kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,793
- 5,042
Dhambi ya usaliti, mbaya dhambi ya usaliti, yaani dhambi ya usaliti ndio dhambi kubwa kwenye usaliti. Yes, dhambi ya usaliti. Mwaka 1960, Kasavubu alimsaliti Patrice Lumumba, akashiriki kupanga, kuinjinia na kuratitbu kuuawa kwa Lumumba, sio kuuwawa tu, bali mauaji ya kinyama, mipango yote alipewa Mobutu kuratibu.
Baada ya Lumumba kuuwawa Kasa-Vubu alimpandisha cheo jeshini Mobutu kuwa Luteni Jenerali, na kumteua kuwa mkuu wa majeshi, yote hayo yalifanyika mwaka 1965. Ona Sasa usaliti unavyotafuna, Mobutu baada ya kupandishwa cheo nae akampindua Kasavubu siku 6 baadaye. Ukila nyama ya mtu huwezi kuacha.
Siku 2 baada ya Kasavubu kupinduliwa Mobutu akapanga njama ya kumkamata Kasavubu, Kasavubu aliposikia akataka kutoroka, Mobutu akamkamata na kumuweka Kasa-Vubu chini ya kizuizi cha nyumbani (under house arrest). Alikaa hapo kwa miezi 15 mpaka alipokubali kutangaza kustaafu siasa na kutojihusisha na siasa, akapigwa kufuli, ubaya hauozi.
Kasavubu alipewa sharti la kuishi nyumbani tu yaani katika shamba lake huko Mayombe, hakuna kutoka nyumbani bila kibali cha Mobutu. Kasa-Vubu alifariki katika hospitali ya Boma miaka minne baadaye yaani mwaka 1969, baada ya kuugua kwa muda mrefu na kukosa uangalizi. Hii ndio dhambi ya usaliti.