Devil’s family(familia ya mashetani) 01

Devil’s family(familia ya mashetani) 01

DEVIL’S FAMILY(FAMILIA YA MASHETANI) 30

ANGALIZO: KAMA UPO CHINI YA UMRI WA MIAKA 18. TAFADHALI USISOME HII HADITHI.

ILIPOISHIA
“Babe”
“Mmm…umerudi?”
“Yaa nimerudi una endeleaje?”
“Nipo poa mume wangu. Umempata shem?”
“Bado”
Jack akavua nguo zake na akaelekea nafuni. Akaoga haraka haraka na akarudi kitandani na akajilaza pembeni ya Valentina.
“Mbona una onekana uma mawazo sana”
“Hakuna”
“Sijakuzoea hivyo”
“Nipo sawa mke wangu pumzika”
“Kama kuna tatizo naomba uniambie mume wangu”
“Hakuna tatizo babe. Pumzika”
Taratibu Valentina akajivuta juu kidogo na akakilaza kichwa chake juu ya kifua cha Jack na kuendelea kulala huku Jack akiwa hana furaha kabisa kwani aliyo kutana nayo baharini yameshangaza na kinacho muumiza kichwa zaidi ni kazi aliyo pewa ya kumuua kaka yake anaye mpenda.

ENDELEA
‘Nawezaje kumua James?”
Jack aliendelea kuwaza na kujiuliza maswali yaliyo kosa majibu.
***
Ndani ya siku mbili za James kukaa hospitalini akaruhusiwa kutoka huku hali yake ikiwa imeimarika.
“Una waza nini mume wangu?”
Rose alizungumza huku akimtazama James ambaye muda wote macho yake yapo nje ya gari akitazama vitu wanavyo vipita barabarani.
“Eti mume wangu?”
“Siwaza kitu mume wangu”
“Najua una pitia kipindi kigumu cha mawazo”
“Rose”
“Abee”
“Najua una biashara nyingi za wazazi wako unazo paswa kuzitazama kwa ukaribu. Je utaweza kuziacha na kuandamana nami kwenda kule ninapo pataka?”
“Nipo tayari”
James akamtazama Rose aliye jibu swali alilo ulizwa bila hata ya kufikiria mara mbili.
“Una uhakika?”
“Ndio babe. Nimeishi maisha yangu kwa asilimia kubwa nje ya nchi. Hivyo kwa hivi sasa naweza kwenda na kuishi nje ya nchi popote upatakapo mume wangu”
James akakishika kiganja cha mkono wa kulia cha Rose.
“Nakupenda snaa James sitanii kweye hili. Mwanzoni sikuwahi kujua nini maana ya mapenzi ila baada ya kukutana na wewe nimejua nini maana ya upendo. Unanipenda kweli James nami nina kupenda sana”
“Asante nahitaji kuanzisha familia na wewe”
“Hata mimi James”
Rose taratibu akambusu James mdomoni hadi anko Ally anaye endesha gari hilo akatabasamu. Wakafika nyumbani kwa wazazi wa Rose.
“Karibu na ujisikie huru”
“Asante mpenzi”
“Hichi ndio chumba changu ninacho ishi toka nikiwa binti mdogo”
“Asante sana mpenzi”
James alizungumza akitazama picha ukutani zinazo muonyesha Rose akiwa na wazazi wake.
“Picha hii nilipiga nikiwa na miaka mitano”
“Ulikuwa mrembo”
“Sana yaani, nilikuwa pis kali”
Wote wakacheka.
“Umefanana sana na mama yako”
“Yaah mama mama aliacha chata yake duniani”
“Kwa kweli, unataka tukaishi nchi gani?”
Rose akamtazama James kwa sekunde kadhaa.
“Nchi yoyote uitakayo wewe”
“Wewe ndio useme”
Rose akashusha pumzi taratibu.
“Kuwa huru”
“Brazil”
“Una papenda?”
“Sana napenda maisha yao wanayo ishi. Naamini tukienda kuanzisha maisha yetu pale tuta ishi kwa aamani”
“Kazi yako ya upelelezi?”
“Haina maana kwa sasa”
“Kwa nini?”
