Devil’s family(familia ya mashetani) 01

Devil’s family(familia ya mashetani) 01

DEVIL’S FAMILY(FAMILIA YA MASHETANI) 57

KILA KILICHO ANDIKWA KATIKA HADITHI HII NI UTUNZI HAKIENDANI NA KISA CHOCHOTE KILICHO WAHI KUTOKEA MAHALA POPOTE ASANTE
*************************************************************************************

ILIPOISHIA
“Tulia hapa”
James akashuka ndani ya gari, akakimbilia lilipo lori la mafuta. Akafika eneo lilipo lori na akamkita dereva akiwa amebanwa ndani ya gari huku akilia.
“Fungua mlango”
Alimuambia dereva kwani mlango ameifunga kwa ndani. Dereva kwa jinsia livyo banwa akashindwa hata kufungua mlango. James kwa kutumia kitako cha bastola akavunja kioo cha upande wa dereeva. Akafanikiwa kuufungua mlango kwa ndani.
“Fuc**”
James alizungumza hukua akishindwa kumchomoa dereva alipo banwa. Kwa haraka akashuka kwenye ngazi za gari. Macho yakamtoka mara baada ya kuona mataki mawili yanayo vutwa na kichwa cha lori yakimwaga mafuta huku cheche cheche zikiwa zikiwa zina jitokea kwenye nyaya zilizo katika.
“Spana una weka wapi?”
“Kwenye toolbox”
Akavunja kuvulia kwa kutimia kitako cha bastola kisha akachkua spana kubwa akapandisha ngazi za lori na kuanza kutanua eneo ambalo dereva amebanwa. Taratibu Rose akashuka ndani ya gari, akatazama eneo alilo elekea James. Akazima gari na akalifunga kitendo cha kupiga hatua mbili tu kuelekea lilipo Lori, mlipuko mkubwa ukatokea kitendo kilicho mshtua sana Rose na mbaya zaidi James yupo eneo la mlipuko.

