Dhana ya umaskini

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Kiasili hakuna kitu kinachoitwa umaskini. Haukuwepo dunia ilipoumbwa.

Umaskini ni zao la akili za binadamu. Ni zao la gunduzi za binadamu. Kwenye asili hakuna umaskini.

Ni sawa sawa na kusema kwamba kuna pundamilia maskini, simba maskini au kondoo maskini.

Lakini kwakuwa binadamu anafikiri umaskini umekuja.

Ufahamu wa binadamu ndio umeleta umaskini. A very distinguished mark between Animal and human beings. It is mind and unfoldment of it.

Umaskini ni zao la binadamu. Haupo kwenye nature. Haupo kwa wanyama wengine ila kwa binadamu tu, sababu ya uwezo wake wa kufikiri, na unatofautiana kati ya taifa moja na jingine, kutokana na uwezo huo huo wa kufikiri.

Hii unfoldment of the mind or evolution of the mind inatofautiana kati ya watu na watu au Taifa na Taifa. Swali la kujiuliza kwanini hii evolution of the mind iliwahi kwa baadhi ya mataifa kuliko mataifa mengine hivyo kuleta maendeleo haya tunayoyaona na kuyaita maendeleo?

Bila hii evolution of the mind and unfoldment of it, Binadamu angekuwa kama mnyama mwingine. Infact binadamu hakui mwili tu bali na akili yake pia, inayomfanya kutawala mazingira yake.

Ni kweli kwamba binadamu wa kwanza walikuwa wakiishi porini na walitofautiana kidogo sana na wanyama kwenye uwezo wao wa kutawala mazingira. This evolution of the mind bring to us all these things we see now.

Swali la kujiuliza hii evolution of the mind itatupeleka hadi wapi na intention yake ni ipi?

Tunajua ufahamu wake binadamu ndio umeleta umaskini na matabaka. Otherwise tungekuwa kama wanyama wengine ambao miongoni mwao hakuna maskini na wote wako sawa. Na asili huwapatia kila wqnachohitaji.

The fact is ; There is something inside of Man which is bigger than man himself. This thing help a man to create things and it evolve over the ages. Sisi waafrika hatulielewi hili. This power within a man and in nature dominate all things.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom