Dhamana ya uongozi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
49,007
2,000
Mtemi wa nchi moja alihalalisha biashara ya madanguro nchini kwake, alitoa hoja kuwa wenye madanguro wanalipa kodi navwanainua uchumi wa nchi. Viongozi wa dini walimsihi sana kuwa madanguro yanaharibu maadili ya vijana. Katika mawazo yake alifikiri ahh si ni watoto wao, watoto wa mtemi hawataingia kwenye madanguro.

Kumbe mtemi huwa anajiiba usiku akiwa na mavazi yake ya kawaida si ya kitemi huwa anakwenda kwenye madanguro. Huwa anavaa ki ajabu sana na watu hawamgundui. Kumbe na yeye ni mmoja wa wateja wakubwa.

Siku moja akiwa anasubiri huduma ndani ya danguro, aliingia binti yake. Kumuona binti yake alishtuka sana, wewe unafanya nini hapa? Kumbe yule binti anaipenda ile kazi wala haifanyi kwa shida na yeye hujiiba nyumbani kwa siri sana.

Mtemi alitokwa na machozi, alifikiri ufuska anaofanyiwa binti yake pale kwenye danguro. Kesho yake aliitisha amri ya kufunga madanguro yote.

Ukiwa kiongozi wewe ni baba wa wote.
 
lhera

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
1,846

Kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom