DEVIL’S FAMILY (FAMILIA YA MASHETANI) 39
KILA KILICHO ANDIKWA KATIKA HADITHI HII NI UTUNZI HAKIENDANI NA KISA CHOCHOTE KILICHO WAHI KUTOKEA MAHALA POPOTE ASANTE
*************************************************************************************
ILIPOISHIA
“Usiowaope”
Valentina alimfariji Rose akimshika kiganja.
“Nina amani kidogo nimerudi ndani ya gari. Eti huwa wana toka ndani ya bwawa?”
“Tungekuja mida ya mchana tusinge simama tulipo kuwa tumesimama kwani hutoka na kuota jua.”
“Ohooo. Nimefurahi sana kuiona hii mbuga”
“Umeridhika? Kwa maana kuna maeneo hatujatembelea?”
Valentina alimuuliza Rose akimtazama usoni.
“Maeneo gani?”
“Maeneo ya kufugia majoka yale makubwa. Huko ndio kuna tisha mwenyewe nilishindwa kuvumilia”
“Ina tosha kwa leo”
Rose alizungumza huku moyoni mwake kukiwaka moto, wa kulipa kisasi kwa wahusika walio husika na kifo cha baba yake na kaka zake.
ENDELEA
“Vipi umefurahi kuwaona wanyama?”
Valentina alimuuliza Rose.
“Sanaa”
Wakafika walipo liacha gari, wakaagana na msimamizi wa mbuga, wakapanda gari walilo toka nalo nyumbani na kuanza kurudi katika nyumba ya mzee Tiger.
“Asante eheee”
Valentina alimuaga mlinzi waliye ongozana naye kisha wakashuka ndani ya gari na kuingia ndani.
“Nimewatafuta mulikuwa wapi?”
Mrs Tiger aliwaulizaza akiwatazama Rose na Valentina.
“Kwanza shikamoo mama”
“Marahaba”
“Shikamoo mama”
“Marahaba Rose. Ehee mulikuwa wapi?”
“Tuliwenda Mbugani mama. Nilimpelekea Rose akashangae shangae wanyama”
“Ohooo kumbe?”
“Ndio mama Valentina alinieeleza kuhusiana na mbuga ya wanyama hivyo nikawa na hamu kubwa sana ya kuona kinacho endelea eneo hilo”
“Mama huwezi amini mkweo ana ogopa mamba”
“Mamba!?”
Mrs Tiger alijifanya kuuliza kwa mshangao.
“Ndio mama. Amewaona mambo hadi ana tetemeka”
“Dooo si muliwaona kwa mbali?”
Mrs Tiger alimuuliza Rose, akimtazama machoni.
“Ndio mama tulisimama mbali”
Valentina alijibu kwa furaha, ila Rose uso wake una tabasamu akijitahidi kuificha hasira yake.
“Wale mamba wamezaliana sana hivyo nina mpango wa kuwauza kwa watu wana penda kula nyama yao”
Mrs Tiger alizungumza akijaribu kumdadisi Rose.
“Ohoo ni wazo zuri mama”
“Okay tuachane na stori za mamba kaogeni, tuje kula kuna mahala nina taka twende pamoja by saa nne hivi”
“Sawa mama”
Valentina alijibu.
“Rose nawe pia?”
“Sawa mama”
Rose akatabasamu na akawa wa kwanza kuondoka huku Valentina akimfwata kwa nyuma.
‘Atakuwa amegundua jambo au?’
Mrs Tiger alijiuliza swali lililo kosa jibu. Rose akaigia chumbani, akamkuta James akiwa bado hajaamka. Akavua viatu na nguo na kuelekea bafuni, akaufunga mlango wa bafuni kwa ndani, akafunuga bomba la maji, akakaa kwenye kona ya bafu na kuanza kulia kwa uchungu sana. Kwa picha ya hisi akawaza jinsi ndugu zake na baba yake walivyo kuwa wana rushwa ndani ya bwawa la mamba.
‘Relax kisasi chako kita fika. Taratibu endelea kuaminka Rose’
Rose aliwaza akilini mwake, akajifuta machozi, akanyanyuka, akasimama mbele ya kioo na kuutazama uso wake.
‘Muda uta fika wa kuwafanya walipe kwa kile walicho kifanya ni lazima walipe’
Rose alizidi kujiapiza.
“Babe”
Sauti ya James ikamtoa kwenye ndimbwi la mawazo.
“Babe”
“Abeee”
“Mbona umejifungia”
Kwa haraka Rose akajipitisha kwenye bomba la mvua na mwili ukalowana maji kisha akafungua mlamgo na James akaingia ndani.
“Upo sawa?”
“Yaa nimechoka tu mume wangu”
Rose akachukau sabuni ya maji na kuanza kujimwagia mwilini mwake. James akajisaidia haja ndogo.
“Babe”
“Naam”
“Mama ametuambia tunywe chai na tutoke naye”
“Utoke na mama yangu?”
“Ndio ila nipo na Valentina”
“Kwenda wapi?”
“Hajatuambia”
“Eheee?”
“Yaa hapa nina oga, kisha nishuke huko chini, nikanywe chai ndio tutoke pamoja”
“Mama yangu simuamini, ngoja nikamuhoji kwanza”
“Tafadhali mume wangu hii ni asubuhi, sitaki marafakano na mama yako, acha niongozane naye”
“Oya hapa tuna zungumzia usalama wako”
“Una hisi ata nidhuru nikiwa nimetoka na yeye? Sidhani kama ana weza kuwa na akili mbaya namna hiyo”
James akamtazama Rose.
“Hawezi kuwa na amani”
“Usimuamini kwa chochote”
“Usijali mume wangu. Bado una endelea kulala?”
“Nilitaka nikalale ila kwa ulicho niambia nimeishiwa usingizi”
Rose akamshika mkono James na akamvuta katikati ya eneo la maji ya bomba la mvua yanapo mwagika. Akamkumbatia kwa nguvu James.
“Nakupenda mume wangu”
Rose alizungumza kwa uchungu na hisi kali.
“Nakupenda pia mke wangu. Una jua nina weza kufanya chochote kwa ajili yako”
Rose akakingiza kiganja cha mkono wake wa kulia ndani ya boxer ya James na kuanza kumtomasa jogoo wa James na taratibu akaanza kusimama. Kuongeza hisia ya anacho kifanya, akaanza kuyonyana dena na James na hisia kali za mapenzi zikaongezeka kati yao. Akamvua boxer James na wakajikuta wakipiga show wakiwa bafuni.
***
Valentina akajifuta maji na taulo kwnai ametoka bafuni kuoga, akaichukua simu yake kitandani na akampigia Jack. Simu ya Jack ikaita hadi ikakata, akarudia kumpigia kwa mara ya pili na simu ikapokelewa.
“Mke wangu”
“Mbona nina kupigia hupokei mume wangu?”
“Nipo kwenye kikao. Vipi umeamkaje?”
“Nimeamka poa. Umelala kweli?”
“Nilale nina raha gani mke wangu. Hapa nimechoka mwili hadi akili”
“Unarudi saa ngapi?”
“Mmm mchana. Kwa maana nikimaliza kikao baadae nina wafanyakazi nina taka kukuaa nao na kufanya nao kikao pia”
Jack alizungumza huku akiyatomasa makalio ya Vaileth aliye lala kifudifudi pembeni yake.
“Sawa mume wangu. Naomba ruhusa mama ameniambia nitoke naye?”
“Muna kwenda wapi?”
“Hajasema”
“Leo?”
“Ndio natoka naye na Rose”
“Mmmmm!”
Jack akakaa vizuri kitandani.
“Sawa”
“Mbona umeguna?”
“Hamna. Kikubwa kuweni makini”
“Sawa mume wangu”
Jack akakata simu. Akajifikiria kwa sekunde kadha.
‘Mama ana wapeleka wapi hawa watu?’
Jack alijiuliza. Akataka kumpigia mama yake ila akasita. Akampigia mlinzi mkuu wa familia.
“Boss”
“Upo nyumbani?”
“Ndio”
“Mama ana toka na wake zetu. Naomba uhakikishe wana kwenda na kurudi salama huko waendapo”
“Nitazingatia hilo”
“Umebahatika kuangalia afya ya mzee?”
“Ndio nimeingia chumbani asubuhi hii hali yake ipo vile vile”
“Sawa. Walindwe hao, kama unavyo elewa mishe za bi mkubwa huwa hazieleweki”
“Nimekuelewa boss”
“Asante”
Jack akakata simu. Akampigia simu James ila haikupokelewa, akampigia kwa mara ya pili na haikupokelewa.
“Mbona humuamini mama yako?”
“Mmmmm?”
“Mbona humuamini mama yako?”
Vaileth alimuuliza Jack huku akijigeuza na kulala chali.
“Ahaa kuna mambo ya kifamilia yana endelea hivyo hatumuamini”
“Mama yenu wa kumzaa?”
“Ndio”
“Mbona yule mama ni mtu mwema”
“Kuwa mwema hamaanishi una aminika mpenzi. Tuachane na hayo, nina wazo”
“Wazo gani?”
“Nahitaji kukupa nyumba na gari, uishi hapa Dar kisha uta waambia nyumbani kwenu kwamba umepewa hivyo vitu na kampuni.”
“Jack jamani mbona una nipeleka haraka mpenzi wangu. Una jua fika kwamba mimi ni mwizi wa penzi la dada yangu”
“Achana na dada yako. Mimi nina zungumzia kuhusiana na wewe na maisha yako.”
Jack alizungumza kwa msisitizo.
“Au una taka niwe na kutomb** tu kisha maisha yako yawe sifuri si ndio?
“Hapana mpenzi usikasirike”
“No kwa maana hapa najaribu nikuwekee wewe maisha yako sawa ila una waza tu dada dada…..Hujui kama dada yako ana mahusiano ya kimapenzi na dada yangu eheee?”
Jack alifoka.
“Ngoja kwanza umesema?”
“Achana na hiyo mada”
Jack akaingia bafuni na kumfanya Vaileth kushuka kitandani na kumfwata bafuni.
“Tuzungumze….umesema dada yangu ana mahusiano ya kimapenzi na dada yako?”
Jack akamtazama Vaileth kwa sekunde kadhaa.
“Ndio”
“Ina maana ni msagaji?”
“Ndio”
“MUNGU wangu!”
Vaileth akajifanya kushangaa.
“Nisikilize nina lijua hilo kabla ya kumuoa ila sitaki ajue kuwa nina jua unanielewa?”
“Ahaa…”
“Unaielewa?”
“Ndio mpenzi
“Nahitaji mwanamke wa kwangu peke yangu ndio maana nipo na wewe”
“Nimekuelewa mpenzi wangu”
“Yaa hivyo tulia nikutengenezee maisha na ikiwezekana nikuoe kabisa. Kama ni kuzungumza na wazazi wako mimi ndio nitakaye zungumza nao”
“Sawa.”
Vaileth alijibu kumridhisha Jack ila moyoni mwake ana ona hatari kubwa kwake, kwani familia yake ina weza hata kumtenga kwa usaliti anao mfanyia dada yake wa tumbo moja.
***
“Shikamoo mama”
“Marahaba. Karibu unywe chai”
James akavuta kiti na kukaa, akawatazama Rose na Vaileth ambao wamesha pendeza kwa ajili ya safari.
“James nataka kutoka na wakwe zangu”
“Munakwenda wapi?”
“Tuta kuwa na mizunguko mingi leo. Ila moja nataka kuwapeleka kwenye kampuni ya vipodozi, nikawatambulishe kwa wafanyakazi. Nina mpango wa kuwapa share na usimamizi wa kampuni hiyo”
Rose na Valentina wakamtazama Mrs Tiger kwa mshangao.
“Mimi sasa hivi nazeeka, dunia ipo kasi kuna ushindani wa kila mahali. Rose wewe una ujuzi mkubwa wa biasharaha hivyo nimeona kila mmoja nimpe share ya asilimia ishirini na tano za kampuni yangu. Mimi nitabaki na asilimi ishirini. Sasa kazi kwenu, mujitahidi kunipatia wajukuu kabla sijakufa”
“Asante sana mama”
Rose na Valentina walijikuya wakijibu kwa pamoja.
“Upo seriously, mama?”
James aliuliza.
“Ndio. Tuta pita kwa mwana sheria wa familia. Ata andaa taratibu zote za kutoa share zangu kwa wakwe zangu baada ya hapo wata saini. Hivyo wote kama hamto jali mutakuwani wakurugenzi wasaidizi wa kampuni. Nahitaji kila mmoja uwezo wake ufanye kazi”
“Nakuahidi mama nita tumia uwezo wangu wote kufanya kazi uliyo nipa”
Rose laijibu akimtazama Mrs Tiger kwa furaha.
“Hata kuleni sasa twende tuna long day”
Mrs Tiger akaendelea kula. James akamtazama mama yake na kuendelea kula taratibu. Mrs Tiger na wakwe zake wakamaliza kula. Wakatoka nje na kuingia katika gari moja aina ya Cadilic Escalade mbele zikatangulia gari mbili za walinzi aina ya Land Cruiser LC 300 an nyuma yao zikafwatia gari nyingine mbili za aina hiyo na safari ya kuelekea katika kampuni kubwa ya Mrs Tiger inayo jishuhulisha na vipodozi ya kila aina ikaanza. James akatoka nje na kutazama msafara huo jinsi unavyo ondoka nyumbani kwake. Akampigia simu Jack.
“Bro nimekupigia hujapokea”
“Nilikuwa bafuni.”
“Wife ameniambia wana toka na mama?”
“Ndio ana kwenda nao katika kampuni yake ya vipodizo na taarifa ni kwamba ana kwenda kumpa kila mkwe wake asilimia ishirini na tano ya share zake katika kamouni”
“Asilimia ishirini na tano?”
“Ndio dogo”
“Mmmm mama ana mpango gani aisee mboa gafla sana.”
“Nashindwa kuelewa aisee. Ina tupasa kuwa makini kwani hizi asilimia ishirini na tano anazo zitoa zina weza kurudi kwa kitu kikubwa zaidi ya hizo. Tuwe macho dogo”
James alizungumza akiwa haamini kabisa kama mama yake ana toa asilimia hamsini ya hisa za kampuni yake na kuwapa wakwe zake hususani Rose ambaye ni mtoto wa adui ya familia ya mzee Tiger.
ITAENDELEA
Mchaka mchaka mpya umeanza. Mrs Tiger ana toa asilimia hamsini za kampuni yake na kuwapa wakwe zake, je ana mpango gani wa siri ambao ana taka kuutekeleza? Ungana nami katika stori hii ya kusisimua sehemu ya 40.