Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,395
- 13,266
Hakuna kejeli hapo wala dharau labda uwe hujapitia maoni mengine ya wadau. Posts kama zile za kibiashara lazima watu watakuwa na maswali au kutaka kuwasiliana na mtoa mada. Sasa ukiingalia post ile na kusoma maoni ya wachangiaji utaona wengi walikuwa na hamu ya kujua bei, walipo wenye biashara, aina nyingine ya bidhaa, nk. Lakini hakukuwa na majibu na wengi wakawa wanashangaa inakuwaje unatoa mada ya kibiashara halafu unapotea wakati wateja wanakiu ya bidhaa yako. Hivyo mimi kudhani kuwa inawezekana mtoa mada kakopi mahali lakini siye mjenzi au mwqenye biashara. Kama unajua kiswahili vizuri utaona nimeanza na neno "Inawezekana" kwahiyo sikusema wamekoipi kwa asilimia 100. Hiyo pia ilikuwa mbinu ya kuchochea mtoa mada ili arudi kujibu maswali. Ningeandika kwa kiingereza ningesema "May be.."Acha kejeli, sio vizuri na si busara unavyofanya.