Devil’s family(familia ya mashetani) 01

Devil’s family(familia ya mashetani) 01

Naamini yupo bize kutukusanyia mavitu
.
.story teller Indigo28 tupo wengi tunangoja uzi wako kaka, hakikisha hukatishwi tamaa na kiumbe chochote, wengine tupo tunafatilia uzi wako.
.
 
DEVIL’S FAMILY(FAMILIA YA MASHETANI) 53


KILA KILICHO ANDIKWA KATIKA HADITHI HII NI UTUNZI HAKIENDANI NA KISA CHOCHOTE KILICHO WAHI KUTOKEA MAHALA POPOTE ASANTE
*************************************************************************************

ILIPOISHIA
“Sijui boss”
Mwanaume mmoja akawafwata walipo simama. Akampigia salute Rose.
“Kuna mpya gani?”
Rose alimuuliza mwanaume huyo. Akawatazama James na Chris.
“Zungumza tu”
“Wezetu jeshi la polisi limetupatia makachero ishirini wamesambaa tuna saidiana kufwatilia mienedo ya kila naaye ingia na aliyopo hapa hospitalini”
“Je kuna chochote mulicho gundua?”
“Hadi sasa hapana”
“Endeleani kuwa makini na kila mtu”
“Sawa boss”
“Sisi tupo ndani”
James alimuambia Chris”
“Sawa mkuu”
James akamshika mkono Rose na wakaingia ndani. Dokta Boaz akawaona na kwa haraka akaingia upande wa kamera ya simu yake na akawapiga picha James na Rose wanao elekea katika lifti kwa ajili ya kuelekea gorofani.

ENDELEA
Lifti ikafunguka na wakatoka nje lifti.
“Mupo salama?”
James aliwasalimia walinzi walio simama katuka kordo ya kuelekea chumba alicho lazwa Jack
“Tupo salama boss”
Wakaelekea hadi ndan iya chumba alicho lazwa Jack.
“Mama shikamoo”
Rose na James walisalimia kwa pamoja na mrs Tiger akaitikia. Wakasalimiana na watu wengine.
“Huyo mshenzi hajakamatwa?”
“Bado mama”
“Wana subiri nini hadi sasa hivi”
“Mama mambo hayaendi kiharaka kama hivyo. Ana taumia akili na alikuwa hatua kadhaa mbele yetu hivyo sio rahisi kumpata”
James alimjibu mama yake akimtazama jinsi alivyo nuna kwa hasira.
“Kwa nini imechukua muda mrefu Jack kuamka?”
“Wana dai sumu ina toka taratibu taratibu. Hivyo ina weza kumchukua hata siku tatu hadi azinduke”
Sophia alijibu.
“Siku tatu hadi nne?”
“Ndio”
“Shem upo sawa?”
“Ndio shem”
“Kabadilisheni nguo. Sisi tutabaki hapa na mgonjwa. Pia hamjakunywa chai”
“Kweli mimi ngoja nielekee nyumbani”
Sophia alizungumza huku akinyanyuka kutoka alipo kuwa amekaa.
“Hata mimi”
Mrs Tiger alizungumza.
“Shem nendani nyumbani mutuache hapa. Muna hitaji kunyoosha viungo, kuoga na mukamuangalie na baba”
“Sawa shem”
Valentina na Vaileth wakanyanyuka.
“Musichelewe sana mama”
“Sawa”
Mrs Tiger wakwe zake wakaondoka eneo alilo lazwa Jack.
“Yule sasa ndio Mrs Tiger.”
Dokta Boaz alimsikia mwana mama aliye kaa karibu yake akizungumza.
“Na wale wengine?”
“Yule mrefu ni mwanaye wa kike. Huyu wa nyuma ni mkwewe na huyu mwengine kwa jinsi anavyo fanana ana weza kuwa ni mdogo wa huyu mkwewe”
“Ohoooo hajazeeka kabisa yule mama”
“Pesa ndugu yangu.”
“Ila kweli”
“Wao wana tembea na walinzi kama hivyo. Sisi tuna tembea na jua kali, toka asubuhi tupo kwenye foleni, wao una hisi wana kaa foleni”
“Ila kweli”
“Maisha mazuri”
“Ila wote tutakufa bwana”
“Hiyo ndio kauli ya kushindwa maisha. Dunia una teseka mbinguni hujui kamma uta kwenda mbinguni au kuzimu”
Wote wakacheka. Dokta Boaz akatazama ujumbe alio tumiwa.
‘Picha yake haina taarifa yoyote kwenye data basae yoyote ya serikali au ulimwenguni’
‘Kwa hiyo hajulikani?’
‘Hajulinani’
‘Atakuwa ni nani?’
‘Sijui ndugu yangu. Kuwa makini’
‘Poa’
Dokta Boaz akarudisha simu yake mfukoni.
“Laptop nimeiacha kwenye gari mke wangu. Naomba ukanichukulie”
James alizungumza akimpa funguo Rose.
“Sawa mpenzi”
Rose akachukua funguo ya gari walilo fika nalo hospitalini. Akaingia ndani ya lifti, akashuka nayo hadi chini. Akatoka ndani ya lifti, akasimama na kumfanya Dokata Boaz kumtazama kwa makini. Rose akapokea simu yake na akaendelea kutembea.
“Mke wangu kuna chupa ya enery drink ipo ndani ya gari. Naomba uje nayo”
“Sawa mume wangu”
Rose akatoka nje, akaelekea alipo simamisha gari. Akaingai ndani ya gari, akaichukua laptop ya James, akafungua friji ndogo iliyomo ndani ya gari. Akaisoma maelezo ya kinywaji hicho kisha akashuka ndani ya gari na akarudi ndani ya hospitali. Akatembea hadi eneo lenye friji kubwa la vinywaji ambapo una ingia kiasi cha pesa, unachagua kinywaji ukitakacho na friji hiyo ina kutolea. Taratibu dokta Boaza akanyanyuka alipo kaa. Akatembeaa hadi pembeni ya friji hilo.
“Shikamooo”
Rose alimsalimia Dokta Boaz pasipo kujua ni muuaji wanaye mtafuta.
“Marahabaa….”
Dokta Boaz alijibu salamu kwa sauti ya mkwaruzo huku akikohoa kohoa.
“Naomba unisaidie kutoa maji”
“Ahaa sidhani kwa kifua chako una paswa kunywa maji ya baridi mzee”
“Nina kiuu”
“Kama una kiu ngoja nitazame namna ya wewe kupata chupa ya maji ya moto”
Rose akamuita mlinzi wa familia ya mzee Tiger aliye simama pembeni yake.
“Ndio madam”
“Mtafutie mzee chupa ya maji”
“Sawa”
“Umekaa wapi mzee”
“Benchi lile”
Dokta Boaz akanyoosha kidole. Rose akatazama kidole cha mkono wa kuliwa dokta Boaz.
“Sawa mzee. Kapumzike tu ata kuletea”
“Pesa yangu hii hapa”
“Hauna haja ya kutoa pesa yako mzee. Nenda”
“Asante binti”
Dokta Boaz alizungumza akitembea kwa kuchechema hadi katika eneo alilo kuwa amekaa. Rose akabeba chupa yake ya maji aliyo ilipia na akaondoka eneo hilo.
“Kuna kitu nataka ufwatilie mume wangu
Rose alizungumza akimpa James chupa energy drink pamoja na laptop.
“Kitu gani?”
“Kuna mzee nilikuwa nina zungumza naye hapo chini muda huu. Mfwatilie”
“Una muhisi ni nani?”
“Wauji siku zote huwa wahana mbinu moja. Ana weza kubadili mbinu tofauti hata kwa mionekano ya mwili au sura”
“Sawa”
James akaigia katika mfumo wa kamera za hospital. Akafwatilia video ya Rose alivyo kuwa amesimama katika friji pamoja na mzee wanaye muhisi.
“Vita sura yake karibu?”
Rose alizungumza na akaatazama mboni za macho yam zee huo.
“Sio muuaji”
James alizungumza.
“Hembu video ya mlipuaji”
James akampa Rose simu. Akatamvuta kwa karibu macho yake. Akafananisha na macho ya mzee aliye kuwa ana zungumza naye.
“Frame zao za macho zipo sawa.
“Ila mboni zao za macho hazifanani?”
“Macho watu wana weza kubadilisha na kuweka hata mboni feki. Mtu ana weza kubadili sura akabadili umbo ila macho ndio eneo ambalo mtu huwezi kulibadilisha abadani”
“Kumbe?”
“Haiwezekani”
“Na tafuta video ya alivyo kuja kutusalimia ile siku”
James akafwata maelekezo ya mke wake.
“Zoom macho yake”
Akavuta kwa karibu macho ya dokta Boaz waliye kuwa wana salimiana naye katika kordo.
“Bingo. Tumempata muuaji.”
“Mke wangu tusije tukamparamia mzee wa watu”
“Una dhani tuta mkurupua…..Hembu rudisha video ya jinsi alivyo ingia hapa hospitali”
James akarudisha nyuma rekodi za kamera za hospitali. Wakamuona jinsi mzee huyo akifika hospitali hapo kwa kutumia dereva bodaboda. Wakamuona alivyo kwenda mapokezi na kutoa kadi yako ya bima.
“Si una weza kuingia kwenye mfumo wake wao wa usajili wa wagonjwa?”
“Ndio:
“Ingia tujue bima yake imesajili kwa jina gani”
James hakupata shida wakaiona bima aliyo toa mzee.
“Anaitwa Suleimani Swedy. Kazaliwa miaka hamsini na mbili iliyo pita. Mke wangu tume mfananisha”
“Iingia kwenye mfumo wa Nida. Tafuta jina lake”
James akafanya alicho elekezwa.
“Ni Mtanzania na namba yake ya Nida imesajili na leseni ya udereva”
“Fwatilia vimesajiliwa muda gani kwemye mfumo wa serikali”
“Ahaa……dakika moja”
James akamatazama Rose usoni mwake.
“Leo asubuhi”
“Ni mtu wetu mume wangu. Mwenyewe kajiona katumia akili”
“Ngoja niwaambie vijana wakamkamate”
‘Wala tucheze mchezo anao ucheza yeye. Tumesha mjua kuwa yeye ndio muhusika wetu hivyo na sisi tuta mfwatilia kama anavyo tufwatilia sisi”
“Ameitwa kwenda chumba cha daktari”
James alizungumza akimuonyesha Rose, jinsi dokta Boaz alivyo nyanyuka kuelekea chumbani kwa daktari.
“Karibui”
Daktari alimkaribisha dokta Boaz na akaanza kujielezea jinsi anavyo umwa.
***
“Mama”
Sophia alimuita mama yake mara baada ya kushuka kwenye gari, huku Valentina na Vaileth wakiwa wana elekea ndani.
“Una ona MUNGU alivyo wa ajabu”
“Una manisha nini?”
“Rose mkwe uliye kuwa humtaki na mukamfanya hadi mumchukie kaka leo hii amekuwa ni msaada mkubwa sana kwenye hili janga tunalo lipitia kama familia”
“Sophia kichwa changu kina niuma. Hembu naomba uniache nikampumzike”
“No nakuambia tu. Hembu piga picha kama Rose na mumewe wasinge kuwapo?”
“Sawa tulifanya makosa”
“Vipi una jisikiaje kuishi na mtu ambaye ume muulia ndugu zake na baba yake”
Mrs Tiger akamtazama Sophia. Kisha akanedelea kutembea kuelekea ndani.
“Una paswa kumuomba msamaha”
“Sinti jaribu kufanya huo ujinga. Unanielewa”
“Ipo siku utamuomba na sio ujinga kuomba msamaha. Endela kushupaza shingo ikiwa mwnaao kule ana pigania maisha yake.”
“Rose niache kwaza”
Mrs Tiger akaelekea chumba alicho lazwa mumewe.
“Karibu madam”
“Asante. Mzee anaendeleaje?”
“Hali yake bado ipo vile vile”
“Naombani munipishe”
Madaktari wawili wakatoka nje.
“Mume wangu famlia yetu ina pitia kipindi kigumu. Wewe una pigani amaisha yako na Jack naye ana pigania maisha yake. Ni nini amacho kimetokea jamani”
Mrs Tige ralizungumza huku akilia kwa uchungu.
“Dhambi zetu zina tutafuna mume wangu”
Mrs Tiger aliendelea kulia akiwa amepiga magoti pembeni ya kitanda cha mume wake.
“Mwili wako ni wa moto”
Vaileth alizungumza huku kiganja chake kikiwa shingoni mwa Valentina.
“Kichwa kina niuma”
“Pole. Fanya nywe dawa?”
“Nita lala kidogo”
“Nikuletee chai?”
“Hapana sijusikii kula”
“Una paswa ule upate nguvu”
“Nita kula baadae”
Valentina akavua nguo mbele ya Vaileth na akaelekea bafuni. Sophia akaingia chumbani hapo.
“Dada yako yupo wapi?”
“Bafuni”
“Naomba utupishe”
“Dada yangu hayupo sawa hivyo mpumzishe kdiogo”
Sophia akamtazama Vaileth, kisha akamsogelea.
“Nawe pia unajua fika haupo sawa. Jack amenieleza kila kitu kilicho tokea baina tenu hivyo naamini na wewe una paswa kupumzisha akili”
Vaileth akakosa jibu akatoka chumbani hapo. Sophia akavua nguo zake na akaingia bafuni.
“Wifi sijisikii kufanya hicho ukitakacho”
“Nimekuja tuoge pamoja”
Sophia alizungumza huku akimkumbatia Valentina mgongoni.
Mrs Tiger akazidi kulia kwa uchungu, gafla hali ya hewa ikabadilika ndani ya chumbacha na ubaridi ukazidi. Akashtuka sana kumuona bibi wa familia ambaye amekufa miaka mingi na yeye amekuwa akimuona kwenye picha tu.
“Usiogope kwa maana kazi iliyo mshinda mumeo na mwanao naamini wewe uta iweza”
Bibi huyo alizungumza na akazidi kumuogopesha mrs Tiger.
ITAENDELEA
Mchaka mchaka mpya umeanza. Dokta Boaz amejiridhisha upelelezi wake pasipo kujua na yeye amesha gunduliwa na Rose je ata chomoka salama safari hii? Ni kazi gani mzimu wa bibi wa familia an ataka kumpatia Mr Tiger? Ungana nami katika stori hii ya kusisimua sehemu ya 54.
 
