Dhana dhanifu juu ya kutekwa Mo Dewji

Dhana dhanifu juu ya kutekwa Mo Dewji

Ma

Makonda ni mwenyekiti wa kamati ya usalama na ulinzi wa mkoa wa mwanza chochote anachosema ni ripoti aliyopewa na walioko chini yake means kamanda wa mkoa na wenzake sasa anakuaje sourse ya habari?

Hizi chuki zitatuua
Nimekuelewa vyema na huyu wa daa anaitwa nani?.
 
Moderator huu ni uchambuzi wa viashiria mbalimbali na uhalisia wa tukio baada ya Mo kutekwa hivyo naomba msiunganishe huu uzi na zile nyingine zinazoripoti

Habari huanza kama tetesi ama uvumi hilo limekwisha fanyika
Baada ya tetesi ama uvumi kuthibitika ni kweli habari husika hukoma kuwa tetesi ama uvumi.

Kinachofuata baada ya hapo ni breaking news hapa kila mtu huongea lake la masikitiko la majonzi la huruma nknk....tuko kwenye hatua hii kwa sasa

Vumbi likishatulia ndio uchambuzi huanza..na sasa ni muda wa uchambuzi na sio tetesi wala breaking news tena!

MO KATEKWA! ndio habari kubwa kwa asubuhi hii ya tarehe 11.October.2018
Kila tuko linalotokea huwa na mlolongo huu
Wazo
Sababu
Mchoro/mpango
Muda
Wahusika
Vitendea kazi
Bajeti
Uchaguzi wa eneo la tukio
Nani afanye nini nknk

Matukio ya utekaji huambatana na
Visasi
Fidia
Vita ya kibiashara
Mambo ya kisiasa
Mapenzi na mahusiano...nknk

Kutekwa si jambo geni masikioni mwetu ,wengi walishatekwa ....wachache wkapatikana wakiwa hai na wengine wafu....wengine hawakupatikana tena.

Kwanini MO?
Huyu si mtu mdogo ni mfanyabiashara mkubwa mwenye mafanikio mengi...amewahi kuingia kwenye kumi bora na ishirini bora za matajiri vijana duniani, Afrika na hata katika mgawanyo wa kikanda... Kumteka huyu maandalizi yake si ya kitoto
Wiki moja Kabla nilimuona akifanya mahojiano na mwandishi mmoja ..sikumbuki ni kituo gani cha luninga ...lakini katika mahojiano yale alitaja mafanikio yake mengi na pia kuelezea ratiba yake ya siku nzima na wiki pia
Kwa maneno yake mwenyewe hii ndio ratiba yake

Anafika ofisini saa 12 asubuhi na kuanza kusoma na kujibu emails mpaka saa mbili asubuhi
Baada ya hapo hujipanga kuingia kwenye vikao vya bodi mbalimbali kuhusiana na makampuni yake.

Akimaliza kwenye saa sita nadhani hupata wasaa wa kupitia magazeti mbalimbi,kupumzika na ikifika saa nane HUENDA GYM kupata lunch na baadae kurudi ofsini mpaka usiku...weekend hukutana na marafiki na hupata muda wa kuwa na familia pia.

Leo alfajiri katekwa akienda/akitoka gym! Ni wazi kwenye yale mahojiano alidanganya kuwa anaendaga gym mchana...hii haina shida ni mbinu shirikishi ya kujilinda

Je, watekaji wanataka nini kwake?

Ni wazi hawana nia ya kumdhuru la sivyo wangeshamaliza mchezo pale pale walipomtekea.

Kwa jicho la haraka hawa wanataka fidia (ransom )na kama hili likithibitika basi tutakuwa tumeingia kwenye zama mpya mbaya sana kiuchumi na swala zima la uwekezaji....

Je kwasasa yuko wapi?
Its a million dollar question...lakini watekaji ni watu waliojiandaa hasa...eneo walilomtekea lina ulinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi yenye vifaa vya uhakika lakini pia kuna CCTV CAMERAS...hivyo basi walijua wanachokifanya na hata kuruhusu waonekane kama ni wazungu ni cover up nyingine...siku hizi kuna vinyago vya kila aina.

Kiinteligensia Dar ni padogo sana na eneo letu la bahari liko huru mno...ni rahisi mno kutega speed boat ufukweni maeneo ya Coco na kuondoka na mtu salama salimini...

Neno la Makonda
Kwa kawaida baada ya mtu kutekwa watu husubiri masaa24 kusikia watekaji watasema nini...kipindi hiki cha mpito mamlaka husika hukaa kimya kabisa zikifuatilia kwa Karin kila taarifa...sanasana zitatoa tu taarifa kuthibitisha tetesi...huwa hazikurupuki kupayuka!

Ndugu yetu huyu kwa nafasi yake ya mkuu wa mkoa kasema WALE WAZUNGU NI WAGENI!
Kajuaje kama ni wazungu kweli
Kajuaje kama ni wageni!?
Ana taarifa zao?
Wamekamatwa?
Kwa kupayuka huku mtu anaweza kuharibu kila kitu ama kugeuka na kuwa chanzo cha habari na kuacha mashaka mengi.....

