Design simple za Nyumba vyumba 2

Design simple za Nyumba vyumba 2

Simple design ya vyumba viwili,
1. masterbedroom size 3.0x4.5m,
2. Bedroom 3.0x3.5m,
3. sitting/lounge 4.3x4.7m,
4. dinning 2.6x3.0m,
5. kitchen 2.3x3.2,
Kuna stoo, public toilet, & bathroom.
Plot ya 20x20 nyumba inakaa vizuri na parking lot.
Makadrio ya gharama za ujenzi (BOQ) upewe tu funguo uendelee na life ni 50 Milioni.
 
Kwa kipindi hiki ujenzi ni gharama sana ukigusia vifaa vya ujenzi, ndio hali halisi, labda kwa ujenzi wa tofali za kuchoma ambazo pia nazo zina msimu wake na bei hubadilika huko zilipo, mijini ni block zaidi.
 
Shukrani mkuu .....hasa Hapo kwenye rooms 3 ......tutawasiliana
 
duh! Mungu sianifanyie muujiza!! moyo wangu umehuzunika lkn macho yamefurahia!
Usihuzunike kwani ukiamini utajenga utajenga tu kikubwa ni kuthubutu, unajua nyumba inajengwa kwa hatua na wala usifikirie kuzichanga mpaka zifike 20 milion, hatua ya kwanza ni kuzichanga unanunua kiwanja kinakuwa pending tu sehemu alafu hatua ya pili unakusanya materials angalau ya msingi, amini usiamini ukiweza kupiga msingi na ukawa una kipato chako mdogo mdogo unamaliza na huwezi amini.

Tatizo wengi linapokuja suala la kujenga anataka kununua kiwanja na kuanza kujenga matokeo yake hela hazitoshi na kila ukipata hela zinaingia kwenye matumizi mengine lakini kwa mtu mwenye kiwanja unakuta akipata laki 2 au 3 nusu anaweza akaitumia kwa mambo yake na nusu akatupa hata tripu mbili za mchanga site kwa kuwa ana sehemu ya kuweka huo mchanga lakini ukiwa huna kiwanja lazima kama binadamu utazitumia tu kwa mambo mengine maana hazitoshi kununua kiwanja na wewe huna kiwanja
 
Kiongozi unaweza kuweka floor plan yake na sample estimation yake??

Sample estimation zipo, floor plan zipo tayari kwa ujenzi. Utapewa ukiwa serious unataka kujenga kweli.
 
Mkuu wewe ndio muhisika wa ujenzi wa hizi nyumba au wewe ni DALALI!
 
Kwa ujenzi wa kawaida na ule unaofuata taratibu za mipango miji, njoo ujipatie ramani za vyumba 2, 3, 4. Mfano hiyo chini hapo ni ya vyumba viwili Ina mita 8 kwa 11 haina corido ubunifu mpya wa sasa, ndani kuna master, chumba kimoja kawaida, choo public, stoo, jiko, sebule na dining. Ujenzi substracture tofali 1206 size 230 mm na superstructure tofali 1758 size 150 mm kuezeka ni bati 38 tu. Hapo mengi zaidi join whatsapp group.

Call or Whatsapp: +255787459850

Nyumba simple haiwezi kuwa n rangi na details yingi hvyo. Splash ya rangi nigharama sana. Pia mapambo yaukutani
 
Nyumba simple haiwezi kuwa n rangi na details yingi hvyo. Splash ya rangi nigharama sana. Pia mapambo yaukutani

Usiogope tumekokotoa cost za vyote BOQ na schedual of material vipo
 
Vyumba 2, kuna master, 1 kawaida, jiko, stoo, lounge/dining, public toilet. Ukubwa wa 8.3x9.6m inatosha plot ya 15x15m. Unique design no Corridor
 
Priced BOQ ni 60Milioni

Huo ujenzi wa ki-BoQ mkuu mmhh!!! nilidhani muulizaji yuko kibongobongo zaidi. Tukienda kwa utaratibu huo tunaweza kutishana tusithubutu kuanza.
 
Back
Top Bottom