ninaamini Meneja anatakiwa kujua mambo mengi na sio mambo ya muziki tu. Meneja anatakiwa kuwa mdadisi na anatakiwa kumuandaa boss wake kulingana na nature ya tukio/occasion iliyopo mbeleni.
Tuangalie jinsi wasanii wengi wakubwa wanavyojiweka wanapokutana na viongozi wakubwa wa kitaifa. Mfano Jay-Z au Michael Jackson alipokaribishwa Uingereza na kukutana na King Charles na aliyekuwa Mkewe (Prince Diana). Kwa ukubwa na umaarufu wa Michael Jackson ulivyokuwa lakini alionyesha Approach nzuri sana kiitifaki.
Diamond kwa ukubwa na umaarufu alionao sasa ni dhahiri anahitaji Meneja msomi lakini mwenye exposure kubwa.