Dharau: Airtel wameanza kufungia laini zisizosajiliwa

Akilitime

JF-Expert Member
Dec 27, 2017
581
757
Naomba kujua, hawa Airtel wanapinga agizo la Mheshimiwa?

Mbona wameanza kufunga line kinyume na tamko la Rais? Mimi ni mhanga wa kufungiwa huduma.

Ushauri: kama hujasajili wahi mapema ili kuepuka usumbufu wa kukosa mawasiliano hapo baadae.

Poa kwa NIDA ingekuwa bora wakaongeza kasi ya utoaji namba za vitambulisho ili watu wakasajili line zao.
 
Akilitime, Mimi ni mmoja kati ya wanaounga mkono dharau za Airtel kwakuwa unaonekana wewe una dharau zaidi. Kauli ya kusema "Airtel wanafunga line kinyume na tamko la 'Rais wenu'" kinaonesha kiasi gani unahisi ikulu hapana mtu pale.

Hata kama humpendi, unapomuadress Rais kwa maana ya taasisi inabidi umtambue tu hakuna namna. Hapa ni sawa na mdogo/mkubwa wako akija akakukuta unafanya tofauti halafu akwambie "mbna unafanya kinyume na maagizo ya baba yako" it means unajitoa kwenye hiyo familia. Hii kauli yako itapendeza zaidi kama wewe si Mtanzania au umekosea bahati mbaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kukuta mamlaka ya mawasiliano ilipeleka WARAKA kwa makampuni ya simu kuhusu kujisajili.

Lakini rais akatoa tu tamko bila makampuni kupelekewa waraka kwa ajili ya kubatilisha waraka wa mwazo.

Hapo ndio mwanzo wa CONTRADICTION.
 
Back
Top Bottom