kaburunye
JF-Expert Member
- May 12, 2010
- 672
- 74
Jamani njoni muone, naleta kwenu habari
kwa wembamba na wanene, nawajia kwa shairi
Huyu Mwanajamiione, kaleta mada hatari
Mapenzi ya siku hizi, ni kweli yamenanihi
Shida wayakimbilia, wakiwa bado watoto
kisha wanatulilia, wamejawa na utoto
kwa kweli hawajatulia, ni kama waota ndoto
Mapenzi ni wa wakubwa, waliokamaa akili
Mapenzi si lelemama, ni vizuri tufahamu
mwulize baba na mama, kama kozi wametimu
badala ya kulalama, heri muwe moja timu
Kama wewe ni mtoto, mapenzi si saizi yako
subiri kwanza ukue, hili shauri nakupa
na kanuni uzijue, tulia na uache pupa
na utoto uutue, na ujinga kuutupa
vinginevyo ni hatari, kukimbilia mapenzi
mwamkumbuka kitila, yule aishi tabata
alijifanya msela, leo sasa anajuta
karudia ukapela, amekumbwa na utata
Mapenzi yana kanuni, ukizikwepa hatari