Mpaka kinachosemwa ni Mo katekwa na majambazi...lakini bado hatuna hakika kwa asilimia zote ninini hasa kimetokea....wakati tukiendelea na huu mjadala tuwe makini na kauli zetu,tusije tukajikuta ni sehemu ya ushahidi..

Tumuombee...tuiombee familia yake ndugu jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha sintofahamu kubwa
s
 
KATEKWA NA WAZUNGU...hapo naunganisha kidot.com..kauli za wazungu ,,MATAMKO ya wazungu,,,n.g.o xxx,,,au ile union inavyosimama agaist Gov...KUNAMIJITU INAPENDA WAZUNGU we acha tu...xzilion through jews,,metsada ,,nimeandika utumbo mtupu.
Duuuu[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
 
Behind the scene hii familia sio takatifu wala safi kivile imefanya mengi mabaya ya kutisha ili kulinda utajiri na himaya yao....tu sympathise lakini tuwe na tafakuri[emoji848][emoji1562]
Hakuna tajiri msafi Mkuu ,kulinda himaya yako you will do whatever it takes hivyo hili sio hata la kujadili .
 
Ma

"Makonda ni mwenyekiti wa kamati ya usalama na ulinzi wa mkoa wa mwanza"

chochote anachosema ni ripoti aliyopewa na walioko chini yake means kamanda wa mkoa na wenzake sasa anakuaje sourse ya habari?

Hizi chuki zitatuua


Hapo nilipoweka fungua na funga semi kuna walakini kidogo. Au labda wakuu mimi nipo nyuma sijui lolote?
 
Nimeiona video moja kwenye ukurasa wa Instagram,wa yule dada wa Marekani,kama Mkuu wa mkoa amesema "amepatikana na wahusika mamekamatwa"
Usimnukuu vibaya mkuu wetu wa mkoa, sikiliza vizuri maneno yake. Aliposema " amepatikana" alimaanisha uchunguzi unaendelea, aliposema wahusika nao wamekamatwa alimaanisha uchunguzi unakaribia kufika mwisho...ametumia kiswahili cha kiuchunguzi sasa sisi raia wa kawaida tusiojua kiswahili vizuri tukamnukuu vibaya
 
Hii ni series ileile ila naona episode hii in walakini kidogo...

Mkuu anasema amenukuliwa vibaya wakati taarifa ameongea live na sio hata kwa maandishi lakini bado amekanusha

niishie hapo nasubiri muda useme kweli
 
Me nadhani sio muda wake huu, kujivika unform za mamlaka husika...naona ingekuwa vema kama tungejaribu kukaa kimya kwanza, na kutoa room kwa mamlaka husika ili iweze fanya kazi yake vema.......then ndipo tunyanyue vidole juu na kukemea ukakasi utakaonyeshwa au kupongeza juhudi bora zilizofanywa na mamlaka husika katika sakata hili.
 
Ma

Makonda ni mwenyekiti wa kamati ya usalama na ulinzi wa mkoa wa mwanza chochote anachosema ni ripoti aliyopewa na walioko chini yake means kamanda wa mkoa na wenzake sasa anakuaje sourse ya habari?

Hizi chuki zitatuua

Fal.a kweli wewe, toka lini Mkuu wa mkoa wa Dar awe mwenyekiti mwanza
Wewe nawe ni ZeRO brain kama unayemtetea, Hujui lolote unawaza tu buku saba yako ya Lumumba.

Acha kukurupuku, Kiazi wewe
 
Behind the scene hii familia sio takatifu wala safi kivile imefanya mengi mabaya ya kutisha ili kulinda utajiri na himaya yao....tu sympathise lakini tuwe na tafakuri[emoji848][emoji1562]
Kwa nn unawahukumu unayajua hayo mabaya waliyofanya mkuu
 
[emoji116]
IMG-20181011-WA0012.jpg
 
Usimnukuu vibaya mkuu wetu wa mkoa, sikiliza vizuri maneno yake. Aliposema " amepatikana" alimaanisha uchunguzi unaendelea, aliposema wahusika nao wamekamatwa alimaanisha uchunguzi unakaribia kufika mwisho...ametumia kiswahili cha kiuchunguzi sasa sisi raia wa kawaida tusiojua kiswahili vizuri tukamnukuu vibaya
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aisee.. haihitaji kiwango cha PHD ili kuweza kutambua kuwa wananchi wa TAIFA hili hatuko salama". hili tukio ni baya mnoo" linafaa kulaaniwa maana linahatarisha usalama wa wekezaji"..., wawekezaji wengi watalikimbia hili taifa na waliokuwa na shauku ya kuwekeza nchini hawato wekeza tena",....

Maana hakuna muwekezaji ambaye atakaye kuwa tayari kuwekeza kwenye taifa ambalo ni tishio kwa usalama"...., hivi punde mtakuja kusikia Tanzania ikitajwa kuwa ni miongoni mwa nchi ambazo sio salama kwa watu kuishi ....


oohhhh jiwe walipeleka wapi hili Taifa
 
Back
Top Bottom