Diallo amlipua Lowassa

asante mzee Diallo mfukunyue huyo low-asa mapema wananchi tupate kumfahamu.

Asante ya nini?afukunyue nini ? Wananchi wapi? ni wewe pekee na wajinga wachache sana wanaweza kukaa na kumsikiliza Dialo, usifikiri kwa kisogo jitambue.
 

Mkuu,,nawewe ndo umendika nn? yaani nyinyi hamtaki Wananch wajue madhambi ya wagombea wenu mnataka muendelee kuwauzia watu mbuz kwenye gunia km 2005 kwa lipi mtu kutoka ccm akaweza kuisaidia Nch hii mnadhani bado watu wengi ni mapunguaan? Tunachojua nyote mnaongozwa na SIASA za TUMBO
 
Uzuri ni kwamba Lowassa anawapuuza watu kama hawa wakina Diallo hana muda wa kubishana nao, maana siyo level zake wataangaika sana ila mwisho wa siku time will tell mwakani siyo mbali

Ukimya wa EL Kwa ma snitch kama hawa ni njia bora na sahihi, watahangaika sanaa wanachokifanya ni kama kupiga ngumi kinyago.
 
Rais zitto kabwe tu hawa wengine msiba tu..sasa yeye diallo kama aliyajua haya kwa nini asiyaseme kitambo na kuyaripot sehemu husika?

Safi sana mkuu, zitto ndiye raisi. sema umri tu.
 

Je ? Unawajua wana ccm wote waliotangaza nia ? Je? Umejiuliza ni kwa nini Lowasa pekee ndiye anaandamwa ? Hayo unayoyaita Madhambi hayapo kwa hao wengine ?!
 
Diallo mlia njaa tu kanafiki ka siku zote.
maovu yake tumeweka ubavuni et leo anatumiwa na kambi ya mtu fulani kumchafua lowasa!
hiyo star tv na redio zake zimetokea wapi!
AFANYE BIASHARA, SIASA IMEMPITA NYUMA

Nimepitia kwa ukaribu uzi huu wa vita ya maneno kati ya timu EL na Diallo. Watu wameacha kujadiri kilicho wekwa mbele yetu na kujikita kwenye personal issues. Je ni kweli EL alikwamisha dili la ccm na MTN? Je afya ya mamvi ni mgogoro? Je ni kweli EL aliwasaidia vodacom SA na akapatiwa hisa za vodacom tz? Je watoto wa EL ni super-dealer wa voda? Hayo ndo tujadiri hapa tuache kuwazia makalio. Kwa ufahamu wangu vodacom tz inamilikiwa na vodacom SA, Roastam aziz, peter noni na alphatel!! Sasa alphatel ni nani? Watetezi wakina pasco watusaidie
 
[h=2]uanguka kwa Hekalu La TB Jushua na Utabiri wa Lowasa kuwa rais!![/h]
Edward Lowassa alianza na Babu wa Loliondo ambapo Marehem Askof Thomas Laizer KKT alikuwa mstari wa Mbele .
Wakati Tiba la Kikombe ikiyumba kutokana na mashambaulizi ya baadhi ya watumishi wa Mungu waaminifu, Lowassa alikimbilia haraka Nigeria na kule ukatoka utabiri kuwa ,Lowassa ndiye Rais 2015.

Baada ya hapo nguvu za Lowassa zimeimarika sana kama kazi ya TB ilivyoimarika hadi CCM wanamuogopa Lowassa.

Kwa sasa Jengo la Tb Joshua limeporomoka na halitainuka tena na pamoja na TB Joshua kutabiri mambo mengi kwa kutumia miungu yake lakini hakuweza kutabiri anguko la jengo lake!!
Sasa yamkini Lowassa ambaye ni muumini wa TB Joshua ajitokeze kwenda huko kutoa pole kama alivyotoa msikiti wa idrisa

Hata hivyo ni hatima ya imani ya Lowassa kufuatia utabiri wa TB ambaye ameshindwa kutabiri anguka la Jengo lake??

Edward Lowasa, atabiriwa na TB Joshua?


13/06/2011 by Strictly Gospel
41

Pichani Lowasa akiwa kanisani kwa TB Joshua kama anavyoonekana kwenye Emmanuel TV, 12 June 2011
MBINU za Edward Lowassa kutaka kurejea kileleni katika ulingo wa kisiasa zimemnasa mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo, imefahamika. Beatrice ambaye alikuwa akijitambulisha kuwa mmoja wa “wapambanaji dhidi ya ufisadi,” waliopachikwa jina la “Mitume kumi na miwili,” sasa anatajwa kuhamia rasmi mtandao wa Lowassa. Gazeti hili limepata ushahidi wa maandishi ya mkono wa Beatrice mwenyewe yanayoonyesha kuwa amekuwa mfuasi muhimu wa Lowassa kiasi cha kushawishi wengine kujiunga katika mtandao wake. Akiandika kwa Pindi Chana, mbunge wa Viti Maalum (CCM), tarehe 14 Februari mwaka huu, Beatrice alieleza mambo matatu katika ujumbe wake kwa Chana. Kwanza, kumshukuru Chana kwa kukubali kulinda kura zake. Pili, kumshawishi kumuunga mkono Lowassa. Tatu, kumweleza juu ya ulokole wake na “mtumishi aliyepakwa mafuta” kutoka Nigeria. Beatrice anamwambia Chana kuwa Lowassa ndiye kampeni meneja wake. Hii ilikuwa katika uchaguzi wa makamishina wa Bunge; nafasi aliyogombea na kushinda. “Mungu ni wa ajabu, (Lowassa) ameniombea kura pasipo maelezo. Ameandaa lunch na dinner (vyakula vya mchana na usiku) ambako amekuwa akiniombea kura. Ana njia za ajabu za kufanya mambo. Ahsante kwa kukubali kuhesabu kura,” inasema sehemu ya ujumbe huo. Chana, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, ndiye alihesabu kura za Beatrice kwenye uchaguzi wa kutafuta makamishina wa Bunge. Ni kwenye ujumbe huo ambamo Beatrice anatoboa kuwa siri ya ushindi wake ni Lowassa aliyekuwa kampeni meneja wake. Katika kusisitiza hoja yake, Beatrice anasema, “Nimezungumza na TB Joshua wa Emmanuel TV Nigeria aliyenipa unabii kuwa rais ajaye Tanzania ni Edward Lowassa, nikamuambia haiwezekani kwani amechafuka sana.” Anasema Joshua alimjibu, “…alikuwa amechafuka sasa amesafishwa kwani katubu. Akaniambia his past is over (maisha yake ya nyuma si kitu). Akaongeza kwa kusema, wewe Beatrice ningeangalia your past (maisha yako ya nyuma) pengine nisingekuombea kabisa. Akasema my past is over (hajali maisha yangu ya nyuma),” inasema sehemu ya ujumbe huo wa Beatrice. Hata hivyo, Beatrice hakueleza katika waraka wake kwa Chana maisha yake ya nyuma yalikuwa vipi. Wala hajaeleza alifanya nini, hadi kuamini kuwa kama Nabii Emmanuel angeyatazama, basi asingemuombea. Kuvuja kwa taarifa hizi kumekuja wiki tatu baada ya Lowassa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje. Mume wa Beatrice, William Shelukindo alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo iliongoza harakati za kuundwa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba tata wa Richmond. Ni taarifa ya kamati hiyo iliyosababisha Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa waziri mkuu, Februari 2008. Kwa mujibu wa watu waliokaribu na Beatrice na kwa ushuhuda wake mwenyewe, mwanasiasa huyo ameamua kujisalimisha kwa Lowassa kwa kile kinachoelezwa kuwa “Lowassa ndiye rais ajaye wa Tanzania.” Aidha, kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja huku kukiwa na juhudi kubwa zinazofanywa na Lowassa na kundi lake kutaka kujisafisha kwa lengo la kujitosa katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2015. Miongoni mwa mikakati aliyojiwekea Lowassa na kundi lake ni kujitokeza katika maeneo yote muhimu na kutoa kauli ambazo zitafanya wananchi waanze kumkubali kuwa ni kiongozi anayefaa. Katika kutekeleza mkakati huo, Januari mwaka huu, Lowassa alijitokeza kuzungumzia vurugu zilizotokea mkoani Arusha zilizotokana na mvutano katika uchaguzi wa meya wa jiji hilo kati ya CCM na CHADEMA. Katika mnyukano huo, watu watatu walipigwa risasi na polisi na kufariki dunia baada ya polisi kutumia nguvu isiyo ya kawaida kuzima maandamano ya CHADEMA. Kauli hiyo ya Lowassa ilikuwa tofauti na msimamo wa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtaka kuwasilisha maoni yake katika vikao vya chama badala ya kutumia vyombo vya habari. Kauli nyingine ya Lowassa ilihusu nyongeza ya viwango vya mishahara kwa wafanyakazi, kutokana na kile alichoita mfumuko wa bei kuwa mkubwa. Bali wiki moja iliyopita, Naibu Katibu Mkuu wa vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicholas Mganya alimtuhumu Lowassa kwa kutoa kauli hiyo akisema ana ajenda ya siri nyuma yake. Mgaya alisema TUCTA haihitaji msaada wa Lowassa katika kusimamia madai yao. Alisema “mbunge huyo wa Monduli inaonekana ana ajenda yake mgongoni.” Hatua nyingine ya Lowassa katika kujikarabati kisiasa ni kugombea na kupata nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Lowassa amekuwa pia akihudhuria hafla nyingi, hasa za madhehebu ya Kikiristo (KKKT) ambao anaonekana akitoa maoni mbalimbali kama ilivyokuwa Jumapili iliyopita ukumbi wa Dimaond Jubilee kwenye uzinduzi wea albamu ya moja ya kwaya za injili. Kwenye kusanyiko hilo, Beatrice naye alikuwepo. Lowassa alimtaka asome maoni ya gazeti la The Citizen juu ya ushirikina uliokithiri nchini; jambo ambalo Lowassa alizungumzia kwa urefu. ----------- lilipowasiliana na Beatrice ili kupata maoni yake juu ya ushwahiba wake mpya na Lowassa, mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo: Mwandishi: Tusaidie maelezo kidogo juu ya ujumbe uliomwandikia Mheshimiwa Pindi Chana kumjulisha kuwa uliambiwa Edward Lowassa atakuwa rais. Ni kweli? Beatrice: Barua ameandika nani na umeipata wapi? Mwandishi: Hii barua fupi – memo ndani ya Bunge, uliposema Mheshimiwa Lowassa ambaye amesimamia vizuri kura zako za ukamishna wa Bunge. Beatrice: Sina taarifa hiyo. Wala siikumbuki. Unajua ndani ya Bunge tunaandikiana mambo mengi, tena mengine ya utani tu. Na mimi na Mheshimiwa Chana sote ni “walokole,” tunafanyiana utani sana. Mwandishi: Kwani mheshimiwa Shelukindo, mkiwa ndani ya bunge kuna utani mwingi, kwamba huwa mnaandikiana utani sana? Beatrice: Kabisa, unajua tunaandika mambo mengi. Na kama unaandika kwa utani kwa mwenzako inabaki hivyo ni utani tu. Sasa tatizo hao wanaowaletea mambo haya wanatumia mambo haya kutafuta mipango yao ya kufikia mwaka 2015. Alisema, “Mimi najua hakuna anayenibeba ndugu yangu. Mimi ni very solid (ngangari), sibebeki. Nakwambia, mbona mimi nina nguvu nyingi mimi mwenyewe; sihitaji kubebwa. Najua wanajaribu kuonyesha tunabebwa, lakini huo ni ujinga wao wa kufikiri. Mwandishi: Mheshimiwa Shelukindo, kwani nyie waheshimiwa huwa mnatafutana (kufitiniana)? Beatrice: Hiyo inafanyika sana, watu wakishakuwa na mambo yao wanatumia wengine kutimiza dhamira zao. Lakini mimi ninafikiria wananchi. Nimeshaamua kwamba Beatrice nashughulikia shida za wananchi jimboni. Ninatafuta njia za kuwaondolea umasikini, njaa na mambo kama hayo. Sasa wengine wanatafuta tu pa kunishika. Mwandishi: Kwa hiyo Mh. Lowassa ndiye alikuwa kampeni meneja wako katika kutafuta ukamishna pale bungeni, au siyo Mheshimiwa? Beatrice: Lakini kama anafanya kazi ya kampeni vizuri; ni vizuri tu. Isipokuwa kila mtu anajichukulia mwenyewe alivyo. Mimi ni mtu wa kazi sihitaji kusimamiwa hivyo. Na hebu tujadili hili; unajua kaka nyinyi mnafanya kazi kubwa. Sasa hii kusikia, sijui ----------- hivi, sijui hivi, pengine kuna watu wanachomekea vitu vyao. Tunapenda kazi yenu. Mwandishi: Mheshimiwa nakushukuru sana. Beatrice: Karibu sana tutafanya kazi pamoja. Akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, mume wa Beatrice, William Shellukindo, alikuwa na msimamo mkali dhidi ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini na hiyo ndiyo inayoelezwa kuwa sababu ya kushindwa kwake ubunge katika mchakato wa ndani ya CCM. Shellukindo alikuwa mbunge wa jimbo la Bumbuli mkoani Tanga kwa zaidi ya miaka 20, alishindwa katika kura za maoni na January Makamba, mtoto wa katibu mkuu wa CCM anayetajwa kuwa mfuasi wa mtandao wa Lowassa. S0urce by ----------- – 9 March 2011
 


