Devil’s family(familia ya mashetani) 01

Devil’s family(familia ya mashetani) 01

DEVIL’S FAMILY (FAMILIA YA MASHETANI) 28

ANGALIZO: KAMA UPO CHINI YA UMRI WA MIAKA 18. TAFADHALI USISOME HII HADITHI.

ILIPOISHIA
“Marahaba. Poleni kwa kukatisha mapumziko yenu”
“Asante mama”
“Sisi hutukumbatii?”
Jack alimuuliza mama yake.
“Wewe nimesha kukumbatia sana toka nakuzaa”
Jack akatabasamu na wakaingia ndani.
“Baba yenu ana wasubiria”
Mrs Tiger alimuambia Sophia na Jack. Wakaongozana na mama yao hadi katika ofisi ya Mr Tiger. Huku Vaileth na mdogo wake wakielekea chumbani. Wakamsalimia baba yao.
“Kaeni”
Sophia na Jack wakakaa huku kila mmoja wakimtazama baba yao ambaye sura yake inaonyesha dhahiri ana hasira kwa kilicho fanywa na James.

ENDELEA
“Kuanzia hivi leo James sio mtoto wangu. Nimemuondoa kwenye orodha ya wanangu tuna elewana”
“Ngoja kwanza baba. James amefanya nini?”
Jack aliuliza akimtazama baba yake.
“Moja ana taka kumuoa Rose mtoto wa familia ya adui zetu. Uadui wa sisi na familia ya Chiko haujaanza kizazi chenu ni toka kizazi cha baba yangu. Kulisha wekwa kiapo cha damu hakuna mwana familia yoyote kutoka upande wowote atakaye oa katika familia hiyo. Yeye ana leta laana hiyo kwenye familia yangu, nimemfuta sio mwanangu”
Sophia akaanza kuchake na kumfanya kila mtu kumtazama.
“Weee mshenzi una cheka nini?”
Mrs Tiger alizungumza kwa hasira.
“Unavyo sema kuwa ata leta laana ndani ya hii familia..Jamani twendeni mbele na turudi nyuma. Muna hisi hii familia ni ya watakatifu? Tuna laana huko nje tuna onekana wapenda MUNGU watakatifu, watu wema ila uhalisia sisi ni mashetani….Siri za ndani ya hii familia siku zikitoka huko nje sote tutakuwa uchu hususani wewe mama ambaye hujifanya mtakatifu mbele za wanawake wezio. Kiufupi hayo maagano uliyo weka baba ni ya kishetani. Huo ndio ukweli, muta penda kusifiwa na kuambiwa mambo mazuri ila huo ndio uhalisia wa mambo hivyo kama hiyo ndio sababu ya kumkata bro muna bugi. Kuanzisha vita dhidi ya wanao ni kujizika na kusambaratisha familia. Halafu kumbukeni bro ndio aliye shikilia teknolojia ya hii nyumba na kampuni zote. Sasa haya maamuzi ambayo baba umeyachagua yana kwenda kupelekea anguko kubwa la hii familia subiri na uone”
“Unaonaje ukanyanyuka na kurudi kwako eheee”
Mrs Tiger alizungumza kwa kufoka.
“Hapa ni kwetu una onaje ukanyanyuka wewe ukaenda kwenu mama”
“Unasemaje?”
“Umesikia wewe sio damu ya familia ya Tiger hivyo huna mamlaka ya kunifukuza hapa isitoshe utaratibu wa ukoo huu una julikana kila mwana mtoto mwenye damu ya ukooo huu basi ana mamlaka ya hizi mali”
“Mume wangu umesikia matusi ya mwano.
Mrs Tiger alifoka na kumfanya Mzee Tiger kushusha pumzi nyingi.
“Sihitaji ugomvi wa kipumbavu”
“Baba una uhakika kuwa James ana muoan huyo Rose?”
Jack aliuliza kwa sauti ya upole.
“Asilimia mia moja. Na amedhibitisha hilo kwa kuwaaua walinzi wa hii nyumba. Nahitaji uchukue timu yako kwenda kwa yule msichana na umshuhulikie hadi asema ni wapi alipo James”
“Usifanye ushetani wa kila unacho elekezwa na hawa wazee”
“Sophia”
“Baba huo ndio ukweli. Kosa la bro ni kumpenda mtoto wa adui yako hiyo ni akili gani eheeee…….Hembu muacheni James awe huru na mwamke wake. Halafu ngoja kwa hiyo ninyi mulikuwa muna furahi sana kumuona James ana lala na kila aina ya mwanamke si ndio?”