ENDELEA
Kwa haraka Rose akaanza kukimbia kuelekea eneo ambalo lori la mafuta limelipuka. Kabla hajafika mlipuo mwengine wa ukatokea na kumfanya Rose kujificha katika moja ya mti mkubwa kwani mlipuko huo una nguvu kubwa sana iliyo ambatana na upepo.
“Usiinue kichwaa”
James alizungumza huku akikiinamisha kichwa cha dereva chini kwenye korongo walipo angukiwa sekunde chache kabla ya lori kulipuka.
“Asante sana”
Dereva alizungumza huku akimtazama James ambaye baada ya kumchomoa kwenye mskani ulio kuwa ume mbana alimbeba begani mwake na kukimbia naye kwa mwenzo wa haraka sana kwa zaidi ya mita arobaini na akadumbukia naye kwenye gema.
“Jamesss”
Rose aliita kwa sauti ya juu sana na kumfanya James kunyanyuka walipo lala.
“Nipo huku, toka hapo bado lina endelea kulipuka”
James alizungumza kwa sauti ya juu na kumfanya Rose akimbilie walipo.
“Mupo salama?”
“Mimi nipo poa ila jamaa mguu umepata shida”
Rose akatazama mguu wa kulia wa dereva ulio vunjika mara mbili.
“Ngoja niombe msaada kwa jeshi la zima moto.”
Rose akapiga simu kwa mkuu wa Wilaya wa eneo walipo. Akaomba masaada na kuelekeza eneo ajali ilipo tokea. Wakasikia sauti za mashuhuda wa ajali. Ikamlazimu James kunyanyuka eneo walip[o jificha.
“Jamani sogeeni bado yana lipuka hayooooooo”
James alizungumza kwa sauti ya juuu kuwapa tahadhari watu wanao sogelea eneo la ajali. Mzinga mwengine ukatokea na kuwafanya watu kukimbia.
“Wameudhurika?”
Rose aliuliza.
“Wamewahi kukimbia”
Dereva akaanza kulia kwa maumivu makali kwani ganzi aliyo kuwa ameipata.
“Jikaze broo soon jamaa wana kuja”
“Naumiaa brooo……maumivu makali”
“Pole una tokea wapi wewe na familia yako?”
“Nimetokea Mtwara ndio ilipo familia yangu”
“Sawa nitajie jina la lako kamili, mke au mtu yoyote wa familia yako tunaye weza kumpatia taarifa ya ajali yako. Garama na matibabu yote mimi na mke wangu tutasimamia matumizi yote na wakifika waokoaji tuta waeleza ni hospitali gani upelekwe”
“Sawa kaka shukrani, nikutajie namba ya kaka yangu”
Dereva akataja namba ya kaka yake na James akainakili katika simu yake.
“Nitampigia uokozi ukisha malizika”
“Nashukuru”
Ving’ora vya gari mbili za zima moto zikafika eneo hilo na kuanza kuzima moto wa eneo hilo. Kwa kusaidiana na wananchi pamoja naa askari wa jeshi la polisi. Dereva akabenwa kutoka eneo la ajali hadi barabarani ambapo akapakizwa ndani ya gari la wagonjwa. James akamuomba dereva wa gari la wagonjw ani wapi kwa kumpeleka mgonjwa.
“Ila ina bidi ahawahishwe hospitali ya wilaya”
“Natambua ila mpeleke katika hospitali niliyo kutajia. Nitajie namba yako ya simu”
James akaingia katika app ya simu ya mtandao wa pesa. Dereva akamtajia namba ya simu.
“Nimekuingizia milioni, laki mbili ongeza mafuta nyingine kama bonus yako ya udereva. Ukimfikisha hospitali niliyo kuambia utapata pesa nyingine ya ziada kama shukrani imekaaje hiyo”
“Asante sana kaka. Chap ana fika Dar”
Dereva alizungumza mane yote thelathini na mbili yapo nje. James akarudi eneo la nyuma ya gari hiyo ya wagonjwa aina ya Land Cruiser Mkonga ambayo ni mali ya hospitali ya wilaya.
“Muangalieni, ikiwezekana mchomeni sindano ya kutuliza maumivu. Ana kwenda mbali”
“Sawa”
“Bro sijakuuliza jina lako unaitwa nani?”
“Suleimani”
“Nesi una kalamu na karatasi”
“Hapana sina”
“Sawa tuna wafwata kwa nyuma tutafika wote hospitalini”
“Asante kaka”
James akaelekea lilipo gari.
“Vipi?”
“Nimepa dereva chochote kitu ili apelekwe hospitali aliyo lazwa dogo”
“Ila Tanzania bwana. Watu hawawezi kufanya kazi bila ya chochote kitu”
“Hapana mke wangu. Ni kumpa nguvu dereva kumbuka ana fanya kazi za humu ndani ya wilaya yake safari za nje ya mkoa ni chache”
“Endesha hapa mwili mzima umechoka”
James akaingia upande wa dereva huku Rose naye akipanda upande wa abiria, taratibu wakaondoka eneo hilo ambalo tayari limesha jaa watu wanao shuhudia kinacho endelea. Ukimya ukatawala ndani ya gari huku wakilifwata gari kwa nyuma.
“Mchungaji Kimaro, MUNGU amempatia karama ya kipekee sana”
“Kwa nini?”
“Si una ona ajali imetupunyua punyua. Kwa maana isinge kuwa hivyo sasa hivi ingekuwa tuna ongea mambo mengine”
“Ndio hivyo mke wangu. Kila mtu na karama yake. Hapa ina bidi dogo akapatie matibabu nyumbani”
“Kwa nini?”
“Una hisi yule mshenzi ata kubali kushindwa kazi. Ni lazima ata fanya mpango wa kubadili sura kwa mara nyingine na kudili ana adui wa aina hiyo sio jambo dogo. Leo kaja kama mzee, kesho ana weza kuja kama mwanamke”
“Ila ni kweli”
“Akiwa nyumbani ulinzi utakuwa ni imara zaidi”
“Sawa mume wangu. Zungumza na Sophia hilo wazo”
“Poa”
James akakata simu na akampigia simu Sophia na akaweka loud speaker.
“Bro”
“Upo wapi?”
“Hospitalini?”
“Dogo hali yake?”
“Ni ile ile hakuna mabadiliko”
“Sasa hali ya kiusalama kwa dogo haipo vyema. Una onaje tuka mrudisha nyumbani”
“Nyumbani?”
“Ndio madakatri wawe wana muhudumia hapo. Nazungumza na mmiliki wa hospitali kisha utaratibu wa kumuondoa hapo ufanyike”
Sophia akatoka ndani ya chumba alicho lazwa Jack.
“Kuna nini kianendelea bro”
“Naamini una jua kuwa kuna mtu alipanga kumuua tena dogo”
“Ndio”
“Nina hofu huyo mtu ana weza akarudia tena na kutaka kumuua. Mbaya ana badilisha sura yake hivyo ana weza kutumia munekano mwengine na akaja kumuua dogo. So zungumza na Chris aondolewe hapo hospitalini”
“Sawa bro”
“Wamuondoe kimya kimya. Nyumbani itakuwa salama kwakwe”
“Poa bro ngoja nimcheki Chris wewe mpigie huyo mmiliki wa hospitali madaktari watakao kuwa wana muangalia”
“Poa poa
Sophia akakata simu.
“Yupo wapi Chriss”
“Ameshuka chini”
“Mcheki aje chap”
Mlinzi akawasiliana na Chris. Baada ya dakika mbili Chris akafika eneo.
“Broo ina bidi tumuhamishe dogo hospitalini tumrudishe nyumbani”
“Kwa nini boss?”
“Kaka kasema hivyo. Yule muuaji ana weza kurudi na kumua dogo tena”
“Sawa”
“Ngoja ana fanya mpango wa madaktari. Wewe andaa msafara wa kumrudisha nyumbani”
“Ina bidi mufanye mazungumzo na madakatri kujua kama kuna uwezekano wa kumsafirisha kwa helicopter au gari. Mimi nita andaa mazingira yote”
“Hakuna tatizo”
Sophia akarudi ndani.
“Kuna nini wifi?”
Vaileth aliuliza huku akimtazama Sophia.
“Ina bidi tumrudishe nyumbani kwa ajili ya usalama wake. Kama munavyo fahamu kuwa mazingira ya hali yake yana tokana na kutaka kuuliwa. Tuna hofia ana weza kutaka kuuliwa tena hivyo ina bidi tumrudishe nyumbani”
“Sawa wifi”
Sophia akamtazama Valentina aliye fumba macho hukua kiomba.
***
“Boss kuna mwana mama yupo nje ya geti”
“Mwana mama”
“Ndio ana hitaji kuonana na wewe”
Mwanamama bilionea akamtazama mlinzi wake.
“Tumemzuia kuingia kwa maana hatumtambui hana kitambilisho chochote”
“Kama ana omba msaada mpeni pesa aondoke”
“Amesema ana hitaji kuonana na wewe ni muhimu”
“Mkagueni na mumuingize ndani akae eneo la kupumzikia”
“Sawa”
Mwana mama bilionea akanyanyuka na akatembea hadi kwenye kibaraza cha gorofa lake. Akatazama jinsi mwana mama aliye valia vitenge akikaguliwa na mlinzi wa kike kisha akasindikzwa hadi kwenye eneo la kupumzikia.
“Anaitwa nani?”
Alimuuliza mlinzi wake aliye simama pembeni.
“Mama Bite”
“Ndio nani?”
“Labda ukazungumze naye”
Mwana mama bilionea akaongozana na mlinzi wake hadi kwenye eneo la kupumzikia alipo mama Bite.
“Karibu”
“Una walinzi wa hovyo sana”
“Boaz”
“Yaani nimevalia hivi na hakuna aliye nitambua aiseee. Kama ni mtu angetaka kukuua si angesha kamilisha kazi yake”
Dokta Boaz alizungumza huku akivua sura ya bandia aliyo ivaa na kuwafanya walinzi wawili wa mama bilionea kushangaa.
“Nendeni nina mazungumza na boss wenu”
Walinzi wakamtazama mwana boss wao. Akawapa ishara ya kuondoka na walinzi wake wakaondoka.
“Kuna nini kimetokea mbona upo hapa na muonekano kama mwanamke”
Dokta Boaz hakujibu kitu, akaendelea kutoa maziwa ya bandia aliyo yavaa kifuani mwake, akavua makalio ya bandia ambayo ameyavaa.
“Madude mazito. Wanawake muna wezaje kutembea na makalio makubwa na maziwa kama hivi”
“Ndio maana tumekuwa wanawake. Vipi?”
“Poa ilibidi nitumie njia hii kuondoka Dar es Salaam kwa maana huko kote nina sakwa kama dhahabu”
“Imekuwaje”
Dokta Boaz akamuelezea mwana mama huyo jinsi Rose alivyo haribu mipango yake.
“Una picha ya huyo binti?”
“Ni mkwe wa hiyo familia. Mke wa James ila yule dada ni afisa usalama ambaye ana jicho moja kali sana la kuweza kujua mtu huyu ni mwema au si mwema”
“Tuna fanyaje?”
“Ina bidi kuandaa kikosi kazi”
“Kikosi kazi kivipi?”
“Sasa hivi tuna paswa kwenda uso kwa uso kupambana nao. Wamesha block mianya yote ya kumdhuru mwana familia yoyote yule”
“Hao watu tunao watafuta ni kina nani na tuta wapatia wapi?”
“Nina timu ya x specila force watano. Nina watumia mara kadhaa katika mission za ku hita and run”
“Watano wata tosha ikiwa Tiger ana vikosi kabisa”
“Ni kweli ila jamaa wana mziki mkubwa. Jamaa wana uwezo wa kufanya mission ngumu. Nchi iliwatumia kwenye mission nyingi sana”
“Walikuwa ni wanajeshi wan chi hii?”
“Ndio”
“Una uhakika wata ifanya hiyo kazi?”
“Asilimia mia moja. Na ikikupendeza hili swala langu nina omba ulizime. Nimesha ingia kwenye rekodi za vyombo vya usalama, si polisi na wala si shirika la X wana nisaka sana”
Mwana mama bilionea akajirikiria kwa muda kidogo.
“Sawa nita jua jinsi ya kulimaliza hili na kulifuta. Ila kumbuka tuna weza kulifuta kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ila si kwa ile familia”
“Najua”
“Kumbuka wale ndio wameshikilia hii nchi. Endapo tukiwasambaratisha itakuwa ni nafasi yangu nzuri ya kugombania kiti cha uraisi. Siwezi kugombania endapo wapo hai”
“Kwa nini una taka kumuua Tiger na familia yake”
“Unataka kujua?”
“Ndio”
“Leo nitakuambia ni kwa nini nilijiapiza kumuua Tiger na familia yake nzima”
Mwanamama bilionea alizungumza na kumfanya dokta Boaz kukaa vizuri ili kumsikiliza.
ITAENDELEA
Mchaka mchaka mpya umeanza. Wameamua kumrudisha Jack nyumbani ili kumuepusha na muuaji ambaye ni dokta Boaz. Ila dokta Boaz amekuja na mpango mwengine wa kutumia makomandoo kwenda kuivamia familia ya Tiger je nini kita tokea? Ni nini mwana mama bilionea alicho fanyiwa na mzee Tiger? Ungana nami katika stori hii ya kusisimua sehemu ya 58.
 
DEVIL’S FAMILY(FAMILIA YA MASHETANI) 57

KILA KILICHO ANDIKWA KATIKA HADITHI HII NI UTUNZI HAKIENDANI NA KISA CHOCHOTE KILICHO WAHI KUTOKEA MAHALA POPOTE ASANTE
*************************************************************************************

ILIPOISHIA
“Tulia hapa”
James akashuka ndani ya gari, akakimbilia lilipo lori la mafuta. Akafika eneo lilipo lori na akamkita dereva akiwa amebanwa ndani ya gari huku akilia.
“Fungua mlango”
Alimuambia dereva kwani mlango ameifunga kwa ndani. Dereva kwa jinsia livyo banwa akashindwa hata kufungua mlango. James kwa kutumia kitako cha bastola akavunja kioo cha upande wa dereeva. Akafanikiwa kuufungua mlango kwa ndani.
“Fuc**”
James alizungumza hukua akishindwa kumchomoa dereva alipo banwa. Kwa haraka akashuka kwenye ngazi za gari. Macho yakamtoka mara baada ya kuona mataki mawili yanayo vutwa na kichwa cha lori yakimwaga mafuta huku cheche cheche zikiwa zikiwa zina jitokea kwenye nyaya zilizo katika.
“Spana una weka wapi?”
“Kwenye toolbox”
Akavunja kuvulia kwa kutimia kitako cha bastola kisha akachkua spana kubwa akapandisha ngazi za lori na kuanza kutanua eneo ambalo dereva amebanwa. Taratibu Rose akashuka ndani ya gari, akatazama eneo alilo elekea James. Akazima gari na akalifunga kitendo cha kupiga hatua mbili tu kuelekea lilipo Lori, mlipuko mkubwa ukatokea kitendo kilicho mshtua sana Rose na mbaya zaidi James yupo eneo la mlipuko.

ENDELEA
Kwa haraka Rose akaanza kukimbia kuelekea eneo ambalo lori la mafuta limelipuka. Kabla hajafika mlipuo mwengine wa ukatokea na kumfanya Rose kujificha katika moja ya mti mkubwa kwani mlipuko huo una nguvu kubwa sana iliyo ambatana na upepo.
“Usiinue kichwaa”
James alizungumza huku akikiinamisha kichwa cha dereva chini kwenye korongo walipo angukiwa sekunde chache kabla ya lori kulipuka.
“Asante sana”
Dereva alizungumza huku akimtazama James ambaye baada ya kumchomoa kwenye mskani ulio kuwa ume mbana alimbeba begani mwake na kukimbia naye kwa mwenzo wa haraka sana kwa zaidi ya mita arobaini na akadumbukia naye kwenye gema.
“Jamesss”
Rose aliita kwa sauti ya juu sana na kumfanya James kunyanyuka walipo lala.
“Nipo huku, toka hapo bado lina endelea kulipuka”
James alizungumza kwa sauti ya juu na kumfanya Rose akimbilie walipo.
“Mupo salama?”
“Mimi nipo poa ila jamaa mguu umepata shida”
Rose akatazama mguu wa kulia wa dereva ulio vunjika mara mbili.
“Ngoja niombe msaada kwa jeshi la zima moto.”
Rose akapiga simu kwa mkuu wa Wilaya wa eneo walipo. Akaomba masaada na kuelekeza eneo ajali ilipo tokea. Wakasikia sauti za mashuhuda wa ajali. Ikamlazimu James kunyanyuka eneo walip[o jificha.
“Jamani sogeeni bado yana lipuka hayooooooo”
James alizungumza kwa sauti ya juuu kuwapa tahadhari watu wanao sogelea eneo la ajali. Mzinga mwengine ukatokea na kuwafanya watu kukimbia.
“Wameudhurika?”
Rose aliuliza.
“Wamewahi kukimbia”
Dereva akaanza kulia kwa maumivu makali kwani ganzi aliyo kuwa ameipata.
“Jikaze broo soon jamaa wana kuja”
“Naumiaa brooo……maumivu makali”
“Pole una tokea wapi wewe na familia yako?”
“Nimetokea Mtwara ndio ilipo familia yangu”
“Sawa nitajie jina la lako kamili, mke au mtu yoyote wa familia yako tunaye weza kumpatia taarifa ya ajali yako. Garama na matibabu yote mimi na mke wangu tutasimamia matumizi yote na wakifika waokoaji tuta waeleza ni hospitali gani upelekwe”
“Sawa kaka shukrani, nikutajie namba ya kaka yangu”
Dereva akataja namba ya kaka yake na James akainakili katika simu yake.
“Nitampigia uokozi ukisha malizika”
“Nashukuru”
Ving’ora vya gari mbili za zima moto zikafika eneo hilo na kuanza kuzima moto wa eneo hilo. Kwa kusaidiana na wananchi pamoja naa askari wa jeshi la polisi. Dereva akabenwa kutoka eneo la ajali hadi barabarani ambapo akapakizwa ndani ya gari la wagonjwa. James akamuomba dereva wa gari la wagonjw ani wapi kwa kumpeleka mgonjwa.
“Ila ina bidi ahawahishwe hospitali ya wilaya”
“Natambua ila mpeleke katika hospitali niliyo kutajia. Nitajie namba yako ya simu”
James akaingia katika app ya simu ya mtandao wa pesa. Dereva akamtajia namba ya simu.
“Nimekuingizia milioni, laki mbili ongeza mafuta nyingine kama bonus yako ya udereva. Ukimfikisha hospitali niliyo kuambia utapata pesa nyingine ya ziada kama shukrani imekaaje hiyo”
“Asante sana kaka. Chap ana fika Dar”
Dereva alizungumza mane yote thelathini na mbili yapo nje. James akarudi eneo la nyuma ya gari hiyo ya wagonjwa aina ya Land Cruiser Mkonga ambayo ni mali ya hospitali ya wilaya.
“Muangalieni, ikiwezekana mchomeni sindano ya kutuliza maumivu. Ana kwenda mbali”
“Sawa”
“Bro sijakuuliza jina lako unaitwa nani?”
“Suleimani”
“Nesi una kalamu na karatasi”
“Hapana sina”
“Sawa tuna wafwata kwa nyuma tutafika wote hospitalini”
“Asante kaka”
James akaelekea lilipo gari.
“Vipi?”
“Nimepa dereva chochote kitu ili apelekwe hospitali aliyo lazwa dogo”
“Ila Tanzania bwana. Watu hawawezi kufanya kazi bila ya chochote kitu”
“Hapana mke wangu. Ni kumpa nguvu dereva kumbuka ana fanya kazi za humu ndani ya wilaya yake safari za nje ya mkoa ni chache”
“Endesha hapa mwili mzima umechoka”
James akaingia upande wa dereva huku Rose naye akipanda upande wa abiria, taratibu wakaondoka eneo hilo ambalo tayari limesha jaa watu wanao shuhudia kinacho endelea. Ukimya ukatawala ndani ya gari huku wakilifwata gari kwa nyuma.
“Mchungaji Kimaro, MUNGU amempatia karama ya kipekee sana”
“Kwa nini?”
“Si una ona ajali imetupunyua punyua. Kwa maana isinge kuwa hivyo sasa hivi ingekuwa tuna ongea mambo mengine”
“Ndio hivyo mke wangu. Kila mtu na karama yake. Hapa ina bidi dogo akapatie matibabu nyumbani”
“Kwa nini?”
“Una hisi yule mshenzi ata kubali kushindwa kazi. Ni lazima ata fanya mpango wa kubadili sura kwa mara nyingine na kudili ana adui wa aina hiyo sio jambo dogo. Leo kaja kama mzee, kesho ana weza kuja kama mwanamke”
“Ila ni kweli”
“Akiwa nyumbani ulinzi utakuwa ni imara zaidi”
“Sawa mume wangu. Zungumza na Sophia hilo wazo”
“Poa”
James akakata simu na akampigia simu Sophia na akaweka loud speaker.
“Bro”
“Upo wapi?”
“Hospitalini?”
“Dogo hali yake?”
“Ni ile ile hakuna mabadiliko”
“Sasa hali ya kiusalama kwa dogo haipo vyema. Una onaje tuka mrudisha nyumbani”
“Nyumbani?”
“Ndio madakatri wawe wana muhudumia hapo. Nazungumza na mmiliki wa hospitali kisha utaratibu wa kumuondoa hapo ufanyike”
Sophia akatoka ndani ya chumba alicho lazwa Jack.
“Kuna nini kianendelea bro”
“Naamini una jua kuwa kuna mtu alipanga kumuua tena dogo”
“Ndio”
“Nina hofu huyo mtu ana weza akarudia tena na kutaka kumuua. Mbaya ana badilisha sura yake hivyo ana weza kutumia munekano mwengine na akaja kumuua dogo. So zungumza na Chris aondolewe hapo hospitalini”
“Sawa bro”
“Wamuondoe kimya kimya. Nyumbani itakuwa salama kwakwe”
“Poa bro ngoja nimcheki Chris wewe mpigie huyo mmiliki wa hospitali madaktari watakao kuwa wana muangalia”
“Poa poa
Sophia akakata simu.
“Yupo wapi Chriss”
“Ameshuka chini”
“Mcheki aje chap”
Mlinzi akawasiliana na Chris. Baada ya dakika mbili Chris akafika eneo.
“Broo ina bidi tumuhamishe dogo hospitalini tumrudishe nyumbani”
“Kwa nini boss?”
“Kaka kasema hivyo. Yule muuaji ana weza kurudi na kumua dogo tena”
“Sawa”
“Ngoja ana fanya mpango wa madaktari. Wewe andaa msafara wa kumrudisha nyumbani”
“Ina bidi mufanye mazungumzo na madakatri kujua kama kuna uwezekano wa kumsafirisha kwa helicopter au gari. Mimi nita andaa mazingira yote”
“Hakuna tatizo”
Sophia akarudi ndani.
“Kuna nini wifi?”
Vaileth aliuliza huku akimtazama Sophia.
“Ina bidi tumrudishe nyumbani kwa ajili ya usalama wake. Kama munavyo fahamu kuwa mazingira ya hali yake yana tokana na kutaka kuuliwa. Tuna hofia ana weza kutaka kuuliwa tena hivyo ina bidi tumrudishe nyumbani”
“Sawa wifi”
Sophia akamtazama Valentina aliye fumba macho hukua kiomba.
***
“Boss kuna mwana mama yupo nje ya geti”
“Mwana mama”
“Ndio ana hitaji kuonana na wewe”
Mwanamama bilionea akamtazama mlinzi wake.
“Tumemzuia kuingia kwa maana hatumtambui hana kitambilisho chochote”
“Kama ana omba msaada mpeni pesa aondoke”
“Amesema ana hitaji kuonana na wewe ni muhimu”
“Mkagueni na mumuingize ndani akae eneo la kupumzikia”
“Sawa”
Mwana mama bilionea akanyanyuka na akatembea hadi kwenye kibaraza cha gorofa lake. Akatazama jinsi mwana mama aliye valia vitenge akikaguliwa na mlinzi wa kike kisha akasindikzwa hadi kwenye eneo la kupumzikia.
“Anaitwa nani?”
Alimuuliza mlinzi wake aliye simama pembeni.
“Mama Bite”
“Ndio nani?”
“Labda ukazungumze naye”
Mwana mama bilionea akaongozana na mlinzi wake hadi kwenye eneo la kupumzikia alipo mama Bite.
“Karibu”
“Una walinzi wa hovyo sana”
“Boaz”
“Yaani nimevalia hivi na hakuna aliye nitambua aiseee. Kama ni mtu angetaka kukuua si angesha kamilisha kazi yake”
Dokta Boaz alizungumza huku akivua sura ya bandia aliyo ivaa na kuwafanya walinzi wawili wa mama bilionea kushangaa.
“Nendeni nina mazungumza na boss wenu”
Walinzi wakamtazama mwana boss wao. Akawapa ishara ya kuondoka na walinzi wake wakaondoka.
“Kuna nini kimetokea mbona upo hapa na muonekano kama mwanamke”
Dokta Boaz hakujibu kitu, akaendelea kutoa maziwa ya bandia aliyovaa kifuani mwake, akavua makalio ya bandia ambayo ameyavaa.
"Madude. Wanawake muna wezaje kutembea na makalio makubwa na maziwa kama hivi"
"Ndio maana tumekuwa wanawake. Vipi?"
“Poa ilibidi nitumie njia hii kuondoka Dar es Salaam kwa maana huko kote nina sakwa kama dhahabu”
“Imekuwaje”
Dokta Boaz akamuelezea mwana mama huyo jinsi Rose alivyo haribu mipango yake.
“Una picha ya huyo binti?”
“Ni mkwe wa hiyo familia. Mke wa James ila yule dada ni afisa ambaye ana jicho moja kali sana la kuweza kujua mtu huyu ni mwema au si mwema”
“Tuna fanyaje?”
“Ina bidi kuandaa kikosi kazi”
“Kikosi kazi kivipi?”
“Sasa tuna paswa kwenda usoni kwa uso kutumia nao. Wamesha block mianya yote ya kumdhuru mwana yeyote yule”
“Hao watu tunao watafuta ni kina nani na tutawapatia wapi?”
"Nina timu ya x specila force watano. Nina watumia mara kadhaa katika mission za kuhita and run"
"Watano watatosha ikiwa Tiger ana vikosi kabisa"
“Ni kweli ila jamaa wana mziki mkubwa Jamaa wana uwezo wa kufanya utume ngumu.
"Walikuwa ni macho wan chi hii?"
“Ndio”
“Una uhakika wata ifanya hiyo kazi?”
“Asilimia mia moja Na ikikupendeza hili swala langu nina omba ulizime Nimesha ingia kwenye rekodi za vyombo vya usalama, si polisi wala si shirika la X wana nisaka sana”
Mwana mama bilionea akajirikiria kwa muda kidogo.
"Sawa nitajua jinsi ya kulimaliza hili na kulifuta. Ila kumbuka tuna weza kulifuta kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ila kwa ile familia"
"Najua"
"Kumbuka wale ndio wameshikilia nchi hii. Endapo tukiwasambaratisha itakuwa ni nafasi yangu nzuri ya kugombania kiti cha urais. Siwezi kugombania endapo wapo hai"
“Kwa nini una taka kumuua Tiger na familia yake”
“Unataka kujua?”
“Ndio”
“Leo nitakuambia ni kwa nini nilijiapiza kumuua Tiger na familia yake nzima”
Mwanamama bilionea alizungumza na kumfanya dokta Boaz kukaa vizuri ili kumsikiliza.
ITAENDELEA
Mchaka mchaka mpya umeanza. Wameamua kumrudisha Jack nyumbani ili kumuepusha na muuaji ambaye ni dokta Boaz. Ila dokta Boaz amekuja na mpango mwengine wa kutumia makomandoo kwenda kuivamia familia ya Tiger je nini kitatokea? Ni nini mwana mama bilionea alicho fanyiwa na mzee Tiger? Ungana nami katika stori hii ya kusisimua sehemu ya 58.
Ahsante sana kaka
 
DEVIL’S FAMILY(FAMILIA YA MASHETANI) 58

KILA KILICHO ANDIKWA KATIKA HADITHI HII NI UTUNZI HAKIENDANI NA KISA CHOCHOTE KILICHO WAHI KUTOKEA MAHALA POPOTE ASANTE
*************************************************************************************

ILIPOISHIA
“Una uhakika wata ifanya hiyo kazi?”
“Asilimia mia moja. Na ikikupendeza hili swala langu nina omba ulizime. Nimesha ingia kwenye rekodi za vyombo vya usalama, si polisi na wala si shirika la X wana nisaka sana”
Mwana mama bilionea akajirikiria kwa muda kidogo.
“Sawa nita jua jinsi ya kulimaliza hili na kulifuta. Ila kumbuka tuna weza kulifuta kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ila si kwa ile familia”
“Najua”
“Kumbuka wale ndio wameshikilia hii nchi. Endapo tukiwasambaratisha itakuwa ni nafasi yangu nzuri ya kugombania kiti cha uraisi. Siwezi kugombania endapo wapo hai”
“Kwa nini una taka kumuua Tiger na familia yake”
“Unataka kujua?”
“Ndio”
“Leo nitakuambia ni kwa nini nilijiapiza kumuua Tiger na familia yake nzima”
Mwanamama bilionea alizungumza na kumfanya dokta Boaz kukaa vizuri ili kumsikiliza.

ENDELEA
“Mimi na Tiger tulikuwa na mahusiano ya kimapenzi toka tukiwa secondary school. Mama yangu alikuwa ni waziri mkuu kwa kipindi hicho. Mahusiano yetu yalifanya hadi mama na baba yake kuwa na urafiki wa kibiashara. Shida ilianza kujitokeza pale mama yangu alipo taka kuja kuwa raisi. Mzee Tiger alisha andaa mgombea wake jambo lililo sababisha wakatofautiana na mama. Kipindi hicho nilikuwa ni mjamzito wa mwananangu. Tiger akaniacha na akaoa mke wake wa sasa. Niliumia sana tena sana. Hawakuishia hapo wakamuua mama yangu, wakataka kuniua na mimi na ilinilazimu kukimbia nchini na kubadilisha utambulisho wangu. Niliendesha makampuni ya mama yaliyopo nje ya nchi kimya kimya na kuyakuza katika kiwango cha juu sana. Kuanzia kipindi hicho nilijiapiza kuja kulipa kisasi kwa Tiger na kizazi chake chote. Hivyo kurudi kwangu Tanzania nina mission mbili, moja kumfuta Tiger kwenye uso wa dunia yeye na wanaye. Baada ya hapo nita timiza ndoto ya mama yangu kuwa raisi. Nita futa mfumo wa Tiger kuweka raisi yule wanaye mtaka”
“Kama ni familia nzima basi wazo langu la kuongeza timu zaidi ya hao nilio kuambia. Mimi peke yangu wamesha ni block kwani nguvu waliyo itumia kuwatendea walio kukutendea wewe na mama yako basi ndio nguvu walio nayo hadi leo”
“Sawa nimekuelewa. Kwa tadhimini yako tuna hitaji makomandoo wangapi kwani nita walipa wote ila wewe ndio utakaye ongoza hii oparesheni”
Dokta Boaz akatabasamu.
“Tuna hitaji makomandoo arobaini. Wataalamu wa udukuzi wasio pungua watau au wanne, wale high level hackers ambao wana weza kupambana na mfumo mzima nyumbani kwa Tiger na kama tuna kwenda kuvamia basi tunavamia kweli hatoto acha kiumbe hai atakaye kutwa pale”
“Sawa fanya kile ambacho una ona kina wezekana kuituliza hasira yangu”
“Sawa acha nianze kuwaanda hao makomandoo”
“Nita kutana nao katika nyumba yangu ya Mkuranga”
“Sawa mkuu. Ngoja nikakusanye timu hiyo. Natangulia Mkuranga kabisa kwani hapa Morogoro nimepita kwenye eneo la nyumba yangu na kituo cha watoto maafisa ni wengi sana”
“Sawa hakikisha hili jambo halinifikii”
“Haliwezi kukufikia tuna kutana mkuranga”
“Ngoja nikuletee simu ambayo tuta wasiliana.”
Mwana mama tajiri akanyanyuka na kuelekea ndani, baada ya muda mfupi akarudi akiwa na simu.
“Ni simu maalumu ambayo haiwezi kuwa traced kwa chochote hivyo ni salama kuwasiliana na mimi humo”
“Poa”
Dokta Boaz akavaa maziwa ya bandia, makalio ya bandia, akavaa sura ya bandia na kurudi katika muonekano wa mwana mama.
“Utaalamu wote huo umeupatia wapi?”
“Ukiwa muuaji ni lazima uwe na mbinu nyingi”
“Nime kukubali sana”
“Tuta onana”
“Una hitaji gari kwa ajili ya usafiri?”
“Sina leseni na barabara imetawaliwa na askari wengi. Nita panda basi”
“Sawa. Hadi lini watakuwa wamesha fika?”
“Kesho usiku”
“Silaha?”
“Hilo niachie mimi”
“Sawa”
Dokta Boaz akaondoka nyumbani kwa mwana mama huyo.
***
“Madam kuna mgeni?”
Mfanyakazi wa ndani alimuambia Mrs Tiger aliye lala kitandani, kwani kilicho tokea masaa machache bado hakijamtoka akilini mwake.
“Nani”
“Amejitambulisha kwa jina la mchungaji Kimaro”
“Muambie nina kuja”
Mrs Tiger akajifikiria kwa sekunde kadhaa, taratibu akashuka kitandani, akavaa sendo na kuelekea sebleni.
“Mchungaji karibu”
“Asante sana. Bwana Yesu asifiwe?”
“Amen. Hawajakupa hata maji? Unatumia kinywaji gani?”
“Asante sana. Unaendeleaje?”
“Naendelea vizuri”
“Mzee”
“Ahaa mzee kusema kweli ana umwa”
“Poleni sana. Nilizungumza na James na akaniomba nije nimuone kwanza mzee”
“Ohooo, umewasilian anaye?”
“Ni muda tu toka nimewasiliana naye yamesha pita masaa mawili, nimechelewa kuja kwani kuna huduma nilikuwa nina ifanya mahali. Ila kama kuna mzee yupo hapa basi tuna weza kwenda kumuona”
Mrs Tiger akashusha pumzi nyingi.
“Sawa twende”
Wakanyanyuka na kuelekea katika chumba alicho lazwa mzee Tiger. Madaktari wote wakamtazamam Mrs Tiger kwa mshangao.
“Naombeni mutupishe”
Madaktari wakatazamana.
“Nimesema nipisheni”
“Madam najua una jua ulicho taka kukifanya kwa mzee. Hatukuamini, tunacho fanya ni kulinda usalama wa mzee”
“Muna hitaji niite walizni wawaote kwa nguvu”
“Mama hakuna haja. Endeleeni kuwepo tu, wao wana tibu afya mimi nina tibu kiroho”
“Hili halito waacha nita hakikisha kazi zenu zina kwenda kupotea na muna pokonywa leseni zenu na hakuna sehemu ambayo muta ajiriwa”
Mrs Tiger alizungumza kwa ukali.
“Hamna haja ya kuwafanyia hayo yote. Nimekuja kumuombea mzee, madakatri wata endelea na kazi yao usiwatendee ubaya”
Mchunganji Kimaro alizungumza kwa sauti ya upole na kumfanya Mrs Tiger kutulia.
“James amenitumia video ya kilicho tokea.”
Mchungaji Kimaro akatoa simu yake mfukoni na akamuonyesha Mrs Tiger na madaktari video ya tukio ambalo Mrs Tiger alijaribu kumuua mumewe. Mrs Tiger akaanza kumwagikwa na machozi.
“Naamini mumeona kivuli pembeni yake. Kivuli ambacho kina ashiria kwamba Mrs Tiger hakuwa mwenyewe. Kuna roho zimemshinikiza kufanya alicho ambiwa kukifanya si kweli?”
Mrs Tiger alizungumza huku akitingisha kichwa.
“Kama ni hivyo basi hili swala hatupswi kulichukulia kuwa Mrs Tiger ni mualifu. Tumeelewana?”
Madaktari wakatingisha vichwa. Mchungaji Kimaro akaiweka simu yake mfukoni na akamsogelea mzee Tiger.
“Mchungaji ata pona?”
Mrs Tiger alizungumza akiwa na wasiwasi.
“Ina bidi nimuungamishe”
“Ndio…..!?”
“Kumtubisha dhambi zake hicho ndio ninacho weza kukifanya kwa sasa”
Mchungaji Kimaro akaushika mkono mzee Tiger na akaanza kuomba. Baada ya dakika kumi akauachia mkono wa mzee Tiger. Mashine ya kupima mapigo ya moyo ikaanza kutoa mlio wa hatari huku mapigo ya moyo ya mzee Tiger yakizidi kwenda chini taratibu, kitu kilicho wafanya madaktari kuanza kupambana na jinsi ya kurudisha mapigo yake ya moyo.
“Mbona….mbona….mbona mapigo yana shuka?”
Mrs Tiger aliuliza akiwa amechachawa. Mstari ulio nyooka ukaonekana kwenye screen ya mashine ya kuhesabu mapigo ya moyo. Madaktari wakachukua mashine maalimu ya kustulia mapigo ya moyo, wamshtua mapigo ya moyo mzee Tiger kwa kumueweka mashine kifuani ila mapigo ya moyo hayakurudi.
“Musijishumbe. Mzee amapumzika kwa amani”
Mchungaji Kimaro alizungumza huku akiwatazama madakatri wanao pambana. Mrs Tiger akaanza kulia kwa kilio kikubwa na kumfanya mchungaji Kimaro kuanza kubembeleza.
***
“Ina maana hawajaondoka”
James alizungumza huku akisimamisha gari kwenye magesho ya hospitalini.”
“Ina wezekana”
Wakashuka ndani ya gari. Wakatazama jinsi dereva wa lori anavyo shushwa ndani ya gari ya wogonjwa. Wakatembea hadi eneo alipo dereva la gari la wagonjwa.
“Boss upo vizuri, sana kwenye kuendesha kila nilipo kuwa nina ongeza kasi nina kuona kwa nyuma”
Dereva wa gari ya wgaonjwa alizungumza hukua kicheka cheka.
“Uwezo wa gari pia una changia.”
“Kwa kweli”
“Nitajie tena namba yako”
Dereva akataja namba na James akamuingizia laki tatu.
“Asante sana tajiri. MUNGU azidi kukufungulia milango ya baraka”
“Nashukuru”
James akawafwata manesi walio ongozana na mgonjwa kutoka eneo la tukio na kila mmoja akamuingizia kisia cha laki tano kwenye simu yake.
“MUNGU awatangulie murudi salama”
“Amen”
James akamfwata Rose alipo simama na mlinzi.
“Vipi?”
“Wana sema bado hawajaruhusiwa kuondoka kwa maana madakatri hawajatoa ripoti ya kuruhusu mgonjwa kuondoka”
“Kwa nini muda wote huo?”
“Ina wezekana kwa hali yake ya kiafua wameona kuna hatari kumuondoa hospitalini kwa helicopter au gari”
Mlinzi alizungumza huku wakitembea kuingia ndnai ya hospitali. Wakaingia ndani ya lifti ikawapeleka moja kwa moja hadi katika hadi katika gorofa kilipo chumba alicho lazwa Jack. Wakakutana na Chris.
“Bora mumekuja boss”
“Kwa nini?”
“Wamekataa kutoa ruhusa”
“Nita zungumza nao”
Kila mlinzi akamshangaa James jinsi alivyo chafuka shati lake. Wakaingia ndani ya chumba alicho lazwa James.
“Bora umekuja wamekataa bwana kumruhusu dogo”
Sophia alizungumza.
“Mbona umechafuka”
“Kuna mtu tulimuokoa kweye ajali”
“Wapi?”
“Katikati ya mkoa wa Pwani. So madaktari wamesemaje?”
“Wamesema kuwa ni hatari kumuhamisha mgonjwa kwenye hali kama hii, kwani mstuko wowote ukitoka una weza kupelekea mstuko katika ubongo na endapo likitoka jambo kama hilo lazima dishi licheze”
“Na wakatupa karatasi za kutia sahihi kwamba endapo lolote litakalo mkuta mgonjwa wao kama hospitali hawato husika. Nimeshindwa kutia sahihi, Valentina naye ameshindwa kutia sahihi tumekusubiria wewe utie sahihi”
“Zipo wapi”
Sophia akampa James karatasi zinao oneyesha familia kuruhusu kumchukua mgonjwa na endapo kuta tokea chochote cha kutokea basi hospitali haito husika na madhara yatakayo mkuta mgonjwa.
“Wana sema akili yake ina hitaji kupata utulivu”
Valentina aliongezea.
“Kama ni hivyo mume wangu. Tusimuahimieshe kikubwa watakao kuwa wana ruhusiwa kuingia hapa ni wana familia na madakatri wake”
Rose alimshauri James. James akatulia kwa sekunde kadhaa.
“Babe”
“Mmmm”
“Mbona umezama kwenye dimbwi la mawazo?”
“Moyo wangu umepoteza amani gafla tu”
“Kwa nini?”
Rose alimuuliza James.
“Sijui kwa kweli”
“Shem kama moyo wako umepoteza amani usitie sahihi.”
“Sawa shem”
James akamrudishia Sophia karatasi hizo.
‘Kuna nini kinacho tokea?’
James alijiuliza akiwa ana hisia mbaya moyoni mwake. Simu ya James ikaanza kuita, akaitoa mfukoni na kuona namba ya mchungaji Kimaro. Rose akasoma jina linalo onekana kwenye kioo cha simu ya James.
“Mbona hupokei”
Rose aliuliza. James akapokea simu hiyo.
“Mchungaji”
“Upo sehemu nzuri”
“Ahaa…yes nipo hospitali”
“Habari niliyo nayo kidogo sio nzuri”
“Kuna nini?”
Kila mtu akamtazama James.
“Mzee ametutoka”
James akashusha pumzi nyingi.
“James umenisikia?”
“Ndio nimekusikia mchungaji”
“Jambo la kumshukuru MUNGU ni kwamba amekufa katika bwana. Niliweza kumuugamisha dhambi zake kabla ya MUNGU hajaichukua roho yake”
“Nashukuru kwa huduma na taarifa”
“Utanikuta nyumbani”
“Sawa”
James akakata simu, akamtazama Sophia.
“Kuna nini?”
Sophia aliweza kumsoma James kwa haraka na hata swali ameuliza katika hali ya wasiwasi. James taratibu akakaa kwenye moja ya kiti.
“Baba amefariki dunia jioni hii”
James alizungumza kwa sauti ya upole akiwatazama Sophia na wezake.
ITAENDELEA
Mchaka mchaka mpya umeanza. Anacho kipanga mwana mama bilionea na dokta Boaz ni kibaya sana kwa familia ya mzee Tiger ambayo tayari imesha patwa na pigo moja baya la kuondokewa na nguzo ya familia mzee Tiger? Ungana nami katika stori hii ya kusisimua sehemu ya mwisho 59.
 
