Devil’s family(familia ya mashetani) 01

Devil’s family(familia ya mashetani) 01

DEVIL’S FAMILY(FAMILIA YA MASHETANI) 56


KILA KILICHO ANDIKWA KATIKA HADITHI HII NI UTUNZI HAKIENDANI NA KISA CHOCHOTE KILICHO WAHI KUTOKEA MAHALA POPOTE ASANTE
*************************************************************************************

ILIPOISHIA
“Kumsogelea kivipi?”
“Pale hospitalini kuna friji la kununua vijanywaji hivyo nilitaka kumchunguza vizuri hapo ndipo nilipo chnaga karata zangu vibaya”
“Na wakakuacha utoke nje ya hospitali”
“Ndio na naamini walitaka kunifwatilia hadi ninao ishi”
“Boaz usije ukaniletea matatizo”
“Huwezi kupata matatizo kuwa na amani. Hujapta taarifa zake?”
“Hapana”
“Daaa. Yule binti ni nani ina bidi nimshuhulikie aisee”
“Kwa nini usiachane na huu mpango”
“Nimesha chukua pesa ya watu. Siwezi kuacha hii kazi na mimi sio mtu wa kukatishwa tamaa na changamoto ndogo kama hizi. Ni lazima nikamishe mission yangu”
“Wewe niambie uta zikwa wapi? Morogoro au hapa hapa Dar. Hawa watu wapo seriously na wamesha kuweka kwenye mabado. Kama leo umeweza kupotea chupu chupu basi kesho wata kukamata rafiki yangu. Nakushauri achana na huu mpango. Hii ngoma unayo taka kuicheza ni nzito kuliko uwezo wako. Jizime data rafiki yangu ila naona mwisho wako una kuwa ni mbaya”
Dokta Boaz akatulia kwa sekunde kadha akiufikiria ushauri anao pewa na rafiki yake, japo ana jiamini kweye kazi yake ya uuaji ila anacho elezwa na rafiki yake ni kitu cha maana na asipo kuwa makini ata kufa.

ENDELEA
“Umenielewa ndugu yangu”
“Mimi ninawaza namna gani ya kuwala vichwa hawa wajinga”
“Seriosly?”
“Ndio naaamisha. Sijawahi kushindwa kazi mimi. Kaa uelewe hivyo”
“Sawa mimi yangu macho ndugu yangu. Nita kuunga mkono kwa kile ukitakacho. Ili mradi jambo lako lisijirudi kwangu”
“Usijali. Nimepata wazo”
“Wazo gani?”
“Ngoja nilifanyie kazi akilini mwangu kisha nitakushirikisha. Hakuna kushindwa hapa, ngoja nikalale kwanza”
Dokta Boaz akanyanyuka na kuelelea chumbani, akaingia chumbani na kujilaza kitandani huku akiendelea kufikiria namna ya kupambana na familia ya mzee Tiger.
***
“Una lala una raha gani?”
Mrs Tiger akakurupuka kutoka usingizini. Akamuona bibi wa familia akiwa amekaa kitandani pembeni yake.
“Nimekuja kwa ajili ya kuikamilisha kazi niliyo kuambia. Fanya maamuzi”
Mrs Tiger akaanza kutetemeka huku akijawa na kigugumizi.
“Umeamua nani wa kufa?”
Mrs Tiger akajifikiria kwa sekunde kadhaa.
“Au nikuchukue wewe”
“Hapana hapa”
“Kwa makosa muliyo yafanya ina ina hitajika kafara ya familia. Zungumza nani wa kufa?”
Mrs Tiger akafumba macho huku machozi yakimbubujika.
“Nakusikiliza”
“Mume wangu”
“Sawa. Shuka kitandan unifwate”
Mrs Tiger akamtazama bibi wa familia kisha taratibu akashuka kitandani na kuanza kumfwata bibi.
“Kitu kimoja ninacho kukubali kuhusiana na wewe ni jinsi ulivyo nyumba yangu hii. Mama yako mkwe alijaribu kubadilisha baadahi ya vitu visivyo badilishwa kwenye hii familia ndio maana niliamua kumshuhikia mapema sana. Naamini ulipo olewa ulisha ambiwa nini cha kutoa na nini si cha kutoa”
“Ndio bibi”
Mfanyakazi wa ndani anaye pishana na Mrs Tiger akageuka kushangaa boss wake kuzungumza mwenyewe.
“Madama”
Mrs Tiger akageuka.
“Ehee na kumtazama mfanyakazi huyo.
“Umeniongelesha?”
Mfanyakazi aliuliza.
“Hapana. Kichwa changu hakipo sawa, kaendelee na kazi”
“Sawa”
Mfanyakazi akaondoka.
“Ina maana hawakuoni?”
“Hakuna anaye kuona zaidi yangu”
Mrs Tiger akazidi kushangaa kwani matukio hayo toka ameolewa na mume wake ndio yanamtokea. Wakaingia ndani ya chumba alichopo Mzee Tiger.
“Madam”
“Mumekula?”
Aliwauliza madaktari wawili.
“Ahaa….bado mkuu”
“Nendeni wakawaandalie chakula.”
“Sawa”
Madaktari wakatoka chumbani na kumuacha Mrs Tiger na mumewe.
“Mume wako leo ndio ina kuwa siku yake ya mwisho kuishi duniani, ata lipia makosa ambayo alikubali yatokee kwenye hii familia”
“Makosa gani?”
“Moja wapo ikiwa ni wewe kuanzisha mahusiano na yule kijana”
Mrs Tiger akakaa kimya akimtazama bibi wa familia.
“Mtoe mpira wa oxygen”
“Ehee”
“Ndio”
Taratibu Mrs Tiger akamtoa mumewe mpira wa hewa ya oxygen inayo msaidia kupumua. Mzee Tiger akafumbua macho na kumtazama mke wake hadi akashtuka.
“Mu….mume wangu”
“Unataka kuniua”
Mzee Tiger alizungumza maneno yaliyo zidi kumvuruga mrs Tiger.
“Chukua mto umalizie”
Bibi wa familia alizungumza.
“Chukua mto”
“Usifanye hivyo mke wangu…….Usiniue”
Mzee Tiger alizungumza na kuzidi kumchanganya mkewe.
“Nimekuambia chukua mto”
Bibi wa Familia alizungumza kwa ukali. Mrs Tiger huku machozi yakimwagika, akachukua mto.
“Usiniue mke wangu………...Nakuomba usiniue”
“Muuueeeee au Jack afeeee”
Mrs Tiger kwa haraka akaanza kumgandamiza usoni mzee Tiger kwa kutumia mto. Mzee Tiger akaanza kurusha rusha miguu yake kwa kukosa pumzi. Galfa mlango ukafunguliwa na wakaingia madaktari wawili.
“Unafanya nini madam”
Daktari mmoja akamuwahi Mrs Tiger na akmapokonya mto. Mrs Tiger akatazama eneo alilo kuwa amesimama bibi wa Familia na hakumuona. Daktari mmoja kwa haraka akmarudishia mzee Tiger mrija wa oxygen.
“Unataka kumuua mumeo?”
Daktari aliye mpokonya simu Mrs Tiger alimuuliza kwa ukali huku akimtazama Mrs Tiger anaye mwagikwa na jasho mwili mzima.
“Kwa nini?”
Mrs Tiger akakaa kwenye sofa la pembeni huku akitetemeka.
“Ingekuwa sio kuunganisha mifumo yake ya hewa na saa zetu ina maana sasa hivi mumeo angekuwa maremu”
Mrs Tiger akakosa cha kuzungumza akabaki akimtazama daktari anaye zungumza kw amsisitizo.
“Unataka tuonekane hatupo makini kwenye utendeji wa kazi yetu?”
“Nisamaheni”
Mrs Tiger akanyanyuka na kutoka chumbani hapo.
“Hili jambo ina bidi tumueleze mwanaye wa kwanza.”
“Vipi hali yake?”
“Imetengemeaa na kurudi kawaida”
“Ngoja nimpigie James”
Daktari aliye kuwa ana mfokea mrs Tiger alizungumza huku akiitafuta namba ya James kwenye simu, akaipata na akampigia simu James.
“Dokta”
“Habar James”
“Salama. Mzee anaendeleaje?”
“Kuna tukio kidogo limetokea”
“Tukio gani?”
“Ahaa tumemkuta mama yako anataka kummalizia mzee kwa bahati nzuri ni kwamba tuliwahi kuingia kwani alarm za saa zetu zili tutaarifu”
“Mama?”
“Ndio James”
“Sawa hali yam zee?”
“Tulimuwahi kumrudshia oxygen na hali yake imerudi kuwa vile vile.”
“Sawa nina shukuru sana kwa hii taarifa. Kwa sasa ngoja niifanyie kazi”
“Tuna shukuru. Tumekupa taarifa mapema ili endapo kikitokea chochote basi mikono yetu iwe misafi”
“Nashukuru”
James akakata simu.
“Kuna nini?”
James akamtazama Rose anaye ndelea kuendesha gari.
“Ngoja dakika moja”
James akaingia kwenye mfumo wa kamera za nyumabani kwao. Akaingia katika kamera ya siri aliyo ifunga chumba alicho lazwa baba yake pasipo mtu yoyote kugundua. Akamuona mama yake akiingia ndani ya chumba akiwa ameongozana na mtu asiye onekana ila kina onekana kivuli chake.
“Hembu simamisha gari pembeni”
Wakasimamisha gari pembeni.
“Ngoja”
James macho yakamtoka kwa mshangao kuona mama yake akiwa nana zungumza na kivuli huku baba yake akiwa naye ana zungumza.
“Umeona”
James aliumuonyesha video hiyo Rose. Wakatazama tukio jinsi linavyo kwenda.
“Aliye simama pembeni ni nani?”
“Haonekani na nikivuli tu”
“Inakuwaje mzee ana zungumza”
“Kuna hali isiyo ya kawaida inayo endelea.”
James alizungumza akimuona mama yake jinsi anavyo mzee Tiger kwa mto usoni. Hadi madaktari walivyo ingia ndipo sauti zikaanza kurekodiwa na kamera hizo.
“Na kile kivuli kimepotea?”
Rose alishangaa.
“Ni jini ujue”
“Jini?”
Rose alizidi kuuliza kwa mshangao.
“Ina wezekana. Hoonekani kwenye kamera, kina onekana kivuli, ana zungumza na mama ambaye ana muona, halafu mzee ambaye ana umwa ana zinduka na kuongea baada ya hapo madaktari kuingia ni kama akawa amezinduka”
“Mmmmm mume wangu ujue hadi damu imenisisimka”
Jack akamtazama Rose.
“Ina wezekana ni wale nilio kuambia”
“Kina nani?”
“Wakuu wa huu ukoo ambao walitaka niuwawe ila mipango yao ya kuniu haijakwenda vyema”
“Mmmm”
“Ndio ona wamempiga mzee, wammepiga dogo na sasa hivi mama ina bidi alazimishe kuwaua”
“Amuue hadi shem?”
“Ina wezekana”
“Mmmm hii ni hatari mume wangu. Mtumie video hiyo mchungaji Kimaro. Kama aliweza kutuombea tukaepukana na hayo mauza uza nina uhakika ana weza kumuombea mama naye akawa sawa”
James akafikiria kwa sekunde kadhaa.
“Ngoja nimpigie simu”
James akampigia simu mchungaji Kimaro.
“Shikamoo mchungaji”
“Marahaba. Tena nilitaka kukupigia simu, umeniwahi”
“Kuna nini?”
James akaweka loud speaker.
“Nimeonyeshwa mukipata ajali mbaya sana wewe na mkeo. Yaani kabla ya chochote tusali”
James na Rose wakatazamana. Mchungaji Kimaro akaanza kusali. Dakika tano zikatosha kwa mchungaji Kimaro kimaliza sala yake.
“Asante sana mchunaji”
“Karibuni. Ulitaka kuniambia nini?”
“Kuna video nina kutumia hapa. Naommba ikiwezekana uende nyumbani”
“Sawa tukutane nyumbani kwenu”
“Mimi na mke wangu kidogo tupo mbali”
“Rudi tukune nyumbani”
“Sawa”
James akakata simu.
“Turudi tu mume wangu”
Rose alizungumza.
“MUNGU wangu!”
James alishangaa mara baada ya kuona lori likishuka kwa mwendo wa kasi kwenye muinuko.
“Mamaaaaaaa”
Rose alipiga kelele ya woga kwani lori hilo lililo poteza breki limewalenga upande wao. Rose akashindwa hata kurudisha gari nyuma. Dereva wa lori akajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kulikwepa gari walilomo James na Rose na akafanikiwa, lori lake likaacha barabara na kuelekea vichakani huku ni kwa mita mbili likipia pelee zikiwa zimelitenganisha gari analo endesha Rose na lori hilo. James akashuhudia jinsi lori hilo lianvyo zidi gonga miti na likasimama kama mita mia moja kutoka ilipo barabara ya lami.
“Babe babe”
James alimshtua Rose aliye fumba macho yake. Rose kwa haraka akaanza kijishika mwilini mwake kuona kama bado yupo hai.
“NIipo hai?”
“Ndio MUNGU ametuepushia. Twende tukamuokoe dereva”
“Nenda mume wangu hata nguvu sina”
“Tulia hapa”
James akashuka ndani ya gari, akakimbilia lilipo lori la mafuta. Akafika eneo lilipo lori na akamkita dereva akiwa amebanwa ndani ya gari huku akilia.
“Fungua mlango”
Alimuambia dereva kwani mlango ameifunga kwa ndani. Dereva kwa jinsia livyo banwa akashindwa hata kufungua mlango. James kwa kutumia kitako cha bastola akavunja kioo cha upande wa dereeva. Akafanikiwa kuufungua mlango kwa ndani.
“Fuc**”
James alizungumza hukua akishindwa kumchomoa dereva alipo banwa. Kwa haraka akashuka kwenye ngazi za gari. Macho yakamtoka mara baada ya kuona mataki mawili yanayo vutwa na kichwa cha lori yakimwaga mafuta huku cheche cheche zikiwa zikiwa zina jitokea kwenye nyaya zilizo katika.
“Spana una weka wapi?”
“Kwenye toolbox”
Akavunja kuvulia kwa kutimia kitako cha bastola kisha akachkua spana kubwa akapandisha ngazi za lori na kuanza kutanua eneo ambalo dereva amebanwa. Taratibu Rose akashuka ndani ya gari, akatazama eneo alilo elekea James. Akazima gari na akalifunga kitendo cha kupiga hatua mbili tu kuelekea lilipo Lori, mlipuko mkubwa ukatokea kitendo kilicho mstua sana Rose na mbaya zaidi James yupo eneo la mlipuko.
ITAENDELEA
Mchaka mchaka mpya umeanza. Mrs Tiger ameshindwa kumuua mume wake baada ya madaktari kuingilia kati je bibi wa familia ata msumbua tena? James katika harakati za kumuokoa dereva, lori la mafuta limelipuka je James ata kuwa hai? Ungana nami katika stori hii ya kusisimua sehemu ya 57.
Ni hatari
 
Back
Top Bottom