“James upelelezi ni kazi ninayo ipenda. Na nilijiunga kwa kuifanya kwa mapenzi yangu tu. Ila nilicho kuja kukigundua katia mataifa haya ya giza ambayo viongoz wake walio wekwa madarakani hawana nguvu juu ya wale walio waweka madarakani basi huwa nina ona hakuna haja ya mimi kuwa mpelelezi kwani kama walishindwa kunisaidia ukweli kwenye kupotea kwa baba yangu na kaka zangu una hisi kuna kitu gani wata weza kunisaidia?”
Rose alizungumza kwa uchungu akimtazama James usoni mwake.
“Jibu nililo pewa na mkuu wangu ni kuwa siwezi kuipeleleza familia yako nikaona kuna haja gani ya mimi kuendelea kuwa mpelelezi”
“Katika familia mbaya na hatari sana kwenye hii n hi basi ni familia yangu. Baba na mama yangu ni watu hatari sana. Nitofauti sana na jinsi vile watu wanavyo waona kwenye tv au jamii. Wale ni Chui walio jivisha ngozi za kondoo.”
“Una mpango gani dhidi yao?”
Rose aliuliza swali la kimtego.
“Kwa sasa nahitaji mimi na wewe tukawe sehemu salama. Baada ya hapo nitajua nini cha kufanya”
“Sawa mume wangu”
“Tuta tumia ndege yangu kuondoka Tanzania?”
“Una ndege?”
“Ndio ila hakuna mwanafamilia anaye tambua”
“Una muda gani toka umeimiliki?”
“Miaka miwili hivi sasa.”
“Wee”
“Kitu ambacho MUNGU alinipa akili ni kujitengenezea maisha nje ya familia yangu. Nilikuwa naishi maisha ambayo wana familia wangu waliyaona ni maisha yasiyo na future yoyote hivyo nilikuwa nina jiwekeza na nina fungua kampunia za teknolojia duaniani pasipo wao kujua. Hata hili la kuwaua walinzi wenye mafunzo ya hali ya juu itakuwa ni meseji tosha kwao kuwa sikuwa kama vile wanavyo nichukulia. Kwani waliniona mimi ni kama lover boy fulani hivi sina nguvu na hata majukumu mazito alikuwa ana kabidhiwa mdogo wangu”
“Waoooo”
“Ndio hivyo mpenzi. Nahitaji tuondoke ikiwezekana leo”
“Leo naomba niweke mambo sawa ndani ya kapumni hizi za baba. Kuna baadhi ya vitu ni lazima niviweke kwenye mstari ulio nyooka”
“Sawa mke wangu”
“Ngoja nimuambia anko Ally awaite wakurugenzi wote hapa nyumbani kwa ajili ya mkutano”
“Katika kampuni za baba yako kuna mfumo ambao una weza kuwasimamia wakurugenzi hata kama wewe upo mbali?”
“Upo ila wengi wana uchezea kwenye mahesabu”
“Naweza kuuona?”
“Ndio twende ofisini”
Wakatoka chumbani na wakaingia ofisini kwa mzee Chiko.
“Baba alikuwa ana tumia mfumo huo kupata taarifa za kampuni zake”
Rose alizungumza huku akiwasha computer ya baba yake. Akamuonyesha James mfumo huo.
“Mbona ni mfumo wa kizamani”
“Kumbe?”
“Ndio ni mfumo wa kizamani sana mpenzi. Ndio maana hata wakurugenzi wenu wana weza kuchepusha pesa za kampuni vile wanavyo jisikia wao. Ngoja nikutengenezee mfumo ambao hakuna ambaye ata weza kuuchezea hata awe na mdukuzi wa aina gani. Kila kifaa electron kinacho tumia mfumo ndani ya kampuni zako utakuwa una weza kufwatilia taarifa zake”
“Inawezakana kufanyika hivyo?
“Kwa asilimia mia moja. Tenknolojia ipo juu sana hivi sasa na sio tu utaweza kufwatulia taarifa za kikazi bali hata cctv zilizo fungwa kwenye maofisi zote na kila kitakacho kuwa kina zungumzwa ndani ya ofisi kitanaswa kupitia laptop, simu za ofisi, kamera za ofisi au tablet za ofisini. Hakuna ambaye ata kuwa salama kwenye mfumo mpya nitakao uunda”
“Mmmmm mume wangu ina wezekananaje simu au computer ikanasa sauti za watumishi?”
