Diallo: Rais ajaye awe dikteta mzalendo

Diallo: Rais ajaye awe dikteta mzalendo

Kagame Haendekezi Ujinga, Ndo Maana Hata Jana Kampiga Chini Waziri Mkuu Wake, Siyo Kama Kwetu Bongo Viongozi Wanabebana Tu Na Kulindana Kwa Maslahi Hao Binafsi
 
Naomba Kagame Aje Tz Asimamie Rasilimali Zetu Kwa Mda Wa Miaka 2 Tu, Maendeleo Tutayaona.!!
 
Tanzania hainna akina Kagame wake? tuache ushabiki wa kipuuzi wa kushabikia watu wasiofaa kwa sababu tu eti wana mkwanja mrefu na hivyo kuamini kwamba watatufikisha kanaani tunayoitaka.Tanzania tunao akina kagame wengi tu,ila kwa sababu mifumo yetu ipo loose sana kuna nafasi kubwa sana ya watu wa ovyo kupata uongozi katika nchi hii ya Tanganyika.Angalia leo hii mara huyu,mara yule kila mu anaamini kabisa ana uwezo wa kuingia kwenye ofisi yetu kubwa kabisa ya nchi hii.Huu ni mzaha mkubwa kabisa!

Kinacho cost hili taifa ni mfumo mbovu wa kupata viongozi tu hawaangalii utendaji wa mtu kikazi wanaangalia nani akiingia atanilinda na kukosekana uwajibikaji na ufatiliaji kisheria ndo mana mambo mengi hayaendi tukipata kiongozi mwenye nia thabiti kama Nyerere asiyecheka na.mtu asiye mzalendo na mwajibikaji tutafika ila tukiendelea na system ya kuyafta uongozi kwa kuangalia masilahi binafsi hatutafika mbali ingawa tuna resources mbalimbali
 
Kama unakaa Tanzania na hujapata nafasi ya kutembelea nchi ya Rwanda utaingia mkenge wa propaganda zinazoenezwa juu ya udikiteta wa rais Paul Kagame. Ni kweli kwamba Kagame ana mkono wa chuma hasa kwa waasi wa kihutu waliofanya mauaji ya kimbari na kukikbilia nchi jirani. Lakini kwa muda mfupi sana wa miaka kama 15 ya utawala wake Rwanda ni paradiso ya Africa.

Siamini kama Rwanda kwa mfano linaweza kutokea suala kama hili la viuongo vya miili ya binadamu lililofedhehesha nchi yetu. Pamoja na starehe kubwa zilizo Kigali lakini kila unapogusa kuna ulinzi wa uhakika. Rwanda ukisimama popote hata polini huwezi kuchukua dakika tano hujaulizwa nia yako. Nchi yetu sasa unaweza kumwaga mamia ya vifurushi vyenye miili ya binadamu ikashinda pale mpaka usiku watu kushutuka.

Tumeongozwa na mfumo dhaifu kwa miaka 9 sasa, mfumo ambao ni rahisi kusikia askari wamekamatwa na meno ya tembo au wameshirikiana katika uvamizi wa benki. Si ajabu kusikia askari wanavusha madawa ya kulevya uwanja wa ndege au wamekamatwa wakiiba mizigo ya watu bandarini! Ukizingatia yote hayo, si kosa kufikiria kuwa na Kagame wetu. Kagame aliwahi kusema apewe bandari tu, ailishe Tanzania!

Tafakari!

Pamoja na kuwa kagame damu nyingi za wahutu zinamusuta, lakini katika swala zima la kiuongozi anafanya vizuri, lazima apewe pongezi, kagame ni kiongozi ambaye anaweza kukemea na viongozi wa chini wakafata maagizo yake, lakini mrembo wetu yy kila mara ni kucheka tu, wakati taifa linaharibikiwa tunaona, hivi, imefika hatua Raisi wetu hawezi hata kukemea, watu wanaiba vingne wanadondosha miguuni mwake lakini hasemi kitu, na kwa sasa amefunga ndoa na china tu wataiba mpaka makalio ya ikulu
 
Sometimes nafikiria kwanini uraisi usiwe kama tasisi fulani yenye board members inayoongozwa na raia wake;ila raisi anaweza kuwa mtu yeyote hata mgeni. Ambaye atakayesimamia mipango, economics structure and development.
Nimefikira hv kutokana na kwamba toka kuja kwa kitu democracy ndani ya Africa mambo ndio yamekuwa magumu kupitiliza.
Wazawa wanaharibu nchi yao kama sio kwao bora hata ya mgeni.
Labda tukijaribu mfumo tu kama wa kocha wa team anatuongoza akimaliza contract anaondoka zake.

Hawa viongozi wa watz na sio viongozi tu hata imekuwa culture ya watz kwamba,kuiba,rushwa na cha juu ni kitu cha kawaida sana.



The king.
 
Kama Kuna Mtu Anamchukia Kagame Basi Atakua Na Mtindio Wa Ubongo
 
Hakuna haja ya kagame, dr slaa atosha. Kaonyesha uwezo na ujasiri mkubwa tangu akiwa bungeni hadi sasa ktk ukatibu mkuu wa chama chake. Wasaliti na masalia ya mamluki yote kayabana mbavu kama alivyoyabana mafisadi ya nchi hii ndani na nje bunge enzi hizo.
 
Ni rahisi sana, hamia tu hapo kigali si mbali sana, hatuhitaji "MTU" kama yeye ile tupate maendeleo, Tanzania will develop in its own way...
 
Thread yako ulikuwa umeamiliza vizuri ila umeharibu kuianza na Kagame, go to hell with your Kagame.Kama unaamini Rwanda ni safi basi hamia huko tuachie Tanzania yetu.Nyie ndiyo wale mnakuwa kwenye ndoa mwisho wa siku mnagombana na mke wako then unaanza kusema ningemuoa Asha yule mwenye wowo kubwa haya yasingetokea.Mwanaume wa ukweli anakaa kimya na anasolve issue yake kimya kimya



Jakaya ni kichuguu cha masika .kagame ni mlima Everest
 
Achane Ujinga Na Propaganda Za Kitutsi,kagame Nijanga Labda Kwa Mtu Anaye Faidika Naye Kama Nimtu Jembe Kwanni Asiruhusu Tume Huru Yamauaji Ya Rwanda?Ama Mnakuwa Wajinga Kwakupewa Pipi!Mh Kikwete Hana Damu Ya Mtu,atakama Anaudhaifu Wake Kiuchumi Anaweza Kurekebishika,je Roho Za Watu Kagame Anazotoa Unaweza Kuzirejesha?Na Kiwete Auwe Wapinzani Ili Uchumi Ukuwe?Acheni Propaganda Za Kitutsi Kusafisha Mtu,kagame Ni Hatari Nani Nyoka!
 
Hakuna haja ya kagame, dr slaa atosha. Kaonyesha uwezo na ujasiri mkubwa tangu akiwa bungeni hadi sasa ktk ukatibu mkuu wa chama chake. Wasaliti na masalia ya mamluki yote kayabana mbavu kama alivyoyabana mafisadi ya nchi hii ndani na nje bunge enzi hizo.
Ah! Chama kinakufa mikononi mwake we bado unamsifia tu, mara kajikopesha 20m kinyemela bado hujaona udhaifu wake tu
Taja mwengine huyo hafai.[emoji547]

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom