DGIS Diwan Athuman jiulize DDGIS Makungu alitumbuliwa au alipelekwa Tabora kujinoa kushika hatamu?

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
276
1,428
Kuteuliwa kwa Diwan Athuman kuna manufaa kwa Taifa na ustawi wa taasisi hii nyeti kwa nchi yetu. Lakini kuteuliwa kwake kuna changamoto kwa sababu hajui vigezo vilivyotumika kumpa hiyo nafasi na siku akiondolewa hatoweza kuhoji kwanini kaondolewa na yawezekana akakabidhiwa ubalozi na maisha yakasonga.

Aliondolewa msaidizi wa kapilimba akapelekwa Tabora, ameondoka Kapilimba lakini pia wameondoka wazee wengi waliokuwa wana malengo ya kuwa wakurugenzi wa taasisi hii na hakuna aliyejiuliza Kama wameridhika au la.

Namwona Makungu akiteuliwa kuchuku nafasi hii siku za mbeleni, nawaona walioondolewa wakiendeleza Vita vya madaraka chini chini. Mhe. Mkulu yampasa kuwa making sana na taarifa anazopewa maana wapo wakwamishaji wengi kuliko wenye nia chanya na nchi yetu. Vita ya madaraka imekuwa kubwa sana na wakuu wengine wa vyombo vyanaendelea kutokuwatendea imara kwa kuwa wapo wakubwa wanaopenda wenzao wakosee wateuliwe wao.

Wapo wanaoona ni haki vyombo vikiyumba kwa sababu wanaamini wanayohaki ya kuteuliwa. Kila binadamu anamapungufu yake na mapungufu hayo hayawezi kufutika kwa kufitinishana Bali yatafutika kwa watu kusimamia haki na kurekebishana, Diwani ufanyapo kazi fanya kwa uwezo na utaalam wako huku ukisimamia wivu wa taasisi yako na taasisi nyingine washirika. Tusingependa kukuona unaondoka Kama mtangulizi wako na wala tusingependa kuona unaruhusu wakuu wengine waondoke au waondolewe kwa uzembe, shikamaneni mkaishinde Vita inayowatenganisha ninyi walinzi wa nchi yetu. Umepewa mamlaka ya kushauri na kushauriana na wakuu wengine wa vyombo na umepewa madaraka ya kuwakanya kwa kuwa wewe ndiye Mwenye taarifa za awali dhidi ya kila adui anayeibuka. Warejeshee ujasiri wapiganaji na kuwafanya wakiamini huku ukiwaelekeza umuhimu wa kujisimamia na kushikamana siyo kusimamiana na kudukuana.

Endapo atarejea Makungu akute misingi imara imeandaliwa ili ajifunze kwako na kusonga mbele, hata Kama ikitokea hatorudi Basi mrithi wako akute Taifa linaishi kwenye misingi na lipo imara.

Nakutakia kazi njema wewe na wakuu wote wa vyombo nikiwaomba mshikamane na kulingana mkipambana na nguvu ya siasa inayowagawa kwa maslahi ya watu binafsi.
 
Nakupongeza sana kwa ushauri mzuri na lugha ya staha uliyotumia. Ushauri chanya kama huu ni nadra sana kuupata hapa jukwaani.

Naamini Diwani kaupata ujumbe, ama moja kwa moja au kupitia wenyeviti wa mitaa na vitingoni wanaomsaidia.

Naamini unayo mengi ya kujenga kwa maslahi ya Taifa ama kupitia Taasisi hii au zingine

Natamani iwepo Forum maalum inayosimamiwa na Taasisi hii ili kupokea taarifa, maoni, tetesi na ushauri.