“Mke wangu sasa hivi hivi vifaa tunavyo vitumia sio salama unapo kuwa na mazungumzo nyeti. Nitafutie simu mpya nikuonyeshe”
“Kuna simu nilinunua ngoja nikaichukue”
Rose akaondoka na baada ya dakika akarudi akiwa na simu.
“Niliohofia kukupa simu ukiwa hospitalini kwa maana ungehatarisha ualama wako”
“Hahahaaa hakuna kitu kama hicho.”
“Hofu yako ndio ilikuwa ina niogopesha babe”
James akajisajili katika simu mpya, akaingiza mfumo wake wa udukuzi ambao ameuunda yeye mwenyewe.
“Mfumo huu niliuunda kwa ajili ya shirika lenu la ujasusi. Ila nikaona uta tumiwa vibaya sana na maafisa wake kwani utawezesha siri nyingi kuvuja”
James akaingia katika rekodi za vifaa vinayo tumika katika nyumba ya wazazi wake ikiwemo hadi simu za mikononi kuanzia ya baba yake, mama yake, Jack, Sophia, Valentina na watumishi wote wa ndani.
“Kwa hiyo hata nikiwa offlien nina weza kusikiliza mazungumzo yao waliyo yafanya simu zao zikiwa karibu na wao”
“Wana jua kuwa una wafwatilia?”
“Hapana huu mfumo ni mimi mwenyewe ndio ninao ujua”
James akatazama mazungumzo yaliyo rekodiwa na simu ya Jack siku mbili zilizo pita majira ya saa tisa usiku. James akajifikiria kwa sekunde kadhaa kisha akaifungua audio hiyo. Wakaanza kusikiliza mazungumzo ya Jack na baba yake kuanzia wakiwa sebleni hadi kufika eneo la katikati ya bahari na mazugumzo hapo yakakatika.
“Ina onekana baba yako ana kuchukia sana kwa kutaka kunioa mimi”
“Nikuulize jambo?”
“Niulize”
“Upo tayari kufunga ndoa na mimi?”
“Ndio nipo tayari mume wangu”
“Kweli?”
“Ndio mume wangu”
“Nakuoa leo mbele ya wafanyakazi wako”
“Leo?”
“Ndio leo”
“Mbona una harakisha?”
“Kwa sababu nikikuoa kuna vitu hawato weza kutufanyia”
“Vitu gani?”
James akashusha pumzi taratibu huku akimtazama Rose.
“Ipo hivi kuna siri ya utajiri wetu. Siri za nguvu za giza ambazo ndio zinazo linda huu utajiri ambao kila siku una kuwa una ongezeka.”
“Sasa ukiniona mimi mambo gani wata shindwa kutufanyia?”
James akanyanyuka na kumtazama Rose.
“Mtoto wa kwanza kwenye ukoo wetu huwa hapaswi kuoa. Endapo ata oa utajiri utaingia katika anguko ambalo waanzilishi wake hawapendi kitu kama hicho kiweze kutokea. Mbili nikikuoa hawato weza kuniua kwa nguvu za giza kwani kila mtoto wa kwanza kwenye ukoo wetu akisha fikisha miaka arobaini na mbili ana kufa. Hapa nina arobaini kamilia hivyo nimebakisha miaka miwili nife”
“Tatu kila mimba anayo ipata mwanamke ambaye sija muoa wana itoa. Ndio maana una weza kukuta hadi leo nimetembea na wanawake wengi sana ila sijafanikiwa kuwa na hata mtoto mmoja. Si kwamba nilio kuwa nina tembea nao walikuwa hawapati mimba? Walikuwa wana pata mimba ila walikuwa wana zito”
“Mmmmm! Baba yako ni mtoto wa ngapi kwao?”
“Wa pili. Kaka yake alifariki akiwa na miaka miwili tu. Ndio maana una weza kuona kuwa yeye ana onekana ni kama wa kwanza kwao”
“Umejuaje hizo siri zote mume wangu?”
“Kuna kitabu kipo katika library iliyopo chini ya ardhi katika makazi ya mzee pale. Mimi kwetu ndio nilikuwa nina penda kusoma hivyo nilibahatika kukisoma hicho kitabu nikiwa nimerudi chuo. Kuanzia hapo nikawa makini sana na kujitengenezea maisha yangu nje ya pesa ya familia. Pesa ambayo imejaa laana ya damu na pia nilipambana nihakikishe nina kuwa na ujuzi mkubwa katika tenkonolijia ili niweze kuapata pesa ndefu.”
“Nimekuelewa mume wangu. Nipo tayari kufunga ndoa na wewe”
“Mapigia mchungaji pamoja na sonara ninaye mfuamu atupe picha za pete kisha azilete”
“Sawa mpenzi wangu. Nakupenda sana”
Rose akamyonya denda James kwa hisia kubwa na James akaanza kuwasiliana na sonara ambaye ni rafiki yake na akatuma picha kadhaa za pete na wakaanza kuchagua.
***
“Siku ya tatu hii hadi leo mumeshindwa kujua ni wapi alipo eheee….Nina walipa pesa zote za nini nina wapa saa ishirini na nne muwe mumempata tunaelewana?”
Mzee Tiger alizungumza kwa kufoka, akakata simu huku akimtazama Jack akaingia ofisini kwake.
“Watu wako wamefikia wapi?”
“Bado wana mtafuta”
“Ina maana James amewazidi akili ninyi eheee?”
Mzee Tiger akazidi kufoka.
“Tuta mpata. Nimetega watu wangu kila mahala na hata pale nyumbani kwa Chiko, kuna watu tumewatega kufwatilia na kujua kama yupo pale au laa”
Mzee Tiger akaka katika kiti chake cha kuzunguka. Galfa hali ya hewa ikabadilika na manukano ya harufu nzuri yakatawala ofisi nzima.
“Kuna nini baba?”
“Bibi yako”
Mzee Tiger alizungumza akitazama ukuta wa upande wake wa kulia. Jack akashtuka kumuona bibi yake ambaye alikutana naye siku mbili zilizo pita. Mzee Tiger akampa ishara ya kunyanyuka Jack na kafanya hivyo, wakainama kidogo kama ishara ya heshima.
“Nyanyukeni”
Wakanyanyuka.
“Jack bado hujanizoea tu”
“Aaaaha….”
Jack akapata kiguumizi.
“Ina bidi unizoee”
“Sawa bibi”
“Sema mkuu”
Mzee Tiger alizungumza kwa sauti ya kunong’ona.
“Wala hana haja ya kuniita mkuu. Huyu ndio mjukuu wangu pendwa hivyo ana weza kunita bibi tofauti na ninyi”
“Mumefikia wapi kwa swala la James?”
“Kusema kweli hadi sasa hatujampata mkuu. Hatujui ni wapi alipo. Tumetumia hadi maafisa wa serikali kumtafuta ila hatujampata kabisa. Tuna omba msaada wenu”
“James ana oa leo. Ana muoa Rose leo”
Mzee Tiger akatazamana na Jack kwa mshangao.
“Na endapo ata muoa Rose basi Jack kuna malipo uta paswa kuyalipa kwani kazi itakuwa ni ngumu zaidi ya leo”
“M…amalipo?”
“Ndio kila jambo huwa lina utaratibu wake na kanuni zako. Baby yako mzaa baba yako, alimuua mwanaye wa kwanza alipo kuwa na miaka miwili tu kuepusha adhabu kama hizi ambazo wewe uta kutana nazo”
Jack akamtazama baba yake huku akitetemeka.
“Wewe ndio umekalia kiti cha utajiri wa familia yako. Hivyo kama kiongozi una beba majukumu yote ambayo kiongozi hubeba kwa watu wake anao waongoza. Endpo James akamuoa Rose basi ia tulazimua kumtoa kafara mke wako Valentina. Ndoa ya Rose na James ina fungwa baada ya masaa mawili yajayo. Ukichelewa kuizuia na kumuua James na Rose basi leo usiku mke wako atakufa”
Jack na mzee Tiger macho yakawatoka kwa mshangao huku wakishuhudia bibi akipotea mbele yao na kumfanya Jack akae kwenye kiti chake huku akitetemeka kwa woga.
ITAENDELEA
Mchaka mchaka mpya umeanza. James ameamua kumuoa Rose. Ndoa yake na Rose ita sababisha kifo cha Valentina je ni kitu gani ambacho Jack ata kifanya kuyaokoa maisha ya mkewe ambaye hawana hata wiki mbili toka wamefunga ndoa? Ungana nami katika stori hii ya kusisimua sehemu ya 31.
 
Huku vipi mbona joto jingi washeni hata feni jamaa
 
DEVIL’S FAMILY (FAMILIA YA MASHETANI) 31

ANGALIZO: KAMA UPO CHINI YA UMRI WA MIAKA 18. TAFADHALI USISOME HII HADITHI.

KILA KILICHO ANDIKWA KATIKA HADITHI HII NI UTUNZI HAKIENDANI NA KISA CHOCHOTE KILICHO WAHI KUTOKEA MAHALA POPOTE ASANTE
*************************************************************************************

ILIPOISHIA
“James ana oa leo. Ana muoa Rose leo”
Mzee Tiger akatazamana na Jack kwa mshangao.
“Na endapo ata muoa Rose basi Jack kuna malipo uta paswa kuyalipa kwani kazi itakuwa ni ngumu zaidi ya leo”
“M…amalipo?”
“Ndio kila jambo huwa lina utaratibu wake na kanuni zako. Baby yako mzaa baba yako, alimuua mwanaye wa kwanza alipo kuwa na miaka miwili tu kuepusha adhabu kama hizi ambazo wewe uta kutana nazo”
Jack akamtazama baba yake huku akitetemeka.
“Wewe ndio umekalia kiti cha utajiri wa familia yako. Hivyo kama kiongozi una beba majukumu yote ambayo kiongozi hubeba kwa watu wake anao waongoza. Endpo James akamuoa Rose basi ia tulazimua kumtoa kafara mke wako Valentina. Ndoa ya Rose na James ina fungwa baada ya masaa mawili yajayo. Ukichelewa kuizuia na kumuua James na Rose basi leo usiku mke wako atakufa”
Jack na mzee Tiger macho yakawatoka kwa mshangao huku wakishuhudia bibi akipotea mbele yao na kumfanya Jack akae kwenye kiti chake huku akitetemeka kwa woga.

ENDELEA
“Hei Jack usiogope ni wewe kumshuhulikia huyo mpumbavu”
Mzee Tige alizungumza akimtazama Jack ambaye anaendelea kutetemeka kwa woga.
“Ukituliza akili una weza kujua ni wapi alipo kaka yako na ukatekeleza mpango wako”
Jack akamtazama baba yake.
“Kwa nini mke wangu?”
“Sijui kwa nini wamemchagua mkeo. Ila una paswa kutekeleza kle wakisemacho”
“Baba hii sio sawa. Huu ni uonevu….Hata kama nina roho nguvu ila kwa mke wangu hapanaa……Siwezi mimi kuendelea kuwa hivi siwezi bwana”
Jack alilamika akiwa na hasira.
“Una maanisha nini?”
“Sitaki kubeba majukumu ya kifamilia. Sitaki mimi…..Wakiachana na mambo yote James ni kaka yangu ni damu yangu. Kama ni mauaji wafanye wenyewe kwa nini wana taka kuipa mikono yangu damu tena ya familia. Kuna raha gani za utajiri ninazo weza kufurahia nikiwa nimemuua kaka yangu. Ina tosha mimi sio mashine ya mauaji baba sitaki tena”
Jack akanyanyuka kwenye kiti alicho kikalia, akatoka ofisini kwa baba yake na kumfanya mzee Tiger abaki akiwa na mshangao
“Jack Jack”
Mrs Tiger alimuita Jack aliye kutan anaye kwenye kordo ila Jack hakuitika zaidi ya kumpita. Mrs Tiger moja kwa moja akatembea kwa mwendo wa haraka na kuingia ofisini kwa mume wake.
“Kuna nini mume wangu. Nimepishana na Jack akiwa na hasira kafanyaje?”
“Amegoma kuendelea na kazi ya kumsaka ndugu yake ili amue”
Mrs Tiger akashusha pumzi nyingi.
“Ita vikosi vyako vyote viingie kazini. Una mpa mzigo mkubwa sana Jack”
Mzee Tiger akatingisha kichwa akimaanisha amekubaliana na wazo la mkewe. Hakuwa na muda wa kupoteza na akampigia kiongozi mkuu wa vikosi vyake vya walinzi na akampa kazi ya kuamrisha vikosi vyote kumsaka James popote alipo na kumuua.
Jack akaingia chumbani kwake, akamkuta Valentina akiwa ana toka bafuni kuoga.
“Vaa nguo haraka”
“Mume wagu”
“Nimekuambia vaa nguo haraka”
Jack alizungumza kwa kufoka hadi Velentina akaanza kutetemeka kwa woga kwani toka ameanza mahusiano na Jack hajawahi hata siku moja kufokewa. Jack akagundua woga ulio mvaa mke wake.
Akamsogelea na kumshika viganja vya mikono yake.
“Mke wangu nisamehe. Mambo yana nivuruga akili hadi nimekufokea. Naomba uvae kuna sehemu nahitaji tuelekee”
“Upo sawa?”
“Sipo sawa mke wangu. Tafadhali vaa”
“Sawa”
“Chap chap”
Valentina akavaa huku akimtazama Jack anaye mfwatilia katika kuvaa kwake.
“Chukua funguo ya gari lako”
“Hatutumii gari lako?”
“Kwani lako ni bovu mke wangu?”
“Samahani”
Valentina akachukua funguo ya gari aliko zawadiwa na Jack siku ya send off. Wakatoka nje.
“Nipe funguo”
Valentina akampatia Jack funguo ya gari, wakaingia ndani ya gari na kuondoka nyumbani kwao.
“Hatuna walinzi leo?”
“Sio kila tunapo kwenda ni lazima tufwatane na walinzi”
Jack akaendelea kuendesha gari kwa mwendo wa kadia Valentina akajawa na woga. Wakafika katika kanisani.
“Tumekuja kufnaya nini mume wangu?”
“Kuonana na mchungaji”
Jack akawa wa kwanza kushuka ndani ya gari. Valentina naye akashuka na wakaongozana moja kwa moja hadi katika ofisi ya mchungaji.
“Habari zenu”
“Salama karibuni sana”
“Asante. Mchungaji Kimaro tumekuta?”
“Ndio. Ila ana mgeni. Tafadhali naomba mumsubirie”
“Asante”
Wakaka kwenye viti vya kupumzikia huku muda wote Valentina ana tamani kumuuliza maswali Jack ila ana shindwa. Baada ya dakika ishirini mchungaji akatoka akiwa maeongozana na mgeni wake aliye kuwa ndani ya ofisi.
“Mchungaji shikamoo”
“Marahaba Jack….”
Jack akataka kumpa mkono mchungaji ila mchungaji akaukataa mkono wake.
“Karibuni ofisini”
Valentina akashangaa kuona mchungaji ana kataa kupokea mkono wa Jack kitu ambacho sio cha kawaida. Mara nyingi huwa wanapo kutana naye ana wasalimia hadi kwa makumbatio.
“Kaeni”
“Asante sana mchungaji”
Jack alijibu.
“Umefanyaje Jack?”
Jack akapata kigugumizi cha kujibu swali la mchungaji kwani ana elewa ni kwa nini mchungaji amewauliza hivyo.
“Hayakuwa maamuzi yangu mchungaji”
Jack alizungumza huku machozi yakimlenga lenga.
“Mwanangu Valentina naomba utupishe”
“Sawa mchungaji”
Valentina akanyanyuka na akatoka ndani ya ofisi ya mchungaji.
“Nielezee kwa maana nina ona maungamo uliyo ingia”
Jack akajifikiria kwa dakika kadhaa na akaanza kumuelezea mchungaji kuanzia alivyo pelekwa katikati ya bahari baba yake. Akamuelezea yaliyo tokea na hata taliyo tokea ofisini kwa baba yake. Hadi Jack ana maaliza kuzungumza machozi mengi yamemwagika.
“Pole sana Jack. Hakuna lisilo shindikana mbele za MUNGU kila kitu kina wezekana.”
“Amen”
“Hakuna jini ua mzimu unao weza kuyachukua maisha ya mkeo.”
“Naogopa mchungaji”
“Ndio maana MUNGU amekupa rehema ya kutoka ulipo toka na kuja hapa ili nikuombee. Muite Valentina”
Jack akaifuta machozi, akafungua mlango wa ofisi ya mchugaji, akamuita Valentina kwa ishara na akaingai ofisini kwa mchungaji.
“Pigeni magoti chini”
Wakapiga na akawawekea mikono kichwani na akaanza kuwaombea. Gafla Jack akaanguka chini na kuzimia kitendo kilicho mshtua sana Valentina.
“Usiogope nguvu za MUNGU zina zidi kupita ndani ya mwili wake.”
Mchungaji Kimaro alizungumza na akaendelea kumuombea Valentina.
“Pepo la usagaji likuondoke na liachie maisha yako”
Mchungaji Kimaro akazidi kuomba kwa zaidi ya nusu saa ndipo Jack akazinduka, akatazama kidole alicho vishwa pete na bibi yake na hakuiona. Akamtazama Valentina anaye lia hadi macho yametawaliwa na uwekundu.
“Mupo free kutoka katika vifungo vya mapepo, majini, vifungo vya familia. Hakuna nguvu yoyote ya giza itakayo waweza”
“Asante sana mchungaji. Itakuwaje kwa kaka yangu?”
“Kaeni kwanza”
James na mkewe wakakaa kwenye viti.
“Kaka yako hato pata madhara yoyote kutoka mahali popote”
“Una uhakika mchungaji?”
“Ndio. Nililikuwa nina muombea sana juu ya maisha yake na apate mwenza wa kufunga naye ndoa na MUNGU ni mwema ana funga ndoa leo”
“Una taarifa ya yeye kufunga ndoa?”
“Ndio”
“Ni wapi na saa ngapi?”
“Hapa kanisani”
Jack na Valentina wakajawa na mshangao.
“Yaani wamesha funga au wana tarajiwa kufunga?”
“Natarajia kuwafungisha ndoa muda si mrefu”
Jack akashusha pumzi taratibu akimtazama mchungaji Kimaro kwa mshangao.
“Amenieleza mazingira ya yake ndani ya familia. Hivyo nikakubali afanye kile anacho taka kukifanya yeye na mpenzi wake”
“Wana kuja muda gani?”
“Walisha fika”
“Wamefika!?”
“Ndio. Ngoja nifanye utaratibu wa kuwakutanisha naye. Ila tafadhali usije kumsaliti ndugu yako”
“Siwezi mchungaji nina jiona nimekuwa mpya kwenye haya maisha”
“Sawa nisubirini”
Mchungaji Kimaro akanyanyuka na akatoka ofisini kwake. Akaelekea katika chumba cha siri cha maombi alipo James na mkewe Rose.
“Poleni kwa kuwaacha muda mrefu”
“Usijali mchungaji.”
“Kwa hali isiyo ya kutegemewa mdogo wako Jack amefika na mkewe hapa kanisani”
“NINI…..”
“Kuwa na amani. Amekuja kwa maombi kwani dhambi aliyo kuwa ana sukumwa nayo ya kukuua hadi akavishwa pete za kijestani amekuja kwa ajili ya kuombewa na kuondoakana na dhambi hiyo.”
“Una uhakika mchungaji?”
“Nimefanya naye maombi na siku zote MUNGU hadanganyi na kwa kuwa tulikosa wasimamiaji wa harusi yenu. Mdogo wako ana weza kukusimamia harusi”
James akamtazama mke wake mtarajiwa. Ambaye amefikia naye kanisani hapo kwa kutumia usafiri wa taksi japo hapo mwanzoni walipanga kufunga ndoa nyumbani kwa wazazi wa Rose ila kwa usuhauri wa mchungaji Kimaro, ikawalazimu kufika kanisani hapo.