DEVIL’S FAMILY(FAMILIA YA MASHETANI) 54


KILA KILICHO ANDIKWA KATIKA HADITHI HII NI UTUNZI HAKIENDANI NA KISA CHOCHOTE KILICHO WAHI KUTOKEA MAHALA POPOTE ASANTE
*************************************************************************************

ILIPOISHIA
“Naomba utupishe”
“Dada yangu hayupo sawa hivyo mpumzishe kdiogo”
Sophia akamtazama Vaileth, kisha akamsogelea.
“Nawe pia unajua fika haupo sawa. Jack amenieleza kila kitu kilicho tokea baina tenu hivyo naamini na wewe una paswa kupumzisha akili”
Vaileth akakosa jibu akatoka chumbani hapo. Sophia akavua nguo zake na akaingia bafuni.
“Wifi sijisikii kufanya hicho ukitakacho”
“Nimekuja tuoge pamoja”
Sophia alizungumza huku akimkumbatia Valentina mgongoni.
Mrs Tiger akazidi kulia kwa uchungu, gafla hali ya hewa ikabadilika ndani ya chumbacha na ubaridi ukazidi. Akashtuka sana kumuona bibi wa familia ambaye amekufa miaka mingi na yeye amekuwa akimuona kwenye picha tu.
“Usiogope kwa maana kazi iliyo mshinda mumeo na mwanao naamini wewe uta iweza”
Bibi huyo alizungumza na akazidi kumuogopesha mrs Tiger.

ENDELEA
“Usiniogope”
Mrs Tiger akazidi kujawa na woga.
“Unajua ukiachana na mumeo na mwanao kushindwa kuyapigania maisha yake pale hospitali. Ila ulisaliti hii familia.”
“Nimesaliti familia?”
“Ndio. Umelala na mwanaume mwengine tofatuti na mumeo una jua madhara yake?”
Mrs Tiger akazidi kuvurugwa akili.
“Ndio maana tulikufanya umuue mapema kwani nuksi zake ulizingiza kwenye hii familia ndio maana ukasababisha mwanao aaendelee kupitia shida anayo ipitia”
“Naombeni munisameheee……”
Mrs Tiger alizungumza akilia kwa uchungu.
“Kwa sasa una uchaguzi mmoja”
“Uchaguzi gani?”
“Kuchagua kati ya mumeo na mwanao Jack nani afe”
Mrs Tige macho ya mshangao yakamtoka akimtazama bibi wa Familia.
“Una masaa matatu ya kuamua ni nani afe”
“Matatu?”
“Umenisikia vizuri sina cha kurudia”
“Sasa nita waibuje”
“Nita kuja”
Bibi akapotea mara baada ya kumuona Vaileth akiwa nje ya mlango wa chumba kwa ajili ya kuingia ndani ya chumba. Vaileth akagona mlango na kwa haraka Mrs Tiger akayanyuka chini alipo puga magoti.
“Ingia”
Alizungumza huku akijifuta machozi.Vaileth akaingia.
“Sahamani mama nimekuja kumuona mgonjwa”
“Bila samahani Vai, njoo tu”
Mrs Tiger akatembea hadi alipo Mrs Tiger.
“Mzee ana hali gani?”
“Toa alivyo pata tatizo hali yake ipo vile vile”
“Pole sana mama. Natambua una pitia kipindi kigumu sana cha Jack an kumuguza baba?”
“Sana, kwenye maisha yangu sijawahi kupitia kipindi kama hichi”
“Namaini MUNGU ata ata wasaidia wote wapone”
Mrs Tiger akamatazama Vaileth bila ya kumsemesha chochote.
“Mama”
“Abee”
“Au basi”
“Zungumza tu”
“Mama huu sio muda sahihi wa mimi kuongea”
“No ongea”
Vaileth akajifikiria kwa sekunde kadhaa.
“Tumuombee tu Jack na baba wapone. Jack yeye mwenyewe ata kuja kukuambia”
“Kuniambia nini?”
“Mama kwa mimi siwezi kuzungumza. Na sasa sio wakati sahihi samahani”
Vaileth akatoka ndani hapo na kumuacha Mrs Tiger akiwa na mshangao.
***
Sophia akamshika mkono Valentina na wakatoka bafuni wote wakiwa uchi.
“Nasikia kichefu chefu”
Valentia akarudi kwa haraka bafuni, akaanza kutapika. Sophia akamgusa Valentina na kiganja shingoni.
“Huna joto lakini”
“Itakuwa ni mchafuko na kukaa na njaa toka jana”
“Ngoja nikakuandalie kifungua kinywa”
“Asante”
Velentina akamtazama wifi yake anaye toka bafuni. Sophia akavaa nguo zake na kuelekea moja kwa moja jikoni. Akaaeleza wapishi nini cha kuandaa kwa kidungua kinywa chake. Akamuona Vaileth akiwa ana elekea ufukweni.
“Andaeni vizuri na wekeni limao jungi”
“Sawa boss”
Akatoka nje kwa kutumia mlango wajikoni. Akamfwata Vaileth anapo elekea.
“Vipi wifi?”
Vaileth akageuka na kujifuta machozi.
“Unalia nini?”
“Eheee?”
“Mbona una lia?”
“Hamna wifi”
“Kwa sasa hupaswi kulia. Unapaswa kumuombea Jack apone haraka na arudi kwenye majukumu yake ikiwemo jukumu la kukupa utau wewe”
“Wifi wewe huelewi tu”
“Sielewi nini”
Vaileth akaka kimya.
“Niambie una tatizo gani?”
“Nina mimba. Nimepima nina mimba ya Jack”
“Una sema kweli?”
“Ndio”
“Nina Mimba yake”
Sophia akatabasamu.
“Woooo kwa hiyo wewe ni mama kijacho?”
“Ndio nimepima tulivyo fika hapa. Nimechananyikiwa”
“Khaa una changanyikiwa na nini?”
“Wifi dada yangu akijua ita kuwaje? Achana na dada, wazazi wangu wakijua itakuwaje….Una hisi wata nipa baraka ya mimi kuwa na Jack”
“Kwa nini muda wote una wazazi watu wengine pasipo kujiwazia wewe mwenyewe? Ukitaka kufanya jambo lako kwenye haya maisha usiwazie watu wengine nini wata sema. Naamini ulivyo mkubalia Jack ni akili yako ndio iliamua. Hukuwashiwisha na mtu si ndio?”
“Ndio”
“Basi pambana na hili lililo mbele yako. Usiope mimba imesha ingia na itakuwa ni furaha sana kwa Jack. Umenielewa?”
“Ndio wifi”
“Tulizana hivi sasa acha mawenge. Wezeka nguvu kumuombea mumeo anaye pigania maisha yake. Sawa”
“Sawa wifi”
“Haya chai inaandaliwe twende ukanywe”
“Endapo kitatokea chochote naomba uzungumze na dada”
“Usijali”
Wakarudi ndani kidogo Vaileth akijihisi amani moyoni mwake.
***
“Umeiiona video yake”
Rose alizungumza kwa simu.
“Ndio mkuu”
“Mfwatilie bila ya yeye kujua ni mtu hatari sana na ana uwezo mkubwa wa kuhisi hatari. Ukikosea tu basi tana mpoteza na anaweza kwenda kubadili muonekano wake”
“Sawa mkuu”
Mpelelezi wa shirika la X aliye pewa kukumu la kufwatilia Dokta Boaz akawasha gari lari lake huku akimtazama Dokta Boaz anavyo toka katika mlango wa hospitali, akitembea kwa mwendo wa kuchechema.
‘Wazembe sana hawajanistukia’
Dota Boaz alijipongea huku akitoka nje.
“Mzee Boda?”
“Ndio”
Dokta Boaz akapanda pikipiki.
“Tuna kwenda wapi?”
Akamuelekeza bodaboda eneo la kuelekea. Mpeleezi aliye pewa jukumu la kumfwatilia dokta Boaz akajikita akitoa mshunyomkai mara baada ya daladala kusimama mbele yake na kufunga njia ya yeye kutoka. Akamshuhudia dokta Boaz akitokomea.
“Huyu ndio mpelelezi uliye mpa kazi”
James alimuulzia Rose wote wakitazama video inayo rekodi kinacho endelea nje a geti la hospitali.
“Mpuuzi alishindwa kutumia pikipiki”
“Ndio tumesha mpoteza”
“Ingia katika mfumo wa kamera za barabarani”
“Kwa jinsi boda wanavyo pita chochote hatuwezi kumpata”
“Pikipiki nyingi siku hizi zina fungwa GPS hembu fwatila kama pikipiki hiyo imefungwa pgs”
James akafanya kama alivyo elekezwa na mkewe.
“Haina”
“Kijinga tu tumempoteza. Sasa ana elekea wapi”
Rose alizungumza akitazama gari ya mpelezi ikitoka eneo hilo. Akampigia simu mpelelezi.
“Mkuu”
“Una kwenda wapi ikiwa tumesha mpoteza”
“Bado hatujampoteza”
“Kwa nini?”
“Kwa sababu aliye mpakiza ni kijana wetu. Hivyo nimesha wasiliana naye”
“Muambie awe makini”
“Sawa mkuu”
“Bora aliye mbeba naye ni mpelelezi.”
“Duuu ina nafuu. Tusubirie watupe ropiti gani”
James alizungumza akiwa na matumaini mapya. Akamtazama Jack ambaye bado hajazinduka.
***
“Niache hapo mbele”
Dokta Boaz alizungumza huku akimuonyesha duka kubwa la dawa.
“Sawa boss”
Dereva pikipiki akashuka. Dokta Boaz akatoa noti ya shilingi elfu tano na akampa bodaboda.
“Nisubirie”
Dokta Boaz akatembea kwa kuchechemea.
“Nahitaji back up”
Bodaboda alizungumza huku sikioni mwake akiwa amevalia earpiece ndogo sanaga mbayo sio rahisi kuonekana. Dokta Boaz akaingia ndnai ya duka hilo la vioo. Bodaboda akaendelea kumfwatilia. Dokta Boaz mara baada ya kumaliza kunuua dawa anazo zihitaji akatoka ndani ya duka na akamfwata bodaboda alipo simama.
“Nipeleke hapo mbele”
“Sawa”
Dokta Boaz akapanda pikipiki wakatembea hadi karibu na soko.
“Sasa niache hapa sokoni. Nachukua mahitaji”
“Kama huto jali tajiri nita kusubiria tu”
“Nita kuchelewesha.”
“Hakuna shiada mzee wangu”
“Usije ukanidai kiasi kikubwa cha pesa.”
“Usili boss”
Dokta Boaz akashuka katika pikipiki. Kwa uvaaji wa bodaboda akashindwa kabisa kujua kama ni mpelelezi.
‘Mumfika wapi?’
Dakika tano kutoka hapo ulipo.
“Nyingi sana mkuu. Ameingia sikoni, ana weza akatoka hapa tukamkosa”
“Mfwatilie”
“Ata nishtukia. Kwani ndani ya soko hakuna watu wetu”
“Ngoja nicheki”
Mpelelezi aliye pewa kazi na Jack akaingia katika mfumo wa shirika la X na akaangalia eneo la soko alilo ingia dokta Boaz kama wana wapelezi. Akakuta kuan wapelelezi sita wakiwa ndani ya soko wanne kama wauzaji na wengine wawili kama wabeba mizigo. Akawatumia picha ya Dokta Boaz na akawapa amri ya kuhakikisha wana mfwatilia dokta Boaz pasipo yeye mwenyewe kujua.
***
“Mama yupo wapi?”
Sophia alimuuliza mmoja wa wafanyakazi wakiwa wana andaa kifungua kinywa mezani.
“Yupo chumbani kwa baba”
“Hajatoka hadi muda huu?”
“Hajatoka”
“Nakuja”
Sophia akanyanyuka akimazama Valentina na Vaileth alio waacha meza ya chakula. Akaingia katika chumba alicho lazwa mzee Tiger.
“Mama vipi?”
“Mmmm!”
“Chai tayari”
“Sijisikii kula”
“Tambua una vidonda ya tumbo. Fanya tukanywe chai”
“Sophia sijisikii mwanangu. Hembu niache kwanza”
Sophia akamatazama mama yake.
“Una tatizo gani?”
“Una jua baba yako na mdogo wako wote wana umwa. Una uliza nina tatizo gani kweli”
“Najua nakujua vyema kuliko wanao wa kiume. Nimekuuliza una tatizo gani?”
Mrs Tiger akashusha pumzi nyingi.
“Nenda tutazungumza baadae”
“Mama zungumza kama na wewe una taka ulazwe jua mimi sina uwezo wa kuwaangalia wote watau mukiumwa. Zungumza kama una jambo la kushauriwa ushauriwe”
“Kati ya baba yako una chagua nani aendelee kuishi”
“Jack. Mzee kashakula chumvi namambo aliyo yafanya yana tosha aisee. Mika sabini ni mingi sana muache apumzike kwa amani”
“Yaani baba yako ndio una mchukia kiasi hicho”
“Mama tuache unafki hilo swali nikuulize wewe. Kati ya Jack na mzee nani ambaye una taka abaki hai duniani?”
Mrs Tiger akakosa jibu na akabaki akimtazama Sophia na akilini mwake ana waza endapo bibi wa familia akimtokea kwa mara ya pili ni nani atakuwa tayari afe ikiwa mume wake ana mpenda na Jack mwanaye ana mpenda.
ITAENDELEA
Mchaka mchaka mpya umeanza. Mrs Tiger amepewa achague kati ya mumewe na Jack ni nani ana paswa kuendelea kuishi je nani ata mchagua? Dokta Boaz ana endelea kufwatiliwa je ata fanikiwa kuwatoka wapelelezi sita walipo ndani ya soko? Ungana nami katika stori hii ya kusisimua sehemu ya 55.
 
DEVIL’S FAMILY(FAMILIA YA MASHETANI) 55


KILA KILICHO ANDIKWA KATIKA HADITHI HII NI UTUNZI HAKIENDANI NA KISA CHOCHOTE KILICHO WAHI KUTOKEA MAHALA POPOTE ASANTE
*************************************************************************************

ILIPOISHIA
“Nenda tutazungumza baadae”
“Mama zungumza kama na wewe una taka ulazwe jua mimi sina uwezo wa kuwaangalia wote watau mukiumwa. Zungumza kama una jambo la kushauriwa ushauriwe”
“Kati ya baba yako una chagua nani aendelee kuishi”
“Jack. Mzee kashakula chumvi namambo aliyo yafanya yana tosha aisee. Mika sabini ni mingi sana muache apumzike kwa amani”
“Yaani baba yako ndio una mchukia kiasi hicho”
“Mama tuache unafki hilo swali nikuulize wewe. Kati ya Jack na mzee nani ambaye una taka abaki hai duniani?”
Mrs Tiger akakosa jibu na akabaki akimtazama Sophia na akilini mwake ana waza endapo bibi wa familia akimtokea kwa mara ya pili ni nani atakuwa tayari afe ikiwa mume wake ana mpenda na Jack mwanaye ana mpenda.

