Dhambi ya kubagua wapinzani inawatafuna CCM

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,307
12,604
Kuwepo kwa vyama imara vya upinzani nchini na wabunge wengi wa upinzani bungeni ndiko kunakowaunganisha wanachama na wabunge wa CCM na kujiona ni kitu kimoja dhidi ya vyama na wabunge wa upinzani. CCM kwa kufanya dhambi ya kuviua vyama vya upinzani na kuwa na bunge la Chama kimoja kunasababisha wabunge wa CCM waanze kujitafuta na kujikita kumbe Kuna wabunge wa CCM kutoka Zanzibar, kutoka Mtwara corridor, kutoka Kanda ya kati, kutoka Kanda ya ziwa, kutoka kigoma, kutoka kanda ya mashabiki, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya juu kusini. Ubaguzi wakishaufanya wataendelea kujitafuta na kujikuta kumbe Kuna wanaCCM wakristo na waislamu, wakatoliki, walutheri, waanglicana, wasabato, na Wanamaombi. Dhambi ikikolea zaidi Watazidi kujitafuta na kujikuta kumbe Kuna wanaume na wanawake ambao ni wanaCCM.

Wakati dhambi ya ubaguzi ikitendeka wale wanaobaguliwa watabaki kuwa salama na wamoja kifikra na kimkakati, na Watazidi kupata nguvu kubwa za ajabu kutoka kwa watanzania na hata wanaCCM wenyewe wa kutoka kwenye makundi yanayojihisi kubaguliwa ndani ya serikali ya CCM kimiradi ya maendeleo na uongozi.

Hii sio theory yangu Mimi kavulata, bali ni theory ya Mwl Nyerere aliyoitoa akiwa baba wa Taifa. Mwl Nyerere ndiye aliyeleta vyama vingi Tanzania hata baada kura ya maoni kuvikataa, kuvipiga vita ni kumpiga vita Nyerere na kumdharau. Lazima HakiyaMumgu hasira zake zitaitafuna CCM na kwisha kabisa, kufa ghafla kwa JPM na kujiuzulu kwa Spika hakujawahitokea Tanzania, inawezekana Kuna mengine makubwa yatafuata kama sehemu ya adhabu za mzee Nyerere kwa wanaCCM.

Nyerere alileta vyama vingi kuisaidia CCM kujikosoa, Yale yaliyosemwa na Ndugai yangesemwa na wapinzani hata kwa kutumwa na wanaCCM wenyewe. Kutosekana kwa upinzi kulimlazimu Spika ayaseme yeye mwenyewe, ona amekanyaga high tension wire.
 
Back
Top Bottom