DEVIL’S FAMILY (FAMILIA YA MASHETANI) 59(Final).
KILA KILICHO ANDIKWA KATIKA HADITHI HII NI UTUNZI HAKIENDANI NA KISA CHOCHOTE KILICHO WAHI KUTOKEA MAHALA POPOTE ASANTE
*************************************************************************************
ILIPOISHIA
“Upo sehemu nzuri”
“Ahaa…yes nipo hospitali”
“Habari niliyo nayo kidogo sio nzuri”
“Kuna nini?”
Kila mtu akamtazama James.
“Mzee ametutoka”
James akashusha pumzi nyingi.
“James umenisikia?”
“Ndio nimekusikia mchungaji”
“Jambo la kumshukuru MUNGU ni kwamba amekufa katika bwana. Niliweza kumuugamisha dhambi zake kabla ya MUNGU hajaichukua roho yake”
“Nashukuru kwa huduma na taarifa”
“Utanikuta nyumbani”
“Sawa”
James akakata simu, akamtazama Sophia.
“Kuna nini?”
Sophia aliweza kumsoma James kwa haraka na hata swali ameuliza katika hali ya wasiwasi. James taratibu akakaa kwenye moja ya kiti.
“Baba amefariki dunia jioni hii”
James alizungumza kwa sauti ya upole akiwatazama Sophia na wezake.
ENDELEA
“Baba amekufa?”
Valentina aliuliza kwa mshangao.
“Ndio mchungaji Kimaro amenipatia taarifa hiyo na yupo nyumbani hivi sasa. So Babe”
“Abee”
“Naomba ubaki na wezako mimi na Sophia tuna kwenda nyumbani kuweza kujua utaratibu wa nini kifanyike”
“Sawa mume wangu”
“Kwa sasa hii taarifa itabaki kwa sisi wana familia. Musiwaeleze watu wa nje hata kama ni ndugu wa familia zenu. Tuna hitaji kuweka mambo sawa baada ya hapo tuta waambia”
“Sawa shemeji”
Valentina alizungumza kwa sauti ya unyonge.
“Ikitikea dogo amezinduka pia musimuambie chochote”
“Sawa mume wangu”
James ampiga busu la mdomoni Rose na wakatoka nje ya chumba akiongozana na Sophia. Rose akamfwata.
“Vipi?”
James alimuuliza Rose.
“Badae nita kwenda home kubadilisha japo mavazi, hapa nina jihisi mzito sana”
“Sasa hawa viumbe wawili wata weza kweli kubaki wenyewe?”
“Wapo na walinzi?”
James akashusha pumzi taratibu. Akamuita Chris kwa ishara na akawafwata mahali walipo simama.
“Ndio boss”
“Mzee amefariki jioni hii. Mimi na dogo tuna kwenda nyumbani. Wife hapa ana kwenda kubadili mavazi hivyo nita hitaji ulinzi wa kutosha sana kwani ana baki Valentina na mdogo wake.
“Mzee Tiger?”
“Ndio”
Chris akashusha pumzi nyingi kwani mzee Tiger alikuwa ana mchukulia kama baba yake.
“Kwa sasa usiwataarifu walinzi wengine. Waangalie sana hawa watu”
“Sawa mkuu”
“Mimi nita baki baki baadae ndio nita ondoka siwezi kuwaacha Valentina na Vaileth wenyewe”
“Sawa mke wangu. Chris kuwa makini kuliko wakati wote”
“Hakuna shaka boss”
James na Sophia wakatoka nje na kuingia ndani ya gari la Sophia na taratibu wakaondoka hospitalini.
“Bora amekufa”
Sophia alivunja ukimya huki akiandesha gari kwa mwendo wa kawaida.
“Kwa nini?”
“Kaka, mzee ndio chanzo cha haya mambo yanayo endelea kwenye hii familia. Kuna nyakati nina jutia kwa nini nilizaliwa kwenye hii familia. Ona tuna pesa tuna kila kitu ila amani ya moyo hatuna. Hapa tuna ishi na kujua muda na wati wowote ule tuna weza kuuwawa. Sasa haya ni maisha?”
James akanyamaza.
“Kama mzee alidiriki kutaka kukuua live live, MUNGU ameamua amuondoe yeye kabla yako. Ni jambo la heri broo”
“Kifo ni kifo. Japo ana mabaya yake ila tusisahau mema aliyo tufanyia hadi hapa tulipo fika.”
“Bro aliyo yafanya ni jukumu lake kama baba. Hatukusema atuzee so kutupa elimu na mambo mengne hayo yalikuwa ni majukumu yake na mkewe”
James akamtazama Sophia ambaye kifo cha baba yake hakijamuumiza sana.
“Tuna mzika lini”
“Duuu mtu kafa jioni hii hatujakaa kama familia una uliza ana zikwa lini”
“Natamani tugekuwa waislamu najua kesho tu tungesha maliza msiba.”
James akatingisha kichwa akisikitishwa na maneo ya mdogo wake.”
“Ita tulazimu kusubiria dogo azinduke kwani hatuwezi kumzika baba bila ya yeye kuamka”
“Khaaa tuweke misiba siku….”
“Sophia. Mimi kwenye hili ndio nilipaswa kukasirika, ila wewe”
“Bro wewe ni kaka yangu. Unajua fika kuwa sipendi uonevu unao tokea so kwenye hili niache kwanza”
“Sawa ndio kasha kufa”
“So uta uheshimu mgawanyo wake wa mali au nikusaidie kwenda mahakamani?”
“Sophia nina mali zangu. Sihitaji mali za mzee”
“Duuu haya”
Wakafika nyumbani kwao. Tayari baadhai ya wakurugenzi wa makampuni yao wamesha fika huku ulinzi ukiwa umeimarishwa vya kutosha. Wakashuka ndani ya gari na kuigia ndani, wakakuta baadhi ya marafiki wa baba yao nao wakiwa wamesha fika huku wakurugenzi baadhi wakiwa wamefika. Kila mtu akamshangaa James aliye chafuka ila hakulijali hilo, baada ya kuwasalimia wageni walio fika wakelekea moja kwa moja katika chumba alicho kuwa ana hifadhiwa baba yao. Wakamkuta mama yao, akiwa na mchungaji Kimaro, madakatri pamoja na wanasheria wawili wa familia. Mrs Tiger akaazidisha kilio mara baada ya kuwaona wanaye wawili wakiwa ndani hapo.
“Nombeni mutupishe tubaki na mchungaji”
James alizungumza na kila mtu akatoka. James akamsogelea mama yake alipo kaa pembeni ya kitanda cha mzee Tiger.
“Pole sana mama”
Mrs Tiger akaendelea kulea.
“Tuna weza kufanya ibada ya kumuombea?”
James alimuuliza mchungaji Kimaro.
“Ndio tuna weza”
“Tumuombee”
James alizungumza kwa sauti ya utulivu sana. Mchungaji Kimaro akasali kwa dakika tano na akamaliza sala.
“Mwili wake umesha chomwa sindano?”
James alimuuliza mama yake aliye vimba macho kutokana na kulia.
“Hapana.
“Mwili wake ina bidu upelekwe Mchori.”
“Sitaki mume wangu apelekwe Mochwari”
Mrs Tiger alizungumza.
“Mama una taka baba akuozee humu?”
Sophia aliuliza.
“Nimeagiza chumba cha chini kile kifungwe mifumo ya barafu hivyo tuta muhifadhi huko. Mwili wa mume wangu hauto kwenda popote kule”
Mrs Tiger alizungumza kwa msisitizo.
“Sawa upendavyo mama.”
Sophia akanyanyuka na kutoka chumbani hapo. Mchungaji Kimaro naye akatoka chumbani.
“Andaa statement ya kutangaza kifo cha baba yako”
“Mapema yote?”
“Sasa nini tuna ficha. Ulimwengu na wapendwa wake wana paswa kujua kinacho endelea”
“Sawa mama”
“Jack?”
“Bado hajazinduka”
“Hali yake?”
“Vile vile kama ulivyo muacha”
“Sawa tangaza kifo cha mzee”
“Poa Bi Mkubwa”
James akatoka chumbani hapo na akamuacha mama yake. James akamuita daktari mmoja kwa isha ishara.
“Mumesha andaa ripoti ya kifo cha mzee?”
“Bado”
“Iandaeni nataka kutanga kifo chake”
“Sawa”
James akaelekea chumbani kwake.
“Mchungaji”
Sphia alizungumza huku akimtazama mchungaji Kimaro anaye mfwata.
“Tuna weza kupata muda wa kuzungumza?”
“Ndio”
Wakatembea hadi la kupumzikia.
“Ndio mchungaji”
“Samahani kwa hichi nitakacho kuulia. Kwa nini huonyeshi kuumizwa na kifo cha baba yako kabisa.”
“Mchungaji namini kwenye biblia kuna mstari unasema acha wafu wawazike wafu wezao si ndio?”
“Hujakosea”
“So kipi kitabadilika kwenye hili? Nikilia kuwa ndio machozi yangu yana weza kumrudisha huyo mzee na kuwa hai au?”
Mchungaji Kimaro akaka kimya.
“Sipendi kuweka unafki kama anao ufanya mama”
“Unafki gani?”
“Mengine yana baki ndani ya familia. Fanya kilicho kuleta usitake kujua zaidi”
Spophia akataka kuondoka ila mchungaji Kimaro akamshika mkono.
“Binti yangu una paswa kuachilia hicho kinacho kusumbua ndnai yako. Hupaswi kuwa hivi kama ulivyo kuwa. Bado uan nafasi kubwa ya kutengeneza na MUNGU wako. Ukihitaji msaada wa kiroho uta nifahamisha. Nakuombea kwa MUNGU akakubadilishe hiyo roho na isiwe hivyo ilivyo kwako kwa sasa”
Sophia akautazama mkono wake ulio shikwa na mchungaji Kimaro, taratibu mchungaji Kimaro akauachi mkono wake.
“Samahani”
Sophia hakuzungumza chochote na akaondoka eneo hilo huku akipiga simu.
“Boss”
“Muandae mtoto muje Dar”
“Uisku huu”
“Kesho babu yake amekufa”
“Babu yake….Mzee Tiger?”
“Kwani ana babu gani mwengine. Mbona una uliza majibu?”
“Samani boss”
Sophia akakata simu kwani mwanaye amemuacha na mtumishi wa ndani Arusha nyumbani kwake. James akatazama suti aliyo iweka kitandani huku akiwa ametoka bafuni kuoga. Akavua taulo na akanza kuvaa nguo moja baada ya nyingine. Akajitazama kwenye kioo na kujuona akiwa amependeza. Akampigia simu Rose.
“Mume wangu”
“Upo wapi?”
“Ndio naingia nyumbani”
“Sawa nataka kwenda live. Nitangaze kifo cha mzee”
“Loe hii?”
“Ndio”
“Kwa nini musitangaze kesho”
“Bi mkubwa ndio ana hitaji nitangaze leo hii”
“Ni kwa sababu ya ule video au?”
“Hata sijui na tayari nimesha kutana na rafiki zake, wafanayazi, kiufupi hakuna cha kuficha mke wangu”
“Sawa mume wangu. Mimi ngoja nioge, kisha nirudi hospitalin”
“Poa mke wangu”
“Nakupenda James”
“Nakupenda pia mke wangu”
James akakata simu. Akaiweka simu mfukoni kisha akatoka nje.
“Tayari”
Mfanyakazi mmoja alizungumza hukua akiongozana na James hadi katika ofisi ya mzee Tiger ambapo tayari kamera tatu zimesha andaliwa kwa ajili ya kurusha matangazo hayo kwenda live. Akatazama picha kubwa ya familia iliyo bandikwa ukutani ikiwaonyesha wote.
“Niitie madaktari”
“Sawa”
Mfanyakazi akatoka na taratibu James akaka kwenye kiti cha baba yake. Akatazama ukubwa wa meza hiyo iliyo nakshiwa na madini. Mfanyakazi akarudi akiwa ameongozana na madaktari wawili.
“Naamini ripoti ipo tayari?”
“Ndio mkuu”
“Nataka kwenda live je kuna haja ya kuwaeleza watu kuhusian ana ugonjwa ulio mundoa mzee?”
“Ni maamuzi yenu kama familia. Ila unaweza usiende indatils sana”
James akajifikiria kwa sekunde kadhaa.
“Amekufa muda gani?”
“Saa kumi na moja na dakika ishirini na saba”
“Sawa. Washa kamera si umeziunganisha na mitandao ya akaunti zetu zote mitandao ya kijamii”
“Ndio boss”
Mfanyakazi akawasha kamera na James akashusha pumzi taratibu kisha akaanza kuzungumza.
***
“Karibuni sana”
Dokta Boaz alizungumza akipeana mkono na kiongozi wa timu ya makomandoo walio fika eneo alipo kwa kutumia gari zipatazo kumi zinazo fanana.
“Shukrani sana kaka. Naona una sakwa kama kakakuona”
“Hahahaa wee acha tu nimesha yavuruga ila bado sija maliza misson yangu. Kama tulivyo zungumza kwenye simu. Naamini umeongeza vijana wa kazi”
“Nina timu kubwa hata ungehitaji kubwa zaidi ya hii ningekuletea”
Dokta Boaz akawatazama makomandoo wanao shusha mabegi kwenye magari na kuingiza ndani.
“Hawa wana tosha”
“Malipo yangu aamini tuna malizana le oleo?”
“Hakuna shaka bro. Pesa ina letwa na boss mwenyewe”
“Sawa”
“Karibu ndani”
Dokta Boaz alizungumza huku akitoa simu yake mfukoni na kumpigia boss wake.
“Boaz”
“Wamesha fika eneo gani?”
“Ndio naingia njia ya kuja huko huku dakika tano utaniona. Wamefika”
“Nakuja hapo”
Dokta Boaz akakata simu na kuendelea kuwatazama makomandoo jnsi wanavyo shusha mabegi ambayo ndani yake yana silaha. Mwana mama akafika eneo hilo akiwa na mlinzi wake.
“Karibu sana boss”
“Nashukuru. Ehee msafara wote wa haya magari ni hawa jamaa?”
“Ndio jamaa wapo vizuri sana. Mzigo wao umekuja nao?”
“Ndio. Shusha hizo begi kwenye gari”
“Sawa boss”
Mlinzi wa mwana mama akashusha begi mbili kubwa zilizo jaa vibunda vya pesa za Kimarekani.
“Kiasi gani?”
“Dola mlioni kumi kama ulivyo hitaji na kuna mabegi mengine manne kwenye gari”
“Sawa. Ngoja”
Dokta Boaz akaingia ndani akarudi na kiongozi wa makomandoo.
“Mzigo wako umefika. Dola milioni kumi in cash. Na huyu ndio boss wangu ambaye ana kazi anayo hitaji muifanye kwa asilimia mia moja”
“Hakuna shaka hukakosea kuileta kazi kwetu na nina taarifa sijui kaa munayo”
“Taarifa gani?”
Boss wa James aliuliza kw ashauku.
“Mzee Tiger amekufa. Na hii hii taarifa yake.”
Akawaonyesha kinacho endelea katika taarifa ya habari.
“James ndio anaye tangaza hii ni habari ya kweli boss”
Dokta James alizungumza akitabasamu.
“Waoooo….!! Ni wakati wa kwenda kuwaua wote, siku ya mazishi ndio siku ambayo muta kwenda kuwazika familia nzima waungane na baba yao. Je muna weza kuifanya hiyo kazi?”
Mwana mama bilionea alimuuliza kiomgozi wa makomandoo na akatingisha kichwa akimaanisha kwamba kuifanya kazi hiyo kwa upande wao ni sawa na kumsukuma mlevi kwenye kiporomoko chenye utelezi.
MWISHO
Namshukuru MUNGU kwa kuniwezesha kuiandika hadithi hii kuanzia sehemu ya 1 hadi mwisho ilipo ishia. Naamini umeburudika na kujifunza mambo mengi sana.