Mzee Tiger na mkewe wakakaa kimya.
“Mdogo wangu. Mimi na James ndio tulio kulea ukiwa mdogo. Hawa wazee walikuwa wapo busy kutafuta pesa. Upendo ambao tulitengeneza kati yetu tafadhali usiende ukaharibu bond tuliyo iweka kwet sisi watatu. Hawa wazee wata kufa na kukuacha peke yako. Wewe waendekeze shauri yako. Umenielewa”
Sophia akanyanyuka na kumtazama mama yake.
“Ulipaswa kuwa mama mwenye huruma hadi kwa wanao wa kuwazaa. Ila roho mbaya itakufanya ufe kifo kibaya sana wewe endelea”
Sophia akatoka ofisini kwa baba yake.
“Huyu mtoto jeuri ya kunijibisha ameitolea wapi?”
“Vya kurithi vina zidi”
“Una mtete tu mwanao. Kwa nini huongei linapo kuja swala Sophia una mchechekea chekea.”
“Mama naomba nizungumze na baba tafadhali”
Mrs Tiger kamatazama Jack.
“Tafadhali”
“Sawa”
Mrs Tiger akanyanyuka na akatoka ofisini kwa mumewe.
“Baba kwa nini una taka kuiacha familia kwenye mgawanyiko kama huu.”
“Una maanisha nini?”
“Umnieleza kuhusiana na hali yako ya saratani. Kwa nini una taka ufe ukiwa umeacha hali kama hii”
“Una jisikia unacho kizungumza Jack waza nje ya boksi, acha kuwaza kama dada yako. Ni majuzi tu hapa tumemuua Chiko baba mzazi wa Rose. Leo hii aka yako ana taka kumuoa Rose tena Rose ambaye ni mpeleezi….Huoni anguko kubwa lina kuja dhidi yetu? James amehifadhi taarifa ngapi za siri za biashara zetu?”
“Nyingi”
“Hujawahi kusikia mwanamke ana weza kuwa undercover na akaolea na muhalifu na akaishi naya hata miaka kumi na akawa ana mpeleleza na mwisho wa siku akamuangusha katika wakati ambao mwanaume huyo hautarajii?”
“Nimesikia”
“Sasa unacho jizima data kwenye hilo ni kipi? Unanielewa lakini?”
“Nina kueleawa baba”
“Mtafute yule malaya Rose na uniletee akiwa hai. Kazi hii ifanye wewe mwenyewe”
“Sawa baba”
“Tukizembea kila ktu kina kwenda kuanguka”
“Nimekuelewa baba”
“Fanya hivyo”
Jack akanayanyuka akamtazama baba yake kwa sekunde kadhaa.
“Kama una jambo unataka kuzungumza zungumza”
“Hapana baba”
Jack akatoka ofisini kwa baba yake. Akakelekea chumbani kwake na akamkugta Valentina akimalizia kupanga nguo walizo nunua Dubai.
“Kumekwendaje huko?”
“Nahisi kupasuka kichwa tu”
Jack alizungumza akivua nguo moja baada ya nyingine.
“Kivipi?”
“Ahaa achana nayo. Ngoja nioge nitoke”
“Hata hupumziki”
Jack hakumjibu chochote mke wake zaidi ya kuingia bafuni, akaoga kisha akarudi chumbani na kukuta tayar Valentina amesha muandalia nguo za kuvaa.
“Shem umejua alipo?”
“Ndio nian kwenda kumtafuta”
“Wapi?”
“Nitajaribu kuzungumza na watu wangu kisha wao wata nijulisha ni wapi alipo shemeji yako”
“Sawa mume wangu kuwa makini”
“Usijali”
Jack akambusu mke wake mdomoni na akatoka chumbani kwake. Akakutana na Sophia katika kordo.
“Una kwenda wapi?”
“Kumtafuta James”
“Umejua ni wapi alipo?”
“Hapana”
“Kuwa makini usiingie kwenye upuuzi wa hawa wazee. Umenilewa?”
“Nakuelewa sisy”
“Kuwa makini. Unavyo hisi wana kupenda ila wana kupoteza. Roho waliyo kupandikiza haikufanyi kuwa wewe ulivyo. Haya shauri yako. Mkeo yupo wapi?”
“Chumbani”
“Kuna nguo niliweka kwenye begi lake hivyo naingia kuzichukua”
“Poa”
“Ukimpata James kuwa mtu wa kwanza kuniambia”
“Poa”
Jack akatoka nje, akaingia ndani ya gari akiwa na mlinzi wake mmoja na wakaondoka.
“Kuan nin kina endelea wifi?”
Valentina alizungumza akiitazama gari ya Jack inavyo elekea getini.
“Ahaa….tusiongelee hizo mambo. Nimekuja kukuambia jambo moja”
“Jambo gani?”
“Kesho nina rudi nyumbani kwangu Arusha”
“Mbona gafla”
“Najua una jua kuwa nilikuja kwa ajili ya harusi. Harusi imekwisha naondoka zangu”
“Ila kaka yako amepotea kwa nini auna harakisha”
“Mtu wa miaka arobaini ana poteaje……Kuna simu wata nifahamisha kinacho endelea”
“Na mimi nina baki na nani?”
“Khaa mumeo. Ukinitaka utakuja Arusha”
“Jamani babe”
“Badae”
Sophia akatoka chumbani kwa Jack na kumuacha Valentina akiwa ana shangaa shanga asijue nini cha kufanya.
“Mbona una shangaa”
“Mama karibu”
“Asante poleni kwa kuwakatishia mapumziko yenu ya harusi”
“Usijali mama tuna weza kwenda hata wakati mwengine.”
“Ni kweli binti yangu. Nimepita tu kuja kukuona”
“Asante sana mama”
“Tutoke utembee tembee kwa maana hapa ndio pamesha kuwa ni kwako”
“Sawa mama”
Valentina akaongozan ana mama mkwe wake na kuanza kutembea maeneo ya bustani za maua”
“Vai”
“Abee mama”
“Kwa nini una taka kuleta uadui kwa wanangu?”
Swali la Mrs Tiger likamshtua kidogo Valentina.
“Sijakuelewa mama una maanisha nini?”
“Unajua nini nina kimaanisha. Kwa nini una mahusiano ya jinsi moja Sophia huku umeolewa na Jack?”
Valentina akatamani ardhi ipasuke imeze, mwili wake akahisi umepigwa na ubaridi mkali sana. Jambo alilo lihisi ana lifanya kwa siri na wifi yake kumba hadi mama mkwe wake ana jua.
“Kwa nini nijibu?”
Mrs Tiger alizungumza kwa ukali ila kwa sauti ya chini. Valentina jasho likaanza kumwagika usoni mwake.
“Amekulazimisha?”
Valentina akashindwa hata kufungua kinywa chake.
“Nisikilize. Ingekuwa sio Jack kukupenda nisinge ruhusu uingize miguu yako kwenye maisha ya Jack. Ila siwezi kuharibu furaha yake kwa sababu ya laana zenu za kipumbavu. Nina ushahidi wa video zenu chafu ukiwa na Sophia. Sasa nikuambie jambo moja na uliweke akilini mwamko. Usije ukadhubutu siku hata moja ukaendeleza uchafu wako na Sophia unanielewa?”
“N…dioooo mama”
“Nikikuona tena unamfanyia Jack using** nitakuua kwa mikono yangu. Cheza na pesa mali za hii familia ila usicheze kamwe na furaha ya Jack hujui nimetumia njiani gani hadi leo hii una muona Jack amekuwa hivi alivyo hivi sasa. Na endapo atakuja kujua uchafu wako na Sophia ata kuua. Jack ni kichaa, mwenda wazimu. Mfurahie tu akiwa na furaha ila siku hata moja usije ukamshuhudia akiwa katika hasira tena hasira uliyo isababisha wewe. Unanielewa”
“Naomba mama unisamehee sinto rudia kufanya tena hicho kitu tafadhli mama”
Valentina alizungumza akilia kwa chungu. Mrs Tiger akatoa simu yake mfukoni na akamuonyesha Valentina video jinsi alivyo warekodi kwa siri wakifanya mapenzi na Sophia.
“Hii ni siku moja kabla ya harusi yako”
Valentina akazidi kuchwanganyikiwa.
“Nafuta hii video sasa ole wako, narudia ole wako urudie hiki ulicho kifanya na huyu mpuuzi mwenzio. Utajuta kwa nini uliolewa kwenye hii familia”
“Nakuapia siwezi kurudia tena siwezi mama”
“Futa machozi yao na tuendelee kutembea”
Valentina akafuta machozi haraka haraka. Mrs Tiger akamtazama kwa sekunde kadhaa na akatabasamu.
“Kuwa na amani mkwe wangu”
Mrs Tiger alizungumza akiwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake na kumfanya Valentina kuzidi kumshangaa mwana mama huyo kwani furaha yake imerudi kwa haraka kana kwamba hakuna kilicho tokea.
***
Taratibu James akafumbua macho yake, akaanza kutazama eneo alipo. Akamuona Rose akiwa amejilaza juu ya sofa huku amejifunika shuka. Akatazama saa ya ukutani na ina onyesha ni saa sita usiku.
‘Amenileta hospitalini?’
James alijiuliza akilini mwake.
“Rose…..Rose”
“Abee”
Rose akaitika huku akiziduka usingizini.Akamtazama James aliye lala kitandani. Kwa haraka akanyanyuka na kumfwata James kitandani.
“Umeamka mume wangu?”
“Ndio. Nipo hospitali?”
“Ndio mume wangu ila katika uangalizi mzuri sana”
“Baba ata nipata mke wangu”
“No hawezi kukupata. Nimezingatia tahadhari zote kabla ya kukufiksha hapa. Hivyo kuwa na amani”
James akashusha pumzi.
“Nimezima kwa muda gani?”
“Masaa mengi tu”
James akashusha pumzi nyingi.
“Imekuwaj ehadi ukawa na hali hii?”
“Kuna wajinga walinizuia kuondoka nyumbani. Hivyo nikawawahisha kufika kuzimu”
“Una maanisha nini?”
“Nimewaua”
Rose macho yakamtoka kwa mshangao.
“Kwa nini umefanya hayo yote?”
“Kwa sababu baba ametaka kuniua”
“Kukua kwa nini?”
“Kwa ajili yako.”
Rose akamtazama Jame ambaye ana maanicha kile anacho kizungumza.
“Hakuna wa kunizuia kukuoa wewe. Hakuna wa kunizuia nisiwe na wewe. Si mama yangu wala baba yangu. Nita kuoa na wewe ndio mke wanagu, mama wa wanangu”
James alizungumza kwa msisitizo na kumfanya Rose kukubujikwa na machozi.
“Nitafutie laptop”
“Ya nini mume wangu”
“Nataka kuwapatia wale mashetani ujumbe mmoja mtakatifu. Ujumbe ambao hawato kaa wausahau hadi siku ya mwisho ya maisha yao”
James alizungumza kwa msisitizo hadi Rose akabaki akimtazama kwa mshangao.
ITAENDELEA
Mchaka mchaka mpya umeanza. Jack maepewa kazi ya kumtafuta Rose na kumkamata je ata fanikiwa kazi aliyo pewa. James amezinduka je ni ujumbe gani ambao James ana taka kuwatumia wazazi wake? Ungana nami katika stori hii ya kusisimua sehemu ya 29.
 
DEVIL’S FAMILY (FAMILIA YA MASHETANI) 29

ANGALIZO: KAMA UPO CHINI YA UMRI WA MIAKA 18. TAFADHALI USISOME HII HADITHI.
ILIPOISHIA
“Kwa sababu baba ametaka kuniua”
“Kukua kwa nini?”
“Kwa ajili yako.”
Rose akamtazama Jame ambaye ana maanicha kile anacho kizungumza.
“Hakuna wa kunizuia kukuoa wewe. Hakuna wa kunizuia nisiwe na wewe. Si mama yangu wala baba yangu. Nita kuoa na wewe ndio mke wanagu, mama wa wanangu”
James alizungumza kwa msisitizo na kumfanya Rose kukubujikwa na machozi.
“Nitafutie laptop”
“Ya nini mume wangu”
“Nataka kuwapatia wale mashetani ujumbe mmoja mtakatifu. Ujumbe ambao hawato kaa wausahau hadi siku ya mwisho ya maisha yao”
James alizungumza kwa msisitizo hadi Rose akabaki akimtazama kwa mshangao.

ENDELEA
“Kwa sasa pona kwanza mume wnagu. Tafadhali usianzishe vita na familia yako ukiwa kitandani na pia usifanye maamuzi magumu ukiwa na hasira. Tafadhali sana kwa sasa nakuomba upone kwanza”
James akamtazama Rose kwa sekunde kadhaa.
“Sawa”
“Nashukuru kwa kunielewa kipenzi changu. Ni nani kwenye familia yako unaye muamini”
“Kivipi?”
“Mtu ambaye una wezakumueleza hali yako?”
James akakaa kimya kwa sekunde kadhaa.
“Ni dogo ila kwa sasa sihitaji kumueleza yoyote ni wapi nilipo. Itakuwa ni hatari kwako. Umenielewa?”
“Nakuelewa sana mpenzi wangu”
“Nashukuru kwa hilo”
Rose akamsogelea James na akambusu mdomoni.
“Asante kwa kunichagua kuwa mke wako”
James akatabasamu huku akimtazama Rose.
***
“Mkuu. Tumeuliza kila mahali ila hatuja pata taarifa zake”
Mlinzi wa Jack alizungumza akiwa amekaa siti ya pembeni ndani ya gari la Jack.
“Turudini nyumbani. Nimechoka nahitaji kupumzika”
“Sawa mkuu”
Dereva wake akawasha gari na wakaondoka nje ya bar ambayo mlinzi wake alikuwa ana zungumza na mmoja wa watoa habari wao.
‘Utakuwa wapi bro…Ina maana upo jijini hapa hapa na nisijue’
Jack aliwaza akilini mwake. Wakafika katika makazi ya baba wazazi wake.
“Usiku mwema”
Jack alimuaga mlinzi wake.
“Nawe pia”
Jack akaingia ndani na akamkuta baba yake sebleni.
“Hajalala mzee?
Jack akakaa katika sofa akimtazama baba yake anaye endelea kunywa pombe kali taratibu.
“Umefikia wapi?”
“Nimejaribu kutumia vyanzo vyangu vyote ili kuweza kupata taarifa ila sijafanikiwa kupata taarifa yoyote ya alipo bro”
Mzee Tiger akamtazama Jack.
“Baba naomba tuongee kiume. Kweli sababu ya Bro kutaka kumuoa Rose ndio inayo kufanya yatokee haya ya kutokea?”
Mzee Tiger akanyamaza kwa sekunde kadhaa.
“Baba?”
“Nakusikia?”
“Kuna sababu gani ya haya yote. Una tambua hali yako ya kiafya kwa nini una taka kuacha tabaka kubwa kama hili kwa sisi wanao?”
Mzee Tiger akanyanyuka.
“Tutoke”
Wakatoka sebleni na wkaatembea hadi katika ufukwe wa bahari.
“Mali hizo zote ni zako. Ikitokea nimekufa leo usiruhusu James kupata share yoyote. Wewe ndio umebeba heshima ya ukoo huu. Siwezi kumuachia mtu ambaye sio jasiri kulinda hizi mali zote. Usifumbie macho usaliti wa aina yoyote ndani ya familia yako. Wapende watoto wako ila usiruhusu wawe wasaliti wa misingi iliyo wekwa katika huu ukoo unanielewa?”
“Ndio nakuelewa baba”
“Nimewapenda ninyi wote. Kila mmoja ana madhaifu yake. Niliamini James atakuwa ni kiongozi mzuri wa familia ila mwishowe amekuja kuvunja mila za ukoo huu hivyo siwezi kuvumilia ujinga hata kama ni mwannagu wa kwanza. Ata adhibiwa kadri ya makosa yake”
“Ila baba nina wazo”
“Wazo gani?”
“Ina wezakana James akawa ana plan nyingine ya kumpeleleza yule binti na tukajua mengi kuhusiana na yeye. Anacho kipanga dhidi yetu”
Mzee Tiger akamgeukia Jack.
“James ni mwanangu. Kila mmoja nina wajua kiundani sana. Ninajua munapo ongea ukweli, nina jua munapo zungumza ukweli. Nina tambua munavyo zungumza uongo najua kila kitu. James amedhamiria kufanya hichi anacho kifanya na ana jua anacho kifanya hivyo ata lipia makosa yake aliyo yafanya unanielewa?”
“Ndio baba”
“Kuna siri una takiwa kuzifahamu. Umefanya mapenzi leo?”
“Hapana”
“Twende”
Wakatembea hadi zilipo boti zao.
“Karibu mkuu”
“Asante. Nifungulieni kamba ya boti hiyo.”
Mzee Tiger akamuonyesha mlinzi boti anayo hitaji kuitumia na wakaingia ndani ya boti. Boti na mzee Tiger akiwasha na wakaanza kuondoka eneo hilo bila ya walinzi.
“Tuna elekea wapi?”
“Ni muda wa wewe kujua nguvu ya ukoo huu”
“Ukoo?”
“Ndio”
“Ni nguvu ya aina gani?”
Mzee Tiger akamtazama Jack na akatabasamu.
“Katika nguvu ya kibiashara na nguvu ya kijamii kuna sehemu ina tokea.”
“Wapi?”
Mzee Tiger akatabasamu.
“Kuzimu”
Jack macho ya mshangao yakamtoka.
“Una ogopa?”
“Kuzimu?”
“Ndio.”
“Baba niambie una nitania?”
“Sikutanii nina kuambia ukweli”
Mzee Tiger akaendelea kuendesha boti hiyo kwa mwendo wa kasi. Wakafika eneo la mbali toka ulipo ufukwe wa bahari huku eneo hilo likiwa na utulivu wa hali ya juu.
“Jack”
“Naam baba”
“Kipindi una zaliwa. Nilikuleta mahali hapa. Nikakukabidhi kwa wakuu ambao ni wasimamizi wa huu utajiri wetu. Walikupokea na sasa wakati wa kujua mengi kuhusiana na siri zao”
Jack akatazama tazama eneo ambalo baba yake amesimamisha boti.
“Usiogope”
Mzee Tiger alizungumza akimtazama Jack usoni mwake.
“Usiogope”
Jack akaanza kuona upepo ukivuma kwa kasi kuzunguka boti yao kitendo kilicho zidi kumshtua.
“Usiogope”
Mzee Tiger akazidi kumsisitizi mwanaye asiogope. Jack akajikaza kiume akitazama watu walio valia mavazi meupa. Wakijichomoza kutoka baharini. Woga ukazidi kumtawala Jack na kujikuta akipepesuka kwani upepo ni mkali.
“Tulia”
Mzee Tiger alizungumza haku akitazama watu hao. Idadi ya watu walio toka ndani ya maji ikafika saba na wote wakaingia ndani ya boti hiyo. Mzee Tiger akainama kidogo kutoa ishara ya kusalimia, akampa ishara Jack na yeye akainama kidogo.
“Karibuni wakuu”
Mzee Tiger alizungumza huku akiwa bado ameendelea kuinama.
“Nyanyukeni”
Sauti ya kike ilisikika na kuwafanya mzee Tiger na Jack kunyanyua nyuso zao.
“Jack amekuwa mkaka mkubwa”
“Ndio mkuu”
“Jack una nifahamu”
Jack akamtazama mwana mama huyo ambaye ni mrembo sana.
“Ha….pana”
“Mimi ni bibi yako”
“B….ib….i”
“Ndio ni bibi mzaa babu yako kizazi cha nne.”
“Umekuwa ukifanya vyema yale yote ambayo tulikuwa tuna yahitaji hapa duniani. Hongera”
“Asante sana”
“Nilikuwa nina muambia baba yako akuleta utujue”
“Nimewaleta bibi”
Mzee Tiger alizungumza akitabasamu.
“Hawa wengine unao waona ni babu zako ambao ni kizazi changu hadi kufika uzao wa babu yako munaye muona kwenye picha nyumbani”
“Ohooo”
“Nyoosha kiganja cha kulia”
Jack akanyoosha kiganja cha mkono wa kulia. Bibi huyo akachukua pete inayo ng’aa na kumvisha Jack.
