Deus Kibamba : Rais hapaswi kupingwa

Deus Kibamba : Rais hapaswi kupingwa

Wadau wekeni namba ya simu ya Deus kibamba ili wapenda Amani wampigie simu kibamba apewe Ukweli wake.
 
Rais wetu anapaswa kuheshimiwa. Wale wanaopinga wawe na heshima wanapoeleza hisia zao.

Kama kweli wenyewe akina ZZK na Lisu ni wakweli mioyoni mwao, wazungumzie pia yale mengi mazuri ambayo Mh. Rais ametekeleza.
 
Usijari. Kwanza nimefurahi kuona hufuraishwi na umungu wa kibinadamu.
Ndg yang nakaslika sana mtu kujipa umungu najiuliza ujasir wanautoa wap..kama mkuu wa mkoa mmja hv alisema et akisema yey n kama amesema Mungu tang hapo stomuheshm tena..weng wanakufuru kwakutaka mafaraka na kulewa sifa..asante mkuu nmekuelewa.
 
Kibamba ni mchochezi.
Mbona juzi tu Dr,Makongiro Mahanga kampinga Rais kuhusu teuzi za wabunge na Rais akabadili teuzi mara moja?
Mimi nadhani Rais wetu ni msikivu na anapenda kusikia maoni yetu katika kila jambo.
 
Sasa kibamba yeye alipokuwa anamkosoa Rais Kikwete wakati huo alikuwa halijui hilo? au kwa sababu Kikwete hakuwa wa dini yake na chuki binafsi zikiwemo ndio maana kila iliyokuwa ikijiita tasisi binafsi ilikuwa ikimchukia JK?

Sent from my TECNO M7 using JamiiForums mobile app
 
Huo utukufu ni kwa zama hizi tu?? Mbona sehemu nyingi duniani hakuna kitu kama hicho? Au hizo sio Ikulu??! Jana umeona USA watu walivyotumia uhuru wao kikatiba kuandamana na polisi hawakutumia nguvu nyingi kuwazuia,
Huko binadamu wote ni sawa
 
Kama unaona Rais anakosea njia rahisi ni wewe kugombea Urais ili utekeleze unayoyaona mema kwako wewe na si kumtukana na kumkebehi kiongizi wa nchi publicly. Hiyo hata mimi siikubali. Hata hivyo Magu mpole sana. Ningekuwa mimi mngeipenda. Mmekaa kusifia Rwanda tu. Wanamheshimu kiongozi wao na hawana manenio ya kumkatisha tamaa kama mlivyo nyie. Mnataka kuona pepo lakini hamtaki kufa. Ajabu na kweli aisee. Watanzania hawajui wanataka nini na kwa wakati upi. Rais mmepewa na Mungu kazi kumkebehi tu. Mpeni support atutoe. Baada ya huyu kama si Majaliwa au hata Samia hakunaga tena. Mtalia na kusaga meno. Kufeni muione pepo. Vumilieni nchi isafishwe hata kwa miaka mitatu tuanze kula mema ya nchi. Mnapakua paja za kuku chungu kikiwa jikoni si mtaipua hata hoho zikiwa zishaisha? Nyie!!!!
 
Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini Dar es Salaam , ndugu Deus Kibamba asema Rais hawezi kupingwa waziwazi,amedokeza iwapo mtu ana mtazamo hasi kwa rais anapaswa kutafakari moyoni badala ya kumzungumzia vibaya rais. Amewaelezea wapinzani wa Tanzania jinsi wanavyomkosoa rais bila kuona mema yake.
Ameyasema hayo katika kipindi cha 360 cha Clouds TV .
Issue sio kupingwa, nadhani issue ni namna unavyompinga mtu. Je, unaongea kwa kujenga hoja za maana?, unaongea kwa kebehi na dhihaka?. Au unaongea kwa nia ya kujenga constructive criticism.

Waalimu wetu wa mashuleni hawawezi kukwepa lawama katika malezi mabovu haswa miongoni mwa wanasiasa walio kwenye umri wa kuzalisha kwa sasa.
 
yuko sahihi ndg.kibamba. urais ni taasisi kubwa na tukufu kimsingi. inapaswa kuheshimiwa
Sasa kwa mfano kama anayeishika hiyo nafasi hajiheshimu watu watafanyaje? Kama kweli urais ni taasisi inapaswa kuanza na anayeishika hiyo nafasi afanye kazi akitambua kwamba ni taasisi na siyo yeye peke yake ndo mwenye maamuzi. Vinginevyo itakuwa ngumu kwa mtu wa kawaida kuiheshimu hiyo taasisi!
 
Back
Top Bottom