Dah mr tiger 🐅 ndo baasi tena lkn dr boaz na mpenzi wa awali wa mr 🐅 wana jambo lao
 
Uzuri wa hii hadithi haitabiriki.

Hongera sana Indigo28
Yeah mwanzo nilijua mama tajiri ni mama yao kina James anataka kuiangamiza familia yake ili arithi mali zote kumbe sio. Sipati picha inayofuata Dr. Boaz akiwa na makomando 40 kuikabiri familia ambayo tayari ipo weak kiuongozi
 
Usisahau wakati Dr. Boaz ayakapokuja na makomandoo wake Mwamba Jack atakuwa ashaamka maana Mwamba Kabisa Bibi aliishampa chaguo Mama Tiger achague nani aondoke nae na Mzee Tiger akachaguliwa na ashaenda.

Hapo usimsahau James Mzee wa mitambo na mkewe Rose! Dr. Boaz akalee watoto yatima!
 
Yeah umenikumbusha kumbe mzee keshakata moto so wale wafu wao watamrudishia nguvu Jack. Tatizo kina Boaz hawajui pale kwa mzee Tiger panalindwa kimwili (Man power) na kiteknolojia ya juu kabisa. Ngoja tusubirie huo mwendelezo. Tanzania ya hadithi hii itachafukaa😆😆
 
Kwa anaetaka kitabu kizima complete
Anicheki 0624728816
 
Ukimaliza niashtue nilete hadithi ya "kikao cha mafisi mbele ya ngiri mlevi"
 
Back
Top Bottom