Nitaanzisha Uzi maalum kwa lengo hilo
 
Umeandika jambo la msingi sana mkuu,
Siku hizi hakuna tena idara kwa sababu viongozi wake wamegeuzana maadui wao kwa wao, siku zote wanawaza kudukuana na kuchomeana kwa wakubwa wao ili kukwapuana madaraka! na hii ni kutokana na ukweli kwamba

1) Tanzania inaamini haina maadui wa nchi, ni kisiwa cha amani, hivyo imejikuta ikitupilia mbali agenda za ulinzi kwa kichaka hiki cha kwamba haina maadui hivyo kusababisha wana idara kugeuzana maadui wao kwa wao ili kusaka vyeo.
Kumbuka!
"Adui wa nchi akifahamika, Wanaidara ya usalama wanakuwa kitu kimoja kumdhibiti adui, na wananchi pia watakuwa wamoja kuwaunga mkono wanaidara," kama adui asipoonekana au akiingilia mifumo ya ulinzi na kujifanya mmoja wa walinzi, hali inakuwa kinyume chake!.

2) Siku zote wana idara wameabudishwa kutii makada wa chama tawala na chama kwa ujumla, hii imepelekea kukosa nguvu za kutekeleza majukumu yao kikatiba kwa kuwadhibiti makada amabao mienendo yao inatilia mashaka kiusalama wa nchi ndani ya chama. Pia wakaaminishwa kuwa adui wa taifa ni wanachama wa vyama pinzani.

Pia wana idara hawawezi kumshauri bwana mkubwa juu ya jambo lolote lile la kiusalama bali yeye ndiyo anawaamrisha kutekeleza amabacho yeye pekee anaamini ni sawa kikifanya kiusalama , mala nyingi ni kuhusu usalama wake mwenyewe na kiti chake, hali ni kinyume na taasisi za upelelezi kwenye nchi zingine ambapo mkuu wa nchi anapaswa kusikiliza ushauri wa idara zake za ulinzi kabla hajafanya maamuzi yoyote kiusalama.

Nimalize kwa kusema kwamba, mimi naamini hivi, Usalama wa nchi yetu upo mikononi mwa mungu tu na watu tunatakiwa kusali au kuswali sana kwa hili!, kitendo cha wao kudukuana na kushangilia pale mmoja wao anapofukuzwa ni dhahili kuwa wamesahaulishwa majukumu yao tangu zamani na wengi kujikuta wanawaza masilahi yao na vyeo kuliko kazi yao kikatiba.
 
Mh Diwani tengeneza whistleblowing channels madhubuti zitakazofahamika na kila mtu..naamini wapo watu (wazalendo) wenye taarifa zinazoweza kulisaidia Taifa lakini hawajui wanazipeleka wapi (usiniambie Polisi sababu unafahamu vizuri mfumo uliopo wa upokeaji taarifa huko vituoni).
Upandewenu weka team makini yenye uwezo mkubwa wa kuchanganua mambo na kupeleka mbele hizo taarifa kwajili ya ufuatiliaji.
 
Kuondolewa kwa Makungu naona kama ulikuwa mkakati wa kumuondoa Kapilimba baada ya yeye kutishia kuondoka kama makungu hatondolewa target ikawa kumpeleka makungu tabora ili kumpoteza kapilimba na jambo lilifanikiwa Makungu anaweza kurudishwa kama kutakuwa na mkakati wa Magufuli kujiongezea muda au kuchezea uchaguzi ila kama hakuna Diwani ataendelea Diwani anatakiwa kuwa makini zaidi idara imegawanyika.
 
Makungu au Robert hafai hata nukta, acha kumpaisha au kumpa cheap popularity hapa, hafai hata kwa bure, Mkuu wa nchi anajua, Makungu tokea alivyokuwa mfanyakazi wa ubalozi Ethiopia, hafai kabisa, he is not an intellectual hata kidogo, JPM alimpiga chini haraka sana sbb alijua ni useless guy. Akampa demotion akawe RAS huko Tabora. Au ww ndio Makungu unajipaisha humu
 
Kuteuliwa kwa Diwan Athuman kuna manufaa kwa Taifa na ustawi wa taasisi hii nyeti kwa nchi yetu. Lakini kuteuliwa kwake kuna changamoto kwa sababu hajui vigezo vilivyotumika kumpa hiyo nafasi na siku akiondolewa hatoweza kuhoji kwanini kaondolewa na yawezekana akakabidhiwa ubalozi na maisha yakasonga.
Wewe na diwani nani yupo kwenye nafasi nzuri ya kuyajua ya Tiss
Halafu hiyo ni kazi ya serikali kama kama ofisa ustawi w jamii au bwana mifugo,tofauti ni vitengo lakini kote huko wapo watu wa Tiss.Acheni watu wafanye kazi
 