“Baki humu ngoja nikazungumze naye”
“Sawa mume wangu kuwa makini”
“Usijali”
Mchungaji Kimaro na James wakatoka ndani ya chumba cha siri na wakaelekea ofisini. Jack na Rose wakanyanyuka kwenye viti walivyo kalia huku wakimtazama James.
“Broo”
Jack alishindwa kujizuia akamkumbatia James.
“Vipi dogo honeymoon yako imeendaje?”
“Poa kiasi kwa maana imekatishwa na taarifa zako”
James akatabasamu.
“Shem”
“Shikamoo shemeji”
“Marahaba. Unaendeleaje?”
“Nina mshukuru MUNGU nipo salama kabisa”
“Poleni nimewakatishia mapumziko yenu”
“Usijali shem. Pole sana wewe”
“Asante”
“Kimetokea nini bro”
James akashusha pumzi taratibu. Akamtazama Valentina na mchungaji Kimaro.
“Ngoja tuwapishe”
Mchungaji Kimaro alizungumza na akatoka chumbani hapo akiwa na Valentina.
“Ni kweli una taka kumuoa Rose Chirwa?”
James akamtazama Jack.
“Ndio”
“Kuna sababu ambayo umeificha kwa wazazi?”
“Hapana dogo. Nina mpenda sana Rose. Na sikutarajia kama nita mpenda na kufikia maamuzi haya. Sina sababu yoyote ya kumuumiza kwa ajili ya maslahi ya familia ambayo imejaa vimbwanga na mambo ya ajabu sana”
Jack akashusha pumzi taratibu. Akamtazama James.
“Kuna wakati ina bidi ende kinyume na matakwa ya watu wengine ili upate furaha yako wewe mwenyewe. Haijalishi maamuzi yako yata wakera wengine ili mradi una ishi kwa furaha ni heri ukaendelea kuitumikia furaha yako”
“Nimekuelewa kaka.”
“Kuna nini kimewafanya hadi muje kuombewa?”
Jack akakaa kimya kwa sekunde kadhaa. Akaanza kumuelezea kaka yake kila kilicho tokea kuanzia usiku wa kuelekea baharini hadi kilicho tokea ofisini kwa baba yake.
“Najua hiyo siri ya ukoo. Ndio maana niliamua kuishi maisha yangu”
“Uliijuaje?”
“Nilisoma kitabu kipo maktaba ya familia sema wewe na Sophia wote hampendi kusoma”
“Duuu”
“Yaah. Ila kwa kuwa mchungaji Kimaro amesha waombea hakuna kinacho weza kumkuta mkeo”
“Hata mimi nina amini hilo”
James akamtazama Jack kwa sekunde kadhaa.
“Usirudi kwenye maisha yale ambayo baba ana taka uyaishi. Ni maisha mabaya sana mdogo wangu. Una weza kuhisi una pendwa ila una jitengenezea uadui usio na sababu ya msingi”
“Ni kweli bro.”
“Tuna paswa na sisi kuwa na familia zetu. Tusiabudu utajiri ambao una matatizo chungu nzima, damu za watu wengi zina mwagika bila sababu ya maana hivo acha hayo maisha”
“Kuanzia hivi sasa nimeyaacha”
“Una mjua baba yako na mama yako. Ukiwaambia umeyaacha wayatakayo hivi una geuka kuwa adui yao. Yaani wazazi wana taka hadi kuniua ni kitu cha ajabu sana”
“Tuachane na hayo bro. Naweza kukusimamia harusi yako?”
James akamtazama Jack kwa sekunde kadhaa bila ya kumpatia jibu la moja kwa moja kwani endapo wazazi wao wata baini Jack amehusika katika kusimamia harusi yao, basi uadui mpya utazaliwa katika ya Jack na wazazi wake.
ITAENDELEA
Mchaka mchaka mpya umeanza. Kwa mara ya kwanza Jack na kaka yake James wamekuta mara baada ya mgawanyiko ulio tokea ndani ya familia Jack yupo tayari kumsimamia harusi James kaka yake je James ata kubali na je maombi yata msaidia Valentina? Ungana nami katika stori hii ya kusisimua sehemu ya 32.
 
Back
Top Bottom