ENDELEA
“Twende tukanywe chai bwana”
Sophia akamshika mkono mama yake na akatoka naye katika chumba alicho lazwa mzee Tigera. Wakajumuika mezani na kuendelea kunywa chai. Ukimya ukatawala huku kila mmoja akiwa kimya akionekana kuwaza anacho kiwaza.
“Mimi narudi hospitalini”
Valentina alizungumza huku akinyanyuka.
“Subiri twende wote”
Sophia alizungumza.
“Na mimi pia nina kuja”
Vaileth alizngumza.
“Mimi nitakuja baadae nahitaji kulala kidogo”
Mrs Tiger alizungumza akiendelea kuywa chai taratibu. Valentina akaelekea chumbani kwake, akaanda nguo chache na akaziweka katika kibegi kidogo. Vaileth akaingia ndani ya chumba cha dada yake.
“Vipi mbona mnyonge”
“Hamna”
“Una nini unataka kuongea?”
“Hamna dada. Shem kweli ata pona?”
“Moyo wangu una matumaini sana juu ya kuwa mume wangu ata nyanyuka tena pale kitadani.”
“Sawa. Ila nimeanza kuiogopa hii familia”
Vaileth alizungumza kwa sauti ya chini.
“Kwa nini?”
“Maadui ni kama hawa unavyo waona. Wana ilenga fmailia hii na sisi tupo ndani ya hii familia itakuwaje?”
“Mdogo wangu. Familia za kitajiri zina mambo yao. Mambo yao ndio kama haya, haiwezi kutokea watu wakaenda kuvamia familia za chini. Hivyo kuna nyakati ina bidi tumshukuru MUNGU kwa kila jambo mdogo wangu. Sawa”
“Sawa dada”
“Kuwepo kwenye hii familia pamefungua milango ya kiuchmi katika familia yetu. Tulivyo kuwa hapo mwanzo na hivi sasa ni tofauti. Au wewe mwenzangu hujaona tofauti?”
“Nimeiona”
“Basi kama ni hivyo sisi tutumie akili kuishi nao. Kwenye mambo yao ya ajabu tuachane nayo na kwenye mambo ambayo tuna ona yana manufaa kwetu basi tuyafwate. Good news ni kwamba nimepewa hisi asilimia ishirini na tano katika kampuni ya mama mkwe”
“Hisa asilimia ishirini na tano?”
“Ndio na mimi ni mkurugenzi”
“Zina thamani gani?”
“Mmmmm pesa nyingi sana mdogo wangu. Kwa maana kampuni kila siku ina panda. Hapa ninacho kiwaza ni kujitafutia eneo nikajenga jumba langu la kufahari, nikafungua biashara ambazo zitakuwa chini yangu na maisha yakaendelea”
“Hongera sana dada”
“Asante. Niambie ni biashara gani una taka kufanya nikuweke kwenye bajeti kwa maana nafasi ndio hii”
“Nitakuambia dada”
Sophia akaingia.
“Nipo tayari tuondokeni”
Valentina akabeba kibegi kidog chenye ngo. Wakatoka nje na wakangia katika gari moja na wakaondoka na walinzi wawili huku mmoja akiwa ni dereva.
***
“Hivi navyo ni sh ngapi?”
Dokta Boaz aliuliza funga la viatu vitabu. Macho ya mwana mama wa pembeni anaye muangalia kwa kuiba iba.
‘Fuc**’
Dokta Boaz alizungumza kimoyo moyo akishtuka kwani angalia ya mwana mama huyo ina asihria kuwa ana mfwatilia.
“Nifungie mafungu mawili”
Dokta Boaza alizungumza huku akimpa mwana mama anaye muuzia viazi noti ya shilingi elfu kumi.
“Nikuwekee kwenye mfuko wa shilingi mia tano au mia tatu?”
“Mia tano”
Akatazama wauzaji wawili wanao uza matunda, akagundua wauzaji hao nao ni wapelelezi na wana mfwatilia yeye.
“Samahani….hapa ni wapi kwenye vyoo vya kulipia”
‘Nenda upande ule wa kulia, kunja kushoto utaona vyoo”
“Asante”
Dokta Boaz akatembea kwa mwendo wa kuchechemea huku macho yake yakiwa makini kutazama wanao mfwatili.
‘Hawa wapuuzi wamenijuaje?’
Dokta Boaz alizungumza hukua akiendelea kuwatazama wanao mfwatilia.
“Vipi?”
Aliye pewa jukumu la kumfwatilia dokta Boaz alimuuliza bodaboda mara baada ya kushuka ndani ya gari
“Yupo ndani ya soko”
Bodaboda alijibu. Afisa w ashirika la X kwa mwendo wa haraka akaingia ndani ya soko. Akapewa ishara na afisa mwengine ambaye ni muuzaji ndani ya soko na akaanz akutembea kwa mwendo wa haraka na wenye tahadhari kuelekea eneo la vyooo. Akafika eneo la vyoo, akatoa ishara kwa mpokeaji pesa kukaa kimya, akachomoa bastola kiinoni mwake. Akaingia katika vyoo vya kiume, akaanza kukagua mlango mmoja baada ya mwengine. Akafika choo cha saba ambacho mlango wake umefungwa kwa ndani. Akajaribu kuusukuma ila haukufunguka. Akagonga mara mbili, ila hapakuwa na jibu lolote. Akarudi nyuma kwa garaka na akaupiga kwa teke na mlango ukafunguka. Akaingia na kuona eneo la juu ya bati la choo kukiwa limefunguliwa ikishiria aliye ingia ndnai ya choo hicho ametokea kupitia katika bati. Akachomeka bastola kiunoni mwake, akatoka.
“Umemuona huyu mzee?
“Ndio ameingia humo ndani”
Akazunguka upande wa nyuma wa vyoo. Hakumuona mtu yoyote, akawatumia meseji maafisa wote walipo ndani ya soko ambao ni wapelelezi wa siri. Msako wa kumtafuta dokta Boaz kimya kimya ukaendelea ndani ya soko ila hapakuwa na aliye weza kumuoana. Akampigia simu Rose.
“Nipe ripoti?”
“Hatujafanikiwa kumpata. Ametoroka ndani ya vyoo vya sokoni alipo ingia’
“Sokoni?”
“Ndio”
“Soko gani?’
Afisa akataja soko alilopo. Rose akaata simu.
“Katika hilo soko kuna kamera una weza kupata video zake”
“Ngoja”
James akadukua kamera zilizo fungwa ndani ya soko. Akafanikiwa kupata rekodi inayo muonyesha dokta Boaz jinsi anavyo ingia ndani ya soko hilo. Wakafwatilia mizunguko yake ndani ya soko.
“Huyu mama ndio kamfanya agundue”
Rose alizungumza kwa hasira.
“Anafanya naye kazi au?”
“Hapana jinsi alivyo kuwa ana mtazama kwa muhalifu anaye weza kusoma macho ya mtu ana gundua kabisa kuwa na afwatiliwa.”
“Huyu jama ana ana onekena ana uwezo mkubwa”
“Kijinga tu wameshindwa kumpata”
“Video yake ya mwisho ni hii kuingia bafuni”
“Huwezi kuangalia eneo la pembeni hapo kama kuna maduka yana kamera?”
“Ngoja”
James akaendelea kukagua eneno la jirani na soko kama kuna maduka yanye kamera.
“Hamna na kamera zilizopo ni kamera za ndani ya maduka yao”
“Ndio tumesha mpoteza kizembe tu”
Mlango ukafungulia, akaingia Sophia akiwa ameongozana na mawizi zake.
“Mbona mumerudi mapema. Tukajua mtakaa hadi mchana”
“Mmmm shem mimi nimeshindwa kuvumilia. Nimekosa kabia amani ya kukaa nyumbani.”
Valentina alizungumza akiweka kibegi chake juu ya meza.
“Umekuja na begi kabisa”
“Ndio shem sirudi nyumani hadi mume wangu awe sawa”
“Ohooo sawa”
“Wifi Rose upo sawa?”
Sophia alimuuliza Rose.
“Yaa nipo vizuri wifi”
Rose alizungumza huku akitazama simu yake inayo ita.
“Ndio”
Rose alizungumza huku akitoke nje.
“Tumefwatilia na kuuliza kuna walio muona akipanda bajaji”
“Fwatilieni sasa hiyo bajaji”
“Kwa bahati mbaya boss si bajaji ya eneo hilo. Ni bahaji aliyo isimamisha barabarani”
“Hilo eneo halina kamera?”
“Tumechunguza na halina”
“Muna wezaje kumuacha mtu akaondoka kirahisi nama hiyo, ni uzembe wa aina gan hiyo eheee?”
Rose alizidi kufoka. Akakata simu huku akimtazama James.
“Wanasemaje”
“Wanasema kapanda bajaji”
“Bajaji ya kwenda wapi?”
“Sijui ni bajaji aliyo pita barabarani”
“Ata kwenda kubadilisha muonekano wake na kuwa katika muonekano mpya”
“Ndio anacho kwenda kukifanya”
“Inabidi twende Morogoro”
“Kufanya nini?”
“Kwenye hicho kituo chake cha watoto. Naamini hapo tuna weza kupata taarifa zaidi”
Rose akajifikiria.
“Naamini kuna polisi watakuwa wamesha kwenda kuchukuru ripoti katika kituo chake”
“Sasa tuna fanyaje mke wangu”
“Ngoja niulizie”
Rose akapiga simu kwa mkuu wa jeshi la polisi na akaulizia kuhusiana na taarifa za dokta Boaza akafamishwa walicho kipata makachero wa jeshi la polisi mara baada ya kuhojiwa wafanyakazi na baadhi ya watoto walipo katika kituo hicho.
“Nashukuru sana mzee wangu”
Rose akakata simu.
“Wanasema wamesha kwenda kuwahoji. Walezi wa kituo hicho wana sema Boaz naye alilelewa katika kituo kingine cha watoto yatima ambacho kipo chini ya kanisa la Katoliki. So baada ya kusomeshwa na kukua, akapata mafanikio naye akafungua kituo chake cha kulea hao watoto”
“Hicho kituo cha Kanisa Katoliki kipo wapi?”
“Morogoro”
“Twende huko mke wangu. Tuna weza kujua mengi kuhusiana na yeye. Masaa matatu hadi manne yana tosha sisi kufika Morogoro”
“Sawa”
Wakarudi ndani ya chumba alicho lazwa Jack.
“Tuna toka, kuna mahali tuna elekea. Kuna jambo tuna kwenda kulishuhulikia”
“Sawa”
Sophia alijibu.
“Chris na wezake wataendelea kuimarisha ulinzi”
“Sawa bro”
James na Rose wakaondoka na hospitalini na kuianza safari ya kuelekea Morogoro huku Rose akiwa ndio dereva wa gari.
***
“Eheee mbona umerudi tofauti na ulivyo kweenda”
“Wajinga wamenistukia”
“Kivipi?”
“Sijui aisee”
“So ulikuwaje ukatoroka”
“Ngoja ni nywe maji aisee hili jua litaniua”
Dokta Boaz akafungua friji, akachukua chupa ya maji na kuanza kunywa. Akaongeza upepo wa AC.
“Kwanza umehakikisha kuwa hufwatiliwi?”
“Ndio.”
“Imekuwaje?”
“Hospitalini kila kitu kimekwenda vizuri. Nimetoka pale nikachukua boda hadi sokoni, kuna chakula nilihitaji kuja kukipika. Sasa nikiwa pale kuna mama mmoja akawa ana nitazama ile ya kupeleleza hapo ndipo nikajua kuwa nipo kwenye mtego kwani kulikuwa na maafisa wengine wakinifwatilai kwa umakini sana”
“Eneo nilio kuwa njia, pekee ya kutoka mule ilikuwa ni kupitia chooni. Niliingia chooni ikanilazimu kutoka kupitia paa la choo”
“Ina maana hapakuwa na gypsum?”
“Haikuwepo zaidi ya bati tu. Nikaruka na kutokea upande wa piili. Nikatembea kwa haraka hadi barabarani ambapo nikapa bajaji iliyo nipeleka hadi maeneo madukukani, nikanunua nguo nilizo vivaa na nikaenda kubadilisha muonekano katika chochoro moja.
“Hawajakuona watu ukivua sura yako ya bandia?”
“Hawajaniona”
“Sasa wamekujuaje?”
“Mimi nahisi ni yue mwanamke niliye kutumia picha yake na kosa nililo lifanya ni kumsogelea”
“Kumsogelea kivipi?”
“Pale hospitalini kuna friji la kununua vijanywaji hivyo nilitaka kumchunguza vizuri hapo ndipo nilipo chnaga karata zangu vibaya”
“Na wakakuacha utoke nje ya hospitali”
“Ndio na naamini walitaka kunifwatilia hadi ninao ishi”
“Boaz usije ukaniletea matatizo”
“Huwezi kupata matatizo kuwa na amani. Hujapta taarifa zake?”
“Hapana”
“Daaa. Yule binti ni nani ina bidi nimshuhulikie aisee”
“Kwa nini usiachane na huu mpango”
“Nimesha chukua pesa ya watu. Siwezi kuacha hii kazi na mimi sio mtu wa kukatishwa tamaa na changamoto ndogo kama hizi. Ni lazima nikamishe mission yangu”
“Wewe niambie uta zikwa wapi? Morogoro au hapa hapa Dar. Hawa watu wapo seriously na wamesha kuweka kwenye mabado. Kama leo umeweza kupotea chupu chupu basi kesho wata kukamata rafiki yangu. Nakushauri achana na huu mpango. Hii ngoma unayo taka kuicheza ni nzito kuliko uwezo wako. Jizime data rafiki yangu ila naona mwisho wako una kuwa ni mbaya”
Dokta Boaz akatulia kwa sekunde kadha akiufikiria ushauri anao pewa na rafiki yake, japo ana jiamini kweye kazi yake ya uuaji ila anacho elezwa na rafiki yake ni kitu cha maana na asipo kuwa makini ata kufa.
ITAENDELEA
Mchaka mchaka mpya umeanza. Rose na James wana elekea Morogoro, je wata fanikiwa kupata taarifa za Dokta Boaz? Dokta Boaz amepewa ushauri wenye ukweli ndani yake ja ata uzingitia au ataendelea kushupaza shingo akiamini katika uwezo wake? Ungana nami katika stori hii ya kusisimua sehemu ya 56.
 
DEVIL’S FAMILY(FAMILIA YA MASHETANI) 56


KILA KILICHO ANDIKWA KATIKA HADITHI HII NI UTUNZI HAKIENDANI NA KISA CHOCHOTE KILICHO WAHI KUTOKEA MAHALA POPOTE ASANTE
*************************************************************************************

ILIPOISHIA
“Kumsogelea kivipi?”
“Pale hospitalini kuna friji la kununua vijanywaji hivyo nilitaka kumchunguza vizuri hapo ndipo nilipo chnaga karata zangu vibaya”
“Na wakakuacha utoke nje ya hospitali”
“Ndio na naamini walitaka kunifwatilia hadi ninao ishi”
“Boaz usije ukaniletea matatizo”
“Huwezi kupata matatizo kuwa na amani. Hujapta taarifa zake?”
“Hapana”
“Daaa. Yule binti ni nani ina bidi nimshuhulikie aisee”
“Kwa nini usiachane na huu mpango”
“Nimesha chukua pesa ya watu. Siwezi kuacha hii kazi na mimi sio mtu wa kukatishwa tamaa na changamoto ndogo kama hizi. Ni lazima nikamishe mission yangu”
“Wewe niambie uta zikwa wapi? Morogoro au hapa hapa Dar. Hawa watu wapo seriously na wamesha kuweka kwenye mabado. Kama leo umeweza kupotea chupu chupu basi kesho wata kukamata rafiki yangu. Nakushauri achana na huu mpango. Hii ngoma unayo taka kuicheza ni nzito kuliko uwezo wako. Jizime data rafiki yangu ila naona mwisho wako una kuwa ni mbaya”
Dokta Boaz akatulia kwa sekunde kadha akiufikiria ushauri anao pewa na rafiki yake, japo ana jiamini kweye kazi yake ya uuaji ila anacho elezwa na rafiki yake ni kitu cha maana na asipo kuwa makini ata kufa.

ENDELEA
“Umenielewa ndugu yangu”
“Mimi ninawaza namna gani ya kuwala vichwa hawa wajinga”
“Seriosly?”
“Ndio naaamisha. Sijawahi kushindwa kazi mimi. Kaa uelewe hivyo”
“Sawa mimi yangu macho ndugu yangu. Nita kuunga mkono kwa kile ukitakacho. Ili mradi jambo lako lisijirudi kwangu”
“Usijali. Nimepata wazo”
“Wazo gani?”
“Ngoja nilifanyie kazi akilini mwangu kisha nitakushirikisha. Hakuna kushindwa hapa, ngoja nikalale kwanza”
Dokta Boaz akanyanyuka na kuelelea chumbani, akaingia chumbani na kujilaza kitandani huku akiendelea kufikiria namna ya kupambana na familia ya mzee Tiger.
***
“Una lala una raha gani?”
Mrs Tiger akakurupuka kutoka usingizini. Akamuona bibi wa familia akiwa amekaa kitandani pembeni yake.
“Nimekuja kwa ajili ya kuikamilisha kazi niliyo kuambia. Fanya maamuzi”
Mrs Tiger akaanza kutetemeka huku akijawa na kigugumizi.
“Umeamua nani wa kufa?”
Mrs Tiger akajifikiria kwa sekunde kadhaa.
“Au nikuchukue wewe”
“Hapana hapa”
“Kwa makosa muliyo yafanya ina ina hitajika kafara ya familia. Zungumza nani wa kufa?”
Mrs Tiger akafumba macho huku machozi yakimbubujika.
“Nakusikiliza”
“Mume wangu”
“Sawa. Shuka kitandan unifwate”
Mrs Tiger akamtazama bibi wa familia kisha taratibu akashuka kitandani na kuanza kumfwata bibi.
“Kitu kimoja ninacho kukubali kuhusiana na wewe ni jinsi ulivyo nyumba yangu hii. Mama yako mkwe alijaribu kubadilisha baadahi ya vitu visivyo badilishwa kwenye hii familia ndio maana niliamua kumshuhikia mapema sana. Naamini ulipo olewa ulisha ambiwa nini cha kutoa na nini si cha kutoa”
“Ndio bibi”
Mfanyakazi wa ndani anaye pishana na Mrs Tiger akageuka kushangaa boss wake kuzungumza mwenyewe.
“Madama”
Mrs Tiger akageuka.
“Ehee na kumtazama mfanyakazi huyo.
“Umeniongelesha?”
Mfanyakazi aliuliza.
“Hapana. Kichwa changu hakipo sawa, kaendelee na kazi”
“Sawa”
Mfanyakazi akaondoka.
“Ina maana hawakuoni?”
“Hakuna anaye kuona zaidi yangu”
Mrs Tiger akazidi kushangaa kwani matukio hayo toka ameolewa na mume wake ndio yanamtokea. Wakaingia ndani ya chumba alichopo Mzee Tiger.
“Madam”
“Mumekula?”
Aliwauliza madaktari wawili.
“Ahaa….bado mkuu”
“Nendeni wakawaandalie chakula.”
“Sawa”
Madaktari wakatoka chumbani na kumuacha Mrs Tiger na mumewe.
“Mume wako leo ndio ina kuwa siku yake ya mwisho kuishi duniani, ata lipia makosa ambayo alikubali yatokee kwenye hii familia”
“Makosa gani?”
“Moja wapo ikiwa ni wewe kuanzisha mahusiano na yule kijana”
Mrs Tiger akakaa kimya akimtazama bibi wa familia.
“Mtoe mpira wa oxygen”
“Ehee”
“Ndio”
Taratibu Mrs Tiger akamtoa mumewe mpira wa hewa ya oxygen inayo msaidia kupumua. Mzee Tiger akafumbua macho na kumtazama mke wake hadi akashtuka.
“Mu….mume wangu”
“Unataka kuniua”
Mzee Tiger alizungumza maneno yaliyo zidi kumvuruga mrs Tiger.
“Chukua mto umalizie”
Bibi wa familia alizungumza.
“Chukua mto”
“Usifanye hivyo mke wangu…….Usiniue”
Mzee Tiger alizungumza na kuzidi kumchanganya mkewe.
“Nimekuambia chukua mto”
Bibi wa Familia alizungumza kwa ukali. Mrs Tiger huku machozi yakimwagika, akachukua mto.
“Usiniue mke wangu………...Nakuomba usiniue”
“Muuueeeee au Jack afeeee”
Mrs Tiger kwa haraka akaanza kumgandamiza usoni mzee Tiger kwa kutumia mto. Mzee Tiger akaanza kurusha rusha miguu yake kwa kukosa pumzi. Galfa mlango ukafunguliwa na wakaingia madaktari wawili.
“Unafanya nini madam”
Daktari mmoja akamuwahi Mrs Tiger na akmapokonya mto. Mrs Tiger akatazama eneo alilo kuwa amesimama bibi wa Familia na hakumuona. Daktari mmoja kwa haraka akmarudishia mzee Tiger mrija wa oxygen.
“Unataka kumuua mumeo?”
Daktari aliye mpokonya simu Mrs Tiger alimuuliza kwa ukali huku akimtazama Mrs Tiger anaye mwagikwa na jasho mwili mzima.
“Kwa nini?”
Mrs Tiger akakaa kwenye sofa la pembeni huku akitetemeka.
“Ingekuwa sio kuunganisha mifumo yake ya hewa na saa zetu ina maana sasa hivi mumeo angekuwa maremu”
Mrs Tiger akakosa cha kuzungumza akabaki akimtazama daktari anaye zungumza kw amsisitizo.
“Unataka tuonekane hatupo makini kwenye utendeji wa kazi yetu?”
“Nisamaheni”
Mrs Tiger akanyanyuka na kutoka chumbani hapo.
“Hili jambo ina bidi tumueleze mwanaye wa kwanza.”
“Vipi hali yake?”
“Imetengemeaa na kurudi kawaida”
“Ngoja nimpigie James”
Daktari aliye kuwa ana mfokea mrs Tiger alizungumza huku akiitafuta namba ya James kwenye simu, akaipata na akampigia simu James.
“Dokta”
“Habar James”
“Salama. Mzee anaendeleaje?”
“Kuna tukio kidogo limetokea”
“Tukio gani?”
“Ahaa tumemkuta mama yako anataka kummalizia mzee kwa bahati nzuri ni kwamba tuliwahi kuingia kwani alarm za saa zetu zili tutaarifu”
“Mama?”
“Ndio James”
“Sawa hali yam zee?”
“Tulimuwahi kumrudshia oxygen na hali yake imerudi kuwa vile vile.”
“Sawa nina shukuru sana kwa hii taarifa. Kwa sasa ngoja niifanyie kazi”
“Tuna shukuru. Tumekupa taarifa mapema ili endapo kikitokea chochote basi mikono yetu iwe misafi”
“Nashukuru”
James akakata simu.
“Kuna nini?”
James akamtazama Rose anaye ndelea kuendesha gari.
“Ngoja dakika moja”
James akaingia kwenye mfumo wa kamera za nyumabani kwao. Akaingia katika kamera ya siri aliyo ifunga chumba alicho lazwa baba yake pasipo mtu yoyote kugundua. Akamuona mama yake akiingia ndani ya chumba akiwa ameongozana na mtu asiye onekana ila kina onekana kivuli chake.
“Hembu simamisha gari pembeni”
Wakasimamisha gari pembeni.
“Ngoja”
James macho yakamtoka kwa mshangao kuona mama yake akiwa nana zungumza na kivuli huku baba yake akiwa naye ana zungumza.
“Umeona”
James aliumuonyesha video hiyo Rose. Wakatazama tukio jinsi linavyo kwenda.
“Aliye simama pembeni ni nani?”
“Haonekani na nikivuli tu”
“Inakuwaje mzee ana zungumza”
“Kuna hali isiyo ya kawaida inayo endelea.”
James alizungumza akimuona mama yake jinsi anavyo mzee Tiger kwa mto usoni. Hadi madaktari walivyo ingia ndipo sauti zikaanza kurekodiwa na kamera hizo.
“Na kile kivuli kimepotea?”
Rose alishangaa.
“Ni jini ujue”
“Jini?”
Rose alizidi kuuliza kwa mshangao.
“Ina wezekana. Hoonekani kwenye kamera, kina onekana kivuli, ana zungumza na mama ambaye ana muona, halafu mzee ambaye ana umwa ana zinduka na kuongea baada ya hapo madaktari kuingia ni kama akawa amezinduka”
“Mmmmm mume wangu ujue hadi damu imenisisimka”
Jack akamtazama Rose.
“Ina wezekana ni wale nilio kuambia”
“Kina nani?”
“Wakuu wa huu ukoo ambao walitaka niuwawe ila mipango yao ya kuniu haijakwenda vyema”
“Mmmm”
“Ndio ona wamempiga mzee, wammepiga dogo na sasa hivi mama ina bidi alazimishe kuwaua”
“Amuue hadi shem?”
“Ina wezekana”
“Mmmm hii ni hatari mume wangu. Mtumie video hiyo mchungaji Kimaro. Kama aliweza kutuombea tukaepukana na hayo mauza uza nina uhakika ana weza kumuombea mama naye akawa sawa”
James akafikiria kwa sekunde kadhaa.
“Ngoja nimpigie simu”
James akampigia simu mchungaji Kimaro.
“Shikamoo mchungaji”
“Marahaba. Tena nilitaka kukupigia simu, umeniwahi”
“Kuna nini?”
James akaweka loud speaker.
“Nimeonyeshwa mukipata ajali mbaya sana wewe na mkeo. Yaani kabla ya chochote tusali”
James na Rose wakatazamana. Mchungaji Kimaro akaanza kusali. Dakika tano zikatosha kwa mchungaji Kimaro kimaliza sala yake.
“Asante sana mchunaji”
“Karibuni. Ulitaka kuniambia nini?”
“Kuna video nina kutumia hapa. Naommba ikiwezekana uende nyumbani”
“Sawa tukutane nyumbani kwenu”
“Mimi na mke wangu kidogo tupo mbali”
“Rudi tukune nyumbani”
“Sawa”
James akakata simu.
“Turudi tu mume wangu”
Rose alizungumza.
“MUNGU wangu!”
James alishangaa mara baada ya kuona lori likishuka kwa mwendo wa kasi kwenye muinuko.
“Mamaaaaaaa”
Rose alipiga kelele ya woga kwani lori hilo lililo poteza breki limewalenga upande wao. Rose akashindwa hata kurudisha gari nyuma. Dereva wa lori akajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kulikwepa gari walilomo James na Rose na akafanikiwa, lori lake likaacha barabara na kuelekea vichakani huku ni kwa mita mbili likipia pelee zikiwa zimelitenganisha gari analo endesha Rose na lori hilo. James akashuhudia jinsi lori hilo lianvyo zidi gonga miti na likasimama kama mita mia moja kutoka ilipo barabara ya lami.
“Babe babe”
James alimshtua Rose aliye fumba macho yake. Rose kwa haraka akaanza kijishika mwilini mwake kuona kama bado yupo hai.
“NIipo hai?”
“Ndio MUNGU ametuepushia. Twende tukamuokoe dereva”
“Nenda mume wangu hata nguvu sina”
“Tulia hapa”
James akashuka ndani ya gari, akakimbilia lilipo lori la mafuta. Akafika eneo lilipo lori na akamkita dereva akiwa amebanwa ndani ya gari huku akilia.
“Fungua mlango”
Alimuambia dereva kwani mlango ameifunga kwa ndani. Dereva kwa jinsia livyo banwa akashindwa hata kufungua mlango. James kwa kutumia kitako cha bastola akavunja kioo cha upande wa dereeva. Akafanikiwa kuufungua mlango kwa ndani.
“Fuc**”
James alizungumza hukua akishindwa kumchomoa dereva alipo banwa. Kwa haraka akashuka kwenye ngazi za gari. Macho yakamtoka mara baada ya kuona mataki mawili yanayo vutwa na kichwa cha lori yakimwaga mafuta huku cheche cheche zikiwa zikiwa zina jitokea kwenye nyaya zilizo katika.
“Spana una weka wapi?”
“Kwenye toolbox”
Akavunja kuvulia kwa kutimia kitako cha bastola kisha akachkua spana kubwa akapandisha ngazi za lori na kuanza kutanua eneo ambalo dereva amebanwa. Taratibu Rose akashuka ndani ya gari, akatazama eneo alilo elekea James. Akazima gari na akalifunga kitendo cha kupiga hatua mbili tu kuelekea lilipo Lori, mlipuko mkubwa ukatokea kitendo kilicho mstua sana Rose na mbaya zaidi James yupo eneo la mlipuko.
ITAENDELEA
Mchaka mchaka mpya umeanza. Mrs Tiger ameshindwa kumuua mume wake baada ya madaktari kuingilia kati je bibi wa familia ata msumbua tena? James katika harakati za kumuokoa dereva, lori la mafuta limelipuka je James ata kuwa hai? Ungana nami katika stori hii ya kusisimua sehemu ya 57.
 
Back
Top Bottom