kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,317
- 12,617
Mishahara ya watumishi ni midogo saaana kuliko huduma/jasho wanayoitoa kipindi chote Cha ujana yao. Mishahara ya watumishi haiwatoshi kuishi, kuSomesha, na kujenga nyumba. Kima Cha chini cha mfanyakazi ni shilingi 4000 kwa siku nzima wakati kule Marekani ni dollar 8 (TSH 18,400) kwa saa TU. Hii inasababisha mtumishi ashindwe kuishi kwa mshahara lakini akatwe hela kidogo sana kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
Wastani wa Umri wa kuishi (life expectancy) wa mtanzania ni miaka 55 tu lakini kikokotoo kinamtaka mstaafu anaestaafu akiwa na miaka 60 apewe 33% TU ya hivyo vijisenti vyake alivyokatwa na kuwekewa kwenye mifuko, kisha fedha nyingine apewe kila mwezi kama mshahara.
Kama ni kweli Wastanni wa Umri wa kuishi ni huu Ina maana aliyekuja na Wazo la kikokotoo hiki alidhamilia kuiba fedha za marehemu. Yaani kwa takwimu hizi za umri wa kustaafu ni kwamba watumishi wengi watakufa miaka michache kabla ya kustaafu na wengine watakufa ndani ya miaka 2 baada ya kustaafu. Maana yake wataziacha fedha zao za mafao na kubakia serikalini na kwenye mifuko au kuliwa na wategemezi ambalo sio kusudi la mfanyakazi.
Hii ni dhambi kubwa sana inayoonekana kwa macho, masikio na moyoni kuliko Ile dhambi ya baada ya kufa ambayo hujui kama IPO au haipo.
Hii Ina maana kuwa wastaafu watakaaoishi hadi miaka 80 ni asilimia ndogo sana kiasi cha kustahili kuhalalisha kikokotoo Cha 33%. Yaani huyu mtumishi ameibiwa mshahara halafu anaibiwa mafao yake pia.
Badala ya kutoa elimu kwa watumishi namna ya kujiandaa na kustaafu na namna ya kutumia mafao yake ya kustaafu mnaona njiia pekee ni kumuwekea hela zake. Hii sio sawa, ni dhuluma mbaya sana.
Lakini pia huwa ninajiuliza, kwani wale wastaafu wengine kutoka kwenye kilimo, ufugaji, uvuvi na biashara ambao ndio wengi sana huwa wanawekewa hela zao za uzeeni na nani wapi? Kwani hawa hawaadhiliki uzeeni kwa kukosa kipato? Kwanini huruma zenu ziwe kwa hawa tu wanaowadai hela zao? Hii ni njia ya kukwepa kuwalipa hela zao kwa kusaidiwa na kifo chao.
Wapeni hela zao buana wakafe nazo wenyewe. Na kama watazitumia hovyo basi wataishi kama wazee wenzao wengine wakulima, wafugaji, wavuvi, wakwezi na wawindaji wanavyoishi.