Kuteuliwa kwa Diwan Athuman kuna manufaa kwa Taifa na ustawi wa taasisi hii nyeti kwa nchi yetu. Lakini kuteuliwa kwake kuna changamoto kwa sababu hajui vigezo vilivyotumika kumpa hiyo nafasi na siku akiondolewa hatoweza kuhoji kwanini kaondolewa na yawezekana akakabidhiwa ubalozi na maisha yakasonga.

Aliondolewa msaidizi wa kapilimba akapelekwa Tabora, ameondoka Kapilimba lakini pia wameondoka wazee wengi waliokuwa wana malengo ya kuwa wakurugenzi wa taasisi hii na hakuna aliyejiuliza Kama wameridhika au la.

Namwona Makungu akiteuliwa kuchuku nafasi hii siku za mbeleni, nawaona walioondolewa wakiendeleza Vita vya madaraka chini chini. Mhe. Mkulu yampasa kuwa making sana na taarifa anazopewa maana wapo wakwamishaji wengi kuliko wenye nia chanya na nchi yetu. Vita ya madaraka imekuwa kubwa sana na wakuu wengine wa vyombo vyanaendelea kutokuwatendea imara kwa kuwa wapo wakubwa wanaopenda wenzao wakosee wateuliwe wao.

Wapo wanaoona ni haki vyombo vikiyumba kwa sababu wanaamini wanayohaki ya kuteuliwa. Kila binadamu anamapungufu yake na mapungufu hayo hayawezi kufutika kwa kufitinishana Bali yatafutika kwa watu kusimamia haki na kurekebishana, Diwani ufanyapo kazi fanya kwa uwezo na utaalam wako huku ukisimamia wivu wa taasisi yako na taasisi nyingine washirika. Tusingependa kukuona unaondoka Kama mtangulizi wako na wala tusingependa kuona unaruhusu wakuu wengine waondoke au waondolewe kwa uzembe, shikamaneni mkaishinde Vita inayowatenganisha ninyi walinzi wa nchi yetu. Umepewa mamlaka ya kushauri na kushauriana na wakuu wengine wa vyombo na umepewa madaraka ya kuwakanya kwa kuwa wewe ndiye Mwenye taarifa za awali dhidi ya kila adui anayeibuka. Warejeshee ujasiri wapiganaji na kuwafanya wakiamini huku ukiwaelekeza umuhimu wa kujisimamia na kushikamana siyo kusimamiana na kudukuana.

Endapo atarejea Makungu akute misingi imara imeandaliwa ili ajifunze kwako na kusonga mbele, hata Kama ikitokea hatorudi Basi mrithi wako akute Taifa linaishi kwenye misingi na lipo imara.

Nakutakia kazi njema wewe na wakuu wote wa vyombo nikiwaomba mshikamane na kulingana mkipambana na nguvu ya siasa inayowagawa kwa maslahi ya watu binafsi.
Inaonekana unujua vizuri sana utendaji kazi wa TISS, unaonaje ukamtafuta DIWANI ili umpe ushauri wako badala ya kubwabwaja hapa jamvini, mambo mengine muwe mnanyamaza yana wenyewe
 
Makungu au Robert hafai hata nukta, acha kumpaisha au kumpa cheap popularity hapa, hafai hata kwa bure, Mkuu wa nchi anajua, Makungu tokea alivyokuwa mfanyakazi wa ubalozi Ethiopia, hafai kabisa, he is not an intellectual hata kidogo, JPM alimpiga chini haraka sana sbb alijua ni useless guy. Akampa demotion akawe RAS huko Tabora. Au ww ndio Makungu unajipaisha humu
Makungu alimpa ulinzi Bashite na wakawa wakikaa kupanga mipango miovu na mingi ilivuja ndipo mtukufu akatumbua haraka zaidi.
 
Back
Top Bottom