Dereva wa Basi la Mwendokasi adaiwa kuwapitiliza Vituo Abiria baada ya kukasirishwa

Kwamba watu walikuwa wengi hivyo akisimama wanaongezeka na wao wamepanda express yenye vituo vichache vya kushusha na kupanda na sio vituo vyote

Kwani hujawahi kuona mtu anapanda Gerezani anashukia Faya ili aende Kivukoni??

Dereva alikuwa anasimama kama wajibu wake wa kazi unavyomtaka kusimama vituo anavyotakiwa!

Hata kama ni mie, ningepitiliza hadi Kibaha pambaf...!!
 
Dereva katoka Gerezani akiwa na hasira gari limejaa milango hadi inataka kupasuka, Akasimama Faya watu wakawa wanamwambia kwa jinsi Gari ilivyojaa sana unatuumiza funga fungua fuata utaratibu sababu gari ni express kama ilivyoandikwa simama manzese kama ilivyo taratibu

Dereva akasimama na Magomeni kwa hasira, hapo gari imejaa vibaya sana na ni express, watu wakaanza kelele tena unatuumiza huku mlangoni na hakuna wakushuka na wala wakupakia, wakwamwabia wapo wakushuka manzese

Dereva akasimama anaanza kuzozana na abiria Kwa hasira

Dereva akawasha Gari kutoka Magomeni hakusimama hata kituo kimoja kwa hasira akaenda kuwashusha Abiria wote Kimara Mwisho hapo Kuna walemavu kibao, akashuka akapotea kusikojulikana, likatokea bonge la fujo pale, watu warudishwe walipotokea fujo kubwa sana, ikabidi Gari achukue Dereva mwingine awarudishe watu waliopitilizwa vituo


View attachment 2938988

Huu mradi unauliwa na wafanyKazi wenyewe ni shida

Nadhani Kwa Mwendo kasi hii shida ya wingi wa watu kuliko magari imeanza kuwatesa kisaikolojia hata madereva wenyewe pia.. Japo Kwa abiria hiyo shida ni hivyo hivyo tangu kitambo tu.. Waongeze magari tu..
 
Hata hili la mwendo kasi nalo pia ccm wame shindwa kuendesha 🤔🤔 sasa wanaweza kufanya nini hawa watu 🤔🤔 alafu ukiwakuta hao wendawazimu wanavyo kisemea chama chao unaweza kudhani wame ifanya Tanzania kua china ya Afrika kumbe inakaribia kuzimu
 
Naona baada ya mwenzao kula makofi Leo akili zitawakaa sawa ... wanawaonaga wa Tz n wapole sana
 
DAR: Dereva wa Mabasi Yaendayo Haraka (Mwendokasi) ambaye jina lake halijafahamika, akiendesha kutoka kituo cha Gerezani kwenda Kimara, amedaiwa kutosimama kwenye vituo vingi vya njiani baada ya kurushiana maneno na Abiria ambao walilalamikia uendeshaji wake

Mdau wa JamiiForums.com amedai licha ya Basi kujaa, Dereva aliendelea kupakia Abiria ambapo walilalamika kuwa anawaumiza kwa kufungua na kufunga milango, hali iliyoibua ubishani. Baada ya kutoka Kituo cha Magomeni Dereva hakusimama, akawapeleka Abiria wote Kituo cha Kimara Mwisho

Anadai walipofika Kimara, Dereva alishuka na kuondoka na baada ya mvutano wa muda mrefu, Dereva mwingine akaamua kuchukua basi husika na kuwarejesha wale waliopitilizwa vituo

Soma Dereva wa Basi la Mwendokasi adaiwa kuwapitiliza Vituo Abiria baada ya kukasirishwa

#JFHuduma #JFUwajibikaji #JamiiForums
 
Hii nayo ni lin kwani maana uyu wa Leo kala vibao na nina zani next time atakuwa na heshima
 
Pale Muhimbili manyanyaso ni mengi sana, gari hazifiki Kwa wakati, unasimama kituoni hata lisaa limoja. Majibu ya wakata tiketi hauna chenji kamili hupati huduma, lugja za hovyo na ubabe. Kuna dereva mmoja anatukana mpk abiria.

Watu wanajazana mpk unaogopa, sijui tunaelekea wapi? Madereva licha ya mabasi kujaaa, wanajaza vituo vingine.
 
Back
Top Bottom