Dharau kama hizi sio nzuri kabisa

Dharau kama hizi sio nzuri kabisa

Jerry santonga

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2014
Posts
647
Reaction score
566
Habari za muda huu makamanda,
Ni matumaini yangu mpo vyema kama kuna mgonjwa basi Mungu amponye
Haya twende na hii

Leo mida ya saa tatu tatu hivi baada ya kumaliza kucheki game la watani wa jadi simba yanga nkarudi na furaha ya arsenal wangu. Sasa baada ya kucheck game nikawa na wana tunakatisha mitaa tunarudi ghetto sasa kuna familia imetoa vyombo nje na vitu vya ndani vingine sasa walikuwa wanasaidiana kuweka vyombo kwenye kirikuu fresh

Ikafikia zamu ya kupandisha kabati la nguo ***** kitu mninga mjerumani wazee wa kazi tukaombwa msaada tuwasaidie tukawa wanne mimi na rafiki yangu flani hivi yule mama na mumewe kijana flani hivi wote vijana tu

Sasa wakati tunalitoa ndani zigo remix la kabati hilo mninga mjeruman mwanamama akawa anasaidia mumewe akamwambia acha nenda ndani si tutalifikisha kweli na sisi tukachagiza shem acha linafika manina sasa sijui hakusikia yule. Mdada akaambiwa tena acha tu na mumewe khaa akamjibu usijali mume mi naweza si nawasaidia alafu hili zito ujueeee

Mzee baba hiyo mineno iliyomtoka mchizi acha ninukuu maana naona ni kama dharau sana aisee kwan wanawake wanaweza
MCHIZI ALISEMA"ALAFU WEWE SI UMEAMBIWA UACHE HAPO NGUVU UNAYOITOA HAITINGISHI HATA MZANI WA KUPIMIA DONA UNAJISUMBUA TU UNASEMA UNAWEZA NINI WEWE WE SI MWANAMKE TU ARRRGH MTU UKIWEKEWA SAMBUSA UTULIE TU HUNA NAMNA WEWE NI WA KU...AKASONYA

Mwisho wa kunukuuu mwanamke wa watu akazama ndani kwa aibu dah sie tulivyolipandisha hatukutia hata neno ila tulisemezana jamaa amemdhalilisha mkewe sijui au hawala yake

NB.
Tusiwadharau wanawake..mambo ya kumwambia mtu amewekewa sambusa au kitumbua sio mazuri hasa inapokuja kwenye utendaji kazi...
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom