GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 309
Kama unakaa Tanzania na hujapata nafasi ya kutembelea nchi ya Rwanda utaingia mkenge wa propaganda zinazoenezwa juu ya udikiteta wa rais Paul Kagame.
Ni kweli kwamba Kagame ana mkono wa chuma hasa kwa waasi wa kihutu waliofanya mauaji ya kimbari na kukikbilia nchi jirani. Lakini kwa muda mfupi sana wa miaka kama 15 ya utawala wake Rwanda ni paradiso ya Africa.
Siamini kama Rwanda kwa mfano linaweza kutokea suala kama hili la viuongo vya miili ya binadamu lililofedhehesha nchi yetu. Pamoja na starehe kubwa zilizo Kigali lakini kila unapogusa kuna ulinzi wa uhakika.
Rwanda ukisimama popote hata polini huwezi kuchukua dakika tano hujaulizwa nia yako. Nchi yetu sasa unaweza kumwaga mamia ya vifurushi vyenye miili ya binadamu ikashinda pale mpaka usiku watu kushutuka.
Tumeongozwa na mfumo dhaifu kwa miaka 9 sasa, mfumo ambao ni rahisi kusikia askari wamekamatwa na meno ya tembo au wameshirikiana katika uvamizi wa benki.
Si ajabu kusikia askari wanavusha madawa ya kulevya uwanja wa ndege au wamekamatwa wakiiba mizigo ya watu bandarini! Ukizingatia yote hayo, si kosa kufikiria kuwa na Kagame wetu. Kagame aliwahi kusema apewe bandari tu, ailishe Tanzania!
Tafakari!
Tunakujua sana wewe ni kibaraka wa PK na ni mnyarwanda. Tuachie yetu nenda kigali