Mimi jamaa toka mwezi wa 5 mwaka Jana hadi Leo.
Nilimtishia kwenda Polisi akasema atalipa hii wiki ya pili sasa.
Juzi kati nimesikia kauza nguruwe wake 20 bado hata SMS hanitumii.
Yaani nikikumbuka jinsi huyu dogo tulikotoka basi tu.
Na kila siku anaenda home kwa mother kujidai anamsalimia na kuleta shobo kwa ndugu zangu
Pole sana brother! Kama ilivyo katika mambo ya "investments" wanasema You should invest something/money which you are willing to loose! Vivyo hvy katika kukopesha rafiki, hii kwa mtazamo wangu lkn...Ni vyema kwa rafiki ukamkopesha pesa ambayo hata asipokulipa hutoumia sana, marafiki mara nyingi hupeana ela kuliko kukopeshana. Usije mtupa au kumpotezea rafiki yako huyo sababu hajakulipa pesa (kama ni rafiki haswa), kuna siku isiyo na jina utakwama sana,narudia tena utakwama haswa, atakuja kukusaidia kwa pesa ndogo sana klk hata uliyomkopesha na ukamshukuru utafikiri kakupa ahadi ya kukuongezea kuishi miaka 150.
Angalia mfano huu wa kweli: kuna jamaa(chukulie anaitwa michael) alikua na rafiki (Shaban-sy jina halisi) walisoma wote shule ya boarding miaka ya nyuma, kuna siku Shaban alisafiri kwenda likizo na kumuachia Michael mabegi yake na vifaa vyake mhm, Michael hakwenda likizo. Baada ya Shaban kurudi baada ya likizo, hakumkuta Michael , kumbe alifanya mpango na kuhama shule na akaondoka na vitu binafsi vya Shaban ikiwemo nguo za gharama. Shaban akapotezea na ubaya au uzuri kipindi hicho hakukuwa na mawasiliano ya simu.
Miaka kadhaa ikapita, wote wakiwa na maisha yao lkn wakiwasiliana mara chache mno. Shaban alikwama, alikua anamsomesha mdogo wake chuo kikuu Dar, na huyo mdogo wake alikua mwaka wa mwisho chuoni na alikaribia mitihani yake ya mwisho ili amalize chuo, kwa bahati mbaya sana Shaban alikwama kumlipia dogo ada ya semester ya mwisho chuoni. Alifika hatua Shaban akamwambia dogo wake afanye utaratibu wa kuhairisha mwaka kwasababu amehangaika zaidi ya miezi 4 kutafuta hy pesa amekosa, na mipango yoòoote ya pesa iligoma, hakuna alietaka kumsaidia Shaban achilia mbali kumkopesha. Wote dogo na Shaban walikua ktk mawazo mazito, dogo aliwaza muda aliopoteza na akiangalia wanafunzi wengine wakijiandaa na pepa anazidi kudata....kwa upande wa Shaban anawaza pesa aliyotupa toka mwaka wa kwanza alafu Leo pesa ndogo sana inakuja kuharibu kila kitu, na pia aliwaza , Je akihairisha mwaka atakuwa na uhakika wa kumlipia pesa(ada) tena mwakani ikiwa hii ndogo imemshinda?..pia aliwaza huyu dogo akikaa bila elimu si atakuwa mzigo kwake? Basi mawazo yakawa juu ya mawazo.....zikiwa zimebaki siku 2 kabla ya mtihani wa mwisho wa dogo, Shabani akapekua kwenye phonebook yake akaona jina la Michael akiwa hana uhakika kama atafanikisha lengo lake , yani kama alikua anajaribu akampigia Michael simu na kumuelezea shida yake....unafikri Michael alichukua hata dakika 2? mzigo ukasoma kwa tigopesa na mwisho wa siku dogo akaenda shule.....na kutunukiwa shahada yake.
Moral of this story, ni kuwa maisha ni mzunguko Leo wwe unapata(kama unabidii lkn ya kutafuta ) kesho mwingine anapata........tusiwe watu wa kupenda kulaumu sana kwa yanayotokea katika maisha yetu, kila kitu hutokea kwasababu.