“Hii ni pete ambayo ita kusaidia na kukulinda. Pale itakapo kuwa ina kairbia hatari basi itakuwa ina ng’aa. Watu hawato weza kuiona pete hiyo ni wewe pekee ndio utakaye iona”
“Sawa bibi”
“Kama mtu ni mbaya kwako pete ita ng’aa”
“Sawa bibi”
“Utajua jinsi ya kujiadhari na maadui zako. Hii ni hatua ya kwanza ya wewe kujua siri za ukoo huu. Baada ya hapo nita kuwa nina kuja kukufundisha taratibu hadi ujue hatua zote za kuendelea mali za huu ukoo”
“Sawa bibi”
“Tiger”
“Naam bibi”
“Acha pombe. Hali yako ina zidi kuwa mbaya”
“Sawa bibi. Naomba kuuuliza”
“Ndio”
“Mtoto wangu wa kwanza James amesaliti taratibu za ukoo huu. Nini nifanye?”
Mzee Tiger aliuliza kwa saiti ya upole.
“Jack”
“Naam bibi”
“Msaliti wa hii familia ana paswa kuuliwa. Hivyo kazi yako ya kwanza ni kumuua James na uzao wake atakao upata kwa mwanamke aliye naye. Hivyo hakikisha una muua kaka yako haraka kabla uzao wake haujasambaa kwenye ulimwengu huu”
Jack akabaki ameduwaa kwa mshangao.
“Ndio fanya hivyo”
“Sawa bibi”
“Kwa leo tuishie hapa. Kwaherini”
Upepo mkali ukavuma kwa kasi wakapotea akabaki Jack na baba yake. Mzee Tiger akaiwasha boti na kuanza kuondoka kwa mwendo wa taratibu. Mzee Tiger akamtazama Jack jinsi anavyo tetemeka kwani aliyo yaona yana ogopesha.
“Baba”
“Naam”
“Naota au ninacho kiona ni uhalisia?”
“Ni uhalisia. Ningekuambia kwa maneno ya kwa nini nina kataaa maamuzi ya James kumuoa yule binti usinge nielewa. Sasa una nielewa vyema”
“Ila kumuua kaka yangu siwezi”
“Amesha kuwa adui. Na hichi ulicho kiona huku usimuambie yoyote hata mama yako hapaswi kujua wala mkeo. Unanielewa?”
“Ndio”
“Wale pekee ambao huchaguliwa na wakuu wa huu ukoo peke yao ndio hujua siri hii. Hivyo hata wewe ishi unavyo ishi usije ukatoa hii siri”
“Sawa baba”
“Ishi humo”
“Sawa baba”
“Fwata maagizo yao”
“Sawa”
Mzee Tiger akaendelea kuongeza kasi ya boti. Wakafika katika ufukwe wa jumba la mzee Tiger. Wakashuka ndani ya boti huku ikiwa ni saa kumi usiku.
“Rose ina maana asiuliwe?”
“Kwa nini?”
“Nimeuliza tu kwa maana imetolewa amri ya James kuuliwa?”
“Wote wana paswa kufa.”
“Sawa baba”
“Kapumzike”
“Usiku mwema baba”
“Kumesha kuwa alfajiri. Kapumzike”
Jack moja kwa moja akaelekea hadi chumbani kwake. Akamkuta Valentina akiwa amelala kitandani huku amejifunika shuka. Akakaa pembeni ya Valentina na akamtingisha kidogo.
“Babe”
“Mmm…umerudi?”
“Yaa nimerudi una endeleaje?”
“Nipo poa mume wangu. Umempata shem?”
“Bado”
Jack akavua nguo zake na akaelekea nafuni. Akaoga haraka haraka na akarudi kitandani na akajilaza pembeni ya Valentina.
“Mbona una onekana uma mawazo sana”
“Hakuna”
“Sijakuzoea hivyo”
“Nipo sawa mke wangu pumzika”
“Kama kuna tatizo naomba uniambie mume wangu”
“Hakuna tatizo babe. Pumzika”
Taratibu Valentina akajivuta juu kidogo na akakilaza kichwa chake juu ya kifua cha Jack na kuendelea kulala huku Jack akiwa hana furaha kabisa kwani aliyo kutana nayo baharini yameshangaza na kinacho muumiza kichwa zaidi ni kazi aliyo pewa ya kumuua kaka yake anaye mpenda.
ITAENDELEA
Mchaka mchaka mpya umeanza. Jack amekutana na wakuu wa ukoo wake ambao hakuwahi kuwaza kama ipo siku atakutan anao ila kazi aliyopewa ya kumuua kaka yake James ina zidi kumchanganya je nini kita tokea? Ungana nami katika stori hii ya kusisimua sehemu ya 30.
 
Back
Top Bottom