Developers wa Tanzania, kwanini tusiungane?

Mm nilitegemea kuwepo na subsections za programming languages e.g Assembly,C,C++,Java,Python,C#,PHP and so forth
I'm not sure that will work either. Tulitafutana Developers tukachangishana na kuanzisha forum ila haijawahi take off kwa sababu ya lack of contributors. Watu wako tayari kusaidia maswali lakini wauliza maswali hawapo!

Forum Yenyewe ni hii hapa: Tanzania Technocrats Forums

WhatsApp pia haisaidii. Kama alivyosema njunwa hapo ni vigumu kutafuta topic ambayo imeshajibiwa ikusaidie kwenye WhatsApp. Pia kwa kuwa Programming ni kubwa na pana hamuwezi kuwa na group moja la kutatua kila tatizo.

Baada ya kusema hayo, sioni njia ya kuwasaida developers wa Tanzania kama hawajaamua kuunga mkono juhudi za kuwasaidia. Miaka inasonga na wengine umri uakimbia, who knows when I will wake up next second in heaven and say bye to earth? Na maujuzi yote nitakufa nayo na huko niendako hayatahitajika.

As I said before I have tried every way, laki ndio hivyo tena mwamko sifuri. Nadhani kwanza tuunge mkono juhudi za walioanza. Sio lazima uwe founder ili uache legacy. Hata kuwa contributor pia ni legacy.

Wasalaam!
 
Sifa za wabongo wengi
1. Waoga
2.Hawana uthubutu
3.Wepesi kukata tamaa
4.Hawaangalii kesho, bali wanajali sana leo atapata nini.
5.Wanaogopa kupata hasara, ila wanasahau pia hasara ni somo zuri la kupata faida.
Nyongeza-No.6.Wabinafsi
 
Sifa za wabongo wengi
1. Waoga
2. Hawana uthubutu
3. Wepesi kukata tamaa
4. Hawaangalii kesho, bali wanajali sana leo atapata nini.
5. Wanaogopa kupata hasara, ila wanasahau pia hasara ni somo zuri la kupata faida.

Ila napenda kusema kuwa vyote nakubaliana navyo kwa asilia 100% pamoja na nyongeza ya Mkuu stephot kwamba WABINAFSI

Ingawa huu uzi lengo lake lilikuwa ni kutaka kujua nini tukifanye tuungane, na mimi sijajibu hoja kwa sababu nilikuwa nataka niwajuze na nyie hii habari niliyosoma kutoka AllAfrica.com.

Tukirejea kwenye hoja, binafsi mie ningependa kusema "Wepesi kukata tamaa" ni tatizo langu na nimeona hilo kutoka kwa watu wengi.
Kwa nini mie nimekuwa nakata tamaa mapema kwa maana sijawahi kuwa naweka malengo kwenye kitu vitu ninavyopenda kufanya.

Kitu kimoja nimegundua, kuwa inabidi kuwa na watu munaoendana kitabia na mambo ya kufanya.
Kwa mfano hakuna siku ambayo nilijifunza mengi kama siku niliyokutana na Stefano Mtangoo .. Huyu mtu ni asset moja kubwa sana. Ana mawazo na uelewa mkubwa sana. Amefeli mara nyingi na amejifunza mengi. Mengi nimetoa kwake.

Turudi kwenye mada, ili watu waweze kuungana inabidi tuweze kupata kitu/ vitu vya kutufanya tuweze kuwa pamoja. Mfano, more tech centers isiwe Buni tuu.. Ziwe zaidi ya 50. Hii itasaidia watu kuwa pamoja zaidi na wenye mawazo sawa. Hapo ndio unarudi kwenye "Gov Policy", kusema ukweli sijaona kama tehama ni kipa umbele kwenye mkakati ( naomba nirekebishwe kama sikuona ilipo). Ila hapa ningependa nilaumu makampuni ya mid-size ya IT kwa Tanzania, kwani hapa ndio wao walitakiwa watumie nafasi, kwa ku-host small meetings about tech ili kupromote technology na vile vile kwa wao kujitangaza kwa bureee, na pia kupata talent mpya kwa kampuni zao. Hii natoa challenga kwa kampuni kama Fasthub , Raha , na mengineyo mengi..
Kitu kingine ambacho tunatakiwa kufanya ni "kupromote tech kwa watoto na sio wazee", hii itasidia sana kubadilisha mtazamo wa watu kwa muda mfupi sana.

Nawakubali sana Jumanne wa Buni, J.P, Feruzi wa Kinu, na wengi ambao nimekutana nao.

Safari bado ni ndefu. Tutafika tuu. Tusilaumu kila kitu. Tuwaunge mkono wanaojaribu kufanya vitu.

Source: Tanzania Software Developers Fail to Seize Rare Chance

 


Nimekuelewa sana mtaalam
 

Utusamahe bure mtaalam maana atujue tulitakalo. πŸ™‚
 
Dah mkuu aise kiukwel na mimi nilikua na idea flan hvi we can do something kwakwel
 
Hakika sisi ni madevelopers wabinafsi. Hadi sasa no progress, kweli Poor produce Poor πŸ™‚
 
Hakika sisi ni madevelopers wabinafsi. Hadi sasa no progress, kweli Poor produce Poor πŸ™‚
Inabidi wewe ndo organize watu...kama ulivokwisha jitolea na kuwaweka katika forum fulani!

Yaani wewe muanzisha thread hii ilibidi ujitolee kutoa guides na kuwapata watu walio na utayari wa kuunga mkono katika kuungana kushare knowledge!
 
Inabidi wewe ndo organize watu...kama ulivokwisha jitolea na kuwaweka katika forum fulani!

Yaani wewe muanzisha thread hii ilibidi ujitolee kutoa guides na kuwapata watu walio na utayari wa kuunga mkono katika kuungana kushare knowledge!

Ni kwel ila niliwaambaia ambao wako interested wanichek fb tuanze mchako wa kushare ideas lakin wamerespond wawil mm nifanyeje hapo mkuu em we sema.
 
Hakika sisi ni madevelopers wabinafsi. Hadi sasa no progress, kweli Poor produce Poor πŸ™‚
tupeane moyo na kuleta mchango chanya..
sio tutupiane vijembe.. na kulaumiana..!!

kwa mfano ungeweza kutengeneza pool hapa ..ya kuomba vitu gani vinaweza vikafanywa ili tuweze kuungana...
naona kuna watu wameenda inbox Detective J na PATO8221, kwa nini wametoka nje ya uzi na kwenda inbox?

Tungeaza kwa kutoa mapendekezo mambo gani yanaweza kufanyika ili devOps waweze kuungana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…