Dewji: Hakuna Kitu kinaua Urafiki kama Mikopo!!

Nikiwa na miaka 25.11 aliwahi kuja mzee wangu mmoja (55+) ambae nikimuheshimu sana naye akiniheshimu na kunijari sana, tulikuwa marafiki wakubwa tu na ofisi zetu zilikuwa jirani kitu kilichoongeza urafiki wetu japo alikuwa pia tunatoka wote sehemu moja yaani kabila moja, mnamo tarehe 10 October 2015 alinifuata akaniomba nimuazime 1,000,000/= kwaajili ya kuboresha vitu vyake fulani fulani na kuhahidi baada ya wiki 3-4 atanirejeshea, nami sikuwa na hiyana kwakuwa nilikuwa nayo nikampatia! muda tuliokubaliana ulipita ila akaja kunipa 800,000/= mwaka 2016 February akaniambia bado laki 2 nimvutie subira kidogo au lah kama sipo tayari basi nimsubilie anipe zote siku ya 3! nikaona hapana ngoja niichukue sijui la mbele! Alahaulah Lakwata mpaka naandika hapa sasa 2018 September 27 hajanimalizia 200,000/= simu zangu kupokea shida kila siku mara nyumba yake imeungua, mara baba anaumwa kalzwa kila siku nikimtafuta nasikia ana tatizo jipya na sasa tunakaa mikoa tofauti. DENI LINAUA URAFIKI..TRUE
 
wakopaji wana gia mpya utasikia una laki mbili hapo niazime baada ya siku mbili narudisha laki mbili na nusu mpe sasa imetoka hiyo nilishapigwa kwa staili hii aisee!
 
wakopaji wana gia mpya utasikia una laki mbili hapo niazime baada ya siku mbili narudisha laki mbili na nusu mpe sasa imetoka hiyo nilishapigwa kwa staili hii aisee!
Hongera kwa watoto wazuri. Ila usipende kuwaweka kwenye Avatar hasa sehemu nyeti kama JF
 
Mi nomegombana na dada angu mtt wa mama mkubwa hatuongei kabisa. Mara ya kwanza kanikopa nikasema ili asirudi tena ngoja nimwambie asirudishe heee baada ya muda akaja tena safr hii kakopa nyingi akanambia atarudisha wiki hiyo hyo doo leo ni mwaka unakaribia kila siku yale yale. Nimemnunia
 
Nikiona sikuelewi nakwambia huku nakuangalia sina, vinginevyo huwa nakupa tu. So,hiyo imepelekea kutokukopwa kabisa.
 
Pole sana mkuu. Imeandika kwa uchungu sana.
Japo wanasema dawa ya deni ni kulipa, watu wapo kinyume na hili kabisa.
Mi nomegombana na dada angu mtt wa mama mkubwa hatuongei kabisa. Mara ya kwanza kanikopa nikasema ili asirudi tena ngoja nimwambie asirudishe heee baada ya muda akaja tena safr hii kakopa nyingi akanambia atarudisha wiki hiyo hyo doo leo ni mwaka unakaribia kila siku yale yale. Nimemnunia
 
Hold on jamani mi nshapata na kupotea yaani siyo mara moja au mbili ila naamini ntakuja kuwa sawa sina doubt ktk hilo sasa rafiki wangu wa kike yeye yuko vizuri sana naye siruhusiwi kumkopa!? Najua naweza lose money au nikapata hela ila naelewa mwisho wa siku hata kama ni ten years ntakuja kuwa financial stable.
 
Viongozi wa Simba rudisheni pesa za watu.
Alafu mpaka jamaa kaandika ujue anamdai jamaa/ majamaa mkwanja mrefu.
 
Mswahili hajui kulipa ila anajua kuomba

Yaani wakati ana shida utafikiri muungwana na mkarimu sana ambae atalipa kwa mda, viapo vya kila aina na unyenyekevu juu

Ngoja tarehe ifike utajuta kumjua
Dawa ni kutoa robo ya anachouliza halafu mwambie zingine kaombe kwingine

Akikuambia nipate wapi ndugu yangu mwambie kwa Baba yako
 
Mim niliwahi mkopa mtu ambaye alikuwa na shida na n mchiz wangu sana tu Ambae amekuwa akinikopa na kurudisha japo wakat mwingne ilibidi niwe nambwekea ndipo analipa sasa iyo cku nmemkopa akaahid angelinilipa baada ya muda fulan ukapita huo muda nkakaa wiki baadae namkumbusha anakuwa Mkali na hadi Leo hajalipa ndipo nlipotambua sumu ya kukopesha watu wa Aina yake sasa cjamwambia chochote namngoja ajichanganye aingie kingi kuja kunikopa Yy mwenyewe nahic atajiongeza tu coz nackiaga hasira kila nkikumbuka alivyonijia akiwa na shida muda huo mwenyewe nlikuwa nmejibana hela yangu Kwa ajili ya shida zang binafsi Af Yy ananichukulia Poa sema tokea hapo nlipata somo
 
Dah Mpaka Mo anaandika hivi ni kwamba kafulia au?

Kufulia Kwake Yeye ni kutoka Kula Hamburger na kuhamia katika Piza ila Mimi na Wewe tunatoka katika Ugali wa Dona na tunahamia katika Uji wa Chumvi huku tukikodoleana ' Mimacho ' yetu iliyotumbuka kama ' Ndulele ' mbichi na kupeana stori za Kiabunuwasi na kupeana moyo ' Kingumbaru ' zaidi.
 
Mbona inajulikana siku nyingi?! Yaani yeye ndiyo kajuwa leo?! Kweli ukirithi biashara za baba zetu ni kazi kuziendeleza...
 
Ila ukitaka rafiki asikukope tena, fanya hivi

Akikukopa laki moja, mwambie una 50k.

Alafu ukiona harudishi unamkumbusha akisema hana mpotezee.

Huyo hakukopi tenaaaaaaa!!

Mana akitaka kukopa anajua anadeni kwako.

Sometime natumia mbinu hii kwa wasumbufu
Kuna watu wananyea kambi na wanarudi kulala humo.
 
Back
Top Bottom