Hakuna jambo linalostaajabisha na kuudhi kama pale mtu anapoacha kufanya counter argument na badala yake akaanza kumjadili au kum-attack mtoa mada. Hii ni tabia ya kijinga sana. Ile sifa ya jamii forums kama jukwaa la great thinkers inapotea kwa kasi ya ajabu.

Mtu akitoa madai/ hoja ya uongo, jibu kwa nguvu ya hoja kuonyesha ukweli/ usahihi ni upi. Toka enzi na enzi hii ndio namna mijadala ya watu wazima na wasomi ilivyokuwa inafanyika,hii ndio namna pekee na halali kimantiki ya kujibu hoja mtu aliyepevuka kiakili anayotumia. Anything more or less than that fact is nothing but rundo kuuuuubwa la takataka na uchafu.
 
Siamini kama kweli ni Dialo aliyeandika haya, Nimesoma na kuishi kwa muda na wasukuma, ni watu smart sana . Kama ndiye aliyeandika haya amepotoka sana na hana pa kuficha uso wake.
 
Jambo muhimu kuelewa ni kuwa ni kuwa Diallo is just another culprit!! haihitaji akili ya chuo kikuu kufahamu kuwa hili ni pandikizi lililofanikiwa kutinga katika safu za uongozi bahati mbaya!!. Diallo mama kuku wa shinyanga uliyemtelekeza hadi akapata stroke yupo au ameisha aga dunia! CCM imejaa viatu!!
 
hivi lowassa ameshaanguka mara ngapi jukwaani?majizi mkija kuacha kulumbana mtaikuta chadema ikulu...
 

Kwanza Tengua Kauli yako . Hii si vita ya Maneno Kati ya Lowasa na Dialo . Kumbuka hapa Lowasa hajaongea kitu yupo Kiimya tu, sasa watu wapo busy kujadili huu uzushi na Uchanganishi mpya Ulioanzishwa na Dialo ambaye anaonekana kucopy Yale Yale ya mtaani kisha kuja na Uongo wa kawaida akidhani utawasaidia kumshusha Chini Lowasa. Ebu jaribuni kutafakari ni kwa nini kila siku Lowasa , lowasa ? Wanaogopa nini ? Waacheni wananchi ndio wataamua Rais wao.
 

hakuna cha lengo wala nini, mbona ulipohama ulituambia........kamanda kushindwa katika maisha sio wajibu wa serikali 100% bali kazi kubwa ya serikali ni kuweka miundombinu tu, zaidi ya asilimia 96% is your job kuhakikisha u tackle poverty
 
Dialo anaoneka mpuuzi tu, mbaya zaidi mtu unayemshambulia hana muda na wewe, Dialo wewe pambana kurudisha ubunge wako mipasho haitakusaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…